SIMULIZI YA MAISHA: NILIMUUA MAMA YANGU MZAZI ILI NIOLEWE NA BABA | EP 43
Na Sam Darfur 0717256498
RECAP: SEHEMU ILIYOPITA
Kama ambavyo tulivyopanga, basi tulifanya hivyo kwa kujifumbisha macho. Dakika moja mbele Sammy aliingia ndani, kisha akazima taa na kuwasha tena lengo kupima kama tulikuwa macho ama lah.
Alipoona kwamba tumelala, alisogelea maiti na kuchukua nywele moja lakini, nilisema.
“Kwahiyo ndio kazi ambayo imekuleta hapa sio?” niliona akitetemeka huku akitupa nywele chini na kutaka kuondoka lakini Betrice aliekea katika mlango na kufunga kwa funguo kisha aliitupa kwa nje
SEHEMU YA 43
Weka Like kwanza ndo uanze kusoma. Hiyo like yako ni muhimu sana kwangu.
Baada ya mlango kufungwa sasa tuliamua kuweka kikaangoni Samrathy, tulimkazia macho na swali la kwanza lilikuwa mbele yake.
“Enhe! Mzanzibar hewa, kuna nini ambacho ulikuwa unakitafuta huku?” nilimuuliza huku nikimtazama usoni.
Kwa aibu aliamua kuinamia chini lakini Betrice alimuinua sura yake kisha akalitengeneza kohozi na kumtemea usoni.
Akamuuliza kwa mara ya pili
“Si ujibu, ulitaka kuchukua nywele ili upeleke wapi?” swali hili nalo alijifanya hajasikia.
Nilimzibua kibao kimoja kitakatifu katika sikio la upande wa kulia hadi kile ambacho alikuwa akikisikia katika masikio yake nilikisikia na Mimi. Alianza kujifanya kulia lakini tulimziba nguo mdomoni na kumlaza chini.
“M’bumunde hadi ajue sisi ni kina nani?” Betrice alisema
Sikutaka kuchelewa zaidi ya kuchangamkia fursa, nilimpiga huku akijaribu kulia lakini sauti yake ilikuwa haitoki zaidi ya kugumia kama mtu ambaye alikuwa akigua hivi.
“Umeamua kumuua ndugu yangu na sasa unataka kuniua na mimi si ndio?” nilisema huku nikiendelea kumpiga.
“Mpigie wewe acha kumuonea huruma” Alisema Betrice.
Betrice naye hakutoka nyuma, kama wanavyosema wanapovuna ndipo wanaposhiba. Usitegemee watu wavune halafu uende ukachukue mazao watakuambia kwamba wameuza au hawajavuna mengi. Basi Betrice aliona anakila sababu ya kumfundisha adabu yule mwanamke.
Baada ya kumpiga kwa muda mrefu tulikuwa na wazo kwamba kama tukimuua mule ndani kungekuwa na matatizo mengine ambayo tungejitafutia, tuliamua kumuacha kwanza huku tukiendelea kumuuliza maswali mengine.
Kumbe hili ndio lilikuwa kosa letu, kwani wakati tunampiga mwenzetu alifanikiwa kuchukua nywele ya Betrice na kuficha katika matiti nasi hatukujua hilo. Tuliendelea kumnyoosha adabu huku tukicheka na kulia hadi tulipoona inatosha tulimuacha awe huru na maswali ya hapa na pale yalifuatia.
“Najua kwamba umepanga kutuangamiza na umeanza na ndugu yangu, Sammy ni nini ambacho tumekukosea au nimekukosea? Kumpa mume wako mali au kuna kingine?”
“Ungetaka kujua sababu ungeniuliza kwanza na sio kunipiga halafu mnakuja kuniuliza” “Kwahiyo unataka kusema kwamba hujamuua Brandina?”
“Ndio, ndio hatujamuua”
“Ok, tukishazika utapata majibu ya maswali ambayo leo nimekuuliza.” Nilisema hivyo kama kumaliza maongezi yetu.
Asubuhi ilipopambazuka watu ambao walikuwa nje walishangaa kwwanini chumba kile kilifungwa, walipofungua walitukuta tukiwa tumelala watatu huku maiti kiwa kitandani. Walijaribu kutuuliza maswali lakini hakuna ambaye alijibu.
Niliona Sammy akiondoka akiwa amejifunika mtandio usoni, nilijaribu kumfuata lakini Loy alinizuia huku akijifanya kwamba yeye ndio alikuwa na haki ya kumhoji mke wake.
“Kaa kwanza nakuja” Loy alisema
“Unajua anaenda wapi yule?”
“Nimesema kaa nakuja wewe shida yako nini?” alisema Loy kisha huyo aliondoka na kumfuata mke wake katika eneo la maegesho ya magari.
Niliwaangalia jinsi ambavyo walikuwa wakirumbana wakiwa katika gari, akili yangu ikaniambia kwamba hakuna kingine ambacho walikuwa wakirumbania zaidi ya kile ambacho kimetokea jana kwa bahati nzuri, niliona Loy akishuka kwenye gari na mke wake aliamua kuondoka.
Watu wengine ambao walikuwa nje wakitazama tukio lile walipatwa na mfadhaiko, hakuna ambaye alielewa kwanini mke wa Loy alikuwa akiondoka lakini ndani ya moyo wangu nilisema kwamba kila kitu kimeenda sawa.
Nilirudi ndani ambako nilimkuta Betrice akiwa anawatazama watu ambao walikuwa wakiweka mwili katika jeneza. Nilimuita kwa pembeni ili tuzungumze kwa kile ambacho kilitokea nje. Alinielewa na alikuja eneo ambalo mimi nilikuwepo.
“Tumelichokoza, tunatakiwa kulivaa sawa mwaya” nilisema huku nikimtazama Betrice ambaye alitaka kujua nini ambacho tulikuwa tumelichokoza.
“Sammy ameondoka na sijui ameenda wapi hata hivyoLoy anaonekana kama mtu ambaye amechukia hivi” niliongeza
“Bwana kama bwai itakuwa bwai tu, sio muda wa kuchekea vinyonga hapa au ngoja nitangaze” Betrice alisema kisha alianza kupiga hatua hadi sebureni ambako Mjomba alikuwa akiongea na Baba.
Alipofika tu, hakutaka mambo mengi zaidi ya kumwaga mchele alisema.
“Wewe sijui unajiita Loy, mara Loyce acha kitu ambacho unakifanya halafu mwambie mke wako huu mziki ambao anataka kuufungulia hivi sasa atashindwa kuucheza wala kuusikiliza. Nimemaliza” alisema kisha alirudi hadi sehemu ambayo nilikuwepo.
Mzee Jawan alijikuta akiwa njia panda hata watu wengine ambao walimsikia Betrice hawakuelewa nini haswa ambacho kilikuwa kinaendelea.
“Jamani kwani kuna nini?” aliuliza Mzee
Jawan
“Sifahamu, kwani huyu Binti ni nani haswa?”
Loy naye alirudisha swali kwa Mzee Jawan
“Ni mtu ambaye yupo hapa muda mrefu tu, mke wako yupo wapi?”
“Kaenda hospital anasema kwamba mwili unamuuma” alibuni uongo.
Niliona Baba akiinuka na kunifuata kisha akaniuliza maswali mengi sana kuhusu kile ambacho kilikuwa kimetokea lakini nilimwambia kwamba si muda kujadili mambo yale zaidi ya kujua namna gani tutamzika Brandina.
“Betrice sio mjinga anajua anachokisema heshimu maamuzi yake”
“Ndio amseme mtu mbele watu?”
“Kama huyo mtu haoni kama kuna watu je? Hata hivyo baadaye tutaongea vizuri kwa hivi sasa acha tumpumzishe kwanza Brandina”
“Mh! Sawa hakuna shida ila sijapenda” alisema Mzee Jawan.
Taratibu za mazishi ziliendelea ambapo hadi kufikia saa 11 jioni tulikuwa tayari tumekamilisha kila kitu, tulimpumzisha mpendwa wetu katika nyumba yake ya milele. Nilirudi nyumbani nikiwa na Betrice pamoja na watu wengine ambao walikuwa wakitusindikiza na kutupa pole.
Niliomba wale watu watupishe ili tupate kuongea kama familia yaani mimi, Baba, Mjomba pamoja na Mama hata Betrice pia akiwemo. Kwa bahati nzuri walinielewa.
“Mjomba” nilisema huku nikimtazama usoni
“Nam!”
“Najua hichi ambacho kimetokea kwako sio kigeni sana maana umeona misiba mingi tu ila msiba huu wa Brandina utakuwa mgeni sababu amejinyonga. Yote tisa, nachotaka kusema ni kwamba muda wa kupambana na hali yako umefika. Naomba uniachie kampuni kama kuendesha nitandesha mwenyewe” Nilimwambia huku nikijua kwamba lazima angeleta utata.
Ilikuwa ni kauli ambayo hakuna ambaye angetarajia kama ningeitoa kwa wakati ule, hata Betrice mwenyewe hakujua kama ningesema kwamba nahitaji kampuni. Alinitazama huku akiniuliza kwa ishara ya mikono nami nilimuonesha ishara kwamba kila kitu kipo sawa. Nikamwambia.
“Nipe kampuni yangu. Mwisho wa kikao tunaweza kuondoka sasa” maneno yangu tisa yaliwaacha watu katika sintofahamu lakini nilimaanisha kile ambacho nilikuwa nimekiongea......
Unalalamika inachelewa kutoka wakati nimekushushia bei, kutoka kila season kwa 3000Tsh mpaka bei ya 2500 kwa season zote tatu... Bado unalalamika... Achana na bei ya zamani ya 9000Tsh.... Njoo na 2500 usome simulizi yako.... WhatsApp namba 0717255498..