ANIPHA ๐๐.
Sehemu ya 13.
"we Allen wewe, naomba uamke unafanya nini kitandani kwangu wewe"
"Mmmh jamani nini lakini anipha, mbona wewe ni mgomvi hivyo"
"oooh me Ndio mgomvi si Ndio, aya toka sasa hivi nje ya chumba Changu tena haraka sana"
"sasa Mi nikalale na nani jamani, jana umeniacha nikalala mwenyewe na leo pia unanifukiza kweli jamani"
"nini wewe, unamaanisha jana ulilala chumbani kwangu???"
"Ndio jana nimelala humu, nimekisubiri mpka usingizi ukanipitia bila ya kukuona kweli anipha"
"sitaki kisikia hizo ngojera zako sawa, toka chumbani kwangu mpuuzi wewe yani umelala uko na huyu mwanamke wako alafu unakuja hapa kuniambia sijui nyoko nyoko, toka bwana wee allh"
"Anipha,najua nilikukosea sana lakini nisamehe mama angu eeh, Tanasha sio mpenzi wangu ni rafiki yangu tu nielewe basi jamani"
"๐๐๐Ngoja nicheke kama mazuri, yani mnaitana sijui babe sjui mme Mara mke alafu sasa hivi unaniambia eti ni rafiki yako tu, unaniona mimi mjinga sana si ndio Allen aya toka"
"kweli kabisa anipha, kama huamini twende hata sasa hivi sebleni nikamuite Tanasha kweli tena na hata kuja hapa nilijua kuwa uko hapa na ndio maan nimekuja kwa ajili yako nielewe basi mama eeeh"
"eeeh we kima wewe, embu toka chumbani kwangu hizo story zako kamsimulie Tanasha sawa"
"we nitukane tu vyovyote hata ukitaka kunipiga ni sawa tu ila mimi humu sitoki kabisa yani mpka tuelewane"
"oooh sawa, basi mimi nalala na sitaki usumbufu kabisa na usiniguse kabisa"
Nilirudi kulala, nikajifunika shuka hadi kichwani nikamuacha Allen anaongea mwenyewe mimi nikajifanya kama simsikii kabisa mpaka kunakucha
Asubuhi, kulivyokucha sikumkuta Allen kitandani kwangu nikahisi labda nilikuwa naota mbona Allen hayupo jamani, nikaamka na kwenda bafuni kuoga kisha nikaelekea jikoni kuandaa chai sasa.
"Anipha, njoo tu huku mezani chai ipo tayari mamy"
"afadhali Ndio maan nakupendaga shoga yangu aya ngoja nije"
"Sasa leo shoga yangu hakuna kwenda dukani mpka tumalize mazungumzo kwanza"
"Mmmh kuna nini tena jamani mbona mnanitisha mimi!!!"
"hamna hata kitu tunywe kwanza chai alafu Ndio tutaongea vizuri sasa"
Mimi hapo moyo uko juu juu nikihisi labda ni kwa sababu Allen alilala chumbani kwangu, huenda Mainda alimuona akitoka au Tanasha, jamani me si ndio nitafukuzwa kazi jamani nilimuangalia Allen kwa hasira sana ๐ก๐กlakini yeye wala hata hajali chochote, basi Baada ya chai nikatoa vyombo nikapeleka jikoni hapo nawaza sjui hata Mainda anataka kuongea nini ๐
Baada ya kuweka vyombo jikoni nikarudi sebleni sasa kumsikiliza Mainda.
"Sasa anipha, mimi nimewaita hapa wote nyie Lengo ni wewe kuyamaliza na mwenzio sioni haja ya ninyi kugombana kwa sababu ya mtu mwingine au wewe Allen unasemaje???"
"Ni kweli kabisa sissy Mainda"
"Jamani ngojeni kwanza, mbona mimi sielewi chochote hapa"
"Anipha, iko hivi Allen amekuja hapa lengo lake ni wewe uweze kumsamehe kwa sababu ameshajua makosa yake na Ndio maan yuko hapa"
"Mimi bado siwaelewi kabisa, Allen ni mume mtarajiwa wa Tanasha alafu mmnasema eti anataka mimi nimsamehe kivipi yani"
" Anipha mimi na Tanasha ni marafiki tu hamna kitu kati yetu, na nimekuja kugundua kuwa huna kosa lolote Baada ya kuambiwa na Briana mdogo wangu"
"oooh kumbe, sasa kwa nini hukunitafuta sasa eeeh"
"nimekutafuta sana Anipha bila ya mafanikio yoyote na hata namba ya simu umebadilisha"
"kwa hiyo hapa umenipataje sasa"
"Ni Baada ya sissy Mainda kuniambia kuwa anaishi na mdada anaitwa Anipha, ndio nikamuuliza yukoje Ndio akaanza kunielezea kuhusu wewe hapo"
"aaah kumbe we Mainda ndio umenichoma kwa huyu mbuzi ๐ก๐ก"
"ukweli mimi ndio nilimwambia na Baada ya wewe kunisimulia kuhusu kuachana kwenu, nikajua kuwa ni Allen mdogo wangu maana hizo Ndio tabia za mama yetu"
"Ndio Anipha, wanayoongea Mainda na Allen ni kweli kabisa, mimi na Allen ni marafiki wa muda mrefu sana na nimekuja nae ili kuhakikisha kuwa mnarudiana basi"
"Ndio, Anipha hata mimi mama alimkataa mpenzi wangu kwa sababu ni maskini na Ndio sababu ya mimi kuondoka nyumbani na kuhamia huku Arusha, msikilize basi mwenzio"
"sissy Mainda Sisi tuondoke hapa tuwaache wenyewe waonge si eti"
Mainda na Tanasha waliondoka sebleni na kuniacha mimi na allen sebleni ili toungee sasa muda huo mimi nimenuna hatari nataka kubembelezwa ๐๐๐.
Itaendelea.......
Full 1000
Whatsp 0784468229.