Yule Mzee aliniambia , kupambana sio lazima uonekane unakimbia , hata ukisimama ukiwa umechoka ni aina ya mapambano..
Kabla sijaongea chochote yule mzee akaongeza kwa kusema, kamwe usijaribu kurudi nyuma, hata kama mbele ni giza..
Nikamwambia kuna watu tulitegemea wawe mwangaza wetu wakati wa giza lakini wametukimbia..
Mzee akaniambia, Usiogope watu kukukimbia wakati wa giza, kwa sababu giza huisha lakini anayetembea gizani huwa na macho ya Simba..
Nikamwambia mzee unazeeka na hekima zako , Asante kwa busara zako..
Mzee akaniambia, Hekima sio kuwa na miaka mingi , ni kujua nini cha kufanya kwa kilichokupata kwa wakati sahihi, na ukishajua hilo hata dunia ikupige haitakuondoa katika mstari..
Kituo changu cha kushuka kilifika , nikaagana na yule mzee nikashuka zangu , huku akiniambia Usiogope kuanza upya pale unapofika mwisho..
KINARA SIKU ZOTE Jay S Wadhamas TWENDE MBELE mdundo.com/a/15130 SUPPORT NYOTA YANGU ING'AE
#wadhamasmusiq
@topfans
Follow Darly G Kenya.