Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94

JOTO LA MAPENZI SEHEMU YA 3 -- 4

16th May, 2025 Views 12

SIMULIZI :JOTO LA MAPENZI ????????
MTUNZI : SIMULIZI ZA ANGEL
HURU MEDIA 0750411324
3--------------4

SEHEMU YA 3
TULIPOISHIA………

“Kama njia pekee ya kuondokana na hizi dharau pamoja na manyanyaso ni kuolewa na mwanae, mimi nipo tayari! Nitaolewa nae”

TUENDELEE………..

Sule alimtazama binti yake kwa makini

“umekubali?? Usifanye maamuzi ambayo utayajutia baadae Tabia!”

“Si amesema miezi mitatu tu? Nitavumilia hiyo miezi mitatu ili kusudi usamehewe deni letu”

“tabia una uhakika?” Sule aliuliza kwa mara nyingine

“Ndio baba! Nina hakika! Kwaajili yako nipo tayari”

Basi Sule alisimama pale chini huku akitabasamu! Alijiweka sawa na kukaa kwenye kiti, muda huo nae Mama Tabia alitoka chumbani na kwenda kukaa pembeni ya mumewe.

“Tabia! Nakutegemea wewe, najua maamuzi uliyofanya ni magumu ila ndo ivyo hatuna namna! Naomba tu uvumilie ili tumalizane na Sanga”

“Sawa Mama”

Tabia alienda chumbani kwake akiwa analia. Akiolewa na mtu mwingine ina maana Hataweza kuwa na Salimu tena, na ndo mwanaume ampendaye.

Lakini kwa sababu ya umaskini na shida anakwenda kujiingiza kwenye mdomo wa mamba! Je angeweza kuvumilia mpaka miezi mitatu iishe bila kukata tamaa??

Labda angeweza… Embu tusubiri tuone….

Basi Baada ya siku moja kuisha Sanga alirudi tena, na mara hii alikua ameambatana na wanasheria wake. Alikua na uhakika kabisa kua siku ile Sule angempa shamba kama fidia. Kwa jinsi ambavyo Sule anampenda binti yake, alijua hawezi kukubali kumuoza kwa kijana wake.

“Enhee Sule, umeamua nini? Unanipa shamba sio?” Alitabasamu

“Hapana, Tabia ataolewa na kijana wako!”

“Una…sem..a?” Alipigwa na butwaaa! Macho yakamtoka vibaya mno! Ghafla akashikwa na hasira

“Ndio! Tabia amekubali kuolewa na kijana wako”

“Kama ndo ivyo ulivyo amua hakuna shida! Jua kwamba, iwapo Tabia atashindwa kuishi na mwanangu kwa miezi mitatu ya ndoa basi shamba lako ni mali yangu”

“Na kama akiweza???”

“Nitakusamehe deni lako na hutasikia nikiongelea habari ya shamba lako”

“Sawa! limeisha”

Sule alikubali lakini Sanga hakupenda! Alirudi kwenye gari lake akaanza kupiga kelele za hasira. Mipango yake ya kulipata shamba la Sule ilikwenda kufeli.

Alitoa simu yake mfukoni na kutafuta namba za mwanae! Alipo zipata alimpigia

“mpango umefeli! Kamtoa mwanae”

“Dad! Usipa nick! We niachie mimi huyo binti, nitahakikisha hata mwezi hatamaliza!”

“wewe ndo jembe langu na nina kutegemea sana, unajua jinsi gani project yangu inahitaji lile eneo! Usiniangushe Calian”

“Trust me (niamini), i will make you proud!”

“Okay, tutaongea baadae”

“sawa”

Sanga alikata simu na kurudisha mfukoni. Hasira zake zilipungua kiasi cha kuanza kutabasamu tena! Aliwababewa wanasheria wake, akawasha gari na kuondoka.

Baada ya siku tatu kupita maandalizi ya ndoa yakaanza. Kijiji kizima kilijua Tabia ana kwenda kuolewa na kijana wa mjini, tena mwenye pesa kushinda hata Diwani wao.

Wadada wengi walimuonea wivu, walitamani wangeipata wao iyo bahati. Ila Salimu yeye alikua analia tu!

Mbona kila kitu alikamilisha, alibakisha mahari tu sasa kwanini Tabia atake kuolewa na mwanaume mwingine?? Ama hakua akimpenda? Siku zote walizokua pamoja ina maana alikua anamdanganya??

Maskini Salimu aliumia mno na kujuta kumpenda Tabia, akagoma kabisa kuonana nae pindi alipokuja kumuona.

Akawa anajifungia ndani mpaka siku ya harusi ilipofika. Akashindwa kuendelea kuvumilia, alivaa ndala zake na kupiga hatua ndefu ndefu mpaka nyumbani kwa akina Tabia.

Alipofika huko alikuta watu wengi sana wakipika na wengine wakiimba kwa furaha. Alitupa macho yake kushoto na kulia labda angemuona Tabia ila hakufanikiwa.

Badala yake aliona magari matatu ya bei ghali yakiwasili. Alikua Sanga kafika pamoja na Calian.
Basi wadada wote waliokua lile eneo walipomuona Calian walimshangaa mno.

Nani ambae hatamshangaa Calian jamani? Kijana handsome kama yeye, mtanashati anae jua vizuri kucheza na Tabasamu lake. Akikutazama una data mwenyewe, apo bado hata hajaanza kutoa sauti yake nzuri ya kumtoa nyoka pangoni.

Mpaka Hapo Salimu akapata picha halisi ya kwanini Tabia alimchagua Calian. Alimshinda kwa vingi mno, kuanzia muonekano hadi pesa. Kwa huzuni aligeuka na kuondoka zake!

Upande wa ndani hapakua na furaha hata kidogo, haswa kwa Tabia! Ndoa na Calian ni sawa na jehanamu ndogo.

Mbona Calian ni handsome ana kila sifa nzuri kwanini aseme ni Jehanamu ndogo? Labda tusubiri tuone kama kuna ukweli wowote kwenye kauli yake.

Basi Ndoa ilifungishwa pale, Tabia akawa mke halali wa Bwana Calian. Watu walikula wakanywa na kusheherekea kwa ngoma pamoja na mziki.

Jua lilipo zama tu, Sanga akaomba kuondoka na mwanae pamoja na mkwe wake, Hapo ndipo kilio cha Tabia kikaanza.

“Unalia nini mwanangu?? Eeeh?” Mama Tabia alimuuliza binti yake

“Naumia mama! Itakuaje huko niendako”

“Hakuna shida! Vumilia tu miezi mitatu baada ya hapo unaruhusiwa kufanya chochote kilee! Kikubwa deni letu lisamehewe”

“Sawa mama naomba pia pindi utakapo muona Salimu mwambie nampenda sana na anisamehe!”

“Usijali binti yangu! Ukiwa na shida yoyote mpigie simu Mama Ashura, atani letea ujumbe wako! Ama kama nikiwa karibu tutaongea! Sawa mwanangu?”

“Sawa Mama”

“Haya nakutakia maisha mema ya ndoa”

“Asante Mama”

Mama Tabia alipomaliza kumsihi Bintie, ikawa imebaki zamu ya Sule! Yeye hata hakua na maneno mengi! Alimpa moyo tu kisha akamkabidhi kwa Sanga.

Watu wakashangilia na kupiga vigelele hasa pale Tabia na mumewe walipo panda ndani ya gari na kuondoka.

Mama Tabia akabaki anapunga mkono hadi walipo potea mbele ya usawa wa macho yake.

“Mungu atamsaidia mwanetu! Kila kitu kitakwenda sawa”

“Na ikawe ivo”

Sule alimshika mkewe mkono wakarudi kuendelea na sherehe.

Nakuja……………

JOTO LA MAPENZI ????????

Sehemu ya : 4

????????????????????????????????????????????????????????????????????????

TULIPOISHIA………

Sule alimshika mkewe mkono wakarudi kuendelea na sherehe.

TUENDELEE………

Upande sasaa wa Tabia na mumewe, kila mtu alikua kimya kwenye Gari. Muda wote Calian alikua bize na laptop akifanya kazi zake za ofisi mpaka walipofika kwenye hoteli waliyo takiwa kupumzika kwa siku hiyo.

Walichukua chumba kimoja kikubwa sana! Walikuta wamekipamba kwaajili ya usiku wao wa ndoa! Calian alipoona vile alisonya na kupitiliza bafuni.

Alioga, akabadilisha na nguo zake ndipo akatoka! Akashangaa kumuona Tabia amekaa pale pale alipomuacha.

Hakumjali sana, alizima taa akapanda kitandani na kulala. Maskini Tabia alizimiwa taa na kubaki gizani.

Alisimama, akafungua begi lake la nguo kwa kupapasa. Hakua na nguo nyingi sana ivyo hakupata shida kuchagua! Alitoa na kipande cha kanga kisha akaenda hadi bafuni.

Alipofika huko alipashangaa sana, alitegemea angekuta kopo na ndoo ila kulikua tofauti sana na bafu alilokua amelizoea.

Mpaka choo kilikua cha kukaa, wakati wao wanachuchumaa kwenye shimo kubwa hata ukipitisha ndoo inaingia.

“Sasa hapa naogaje?? Mhhh, balaa hili jamani”

Aligeuka kulia na kushoto akaona kuna sinki lenye bomba. Kidogo akafurai, akalisogelea haraka akalitazama na kusita kidogo.

Ndia kuna bomba la maji, lakini atalifunguaje?? Akajitaidi pale kama angeweza napo akashindwa! Mwishoni akaanza kulia tena! Laiti angekua na hela yale yote yasinge msumbua hata kidogoo.

Kwa umri aliokua nao hata bomba anashindwa kulifungua, je iyo miezi mitatu ataweza kukaa kweli?? Basi akalia weee, alipotosheka alijifuta machozi, akavua gauni lake la harusi na kuvaa gauni lake la shifoni lenye lesi nyeupe upande wa chini. Akachukua kipande cha kanga na kujifunga vizuri ili ikitokea Calian akitaka kumgusa basi akose upenyo.

Alipohakikisha yupo sawa alirudi chumbani na kulala pembeni ya Calian.

“Hey, shuka chini?” Alisikia sauti nzito ikimuambia kwa upole

“Chini??”

“Sirudii mara mbili” Calian akaweka msisitizo

Bila kupinga akashuka chini na kujilaza kwenye kipande cha zulia kilicho tandikwa kule chumbani.

Alafu Kulala chini kwake haikua shida, godoro alilokua analalia Nyumbani kwao lipo kama ulimi, halina tofauti na sakafu. Taratibu akapitiwa na usingizi mzito mpaka palipo kucha.

Asubui alishtuka baada ya kusikia mlango wa chumbani kwao ukigongwa. Alitazama kitandani hakumuona Calian, ivyo akanyanyuka na kwenda kufungua mlango.

“Habari?? Wewe ndo Mrs Calian??” Mhudumu alimtazama Tabia kuanzia juu mpaka chini sababu ya mavazi aliyokua amevaa. Na kingine hakufanania kua mke wa kijana handsome kama Calian

“Ni mimi”

“Okay, utakunywa chai na nini? Ama ungependelea kupata kifungua kinywa gani?”

“Aaah! Viazi? au mhogo!”

Yule mhudumu alicheka na kumtazama Tabia kwa mara nyingine tena huku akiweka dharau ndani yake

“Huku tuna bites tu!”

“ndo nini hizo”

“Hujui Bites??”

“Hapana! Kwani ndo nini?”

“okay, bites ni vitafunwa kama bagia, sambusa, kababu, kalmati, halfcakes”

Vile vyote alivyo tajiwa Tabia hakuvifahamu zaidi ya kalmati! Kijijini kwao kuna mama anaitwa Zuleya huwa anapiga Kalmati na kuuza mia mbili! Alishazila sana mpaka akawa mteja mkubwa wa Zuleya.

“Kalmati! Nataka hizo”

“Hakuna shida! Na chai, ama juisi!”

“Chai, na juisi pia”

“Mh! Chai ya maziwa ama ya rangi?”

“Ya maziwa”

“Sawa nakuletea sasa ivi”

Yule mhudumu aliondoka huku akiwa anacheka sana! Hakuwai kuona binti mshamba kama Tabia! Basi alienda upande wa mgahawa, akabeba vyote alivyo agizwa na Tabia na kumpelekea chumbani kwake.

Tabia alifurai sana alikula kama hana akili nzuri, alitamani kwenda kuongeza makalmati sema ni vile alikua na aibu!

Akamaliza kupata kifungua kinywa akamsubiri Calian ambae hadi mda huo hakujua alikwenda wapi.

Hazikupita dakika tano Calian alirejea, tena alipoingia chumbani hakumsemesha Tabia zaidi ya kuchukua begi lake na kutoka nje.

Sasa Calian anafika kwenye gari ndipo anagundua Tabia amebakia ndani. Alikasirika! Alishusha pumzi kwa nguvu na kumgeukia Dereva wake

“yule mpuuzi kabaki ndani! Nenda kamfuate!”

Dereva alitoka mbio hadi chumbani kwa Tabia. Akamkuta bado amekaa kwenye kiti anashangaa.

“Dada, tuondoke”

“Sawa”

Tabia alisimama akachukua begi lake na kuongozana na yule Dereva mpaka nje alipokuwepo Calian.

Wote walipanda kwenye gari na safari ya kwenda airport ikaanza. Masuala ya gari sijui ndege yalikua mageni kwa Tabia! Alikua akishangaa tu mda wote kitendo kilichokua kina mkera Calian.

Alimvumilia Tabia mpaka walipotua salama ndani ya jiji la Dar-es-salaam, huko Sasa ndipo Calian alianza kumuwashia Tabia moto.

Baada ya kushuka aiport walikuta Dereva mwingine akiwa anawasubiri. Walipakia na kuelekea nyumbani. Walipokua wanakaribia kufika Calian ali amuru Dereva asimamishe gari. Lilipo simama alimgeukia Tabia na kumuambia

“shukaaaa”

“Tumefika???”

“Nimesema shuka..”

Tabia akabaki ameganda maana hakua akijua kufungua mlango! Huko kote walipotoka ni Dereva aliekua anamsaidia kufungua mlango.

“Husiki??”

“Siwezi….siwezi mimi… kufungua.. mlango” aliongea kwa aibu.

Calian akazidi kupandwa na hasira, yani mbali ya Tabia kua maskini pia alikua ni mshamba! Mshamba alie pitiliza.

Ikabidi Calian afungue mwenyewe ndipo Tabia akashuka na kusubiri maagizo.

“unajua mchaka mchaka?” Aliulizwa

“ndio!”

“Okay! Sisi tunatangulia then wewe unatufuata kwa mwendo wa mchaka mchaka! Ukizubaa tu tumekuacha, ukitembea tutakuacha vilevile! Tume elewana?”

“Ndio!”

“Ok Drive”

Dereva alitoa breki, akakanyaga mafuta mwendo ukaanza. Tabia akawa analifuata gari nyuma huku akikimbia! Na Calian akamfanyia makusudi zaidi kwa kumpitisha njia ndefu ili tu amkomoe. Alitaka kabla hata mwezi hujaisha Tabia atamke kwa mdomo wake kua hataki ndoa tena.

Wakati huo Tabia alikua anakimbia huku analia, jasho lilimjaa mwili mzima maana hakuwai kufanya mambo kama hayo hapo kabla. Alijipa moyo kwa kumkumbuka Baba yake aliebakia kijijini, akapata nguvu na kuendelea kuchanja mbuga.

Hadi wanafika getini Tabia alikua kachoka hafai, alijitupa chini kama mzigo huku akipumua kwa nguvu.
Je nini kitaendelea usikose Kupata muendelezo wake Kwa bonge Moja la ofaaaa full yaani mpaka mwisho kwa 1000 TU no ya malipo 0750411324 SUBIRA SEFU njoo na muamala wako uhudumiwe hatupoi hatuboi mambo ni ????????????????.

Za hivi punde ni za 🔥🔥🔥 | Sema Jambo
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork

Welcome gonga94 Continue reading the various stories available here. Click here. Are you an artist then create an account here Signup/Login


mjukuu rewards 100
 

SHEMU KAUTA SEHEMU YA 11

mjukuu rewards 100
 

UTAMU WA MABOSS????❤️15

mjukuu rewards 100
 

UTAMU WA FUNDI NGUO 05 ❤❤.

mjukuu rewards 100
 

SHEMU KAUTA SEHEMU YA 10 ‎

mjukuu rewards 100
 

JOTO LA MAPENZI Sehemu ya : 17

mjukuu rewards 100
 

JOTO LA MAPENZI 16

mjukuu rewards 100
 

JOTO LA MAPENZI 14 -- 15

mjukuu rewards 100
 

JOTO LA MAPENZI 13

mjukuu rewards 100
 

JOTO LA MAPENZI 11-- 12

mjukuu rewards 100
 

JOTO LA MAPENZI 9 -- 10

mjukuu rewards 100
 

JOTO LA MAPENZI 7 -- 8

mjukuu rewards 100
 

JOTO LA MAPENZI Sehemu ya : 6

mjukuu rewards 100
 

JOTO LA MAPENZI Sehemu ya : 5

mjukuu rewards 100
 

JOTO LA MAPENZI SEHEMU YA 1

mjukuu rewards 100
 

THE INFLUENCER Episode 2:

mjukuu rewards 100
 

SHEMEJI WEKAA.. Sehemu Ya 02

mjukuu rewards 100
 

UTAMU WA FUNDI NGUO 03

mjukuu rewards 100
 

Shemu Kautaka SEHEMU YA 09

mjukuu rewards 100
 

BINTI MKIMBIZI* SEHEMU YA...12

mjukuu rewards 100
 

BINTI MKIMBIZI* SEHEMU YA... 11

mjukuu rewards 100
 

BINTI MKIMBIZI* SEHEMU YA... 7

mjukuu rewards 100
 

BINTI MPELELEZI* SEHEMU YA... 6

mjukuu rewards 100
 

SHEMU KAUTAKA SEHEM -08

mjukuu rewards 100
 

SHEMU KAUTAKA SEHEMU 07

mjukuu rewards 100
 

Xabi Alonso tayari

mjukuu rewards 100
 

Rs Berkane imetwaa Ubingwa

mjukuu rewards 100
 

UTAMU WA FUNDI NGUO 01

mjukuu rewards 100
 

MWARABU HUKO MI SIJAZOEA 39

mjukuu rewards 100
 

MWARABU HUKO MI SIJAZOEA 38

mjukuu rewards 100
 

MWARABU HUKO MI SIJAZOEA 35

mjukuu rewards 100
 

MWARABU HUKO MI SIJAZOEA 34

mjukuu rewards 100
 

MWARABU HUKO MI SIJAZOEA 33

mjukuu rewards 100
 

MWARABU HUKO MI SIJAZOEA 27

mjukuu rewards 100
 

MWARABU HUKO MI SIJAZOEA 21--22

mjukuu rewards 100
 

MWARABU HUKO MI SIJAZOEA 14

mjukuu rewards 100
 

MWARABU HUKO MI SIJAZOEA 11

mjukuu rewards 100
 

MWARABU HUKO MI SIJAZOEA 7-- 8

mjukuu rewards 100
 

MWARABU HUKO MI SIJAZOEA 6

mjukuu rewards 100
 

MWARABU HUKO MI SIJAZOEA 4

mjukuu rewards 100
 

MWARABU HUKO MI SIJAZOEA 2

mjukuu rewards 100
 

MWARABU HUKO MI SIJAZOEA 1

mjukuu rewards 100
 

Fanya mambo yako kimya kimya.

mjukuu rewards 100
 

Cristiano Ronaldo, Cristiano Jr

mjukuu rewards 100
 

Visit South Africa

mjukuu rewards 100
 

MORICE MICHAEL ABRAHAM

mjukuu rewards 100
 

UTAMU WA MABOSS 14

mjukuu rewards 100
 

SHEMEJI WEKAA... Sehemu Ya 01

mjukuu rewards 100
 

CHUMBA CHA MPANGAJI 11---12

mjukuu rewards 100
 

SHEMU KAUTAKA SEHEMU -06

mjukuu rewards 100
 

MFANYAKAZI WETU SEHEMU YA 1

mjukuu rewards 100
 

CHUMBA CHA MPANGAJI 10

mjukuu rewards 100
 

SHEMU KAUTAKA SEHEMU -05

mjukuu rewards 100
 

?SHEMU KAUTAKA ?Sehemu-04

mjukuu rewards 100
 

UTAMU WA MABOSS???13

mjukuu rewards 100
 

UTAMUU WA MABOSS ??????12

mjukuu rewards 100
 

CHUMBA CHA MPANGAJI 8--9

mjukuu rewards 100
 

CHUMBA CHA MPANGAJI 6--7

mjukuu rewards 100
 

CHUMBA CHA MPANGAJI 3--4

mjukuu rewards 100
 

CHUMBA CHA MPANGAJI 1---2

mjukuu rewards 100
 

FUNDI CHEREHANI 02

mjukuu rewards 100
 

FUNDI CHEREHANI 01

mjukuu rewards 100
 

SHINDU LA KIHAYA Sehemu Ya 14

mjukuu rewards 100
 

SHINDU LA KIHAYA Sehemu Ya 13

mjukuu rewards 100
 

SHEMU KAUTAKA EPISODE 3

mjukuu rewards 100
 

SHEMEJI KAUTAKAN SEHEMUN-02

mjukuu rewards 100
 

SHINDU LA KIHAYA 09 AGE ????

mjukuu rewards 100
 

SHINDU LA KIHAYA Sehemu Ya 06

mjukuu rewards 100
 

SHINDU LA KIHAYA Sehemu Ya 05

mjukuu rewards 100
 

WATOTO MAPACHA sehemu ya 15

mjukuu rewards 100
 

SHINDU LA KIHAYA Sehemu ya 03

mjukuu rewards 100
 

SHINDU LA KIHAYA Sehemu Ya 02

mjukuu rewards 100
 

SHINDU LA KIHAYA Episode (1)

mjukuu rewards 100
 

CHAKULA CHA MUME

mjukuu rewards 100
 

WATOTO MAPACHA sehemu ya 14

mjukuu rewards 100
 

WATOTO MAPACHA, kipande Cha 13

mjukuu rewards 100
 

WATOTO MAPACHA SEHEMU YA 11

mjukuu rewards 100
 

WATOTO MAPACHA Sehemu ya 10

mjukuu rewards 100
 

SHEMEJI KAUTAKA Sehemu -01

mjukuu rewards 100
 

UTAMUU WA MABOSS ??????11

mjukuu rewards 100
 

UTAMUU WA MABOSS ??????9

mjukuu rewards 100
 

BALAA LA NYUMBA ZA KUPANGA--10

mjukuu rewards 100
 

CHAKA LANGU Episode 1

mjukuu rewards 100
 

Shangazi Kodogo tu ?EPISODE 5

mjukuu rewards 100
 

SHANGAZI KIDOGO TU EPISODE 4

mjukuu rewards 100
 

?SHANGAZI KIDOGO TU ?EPISODE 3.

mjukuu rewards 100
 

UTAMU WA MABOSS?????? 8

mjukuu rewards 100
 

UTAMU WA MABOSS??? 6~7

mjukuu rewards 100
 

UTAMU WA MABOSS?????? 5

mjukuu rewards 100
 

UTAMU WA MABOSS??? 4

mjukuu rewards 100
 

UTAMU WA MABOSS??????3

mjukuu rewards 100
 

UTAMU WA MABOSS??? SEHEMU YA 02

mjukuu rewards 100
 

?SHANGAZI KIDOGO TU ? EPISODE 2

mjukuu rewards 100
 

?SHANGAZI KIDOGO TU ?EPISODE 1

mjukuu rewards 100
 

WE KULA TU BINAMU EPISODE 11

mjukuu rewards 100
 

TAMU YA HOUSEGIRL SEHEMU YA 03

mjukuu rewards 100
 

TAMU YA HOUSEGIRL SEHEMU YA 02

mjukuu rewards 100
 

WATOTO MAPACHA Sehemu ya ,,7

mjukuu rewards 100
 

WE KULA TU BINAMU EPISODE 10

mjukuu rewards 100
 

WE KULA TU BINAMU EPISODE 9

mjukuu rewards 100
 

?WE KULA TU BINAMU ?EPISODE 8 ?

mjukuu rewards 100
 

WATOTO MAPACHA Sehemu ya ,,, 6

mjukuu rewards 100
 

WATOTO MAPACHA Sehemu ,,,,, 3

mjukuu rewards 100
 

WATOTO MAPACHA Sehemu ya """""1

mjukuu rewards 100
 

?WE KULA TU BINAMU ?EPISODE 7

mjukuu rewards 100
 

?WE KULA TU BINAMU ?EPISODE 6

mjukuu rewards 100
 

WE KULA TU BINAMU EPISODE 5

mjukuu rewards 100
 

WE KULA TU BINAMU EPISODE 4

mjukuu rewards 100
 

WE KULA TU BINAMU EPISODE 3

mjukuu rewards 100
 

WE KULA TU BINAMU EPISODE 2

mjukuu rewards 100
 

We Kula Tu Binamu Sehemu 1

mjukuu rewards 100
 

NASEMA KWA MAMA 38,39,40 *38*

mjukuu rewards 100
 

TAMU YA HOUSEGIRL SEHEMU YA 01

mjukuu rewards 100
 

SHANGA TISA EP: 20

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest