Ukimsikiliza Chidi Benz kwenye ngoma ya Mashallah aliuzungumzia muziki wa Bongo Fleva japokuwa ukipagawa utadhani alimzungumzia mwanamke mrembo.
Hii ni sawa na Kanye West. Kwenye ngoma yake ya Homecoming aliamua kuuzungumzia mji wake wa Windy ambao upo Chicago ila humo kidogo alibadilisha jina na kuuita Wendy.
Ukitega sikio utamsikia akisema my name is Windy and I like to blow trees" and "when I grew up she showed me how to go downtown, in the nighttime her face lit up.
Kanye West alizaliwa huko Atlanta, jiji lililokuwa ndani ya Jimbo la Illinois lakini baadaye mama yake, Donda akaamua kuhamia Chicago na mwanaye, so Kanye West akaanza kukulia ndani ya Wendy, Chicago kwa muda mrefu sana.
Japokuwa alificha hapo kwa mstari wa My Name is Windy and I like to blow trees alimaanisha kuwa wakazi wengi wa mji wa Wendy walipenda sana kuvuta bangi. Ni mitaa ya watu weusi, kulikuwa na uhuni wa kila aina na hata uvutaji wa bangi ulikuwa ni wa kiwango kikubwa mno.
Na uzuri wa ngoma hiyo alifafanua kabisa kwamba if you don’t know right now, I’m talking bout Chi town...Huu mji wa Chi upo ndani ya Chicago, sehemu ambayo Kanye West alikuwa akishinda sana na washikaji zake.
Ukiusikiliza huu wimbo amemzungumzia manzi fulani mkali sana, jinsi alivyokuwa akivaa, mwendo wake, uzuri wa sura yake na kila kitu lakini hayo yote aliyokuwa akiyazungumzia yalimaanisha mji wa Chicago na mitaa yake mbalimbali.
Hii ndiyo kazi ya sanaa aliyokuwa akiifanya Kanye West mpaka leo hii. The guys is genius sana japokuwa sometime unaweza kumuona kama hana akili.
Endelea kunifuatiliakatika channel yangu kwa kubofya link hapo chini......
https://whatsapp.com/channel/0029Vaj2egfCRs1iDmk7Bt1W.