Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  artist

PART 4 JINSI UTULIVU ULIVYOPONYA NDOA YANGU

7th Jun, 2025 Views 7

PART 4
JINSI UTULIVU ULIVYOPONYA NDOA YANGU

Nikweli Mume wangu hakurudi nyumbani mwezi mzima na, yani ni mwezi mzima ukakatika hakuna simu hakuna message, zaidi tu naona miamala ya pesa za matumizi basi.
Hii kitu ilinipa mashaka kwani naona kabisa Mume wangu yuko hapa hapa Dar lakini nyumbani haji, sasa yuko wapi?

Kuna siku Bwana usiku nataka kulala, simu yangu ikaita, alikuwa Dada yangu akaniambia Jane unaendeleaje? Nikamwambia sijambo, akaniuliza umejifungua? Nikamwambia hapana bado kama wiki hivi nikafanyiwe operation. Akasema vipi Mumeo mmeachana? nikamwambia hapana tupo wote kwanini unauliza, akasema mmmh mbona naona kuna mahali kapostiwa yuko kwenye sherehe ya Mtoto ni kama vile anamvalisha Pete huyo mwanamke aliyezaa nae. Nikasema whaaat nitumie.

Basi Dada yangu kunitumia picha kweli Mume wangu kabeba Mtoto na wamefanya kama sherehe ya engagement. Nilivyoona vile nikaangalia kidole changu nikakuta kina pete bado nikasema inawezekanaje hii jamani, kweli Mtu anioe halafu akachumbie Mtu mwingine haiwezekani. Hapo hapo nikasikia kama mshale umechoma kwenye moyo wangu, nikaanza kusikia maumivu ya moyo, nilisikia uchungu sana sana. Nikakaa nikaanza kulia kwa uchungu sana, nikasema kweli Roy Wewe wa kunifanyia hivi kweli, kama hakuwa ananipenda kwanini alinioa kwanini? Nililia, nikatafakari sana, mpaka nikaanza kujisikia vibaya. Ikabidi nimpigie Dada yangu aje tu kunisaidia. Dada Alipofika hali yangu ikawa mbaya, akasema Mdogo wangu nisamehe nimekosea kukupa taarifa kwenye hali hii nisamehe, Mimi hata naelewa basi, nimekazana tu kulia.

Baadae hali ikawa mbaya nikawa nashindwa kupumua, ikabidi nikimbizwe hospital. Kufika Hospital kupimwa wakasema Pressure iko juu sana inabidi nilazwe. Doctor akasema mbona hali imebadilika ghafla, hii sio nzuri inahatarisha usalama wako na wa Mtoto. Nikawekwa kwenye chumba cha uangalizi. Nakumbuka nilikuwa nimevimba mwili mzima, miguu, mikono, uso ndio usiseme nilikuwa kama nimeumuka hivi, nilikuwa natisha haswa. Dada yangu akawa analia anajilaumu tu kwanini aliniambia.

Sasa nikiwa mule hospital, kuna Nurse alikuwa ananihudumia akawa ananipigisha story na kunitia moyo, akawa ananiuliza imekuwaje, jitahidi uachilie ili ujifungue salama. Nikawa napiga nae story sana. Kesho yake aliingia tena shift ya jioni, akaja kwenye chumba changu. Akaniambia Madam unaendeleaje nikamwambia sijambo, akasema tena hapa tuna maombi huwa tunashiriki online na Pastor wetu, naomba Leo tuombe wote, nikamwambia sawa nahitaji sana maombi.

Basi muda ukafika akaweka maombi ya SHUSHANI kwenye simu, akaniambia wewe fwatisha tu taratibu omba taratibu utapata Amani. Nakumbuka siku hiyo Pastor aliombea sana kuhusu uponyaji wa Moyo aliomba sana sana. Nilijikuta ninaomba, ninalia mpaka maombi yanaisha nikajiona mwepesi. Nikamwambia yule binti nimeenjoy sana maombi, akasema usijali kesho yapo nitakuja tuombe pamoja.

Sio siri baada ya yale maombi niliona moyo umekuwa mwepesi sana na kama kuna kitu kimetoka, na kwa mara ya kwanza nililala usiku. Nimekuja kuamka asubuhi ni saa moja manesi wamekuja kunipima pressure na kunipa dawa, wakasema tunaona pressure inashuka kidogo tumeona tukuache upumzike. Kweli nikalala tena mpaka saa nne. Ndio nikaamka nikaoga nikanywa uji nikarudi kulala. Jioni ilipofika kale kabinti kanurse kakaja, kakaniuliza vipi unaendeleaje, nikamwambia Leo nimelala siku nzima akasema, nimeongea na Pastor wangu yule wa jana nimemuomba Leo aongee na wewe, kasema baada ya maombi atakupigia akuombee. Nikamwambia nitashukuru sana sana

Kweli maombi ya saa mbili yakaanza, nikaomba haswaa baada ya hapo Pastor akapiga simu nikaongea nae kwa kifupi akaniambia, Kwasasa unachohitaji ni imani tu kwa Mungu, pale unapoona mambo ni magumu hakikisha Imani yako haitetereki. Endelea kumuamini Mungu kuwa atakusaidia hata kama unaona mazingira ni magumu kiasi gani. Amini tu kuwa Mungu anakupenda na hajakuacha, hilo tu. Akaniambia Kwasasa achana na mambo yote na anza kuwa excited na Mtoto wako utakaye mzaa, mshukuru Mungu kwa Neema ya kuwa Mama na muombe akuvushe salama, ukishajifungua sasa tutaonana tuongee vizuri. Kweli Pastor aliniombea sana sana.

Ila kitu cha ajabu wakati anaomba akaniambia nakuomba utangaze msamaha kwa Mumeo, Muombee Mumeo rehema na mwambie Mungu kuwa umemsamehe ili Mungu akupe amani.

Baada ya pale nilijisikia vizuri sana, nikamshukuru yule Binti Nurse kwa kuniunganisha na Mtumishi wa Mungu, nikamwambia kuanzia Leo Mimi ni mwana Shushani.

Kesho yake nikapimwa pressure imeshuka kabisa, Doctor akasema kwa hapa naweza kumtoa Mtoto. Kweli mida ya jioni saa kumi na moja nikaingizwa theater nikafanyiwa operation na Mungu mwema ilienda vizuri na nikabarikiwa Mtoto wa kiume. Nilimshukuru Mungu sana, na kama Pastor alivyosema nimfurahie Mtoto wangu, kweli nikawa kila nikimuangalia mwanangu najisikia raha ya ajabu.

Nikaruhusiwa kurudi nyumbani, Mume hakurudi wala kupiga simu , Pastor akasema tulia tu nyamaza kimya, Kwasasa pata nguvu kwanza ukishakaa sawa utamtafuta. Kweli sikumtafuta nika focus na Mtoto nikawa busy na mwanangu basi siku zikawa zinaenda. Pressure iliisha kabisa, nikawa naenda kupima wanasema iko normal, mwili ulikuwa umevimba sana nawenyewe ukanywea kabisaaa, nikarudi kama kawaida.

ITAENDELEA.
   

SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MSHANGAZI EPISODE 1

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MIMBA YA BESTMAN 13

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MIMBA YA BESTMAN 10

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

YAMENIKUTA

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MIMBA YA BESTMAN 9

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

JINSI YA KUTUNZA UKE

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

PART 5 MY HEART

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MY HEART 03--04

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

*MY HEART* *1---2 *

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MIMBA YA BESTMAN 7

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

ANIPHA 6--7.

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MIMBA YA BESTMAN 05

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

side chick episode 3

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

SIDE CHICK EPisode 2

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 18

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 17

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 16

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 8

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 1

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

RATIFA Sehemu ya 32

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

JINA LANGU SHAMSA EP3

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

JINA LANGU SHAMSA EP2

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

JINA LANGU SHAMSA EP1

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

BOYCHILD PART 3

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

DRAMA OF LOVE part 4.

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

DRAMA OF LOVE part 3

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest