Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  artist

PART 5 MY HEART

4th Jun, 2025 Views 9

05*
MY HEART
Nilifika ghetoni kwa Jabir, nilijizuia kuingia baada ya kukutana na bonge la Muziki, kama mnavyojua nyumba za Wanafunzi ni full vurugu tu.
Inaonekana yeye na Washkaji zake walikuwa na party.

Sikutaka kuwa kikwazo kwao, sauti za Wadada wakipiga kelele zilipenya masikioni mwangu na kwa namna fulani hivi nilijikuta ni kisikia wivu.

Niliondoka kwa kutembea, sikutaka kusumbuana na dreva wa bajaji wala pikipiki.

"Kwanini Jabir hajawahi kunitambulisha kwa rafiki yake hata Mmoja? kwanini asinialike kwenye party? kwanini hajawahi kuniuliza kuhusu changamoto nazokutana nazo kazini?" Nilijikuta nikijiuliza maswali mengi bila majibu

"Kuanzia sasa na kuendelea sitamfuatilia Jabir, sitaenda kwake bila mualiko.... nitaendelea kuhudumia tumbo lake, nitalipa kodi na ada bila kulalamika. Pindi atakapomaliza Chuo nitaharakisha ndoa kati yetu, anaweza kuwa na wanawake wengi kwa sasa lakini naamini Mimi ndio chaguo lake sahihi" Nilijitia nguvu kisha ni kaenda nyumbani

Siku zilizidi kwenda nikiwa nimedumu katika msimamo wangu wa kutomfuatilia Jabir wala kwenda kwake bila mualiko. Kuna muda alinihitaji lakini niligoma si kwa sababu sikuwa nimemkumbuka, nilitaka kutafuta pesa kwa ajili yake kwa sababu alibakiza siku chache tu amalize chuo.

Sikuwa na mawasiliano na Ali, nafikiri alienda Nje tena. Pengine huko ndiko kuna mke na watoto wake.....kwa miaka yake ile aliyonitajia si rahisi kukosa familia.

Hatimaye Jabir wangu alimaliza Chuo, nilishusha pumzi kana kwamba nimetua mzigo mzito uliokuwa kichwani mwangu.

Siku ya mahafali yake alinialika, nilimtumia Milioni mbili kwa ajili ya kukodi ukumbi kabisa. Sikuona hasara kulipa watu wapike chakula....siku ya leo nilipendeza sana.
Moyo wangu uliniambia ni lazima nitatangazwa kama mkewe mtarajiwa hivyo ilikuwa ni muhimu kwangu kupendeza.

Niliwaalika wazazi wangu pia pamoja na majirani, japo Mhitimu alikuwa ni Jabir lakini kwa namna nilivyokuwa kipaumbele kwa kila kitu unaweza kusema Mimi ndiye Mhitimu.

Wazazi wa Jabir walipendeza pia.... sijui kama nitakuja kutumia pesa kama siku ya leo. Pesa zilinitoka ndugu zangu kiasi kwamba niliishiwa.

Jabir aliwaalika marafiki zake pia wa kike na wa kiume....kwa namna ukumbi ulivyokuwa umenoga isingekuwa rahisi kwa watu kushindwa kusema Jabir ni Mtoto wa kishua.

"Nawashukuru wazazi wangu kwa kunipambania toka elimu ya msingi mpaka Chuo kikuu" Jabir alianza kuongea

Sikuumia kuwatangaza wazazi wake kama Mashujaa kutoka shule ya msingi mpaka Chuo. Ingekuwa ni aibu kubwa watu kujua Mimi pia nilihusika kumsomesha, hivyo hii haikuniumiza.

"Namshuru pia Mpenzi wangu Laura kwa kuwa sehemu ya ufadhili katika swala zima la ada" Jabir aliongea

Sikushtuka pia, huenda jina la Sadie hakulipenda na hata ameamua kunibatiza jina la Laura. Mara nyingi Mwanamke hana dini wala kabila hivyo niliona it's okay kuitwa Laura siku ya leo.

"Laura naomba usimame, siyo kusimama tu naomba upite mbele, nahitaji kila mtu akuone.... Mwanaume pia analipiwa ada" Jabir aliongea

Nilisimama nikiwa naona aibu kusemwa na wazazi wangu kwa kumsomesha Mwanaume.
Nilistaajabu ya Mussa baada ya kumuona binti mrembo akipiga hatua kwenda mbele....

Minong'ono mikubwa iliibuka, nikiwa nimesimama nilimshuhudia Jabir akimvika pete Laura.

Sikuwa na ujasiri wa kushuhudia kifuatacho, niliondoka kwa kukimbia huku nikiwahurumia wazazi wangu kwa fedheha niliyo waachia ukumbini.

Kifo cha baharini kilinifaa kwa wakati huu na siyo kitu chochote.
Niliingia baharini nikiwa mwenye maumivu makubwa.

Nilizikumbuka juhudi zote nilizofanya kwa Jabir....nilikumbuka kwa ukaribu namna nilivyo chinja Jogoo wa Baba aliyekula chumvi nyingi....Sadie Mimi sistahili kuishi tena.
Nilifumba macho yangu kusikilizia kifo....lakini ghafla nilihisi kuna mtu ananivuta

Itaendelea

Full 1000
Whatsp
0784468229.
   

SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


mjukuu rewards 100 Comments 0
 

YAMENIKUTA

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MIMBA YA BESTMAN 9

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

JINSI YA KUTUNZA UKE

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

PART 5 MY HEART

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MY HEART 03--04

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

*MY HEART* *1---2 *

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MIMBA YA BESTMAN 7

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

ANIPHA 6--7.

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MIMBA YA BESTMAN 05

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

side chick episode 3

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

SIDE CHICK EPisode 2

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 18

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 17

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 16

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 8

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 1

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

RATIFA Sehemu ya 32

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

JINA LANGU SHAMSA EP3

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

JINA LANGU SHAMSA EP2

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

JINA LANGU SHAMSA EP1

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

BOYCHILD PART 3

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

DRAMA OF LOVE part 4.

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

DRAMA OF LOVE part 3

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

NJERI part 29

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

LOVE Part 1

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest