PART 5
JINSI UTULIVU ULIVYOPONYA NDOA YANGU
Baada tu ya kujifungua niliwataarifu wakwe zangu lakini hawakuja kumuona Mtoto, wakasema kijana wao aliwakataza kuja nyumbani kwake hivyo hawawezi kuja bila ridhaa yake. Hii kauli iliniuma lakini niliongea na Pastor akasema wako sahihi kama Mtu kawaambia wasikanyage nyumbani kwake waje kufanya nini, Pastor akasema tulia Lea Watoto wako mengine yatajiset.
Nilikaa miezi mitatu Mume hajapiga simu, hajatuma message wala kutuma Pesa, nikashangaa hata ile hela kidogo ya matumizi aliyokuwa anaituma pia aliacha, nikaamua kunyamaza tu. Pastor aliniambia unapoona hauna majibu mwambie Mungu akupe majibu.
Kuna siku nimekaa zangu nyumbani kidogo akaja yule Mama wa jirani, lakini safari hii alikuja kitofauti. Kwanza tangu nimejifungua hakuonekana na sio kawaida yake na alikuwepo nyumbani kwake ila kwangu hajagusa. Ndio maana alivyoingia nikashangaa Leo imekuwaje? Kufika tu ananiuliza hauendi kwenu? Nikamuuliza kwetu kivipi? Akasema kwenu kwa wazazi wako, hivi kweli changamoto zote hizi za Ndoa bado upo tu, ningekuwa Mimi ningeshaondoka.
Nikamuuliza changamoto gani? Kwani kumetokea nini? Akasema Mumeo ameshakuacha, na inaonyesha hakutaki tena, maana ni miezi kama mitano sasa au sita hajarudi. Nikamwambia Ndio lakini huyu ni Mume wangu wa Ndoa, siwezi kuondoka kizembe hii ni ndoa, akaguna Mmmhmmmh! Haya, ila ningekuwa Mimi ningeondoka. Uzazi wote huo umeganda hapa si ungeenda kwenu kujifungua? Nikaona anaanza kuniudhi. Nikamwambia Ndio lililokuleta?, kama Ndio lililo kuleta basi nakuomba utoke, toka tena haraka sana toka. Akaniambia unanifukuza kama nani hapa, Wewe huna mamlaka hayo, na nikimwambia Mumeo kuwa umenifukuza utaona kitakacho kupata. Nikamwambia Mama tafadhali nakuomba utoke nisije nikakukosea heshima, akasema naondoka ila kwakuwa umenifukuza humu ndani utaondoka, nikamwambia labda kama hii ni nyumba ya Mumeo, akacheka kwa dharau heheeee, utajua mwenyewe ila jua utatoka.
Akasema inaonekana kwenu ni masikini sana na huna pa kwenda ndio maana umeng'ang'ania hapa, aisee nilikasirika nikasema kwa ukali tokaaaa kwa nguvu kama nakemea Pepo akastuka akaondoka, japo alitoa mfyonyo huo hatari.
Nilikosa amani sana nikasema kwani huyu Mama kawaje au kapatwa na nini? Inamaana hata Yeye ni adui yangu. Nilikaa baadae nikampigia Pastor akasema huyo kuna jambo, tuendelee kuomba Mungu ampige upofu na amfichue.
Usiku mida kama ya saa tatu, nikashangaa Mume wangu ananipigia Simu, imagine hajatutafuta tangu nimejifungua mpaka Leo, roho ikasita kupokea. Baadae akatuma message kama umechoka kukaa hapo ondoka acha kuwafanyia watu ninaowaheshimu ujeuri, utaondoka. Nikajua ni yule Mama kamwambia Mr kuwa nimemfukuza. Sikumjibu wala sikupokea nikazima simu nikapumzika maana nilihisi kichwa kinauma.
Mama Ivan alinipigia simu akasema nataka kuja kumuona Mtoto nikamwambia njoo karibu. Basi siku hiyo Mama Ivan anakuja ilikuwa weekend, akaniambia nakuja na gari yenye Tinted nifungulie geti sitaki watu wanione, nikamwambia sawa. Basi akafika nikafungua geti akaingia, ila ile nafunga geti namuona yule Mama wa jirani akapita anachungulia anataka kujua ni nani kwenye gari. Alipita hajanisalimia na Mimi sijamsalimia, nikafunga geti faster, nikamwambia Dada hakuna kufungulia Mtu.
Mama Ivan akashuka faster akaingia ndani, nikamuuliza vipi kwani, akasema sijataka huyo Mama wa jirani anione maana ndio mbaya. Nikamwambia umejuaje maana juzi tumetoka kugombana na Mr kaniambia nitaondoka hapa.
Mama Ivan akasema Mdogo wangu Wewe ni mdogo wangu, umekuwa mwanamke mwenye Upendo sana kwa mwanangu, lakini pia nimekuona ni mwanamke jasiri sana na mvumilivu. Ila kuna mambo yanaendelea natamani nikwambie mdogo wangu, nikamwambia niambie Dada nakuomba
Akachukua simu akanionyesha picha za Mr yuko na Mwanamke na Mtoto, nikamwambia hizi picha Dada yangu alinionyesha alizipata insta japo sijajua huyo Dada ni nani na wakoje na Mume wangu, akasema sasa tulia kipenz ni hivi,
Huyu binti ndio Mtoto wa huyo Mama wa jirani, moyo ukastuka Paaah, akasema na huyo Mtoto huyo Dada kazaa na Mumeo, na juzi wamefanya kama sherehe ya kumgomboa Mtoto na Mumeo kalipishwa na mahari, nikasema unasemaje? Akasema ndio hivyo na hivi kampangia nyumba wanaishi wote
Huyu binti ndio alinitoa Mimi kwenye hii nyumba, yani huyu ndio sababu ya Mimi kuondoka hapa. Akasema tulia nikupe story kipenzi, nikakaa chini huku natetemeka sielewi jamani
ITAENDELEA.