*BINTI MPELELEZI*
SEHEMU YA....18
Na
Mamuh Mohd
(0716730000)
Tulipoishia......
Kumfuatilia alipata uhakika kuwa Kosho wamemteka na isitoshe amesema ukweli...
SONGA NAYO......
"Natakiwa kutumia dhana zangu za siri sasa kufanikisha hili.
Hakuna pengine ambapo wanaweza kumteka Kosho kama sio msituni kule ngoja nitajua".
Yenah aliangaza kutafuta namna ya kutoka katika kasri ile.
Binti hakuwa mtu wa kawaida amepitia mafunzo ivyo ana mbinu nyingi nyingi sana kwake hakuna ambacho kilimshinda.
Binti aliamua kutoka kawaida tu tena alitumia gari si alijua kuendeshwa mwenyewe.
Wanamtambua sasa walinzi wote ivyo hawakumuuliza kitu.
Alielekea msituni kabisa kuna njia ambazo alipita kwanza kuna mahali ambapo alikuwa amefukia vitu vyake vya kazi sasa alienda kuvitoa.
ilikuwa ni darubini na silaha Pamoja na mavazi ya kazi.
Alitunzaga hivyo vitu kwa siku nyingi na ilibaki kuwa siri yake.
Sasa aliamua kuvitumia kwa ajili ya kazi yake hiyo maalum.
Himaya haikuwa na misitu mingi, msitu ulikuwa upo eneo moja tu.
Basi binti nae hakutaka kupoteza muda haraka alielekea huko.
Alikuwa akitumia darubini yake kuangalia vizuri vitu kwa umbali kupitia kila kona.
Basi alifanikiwa kuona Sehemu ambapo mazingira yalimuonesha kuwa kuna kitu kinaendelea.
Yenah bila kupoteza muda aliwahi Sehemu hiyo huku akiendelea kuangaza akitumia darubini yake.
Upande wa malkia alikutana na Sultan akiwa anaangaza kumtafuta yenah.
"Mmewangu sina muda wa kupoteza leo nina ushahidi huyo yenah unaemfuga ndie nyoka hafai hapa ndani.
Sasa twende mwenyewe ukajionee".
"Mpaka lini utaacha kumuandama mwenzako kinachokuumiza haswa ni mimba au?"
Mmewangu nipe hii nafasi haitajutia na ikitokea nakudanganya basi fanya uamuzi utakaotaka".
Sultan kuambiwa vile basi akamuambia malkia waende sasa akamuoneshe huo ushahidi.
Walifika hadi kwa dereva samwel Ndipo malkia akamuambia awapeleke kule msituni ambapo hapakuwa mbali sana na pale sema kwakuwa ni viongozi hawawezi kutembea.
Samwel aliendesha gari lakini huku akikumbuka kipigo alichokipata usiku ule na mtu ambaye hajamfahamu ni nani.
Alijiona kama ameponea chupu chupu hana hamu.
Basi wakati huo yenah alifika eneo na kumkuta Kosho amefungwa kuna vijana wakimlinda pale.
Binti wakati huo alivalia nguo za polisi na kujifunika kwa mask hadi usoni huku ameshika silaha ya moto.
Vijana wale waliogopa eeeeh sio kawaida.
Yenah ndipo akawaambia mtafuata maelekezo yangu haya mfungueni huyo kijana haraka.
Basi walimfungua pale huku wanatetemeka sio kawaida.
"Nawaacha sababu hamna hatia mmetingwa na mtu ila mkiingia tena katika anga zangu kunifuatilia hakika nitawadhuru.
Sipo peke yangu tupo wengi sana mkithubutu kusema chochote baada ya hapa hakutakuwa salama nawahakikishia".
Yenah palepale akahisi kama kuna ujio wa watu Sehemu hiyo.
Haraka akatumia darubini yake kuangalia ndipo akamuona Malkia na kijakazi wake akiwa na sultan wanakuja Sehemu hiyo.
Yenah akamshika mkono Kosho na kuwaambia tena vijana wale,
"Silaha hii ninayo lakini nawaacha kwa sababu sasa mjichanganye kusema chochote muone hakikisheni mkiulizwa chochote Mnakana".
Kisha waliondoka seehmu hiyo kwa kupitia upande wa pili kabisa.
Walifika mahali Yenah akajificha na Kosho wakawashuhudia malkia na sultan wanaelekea Sehemu.
"Tumewahi bila shaka malkia anakwenda kumpeleka sultan akijua wewe upo utasema ukweli".
"Ahhh yenah umejitahidi sana sijui ingekuwaje jamanii".
"Usijali".
Walipopita nao waliinuka na kuondoka zao.
Sasa malkia pozi lilimuisha kufika wanakuta vijana wale wamekaa tu Kosho hayupo.
"Nyie yule mfungwa tuliemfunga yupo wapi? Anatakiwa kusema ukweli".
Mmoja wa vijana wale akajibu,
"Mfungwa yupi? Hakuna mfungwa yoyote wewe umetuweka hapa umesema sijui tuongee vitu gani hatuelewi kwa kweli".
"Acheni mambo yenu...semeni ukweli wa kilichotokea".
"Malkia hatuwezi kusema uwongo unaoutaka bana".
Wote walishangaa hata malkia na kijakazi wake walibaki pozi limewaisha jumba bovu limewaangukia....
Full 1000.
Whatsapp no 0716730000
Sijui itakuwaje?
Tukutane Sehemu ya 19.