Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  artist

PART 1; CHOZI LA BINTI MASIKINI Mtunzi: Lipeta S Shaaban

5th Jun, 2025 Views 4

PART 1; CHOZI LA BINTI MASIKINI
Mtunzi: Lipeta S Shaaban

Asubuhi

Katikati ya jiji la waswahili wanapoishi waswahili, wao wanapaita uswahilini. Kelele za ndege aina ya kunguru zinasikika. Giza lilikuwa linatokomea taratibu na mwangaza wa jua la asubuhi likitaradi. Chumbani kwenye nyumba moja iliyochakaa, Bibi Zena akiwa bado yupo kitandani alichukua simu yake iliyokuwa kitandani na kuiwasha.

"Saa kumi na mbili na dakika kumi!" Alisikika akizungumza Bibi Zena kwa mshangao mithili ya mtu aliyeshika butwaa.

"Nililala saa ngapi sijui" Alijiuliza mwenyewe pasipo kujijibu. Aliamka toka kitandani na kwenda hadi sebuleni kwake ambapo meza kubwa chakavu pamoja na viti vichache vya mbao vilipapendezesha sehemu hiyo kwa mpangilio anuwai. Pembezoni karibu na mlango wa kuingia vyumbani kulikuwa na meza ya TV. Alifika pale na kuiwasha redio ndogo iliyokuwapo eneo hilo.

"Taharuki ya tanda kupotea kwa Kenny. Polisi wasema hawahusiki" Hii ilikuwa taarifa kutoka kwenye gazeti moja lililokuwa likisomwa redioni. Bibi Zena alishindwa kujizuia, machozi yalianza kutiririka taratibu.

Bibi Zena alichukua biblia iliyokuwa juu ya meza yake na kufungua na kuanza kuisoma

"...Nitayainua macho yangu niitazame milima; msahada wangu utatoka wapi?
Msahada wangu u katika BWANA, aliyezifanya mbingu na Nchi.
Asiuache mguu wako usogezwe;
Asisinzie akulindaye;
Bwana ndiye mlinzi wako;
Bwana ndiye uvuli mkono wako wa kuume.
Jua halitakupiga mchana,
Wala mwezi wakati wa usiku.
Bwana atakulinda na mabaya yote,
Atakulinda nafsi yako..."

Hiki kilikuwa kifungu cha maneno katika Zaburi ambacho Bibi Zena aliyatumia kama maombi huku akilia kwa sauti ya taratibu ikichanganyika na kikwi.

*******************

Msituni

Huu ni msitu uliopo pembezoni kabisa na jiji la waswahili. Msitu huu unatisha kwa taswira yake kutokana na sifa zake za kuogofya zinazosimuliwa na watu. Si kwa kuwa na wanyama wakali au miti yenye kushikamana. Maisha huwa mafupi sana kwa kila aingiaye kwenye msitu huu.

Chini ya mti mkubwa, anaonekana mtu aliyelowa damu, macho yake yamefunikwa na kitambaa cheusi kilichofungwa barabara kwenye uso wake. Mikono ya huyo mtu imefungwa kwenye mti na miguu yake imefungwa kuukuu kwenye kipande cha gogo kubwa. Hakukuwa na mtu mwingine aonekanaye hapo isipo kuwa yeye. Hakukuwa na sauti isipokuwa ya ndege wa msituni hapo. Huu ulikuwa ni muda wa mchana ulio kamilika.

Kwa dakika chache kupita, wanaume watatu walioshika siraha ndogo za moto au bastola walifika hapo. Wote walikuwa wamevalia suti nyeusi zilizo fanana. Silaha zao walizishika mkononi pasipo kuogopa.

"Sikiliza bwana Kenny, hatuhitaji kukutesa sana. Ikiwa utatuonyesha ulipoiweka memory card uliyoitumia kurekodi tukio letu pale hotelini basi tutakuachia huru." Alisema mwanaume mmoja kati ya wale watatu waliovalia suti nyeusi huku akipitisha silaha yake kwenye uso wa bwana Kenny.

"Ndugu zangu mimi sijarekodi chochote pale?" Kwa kusuasua kutokana na maumivu aliyonayo Kenny alizungumza.

"Sasa kwanini ulikuwa unakimbia?" Aliuliza mwanaume wa pili

"Mmoja wenu alinionyesha silaha kabla ...." Alijaribu kujibu Kenny.

"Kelele..." Alinyamazishwa kwa kupigwa teke la tumbo.

"Sasa sisi tunakuua, utakufa na hiyo memory card yako, sawa?"

Lakini Kenny haukujibu chochote kwani alikuwa akiugulia maumivu makali aliyokuwa nayo.

Kimya kikatawala kwa muda kabla mlio wa risasi kusikika. Ndege wa mitini waliruka kwa hofu. Hata wakawa wanapiga kelele kwa milio yao

***************

Huu ni mwanzo tu tukutane sehemu ya Pili
Ni follow 🙏.
   

SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


mjukuu rewards 100 Comments 0
 

YAMENIKUTA

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MIMBA YA BESTMAN 9

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

JINSI YA KUTUNZA UKE

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

PART 5 MY HEART

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MY HEART 03--04

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

*MY HEART* *1---2 *

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MIMBA YA BESTMAN 7

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

ANIPHA 6--7.

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MIMBA YA BESTMAN 05

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

side chick episode 3

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

SIDE CHICK EPisode 2

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 18

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 17

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 16

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 8

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 1

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

RATIFA Sehemu ya 32

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

JINA LANGU SHAMSA EP3

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

JINA LANGU SHAMSA EP2

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

JINA LANGU SHAMSA EP1

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

BOYCHILD PART 3

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

DRAMA OF LOVE part 4.

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

DRAMA OF LOVE part 3

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

NJERI part 29

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest