Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  artist

YALIYOMKUTA MUUZA UJI 1--2❤🔞 01

2nd Jun, 2025 Views 68


YALIYOMKUTA MUUZA UJI 1--2❤🔞 01

Kwa jina naitwa Salome karibu katika mkasa huu wa muuza uji ili upate kujua changamoto nilizokutana nazo kwenye kazi yangu hasa ya kusumbuliwa na wanaume wakihitaji nitoke nao kimapenzi.

NB: Story hii ni kwa wakubwa tu wenye miaka kuanzia 18 na kuendelea kwa wale waliochini ya miaka 18 🔞🔞 mtupishe kidogo.

Siku hiyo niliamka asubuhi huku nikiwa na uchovu kutokana na mizunguko niliyokuwa nayo siku iliyopita. Nilitazama vyombo vyangu vilivyokuwa vichafu na kuamua kuanza na kazi ya uoshaji wa vyombo asubuhi hiyo.
Baada ya kumaliza nilikuwa na kazi ya kuanza kukologa uji pamoja na kupika chai ili niwapeleke wateja wangu.

Nilipokamilisha kila kitu niliingia mtaani huku nikiwa nimebeba chupa zangu pamoja na vitafunwa ambavyo ni vitumbua.

Safari yangu ilinipeleka mpaka sokoni kulipokuwa na soko kubwa.

Kila asubuhi vijana mbalimbali walikuwa wakipenda kwenda kwenye soko hilo kwa ajili ya kubeba mizigo na ndiyo sababu iliyokuwa ikinifanya niende kuuza ndani ya hilo soko.
"Salome umetuletea vitumbua" kijana mmoja aliongea aliyekuwa akiitwa Peter.
"Kawaida yangu Peter leo niungishe na pia unilipe pesa yangu ninayokudai" niliongea huku nikiweka vitu nilivyokuwa nimevibeba chini.

Peter baada ya kuona nimemkumbushia deni nililokuwa nikimdai aliamua kunijibu.
"Jioni njoo uchukue pesa yako kwenye geto langu Salome na ikiwezekana utanipa kitumbua cha kikubwa" Peter aliongea.

Upande wangu niliona ni kama dharau kwani moja kwa moja nilijua anataka kuniingiza kwenye mtego wa kutaka kunitia nakufanya mapenzi na mimi.
"Kwani ulinikopa tukiwa kwenye geto lako Peter? mimi sio mtoto utake kunila kizembe hivyo naomba unitafutie pesa yangu na unilipe" nilimwambia Peter na baadhi ya vijana waliokuwa wakisikiliza mazungumzo yetu walianza kunitetea kwa kumwambia Peter anilipe pesa yangu.

Baada ya maneno kuwa mengi Peter alitoa pesa niliyokuwa nikimdai na kunilipa huku akiniambia "Unabahati Salome ila siku nyingine utaingia kwenye mtego wangu na ninavyokutamani siku hiyo nitakupelekea moto ambao hujawahi kupelekewa" Peter aliongea na kwakuwa nilikuwa nimeshazoea maneno yake sikutaka kuhangaika nae.

Nilianza kuhudumia vijana waliokuwa wakihitaji uji huku wengine wakihitaji chai na kama unavyojua mazingira ya aina hiyo vijana wakorofi huwa hawakosi.

Nikiwa nimeinama namimina uji kwenye kikombe alikuja kijana mmoja na kunipiga kofi la kwenye makalio.
"Oya sister niwekee uji" aliongea baada ya kunipiga kofi la kwenye makalio.

Sikutaka kuwa mnyonge niliweka chupa yangu chini na kumgeukia kijana aliyenipiga kwenye makalio nakumpiga kofi huku nikimwambia.
"Ndiyo mpaka unipige kofi la kwenye makalio kwani uji upo kwenye matako yangu!?" niliongea huku nikiwa na hasira.
"Dah, Musa na wewe umezengua jamaa yangu, mbona sister yupo fresh tu na hana shida yoyote ile" kijana mmoja aliongea akimwambia Musa aliyenipiga kofi la kwenye makalio na wengine wote waliunga nae na Musa aliamua kuondoka baada ya kuona vijana wenzake wanamponda.

Basi baada ya mda nilimaliza kuuza na kurudi kwenye chumba nilichokuwa nikiishi.

Nilifika nyumbani na nje nilimkuta kijana akiwa kasimama akinisubiri.

Kijana huyo hakuwa mwingine bali alikuwa ni Felix aliyewahi kuwa mpenzi wangu kipindi cha nyuma.
"Eheee!!!, nini kimekuleta hapa Felix!?" nilimuuliza huku nikiweka vyombo vyangu chini nilivyokuwa nimevibeba.
"Salome kwani bado tu una hasira na mimi...!? naomba tuingie ndani basi tukaongelee ndani ili tuumaliza ugomvi wetu" Felix aliongea huku akinibembeleza.
"Uingie ndani na nani!? changanya miguu yako na uondoke hapa haraka kabra mdomo wangu haujaanza kuchanganya gia" niliongea na Felix kwakuwa alikuwa akijua jinsi nilivyokuwa muongeaji aliamua kuondoka na kuniacha mwenyewe.

Nilipumua baada ya kubaki mwenyewe na kabra sijaingia ndani kuna mpagaji mwenzangu aliyekuwa kwenye chumba chake alitoka baada ya kusikia maongezi yetu na kuniambia "Salome ungempa mda kijana wa watu maana amekusubiri kwa mda mrefu"
"Mama J mimi hilo sijali atajua mwenyewe huko" nilimjibu na baadae niliingia ndani.

Baada ya kuingia ndani nilipumzika ili ikifika mida ya jioni nipike uji kwa ajili ya kupeleka gengeni.

Mida ya jioni ilifika na niliandaa uji kwa ajili ya kupeleka gengeni, bahati nzuri aliweza kuja rafiki yangu aliyekuwa akiitwa Shamsa kwa ajili ya kunisaidia na huo ndiyo ulikuwa utaratibu wetu wa kazi.

Tulibeba vitu na kuvipeleka gengeni kwa ajili ya kuuza ikiwa ni mida ya saa moja jioni.

Tukiwa tumekaa mimi pamoja na Shamsa, mteja wa kwanza aliyekuja alikuwa ni mwanaume na sura yake ilikuwa ngeni kwetu hivyo alituomba tumuhudumie na mimi niliifanya kazi ya kumpatia kile alichokuwa akikitaka.

Baadae vijana wengine walianza kuja huku Peter akiwa ni miongoni mwao. Alifika na mimi siku hiyo sikutaka kumuhudumia maana niliujua usumbufu wake kwenye upande wa ulipaji.
"Salome naona siku hizi umeanza kuwa tajiri mpaka unakataa kunihudumia!?" Peter aliongea kwa kulalamika ila baadae Shamsa alinishauri nimhudumie.
"Shamsa huyu mtu ni msumbufu sana ila kwakuwa umenishauri ngoja nimpatie kile anachokitaka" niliongea na kumuwekea Peter uji na baada ya hapo alianza kunywa pamoja na wenzake.

Baada ya Peter kumaliza kunywa uji alinyenyuka nakuanza kuondoka pasipo kulipa pesa kitendo kilichonikera zaidi na kuamua kumuachia biashara Shamsa kwa ajili ya kumfatilia Peter.....ITAENDELEA.

Unajua kilitokea nini baada ya kumfatilia Peter? tukutane sehemu ya pili.

YALIYOMKUTA MUUZA UJI ❤🔞 02

Nilimfata na kuanza kumwita lakini alivyokuwa na dharau aliendelea kutembea pasipo kusimama.
"Huyu anataka kunizoea" niliongea na kuanza kumkimbiza lakini Peter alivyoona namkimbiza na yeye alianza kukimbia akielekea kwenye geto lake.

Alifika kwenye geto lake nakuingia ndani na baada ya mda na mimi niliweza kufika.
"Peter nipatie pesa yangu" niliongea nikiwa nimesimama nje ya chumba chake nikimsihi Peter anipatie pesa yangu.
"Njoo uchukue pesa yako huku ndani" Peter aliongea akinitaka niingie ndani ya geto lake.
"Ivi unafikiri ata nikiingia humo ndani utafanikisha kufanya kile unachokitaka kutoka kwangu!?" nilimuuliza sababu nilijua lengo lake nikutaka kufanya mapenzi na mimi kwa kutumia nguvu.

Peter aliendelea kuweka msimamo wake kuwa kama nataka pesa yangu basi niingie ndani ya chumba chake.

Kama kuna mtu atakuwa amewahi kufanya biashara nazani atakuwa anaelewa umhimu wa faida kwenye biashara na ndiyo maana usishangae kuona mfanyabiashara akikudai shingi mia.

Sikutaka kujali kama pesa niliyokuwa nikimdai Peter ni Tsh 500 na maamuzi niliyoamua kuchukua nikuingia ndani ya chumba chake huku nikiwa na lengo langu.

Nilifika na kumkuta Peter akiwa tayari ameshavua suruali yake na kubaki kwenye pensi.
"Nilijua tu lazima uje humu na leo lazima nikule Salome utake usitake" Peter aliongea kwa kujiamini.

Kwakuwa maisha ya mtaani nilikuwa nimeshayazoea, niliamua kujifunga kitenge vizuri maana nilijua vita vitakavyoenda kutokea sio vya nchi hii huku ndani nikiwa nimevaa suruali kama ilivyokuwa kawaida yangu.

Baada ya kujifunga kitenge vizuri niliamua kumsogelea Peter na kwenda kumkaba.
"Peter naomba pesa yangu!?" niliongea huku nikiwa namvuta shati.

Upande wa Peter kwake alichukulia kama faida kwani kipindi namkaba matiti yangu yaligusa kwenye kifua chake na aliamua kupeleka mikono yake kwa kunishika matiti kitu kilichozidi kunikasirisha zaidi sababu sikuwa na nyege zozote za kufanya mapenzi kwa wakati huo.

Niliona anataka kunizoa baada ya yeye kunishika matit🙄, pale pale nililianzisha kwa kuanza kumpiga huku nikitoa maneno ya kila aina.

Peter hakutegemea kama nitafikia hatua hiyo ndani ya chumba chake.
"Wewe demu msenge kweli unanipiga kisa unanidai miatano tu!?" Peter aliongea baada ya kofi langu kumpata vyema kwenye shavu lake.

Kwakuwa na yeye alikuwa ameshashikwa na hasira alianza kujibu mapigo kwa kunipiga.

Mwanaume atabaki kuwa mwanaume tu kwani Peter alinizidi na mimi uvumulivu ulinishinda na kuanza kupiga kelele kwa ajili ya kuhitaji usaidizi maana Peter alianza kunipiga kama anapigana na mwanaume mwenzake.

Kelele zangu ziliwafanya majirani waliokuwa karibu wasogee kwenye chumba cha Peter kwa ajili ya kuangalia kipi kilichokuwa kikiendelea na kwakuwa mlango ulikuwa wazi waliweza kutuona jinsi tulivyokuwa tukipigana hivyo waliamua kuingia na kuanza kutuachanisha.

"Peter kuna tatizo gani!?" Mzee aliyekuwa mle ndani alimuuliza.
"Si huyu demu ananidai miatano lakini ameanzisha ugomvi usio kuwa na sababu" Peter aliongea.
"Nyooooo, wewe mwanaume muongo sana, sitaki maneno yawe mengi nipe pesa yangu niondoke" niliongea na Peter baada ya kuona watu wanazidi kujazana aliamua kunipatia pesa niliyokuwa nikimdai na mimi niliondoka.

Nilirudi mpaka gengeni na kumkuta Shamsa akipiga story na mwanaume aliyekuwa wa kwanza kutuugisha biashara yetu.
"Salome mbona umchelewa hivyo!?" Shamsa aliniuliza.
"Nilikwambia yule mwanaume ni mpuuzi sana, alitaka kunibaka kwa lazima ndani ya geto lake" niliongea na kumsimulia kila kitu Shamsa bira kujali kama kuna mwanaume aliyekuwa akisikiliza story zetu ambae ni mteja.

Baada ya kumaliza kumsimulia Shamsa mwanaume aliyekuwa akisikiliza Story zetu aliamua kuongea.
"Nipeleka kwa huyo kijana aliyetaka kukubaka" aliniambia na mimi nilifikiria na baadae nilikubali kumpeleka kwa Peter.

Tukiwa njiani tukielekea kwa Peter wote tulikuwa kimya kutokana na sisi kutokuzoeana na kijana niliyekuwa nikiongozana nae alionekana sio muongeaji sana.

Tulifika na bahati nzuri tulimkuta Peter.
"Wewe malaya umeijia nini tena!?" Peter aliongea baada ya kuniona na hakujali kama kuna mwanaume niliyekuwa nimeongozana nae.
"Kijana kwa usalama wako piga magoti" kijana niliyekuwa nae alimwambia Peter.
"Wewe mjinga nini!? nani apige magoti!? emu tokeni hapa kwenye geto langu" Peter aliongea na kutaka kuingia ndani lakini kijana niliyekuwa nimeongozana nae alitoka kwa kasi na kwenda kumshika Peter nakumvuta kwa nguvu.

Peter baada ya kuvutwa alianguka mpaka chini na alivyokuwa mbishi alinyenyuka kwa ajili ya kupigana nae lakini Peter alianza kupigwa kama mtoto na baada ya mda alitulia.

Kijana baada ya kumuona Peter ametulia alijitambulisha kuwa yeye ni mwanajeshi na kutokana na kile alichokionesha Peter alitaka kumchukua kwa ajili ya kumpeleka kituoni lakini kwa upande wangu moyo wa huruma uliniingia nakuamua kumzuia asiondoke na Peter.
"Naomba umuache naamini atakuwa ameshajifunza" nilimwambia Mjeda aliyekuwa amemshika Peter.

Mjeda alikubali kumuachia Peter na baadae tuliondoka na kurudi gengeni huku nikimshukuru kwa kile alichoamua kukifanya mbele ya Peter.
"Ingekuwa vizuri kama ukinipatia namba zako kwa ajili ya usalama zaidi" mjeda aliongea na mimi sikutaka kumnyima zaidi ya kumtajia namba zangu za simu....ITAENDELEA..
   

SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


mjukuu rewards 100 Comments 0
 

PART 5 MY HEART

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MY HEART 03--04

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

*MY HEART* *1---2 *

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MIMBA YA BESTMAN 7

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

ANIPHA 6--7.

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MIMBA YA BESTMAN 05

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

side chick episode 3

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

SIDE CHICK EPisode 2

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 18

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 17

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 16

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 8

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 1

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

RATIFA Sehemu ya 32

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

JINA LANGU SHAMSA EP3

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

JINA LANGU SHAMSA EP2

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

JINA LANGU SHAMSA EP1

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

BOYCHILD PART 3

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

DRAMA OF LOVE part 4.

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

DRAMA OF LOVE part 3

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

NJERI part 29

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

LOVE Part 1

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

NJERI part 28

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

NAWASHWAA Sehemu nne.

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

NJERI part 26

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest