PART 11
JINSI UTULIVU ULIVYOPONYA NDOA YANGU
Ule usiku niliendelea kulia, sikunyamaza hata kidogo. Alijaribu sana kuni bembeleza ila ilishindikana, nilikuwa nauchungu mwingi sana. Huko kote nilijitahidi ila siku ile nikasema hapana Leo kaingia mwenyewe kwenye 18 acha aipate. Nililia usiku kucha mpaka asubuhi sikunyamaza.
Jana kumbe wakati ananitafuta aliwapigia simu wazazi wake, pamoja na wasimamizi wa Ndoa yetu waje. Hivyo kuna muda nikasikia sauti ya Mama mkwe anaongea nikasema hapa ndio penyewe. Tena hawa nilikuwa nawaita waje hawataki sasa Leo watanijua vizuri. Nikiwa niko ndani nikasikia sauti ya wasimamizi wetu wa harusi nao wakaja. Na wao ni wanafki vile vile, niliwaomba sana waje kipindi Roy hatulii nyumbani hawakuja walikatazwa. Nikachekecha akili nikampigia Mjomba wangu na Mkewe nikamwambia Mjomba njoo huku nimefukuzwa nataka kuondoka. Mjomba akastuka akasema nakuja sasahivi, nikamwambia nakuomba uwahi maana hakai mbali na hapa kwetu.
Nikaingia bafuni nikaoga, nikavaa, nikaanza kuchukua mabegi nipange Nguo. Nikatoa Nguo zote kibatini nikaanza kuzipanga. Huku nalia nakwambia sijanyamaza.
Niwe mkweli Moyo wangu ulikuwa na maumivu sana, kidonda kilikuwa kichungu sana, nilikuwa na mzigo mzito wa maumivu na nilitamani kuutua ila sikupata chance, ila nikasema leo ndio Leo, nitalia Leo nitaongea Leo mpaka ajue namna alivyoniumiza.
Basi akaja chumbani akanikuta nakunja nguo naweka kwenye mabag, weeeh akastuka nini tena Jane, nini Mke wangu, sikumjibu kitu ninalia tu. Nikaona katoka halafu Mama Mkwe na yule Matron wangu wakaingia naona aliwaomba waje chumbani, nilivyowaona nilimkumbatia Matron wangu nikaanza kulia kwa nguvu. Nilitoa sauti kama kama nimepigwa. Kuna kitu kilikuwa kinanikaba kwenye koo nikasema Leo nakitoa, Leo acha nilie. Nililia sana, mpaka Mama Mkwe nae akaanza kulia.
Na Yeye Roy alivyosikia nalia nae akaja chumbani, nikaanza kuongea huku na mwambia Mama Mkwe, MAMA NIMECHOKA, MAMA NIACHENI NIRUDI NYUMBANI, NAOMBA NIENDE KWETU MAMAA MAMAA NAUMIA MAMAAA πππ, akawa anasema Jane mwanangu tulia, nikamjibu SIWEZI MAMAAA SIWEZIII NAUMIA MAMAAA NIMECHOKA MIMI NATAKA NIRUDI KWETU
Nikasikia Baba Mkwe anagonga akaomba twende sebleni, basi tukatoka lakini bado nalia NIMECHOKAAA NAUMIA NATESEKAA, sasa kidogo Mjomba wangu akaja na Mkewe ile wanaingia tu, Nikaanza kulia MJOMBA NIPELEKE NYUMBANI MJOMBA NATESEKA MWANAO NIMECHOKA, Mjomba alinikumbatia akaanza nae kulia. Sio siri nililia mpaka nikawa mwekundu, nilikuwa nauchungu sana sana.
Baba Mkwe akauliza Roy kuna nini, imekuwaje? Akasema Mimi sijui imekuwaje siku zote alikuwa sawa nashangaa tangu jana Usiku ameanza kulia hanyamazi. Hapo hapo nikasimama nikaanza kuongea BABA NILIWAOMBA MJE MNISAIDIE MKAKATAA KUJA MKASEMA ROY KAWAKATAZA KUJA KWAKE, MKANIACHA NATESEKA PEKE YANGU BABAA, HATA NYINYI WASIMAMIZI WA HARUSI PIA MLINIACHA MIMI PEKEE YANGU πππ, MOYO WANGU UMEFIKA MWISHO NIMECHOKA NATAKA KUONDOKA πππ
Basi nikamuona Roy kwa Mara ya kwanza kapiga magoti anaanza kulia, akaanza BABA NISAMEHE, MAMA NISAMEHE, MKE WANGU NAKUOMBA NISAMEHE, NIMEKUTESA SANA, SIKUJUA KAMA ULIKUWA UNAUMIA KIASI HIKI, NAKUOMBA NISAMEHE MKE WANGU AKAANZA KULIA NA YEYEE ππ
Hapo hapo nikasema kweli anadiriki kuniacha Mimi na kwenda kutembea na Mtoto wa jirani mpaka kazaa nae kweli? Nikasema Ivan namlea lakini huyo mwingine hapana, na inaonyesha huyo mwanamke anampenda kuliko Mimi, nimetumiwa video akinitukana Mimi matusi ya nguoni kwa huyo mwanamke, anampa mwanamke Pesa nyingi wakati huku nyumbani hatumi chochote. Ananiambia alikuwa kijijini wakati walikuwa wanaishi wote Sinza wamepanga nikaanza kulia tena πππ
Mjomba akamuuliza Roy ni kweli hayo anayosema Jane, akasema ni kweli Mjomba ni kweli nimekosea sana, najilaumu sana. Akaulizwa vipi kuhusu huyo Mtoto, akasema Mtoto sio wangu, nilibambikiwa tu ila Baba wa Mtoto yupo na analea mwanae. Mjomba akasema aisee basi acha Jane aende nyumbani kwanza akitulia atarudi maana mambo ni mengi sana.
Hapo hapo akapiga magoti mbele ya Mjomba, akasema Mjomba naomba mnisamehe, ni kweli nimemtesa Mke wangu sana, naomba msamaha ila naomba unisaidie Jane asiondoke naomba tu unisaidie nakuomba Mjomba. Hapo Baba Mkwe kainamisha kichwa kachoka kabisaaa.
Wote wakakaa kimya kwa muda, baadae nikamuona Mjomba ananiambia mwanangu Jane msamehe Mumeo nakuomba sana, najua amekosea ila msamehe nakuomba mwanangu nakuomba Mimi Mjomba wako. Nililia jamani, nililia sanaaa, baadae nikajiambia moyoni mwangu Jane achilia acha yaishe.
Basi nikanyanyuka nikaenda kumfwata Mume wangu alipokaa nikapiga magoti nikamwambia nimekusamehe Mume wangu, nakupenda sana Mume wangu, yameisha Babaa. Basi akanikumbatia akaanza kulia pale, yani ilikuwa kama Movie.
Basi Mama Mkwe ni mkatoliki, akaanza kusali pale sala ya Baba yetu, salam Maria baadae akamshukuru Mungu. Baba Mkwe akasimama akasema Mwanangu Jane asante sana, asante kwa uvumilivu wako mwanangu, kweli nimeamini unampenda Roy. Akamwambia Roy hii ni last chance, umeona ilivyokuwa ngumu, Mtoto wawatu alikuwa na uchungu sana nakuomba ubadilike, nakuomba sana badilika.
Basi wageni wakaondoka wakatuacha. Mama Mkwe akaomba achukue Watoto wakakae kwake watarudi kesho, nikasema sawa waende tu na Dada.
Basi tukabaki Mimi na Roy ndani, sio siri Moyo wangu ulikuwa na amani isiyo yakawaida, ule mzigo mzito niliutua wote.
Basi niseme Ndoa yetu ikaanza upya hapo, wenyewe mnaelewa nisiongee sana jamani, mambo yakawa si mambo na NILIENJOY mnoo, imagine sijakutana nae mwaka mzima aisee ilikuwa exceptional kwakweli.
Ndoa yangu imerudi, Mume wangu ametulia. Kuna nyumba nyingine alijenga mpya, akaniomba tuhamie huko pale akasema hapataki tena anapauza kabisa, tutanunua kiwanja eneo lingine tujenge.
Kwasasa tumehama huko kabisaaa, tunaishi mbali na huko, tunaishi maisha ya Amani sana.
Namshukuru Mungu sana kwa kunirejeshea furaha yangu πππ
MUNGU AKUBARIKI PASTOR ANNI, HILI SOMO LA UTULIVU NATAMANI UFUNDISHE KILA MWANAMKE ALIYE KWENYE NDOA ALIELEWE,KUWA WANAPASWA KUWA WATULIVU NA WAOMBAJI
UTULIVU UNANGUVU UTULIVU UNALIPA
ππππππ
MUNGU AWABARIKI SANA
MWISHOOOOO.