Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  artist

MELANIA (najutia kukupoteza) MTUNZI HURU MEDIA PAGE Bahari ya simulizi SEHEMU YA: 01 na 2.

1st Jun, 2025 Views 10

MELANIA (najutia kukupoteza)
MTUNZI HURU MEDIA
PAGE Bahari ya simulizi
SEHEMU YA: 01 na 2.

ANZA NAYO…..
????????????????????????????????
Yooooh WhatsApp, KENZO hapa Mtoto wa Tajiri mkubwa sana hapa jijini dar es salaam, Kijana ambaye nikiingia sehemu yoyote ile lazima wanawake wapapatike kutokana na muonekano lakini pia na kumwaga pesa.

Nyumbani kwetu tumezaliwa watoto wawili tu Yaani Mimi na dada yangu, halafu Mimi ndio last born.

Kiukweli mzee wetu ni mtu Mwenye upendo sana, Mara nyingi uwa nasema kuwa upendo na misaada anayotoa baba yangu ndio inamfanya anafanikiwa kila hiitwapo Leo.

Mimi ni msomi Bwana na sijawai kusoma hizi shule za kula ugali maharage Wala makande.

Baba yangu alihakikisha Kuwa sisi watoto wake tunAsoma shule nzuri na tunaishi maisha mazuri ambayo yeye anataka sisi tuishi.

Ukiachana na maisha mazuri, wazazi wetu walihakikisha Kuwa sisi watoto wao tunaishi kwenye maisha Fulani hivi ya huruma, kujiheshimu, kujipenda lakini pia na kuwapenda wengine.

Akili Mbiu ya baba yangu Nyumbani ilikuwa ni kulinda reputation ya familia, Yaani baba yangu na ujinga ni vitu viwili tofauti.

Kenzo Mimi Bwana Naomba nikubali Kuwa familia yangu hainifahamu, Yaani hainijui kabisa, Yaani Kenzo wanayemjua wao na huyu Kenzo ambaye naishi ni vitu 9 tofauti.

Nyumbani kwetu Mimi nilikuwa ni Kama malaika wa nidhamu vile lakini ukija uku kwenye pande zangu weeeeeh ???????? utajua ujui.

Niliishia maisha yangu kwa kuhakikisha Kuwa familia yangu haitambua mambo ya hovyo ninayoyafanya nje ya Nyumbani.

Hapa nyumbani kwetu Bwana, kuna aka kasichana Kanaitwa MELANIA. Melania nimemfahamu tangu sote tukiwa darasa la 7 kwani ndio kipindi ambacho MELANIA na mama yake waliamia pale Nyumbani.

Mama mzazi wa MELANIA alikuwa ni house girl wetu, na kwakuwa hakuwa na sehemu ya kukaa baada ya mume wake kufariki, baba akaamua kumpatia mama MELANIA Nyumba yetu ndogo ya nje ili awezi kukaa na Binti yake.

Maisha yalisonga uku mama akiwafanya MELANIA na mama yake Kuwa ni sehemu ya familia yetu.

Tulipofika kidato cha nne tuliweza kufanya mtihani yetu na kwa Bahati mbaya MELANIA hakuweza kufaulu na hii ilimpa huzuni snaa mama yake ambaye alikuwa akiitaji Mtoto wake Kuwa msomi Sanaa.

Baba yangu alimpa Melania chance ya kumsomesha lakini MELANIA akakata kwa kusema.

“Kiukweli mimi siwezi kurudi shuleni kwa sasa, sababu kuu ni kuogopa kuwapotezea muda lakini pia kupoteza pesa zenu , Kiukweli sikuwai kuelewa uko darasani”

“Unapendelea kujifunza nini ??”

Baba alimuuliza Melania.

“Napenda sana mambo ya urembo, Yaani ususi na make up”

hapo baba yangu alibabe majukumu na kumsomesha MELANIA kwenye chuo kikubwa sana cha urembo na ususi hapa jijini.

Miaka ilikimbia na baada ya miaka mwili Mimi nikiwa naanza chuo mwaka wangu wa kwanza, Melania alikuwa ameshamaliza elimu yake ya urembo na alikuwa yupo Nyumbani akisubilia baba amfungulie saloon.

Ndani ya mwaka huo huo mama MELANIA aliweza kupoteza maisha na kumuacha MELANIA akiwa yatima.

Baba yangu hakutaka kabisa kumuacha Melania na akamchukua kabisa na kumfanya ni familia Rasmi na sio Mtoto wa KIJAKAZI Kama ilivyokuwa mwanzo.

********

Ouk jamani tuachane na yaliyopita na tuendelee uku mbele.

KWa sasa mimi bado ni Mwanafunzi wa chuo na Nipo nachukua masters.

KWa upande wa Melania ni tayali Ana saloon yake mjini na tayali anajulikana kiasi na anapiga pesa kwa Namna moja au nyingine.

Kitu ambacho kipo kwangu ni kwamba sijawai kumpenda huyu Binti ata kidogo, Maombi yangu ya kila siku ni kwamba huyu Binti aondoke Nyumbani kwetu tu na akaishi mbali.

Ukiniuliza sababu ya kumchukua MELANIA ni kWa sababu tu sio ndugu yetu lakini pia ni Mtoto wa kijakazi na nilikuwa naona Kama anatumia tu pesa za familia yangu ikiwa hausiki.

KWa upande wa dada yangu ambaye alijulikana Kama Diana, yeye alikuwa tayali ni mfanyakazi kwenye kampuni ya baba yetu, lakini pia Diana alikuwa akimpenda sana MELANIA.

Chuki yangu kWa Mela nilifanya kWa Siri sana Tena sana ata hakuna mtu alikuwa anaweza kujua.

Ikiwa ni siku ya kazi kaama kawaida, wazazi na dada Diana wote walienda kwenye majukumu na Nyumbani tulibaki Mimi, mela na Mdada wa kazi tu.

Siku hiyo mela hakuwa ameenda kazini kwake kwani alidai Kuwa anaumwa tumbo.

Baada ya kuona Kuwa Nyumbani tupo wenyewe, Nilizunguka nyuma ya Nyumba na kwenda kwenye Nyumba ambayo alikuwa akikaa mela.

Nilifika na pasi na kupiga hodi niliingua na kumkuta akiwa amejilaza kitandani uku akiangalia mambo yake ya urembo kwenye mtandao.

“Kenzo, mbona ili suala la wewe kuingia chumbani kwangu pasi na kupiga hodi unaona ni la kawaida sana ??”

Mela aliniuliza.

“Kwamba ? Yaani kwenye Nyumba ya baba yangu pia unataka Nipige hodi, halafu ni Kama unajisahaulisha Kuwa Mimi ni Nani kwenye huu mjengo si ndio ??”

Nilimuuliza uku nikibinua sura yake kwa kutumia kidevu chake.

“Aaah unaniumiza Bwana “

Mela alinifokea.

Kitendo cha mela kunifokea kilinikela sana na kujikuta nikimchapa kibao Kimoja cha mashavu hapo mela Akatulia na kuniangalia tu.

“Usije ukatumia huu mdomo wako kunipandishia sauti ata siku moja nitakuja nikichakaze sura yako hiyo”

Nilimwambia.

Muda huo huo Niliinuka na kuvua t-shirt yangu na kutupia pembeni mela akazungumza.

“Siko vizuri Leo “

“Hauko vizuri ukiwa Unamaanisha nini ? Ebu jiandae hapo nipige show zangu niende chuo”

Kitu ambacho amkijui ni kwamba, uwa namtumia mela kimwili muda wowote na Saa yoyote ile ninayoitaka mimi.

Mchezo huu umeanza tangu pale tu mama yake alivyofariki, kwani ndio muda ambao mela alianza kuishi Mwenyewe kwenye hii Nyumba yetu ya nyuma.

Sikuwai kujali chochote kuhusu yeye, sikujali Kuwa yuko period au laaah nilichojali ni Mimi kupata mambo yangu.

Kabla hatujaanza chochote kile, simu yangu iliita na Demu wangu ninayempenda sana ndio alikuwa akipiga haraka nikapokea.

“Yes babe….”

“Babe nimewai chuoni kwaajili yako lakini cha ajabu ni kwamba Ujafika mpaka muda huu”

Alizungumza mpenzi wangu na sauti yake ya kudeka.

“Niko njiani Babe, soon nafika kuna jam kidogo”

Nilimaliza kuzungumza na my wangu kisha nikamgeukia mela na kumwambia.

“Jiandae kwaajili ya usiku, hakikisha Kuwa haufungi mlango “

“Sawa “

Alijibu mela.

Naweza nikasema Kuwa hiyo ndio ilikuwa pona ya mela kwa wakati huo lakini isingekuwa simu Basi ningekuwa Napiga vyangu tu.

ITAENDELEA…
MELANIA (najutia kukupoteza)
MTUNZI: UHURU MEDIA
WHATSAPP 0755090082
SEHEMU YA: 02

SONGA NAYO……
????????????????????????????????

Niliingia chumbani kwangu chap nikajiandaa na kuondoka zangu chuoni, nilifika na kukuta mpenzi wangu akiwa ameniletea chakula kutoka nyumbaani kwao.

Sawa Kenzo Mimi Nina wapenzi wengi lakini huyu msichana ambaye anajulikana kama Rachel nampenda kuliko kitu chochote, Yaani ndio msichana ambaye ata akiniita saa 8 za usiku nitaamka na kwenda kumuona.

Majila ya Jioni nilishika njia na kurudi nyumbaani, nilifika Nyumbani kWa kuchelewa sana kutokana na foleni kubwa sana.

Nilifika na kukuta familia nzima ikiwa mezani ikipata chakula lakini Mela hakuwepo.

“Umewai Bwana anzia mezani Kijana wangu “

Baba aliniambia baada ya kuniona, kWa utulivu nikasogea na kuuliza.

“Melania yuko wapi jamani ??”

Kila mtu akanigeukia na kuniangalia kisha wakacheka na kusema.

“Yaani wewe na Mela, Yaani yeye pia alivyokuja kuchukua chakula alikuulizia “

Nilitabasamu tu na kujibu.

“Kwahiyo ameenda kula chumbani kwake au ? Kwani anaumwa sana ??”

Niliuliza nikionesha wasiwasi mkubwa sana juu yaMela.

“Ameitaji utulivu tu, lakini pia muache anaonekana Kuwa hayuko Sawa “

“Sawa “

Nilijibu kWa unyonge na kukaa kwenye meza ya chakula na kuendelea kupata chakula.

Nilikula uku nikiangalia kiti cha mela, Yaani Mimi kwa ndugu na wazazi wangu nilionesha kumjali sana mela, Yaani nilionesha kila aina ya upendo ambapo haikuwa rahisi wao kugundua Kuwa kuna mambo mabaya namfanyia mela.

“Halafu kesho ni siku yake ya kuzaliwa mjue “

Niliwaambia.

Hapo kila mtu ndio alikumbuka ni wazi Kuwa walikuwa wameshasahau.

“I want to make her happy so nitamfanyia surprise ya family party, nitafurahi Kama mtaungana na Mimi katika kumpatia mela Furaha “

Nilizungumza utazani Namaanisha vile kumbe Nina langu moyoni.

Baada ya kumaliza kula kila mtu akaingia chumbani kwake na Mimi nikaingia chumbani kwangu.

Nikachukua simu yangu na kumpigia simu mela lakini hakipokea ata simu yangu moja, Nilimchukia sana Walahi.

Kitu ambacho amkijui ni kwamba, Mimi sijawai kuchati na Mela, mara zote uwa nampigia tu. wasiwasi wangu ni kwamba kuna siku mela anaweza akatumia chatting Kuwaonesha wazazi ukweli wa mambo yote.

Sikukoma kumpigia simu nilipiga simu zaidi ya Mara 10 lakini hakupokea kabisa.

Muda huo huo dada Yangu Diana akaingia chumbani.

“Mbona kama hauko sawa. ??”

Dada yangu aliniuliza.

“Aaah, niko Sawa “

“Mmmh unasemaje uko Sawa na Nakuona kabisa Kuwa hauko Sawa, nambie kaka Angu handsome shida ni nini “

Alizungumza dada yangu uku akinishika kwenye bega.

“Melania Apokei simu zangu ????”

Nilizungumza uku nikitamani kulia.

Kuhusu kulia Bwana nilikuwa natamani kulia kweli ???????? Yaani muda huo upwiru ulikuwa umekaba koo halafu wa kunisaidia ndio Apokei simu.

“Ahaaha, khaaah Mdogo wangu punguza sasa jamani, Yaani unampenda mela mpaka unashindwa kujizuia, Mela amekupa nini ??”’

“Kunipa nini ukiwa Unamaanisha nini ??”

Nilijibu uku nikifuta mchozi ambao tayali umeshanidondoka.

“Na unalia jamani, eeeh ngoja nimpigie mimi “

KWa upande wa dada yangu aliamini Kuwa Mimi nampenda Mela kimapenzi na alifanya kila juhudi kuhakikisha Kuwa mela anakuwa WiFi yake wa halali.

Dada Diana alimpigia simu mela na hakuchukua muda akapokea.

“Mela umelala ??”

Diana alimuuliza mela.

“Hapana sijalala kuna shida “”

Mela aliuliza.

“Shida ipo Tena kubwa sana, kaka yangu anakupigia simu upokei mpaka analia uku “

Alizungumza dada yangu na kuangua kicheko cha hali ya juu akinicheka mimi ????????.

“Nilikuwa nikisali ndio maana sikuweza kupokea, Mwambie niko Sawa Ila kWa sasa nalala tutaonana kesho”

“Aaaah jamani Ebu ongea nae apate amani kaka yangu “

Basi hapo nilichukua simu na kuongea na Mela, Tulizungumza kwa Furaha Sanaa na mwisho tukaagana na dada yangu akarudi chumbani kwake.

********

Siku ziliendelea kwenda uku nikizidi kumtesa mela pasi na kujali maumivu yake.

KWa upande wa mela Bwana alinipenda kindaki Ndaki, Yaani ukiachana na visa vyote ninavyomfanyia mela lakini yeye ni ananipenda kuliko kawaida, ananipenda mpaka ajielewi huyu msichana.

Ikiwa ni siku ya weekend, na ni siku ambayo nilikuwa na birthday party ya Rafiki yangu, niliweza kuwaaga wazazi na kweli wakanipatia ruhusa lakini baba akazungumza.

“Umchukue na Mela uwende nae kidogo akapate kuinjoy “

Aaaah Walahi nilichukia sana, Yaani ni siku yangu ya kuinjoy halafu naanza kuambiwa nibebe watu niende nao, bora ata angekuwa mtu mwingine lakini mi huyu Binti ambaye simpendi ata kidogo.

“Hapana baba me sitaenda kokote “

Mela Alijibu kwani pia na yenye alikuwepo kWa Wakati huo.

“Mela Binti yangu, wewe umekuwa ukijifungia tu Ndani kwako, Yaani wewe maisha yako ni saloon Nyumbani, Nyumbani saloon, aaaah Mara moja moja uwe unatengeneza marafiki wapya sio Kila siku unakwama na huyu Kenzo ooooh ???????? utakosa wachumba wa maana”

Alizuungumza mama yangu na akaingizia utani wake.

Katika watu ambao wanatamani mimi nimuoe mela Leo kesho ni mama yangu na dada yangu Diana.

Yaani umu Ndani kwetu mela anaonekana Kama mailaaika hivi, kiufupi mela anapendwa sana kutokana na tabia zake njema.

Mela alijitaidi sana kukataa lakini mwisho wa siku alishindwa na safari ikawa ni Mimi na mela.

“Hakikisha unamlinda mwenzio na mnarudi wote”

Alizungumza mama wakati huo Mimi na Mela ndio tulikuwa tunaondoka.

Walahi mela alipendeza sana Tena sana, kWa jinsi ambavyo mela alipendeza ata Mimi sikuacha kum tazama na mwisho nikamwambia.

“Umependeza sana Leo “

Mela alifurahi sana akakatabasamu na kubaki akiminyaminya vidole vyake, hii feeling anayoipata mela kwa wakati huo wanaweza kuelewa watu ambao wame fall in love tu, kama ambavyo mela ananipenda Mimi.

Hatimaye tulifika eneo husika, lakini kabla hatujashuka kwenye gari, nilishangaa sana kuona alama ambayo ilikaa kama moja chini ya bega la mela, kWa shauku nikagusa na kumuuliza.

“Ni nini hii??”

“Sio kitu”

Mela Alijibu na kutaka kushuka lakini nilimvuta na kukishika kWa nguvu na Mela akaonesha kuumia.

“NI nini hii “

Nilimuuliza kWa hasira sana, akili yangu iliwaza labda ni mambo ya uchawi maana huyu Binti simuamini ata kidogo.

“Ni njia ya kuzuia kupata mimba Inaitwa kijiti”

Alijibu mela kWa hasira uku akiangalia pembeni .

“Kumbe ndio maana, unajua kila siku najiuliza au Ninashida siwezi kuzalisha kumbe wewe umeweka huu ujinga wako hapa “

“Ujinga gani sasa ? Kujilinda ndio ujinga ? Kenzo wewe ujawai kujali siku za hatari Wala siku zozote zile Itakuwaje nikishika mimba Mimi ????”

Alijibu uku akitaka kulia.

“Hayo machozi yako siyataki kabisa, iko hivi kesho nisikione mwilini mwako”

“Lak….”
Kabla hajamaliza kuzungumza nikafungua mlango wa gari na kushuka .

JE MELA ATATOA KIJITI ? NA VIPI KAMA ASIPOTOA KENZO ATAMFANYA NINI ?

SIMULIZI HI IPO MPK MWISHO KABISA UTAPATA KWA 1000 TU

NAMBA YA MALIPO 0755090082 MPESA JINA LA USAJILI ZAINABU SUNGITA

UKISHALIPIA NJO WHATSAPP 0755090082.
   

SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MY HEART 03--04

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

*MY HEART* *1---2 *

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MIMBA YA BESTMAN 7

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

ANIPHA 6--7.

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MIMBA YA BESTMAN 05

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

side chick episode 3

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

SIDE CHICK EPisode 2

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 18

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 17

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 16

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 8

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 1

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

RATIFA Sehemu ya 32

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

JINA LANGU SHAMSA EP3

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

JINA LANGU SHAMSA EP2

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

JINA LANGU SHAMSA EP1

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

BOYCHILD PART 3

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

DRAMA OF LOVE part 4.

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

DRAMA OF LOVE part 3

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

NJERI part 29

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

LOVE Part 1

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

NJERI part 28

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

NAWASHWAA Sehemu nne.

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

NJERI part 26

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest