Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  artist

JINA LANGU SHAMSA SEHEMU YA KWANZA

2nd Jun, 2025 Views 2

JINA LANGU SHAMSA SEHEMU YA KWANZA
“Kaka eeh, mi nasema ukweli. Yule binti ambaye hupita kila jioni saa kumi na moja... bwana wee... huyo si binadamu wa kawaida,” alisema Festo akimeza mate.

"Unamzungumzia yule mwenye nguo kuvaa nguo za kupendeza hupita kila jioni, yule mwenye miwani ya kisanii?” aliuliza Twaha huku akishika kinywaji baridi alichokinunua kwa mkopo.

“Huyo huyo!” walijibu wote kwa sauti moja kama wanafunzi wa darasa la tatu.

Festo, ambaye hakuwa na kazi yoyote rasmi isipokuwa kuhesabu magari ya kifahari yanayopita barabarani, alikuna kidevu chake kilichojaa ndevu.

“Mie nilidhani ni msanii wa Bongo Movie. Au labda ni mtoto wa balozi.”

“Sasa shida ni jina lake"
"Tuna miaka miwili tunamuona, lakini hakuna anayejua jina lake. Kila mtu anamuita jina tofauti. Mwingine anamuita Vanessa, mwingine Princess.

Walikuwa ni madereva wa bodaboda Tandale, jijini Dar es Salaam. Maisha yao yalizunguka kwenye mbio za kila siku kupata hela ya chakula, mafuta, na kodi. Kijiwe chao kilikuwa pembezoni mwa barabara kuu, mahali pa stori.

"Kaka eeh, kesho ni siku yangu. Nitamtongoza yule mrembo, hata kama ananiangalia kama bodaboda tu. Mimi sioni sababu ya kuchelewa tena.
Maisha ni haya, tukikosa nafasi, ni nani atapata?”

"We subiri kesho apite"
"Nitamtongoza tu" Festo aliongea huku akitabasamu kwa kwa bashasha.

"Kesho uje sasa umependeza, umeoga, na umevaa vizuri. Kama utaonekana msafi atakupa nafasi, la sivyo atakukataa kabisa,” Twaha aliongeza huku akicheka.

“Kazi yenyewe ya bodaboda hiyo... sidhani kama atakukubali,” aliongeza tena kwa sauti ya kejeli, na kijiwe kikacheka kidogo.

********
Saa nne usiku, Festo alipofika nyumbani kwake, alifungua mlango wa chumba chake cha kupanga kilichojaa harufu ya jasho na mafuta ya pikipiki. Hakuwa na mke wala watoto.
Kulikuwa na kitanda, godoro lililoisha na begi la nguo lenye sura ya kuchoka.

Aliweka pikipiki yake pembeni, akavuta pumzi ndefu kisha akalalia kitanda bila hata ya kubadili nguo. Lakini akili haikumpa amani.
Taswira ya msichana yule ilimjia tena na tena. Macho yake yakimkumbuka ipasavyo kabisa.

Akamwaga begi lake na kuchagua suti ya buluu, suti pekee ambayo huwa anaivaa kwa mitoko maalumu.
Japo Ilikuwa imepinda na kufifia rangi, lakini kwake ilikuwa ni silaha ya mwisho.

“Kesho ni siku yangu. Nitavaa hii. Nikienda kurusha swaga kwa yule mrembo… lazima anikubalie,” alisema kwa matumaini.

Msichana huyo alikuwa ni mrembo wa ajabu, na kila jioni alipita kwenye kijiwe chao cha bodaboda, akivutia macho ya kila mtu .
Alitembea kwa mguu, nguo zake za kupendeza zilimfanya aonekane tofauti kabisa na mwendo wake.

Hakuna aliyefahamu msichana huyo aliishi wapi,
Wala hakukuwa na mtu aliyemjua vizuri,
Wanaume wengi walikuwa wakijaribu kupiga mbizi
wakijitahidi kupanga namna ya kumkaribia, lakini haikuwa rahisi.

Akamwaga begi lake na kuchagua suti ya buluu suti ambayo ndiyo huwa anaivaa kŵenda kwenge mitoko. Ilikuwa imepinda na kufifia rangi, lakini kwake ilikuwa ni silaha ya mwisho.

“Kesho ni siku yangu. Nitavaa hii. Nikienda kurusha swaga kwa yule mrembo… lazima anikubalie,” alisema kwa matumaini.

Asubuhi Festo alijitahidi kuoga vizuri kwa maji akapaka losheni ya kunukia, akavaa suti yake ya buluu na kuikamilisha kwa viatu vya ngozi alivyovipiga kwa kiwi nyeusi.

Alipotua kijiweni, kijiwe kilizizima.
“Festo, umependeza. Jioni ikifika, usiogope. Hii ndiyo fursa."

*********
Msichana huyo ambaye hakujulikana jina, alikuwa mzuri hatari.
Alikuwa na uzuri ambao ulipelekea wanaume wenye ndoa kusahau wake zao, na vijana kuacha kucheza kamari kwa dakika moja.

Jioni ilipofika, hewa ya Tandale ilikuwa imepoa, jua likielekea magharibi huku Kijiwe cha bodaboda pakiwa kimya, kila mmoja akiwa makini kufuatilia dakika ambayo msichana yule angepita.

Na kweli, kama ilivyokuwa desturi yake, aliweza kutokea. Mavazi yake yalikuwa ya kuvutia, gauni la mpira , pamoja na miwani ile ile ya kisanii.
Alitembea kwa hatua za uhakika, bila haraka wala wasiwasi, miguu yake ikitua chini.

"Dada samahani, naomba niongee na wewe kidogo,” Festo alisema kwa sauti ya heshima huku akijihisi kutetemeka

Lakini msichana huyo hakujibu. Hakuinua hata uso kumwangalia. Aliendelea kutembea, hatua zake zikiwa tulivu kama vile hakuwa na masikio,

Festo alisimama, akamwangalia kwa mshangao,
"Dada...?”
"Mimi nakupenda, nijue hata jina lako"

Festo alijaribu tena kwa sauti ya chini zaidi. Lakini bado msichana yule hakugeuka, hakuongea. Alitokomea mbele tu, taratibu, hadi akapotelea kwenye mbali.

Festo alibaki amesimama, suti yake ikianza kupoteza maana mbele ya ukimya ule mzito. Moyo wake ulikuwa bado ukidunda, akimuona msichana huyo kwa mbali akipotelea.

Kaka... labda msichana huyu sio wa dunia hii. Au labda... anasubiri mtu wa aina nyingine kabisa.” Twaha aliongea huku akimsogelea Festo.

Mwanamke huyu alionekana hapendi masihara. Kila alipopita, hakuwa na tabasamu, hakuwa na ishara ya kuchangamkia yeyote. Macho yake yalikuwa mbele tu.

Huyu binti ana siri gani? Anaishi wapi? Anaenda wapi kila jioni saa moja kamili? Na kwa nini kamwe haongei?”

Ilikuwa ni jambo la ajabu. Kila mtu alikuwa ameshajaribu kumpungia mkono, kumpa salamu, au hata kumchekea. Lakini hakuwa akijibu. Hakuwa hata akiashiria kuwa amewaona.

Saa nne usiku, Festo alirudi kwake huku akiwa kavunjika moyo. Suti aliyovaa, ile ya buluu aliyoiamini kama silaha ya mwisho, haikumsaidia kitu. Alihisi fedheha, akijilaumu kimoyomoyo, akitembea taratibu huku machozi yakimlengalenga lakini yakikataa kutoka.

Alipofungua mlango wa chumba chake cha kupanga, harufu ya jasho, mafuta ya pikipiki na ukimya mzito vilimkaribisha kama marafiki wa zamani. Aliketi kwenye kitanda chake, akivua viatu vyake polepole kana kwamba vinamchoma.

Alitazama suti yake, kisha akaiweka juu ya begi lake la nguo, ambalo lilionekana kuchoka zaidi yake.

Aliishi maisha magumu hakukuwa na runinga, hakuna feni, wala jokofu. Chakula kilikuwa majaliwa. Kazi yake ilikuwa ni bodaboda kushinda kijiweni mpaka usiku ndipo audio kupumzika.

"Yule msichana ni nani hasa? Na kwa nini moyo wangu hauwezi kuacha kumfikiria" Festo aliwaza huku akikumbuka taswira ya yule msichana.

Kila jioni, bila kukosa, Festo humuona msichana huyo akipita kijiweni kwao pale Tandale. Saa kumi na moja kamili, , anajitokeza barabarani akiwa amependeza kupita maelezo gauni zuri, viatu vya kisasa na ile miwani ya kisanii.

Festo na watu wengine walimsalimia mara nyingi, lakini msichana huyo hakuwa akijibu. Hakutikisa kichwa, hakugeuza shingo, wala hakuonyesha dalili ya kusikia.
Hali hiyo iliwafanya wengi waanze kuzungumza chinichini,
Huenda mwanamke huyo alikuwa ni Bubu.

"Kesho akipita, nitajaribu kumshawishi"
"Aniambie anaishi wapi. hata jina lake nijue" Festo alijiongelesha kisha akaweza kupitiwa usingizi.

*****
Asubuhi ilipofika, Festo aliamka mapema kuliko kawaida. Alijipangusa maji baridi kwa haraka, akavaa tisheti simba. kisha akachukua pikipiki yake na kuelekea kijiweni.
Alikuwa bado na maumivu moyoni, lakini hakuwa tayari kukata tamaa.

Alipofika kazini, marafiki zake walimtania kidogo juu ya suti ya jana lakini alicheka nao, akijaribu kuficha kilichokuwa ndani yake.

Ilipofika jioni, kama saa kumi na moja kasorobo, Na hapo akatokea tena. Msichana yule.

Alikuwa na gauni la kijivu lililokaa vizuri mwilini mwake, miwani ile ile ya kisanii, na begi dogo. Hatua zake zilikuwa za kawaida huku madereva bodaboda waliyokuwa wakipiga stori wote wakinyamaza.

"Dada samahani " Festo alimuita huyo mwanamke.
Tafadhali… naomba dakika moja tu. Jina lako tu. Unaitwa nani?”
Msichana hakusimamisha mwendo. Hakutazama pembeni. Macho yake yalikuwa mbele tu kana kwamba hakuwa amesikia chochote.

JE NINI KITAENDELEA?

HAKUNA KUCOPY WALA KUSHARE
HAKI ZOTE ZIMEHIFADHIWA....
   

SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


mjukuu rewards 100 Comments 0
 

PART 5 MY HEART

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MY HEART 03--04

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

*MY HEART* *1---2 *

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MIMBA YA BESTMAN 7

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

ANIPHA 6--7.

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MIMBA YA BESTMAN 05

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

side chick episode 3

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

SIDE CHICK EPisode 2

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 18

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 17

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 16

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 8

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 1

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

RATIFA Sehemu ya 32

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

JINA LANGU SHAMSA EP3

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

JINA LANGU SHAMSA EP2

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

JINA LANGU SHAMSA EP1

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

BOYCHILD PART 3

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

DRAMA OF LOVE part 4.

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

DRAMA OF LOVE part 3

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

NJERI part 29

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

LOVE Part 1

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

NJERI part 28

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

NAWASHWAA Sehemu nne.

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

NJERI part 26

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest