Story………………...SHE WAS MY WIFE (ALIKUWA MKE WANGU)
Mtunzi……………..Simulizi Za Zooper
Sehemu...ya......01
WhatsApp……....0613083801
Umri………………...18+
ENDELEA.........
Saa12 jioni ndiyo mida yake ya kutoka kazini na kuelekea nyumbani kwake, mkononi alishika mfuko uliokuwa na dagaa ndani pamoja na nyanya chungu akiwa na tabasamu pana usoni, alitembea haraka huku akiwa kainamisha kichwa chini kama mtu anayetafuta pesa aliyoidondosha na baada ya dakika kadhaa alifika na kukutana mlango umefungwa kwa nje na kusogea mpaka sehemu inapokaa funguo na kuichukua na kuufungua mlango.
Macho yalimtoka baada ya kutokuona nguo za mke wake anayeitwa Bibiana, haraka alichukua kimeo chake kilichochoka na kuchakaa na kujaribu kumpigia ila simu ilikuwa haipatikani na wazo alilolipata ni kumpigia mama mkwe wake na bahati nzuri simu ilipokelewa.
"Mama shikamo Bibiana yupo huko!?"
"Hapana hajafika kwani kuna nini!?"
"Sijakuta nguo zake na hapatikani kwenye simu!"
"Usinilete matani wewe kijana namtaka mwanangu"
"Dah!"
"Sio dah, wewe ndiyo unaishi naye sasa unaniuliza alipo mimi najua?"
"Basi samahani mama"
Pozi lilimwisha baada ya mama mkwe kumuwakia na kuamua kukata simu.
"Huyu demu vipi mbona anataka kuvuluga akili yangu mimi aaaaaah"
Alilalama na kumpigia swahiba wake wa karibu.
"Oya umeshafika home!?"
"Aise kuna msala huku!"
"Upi tena!?"
"Bibiana katoroka!"
"Au karudi kwao!?"
"Sidhani maana nimempigia mama mkwe kasema hayupo!"
"Nakuja hapo gheto sasa ivi tu!"
"Poa poa!"
Baada ya mda alifika na kumkuta swahiba kavulugwa.
"Oya Niko eeeh au ulikorofishana naye!?"
"Wapi sasa!?, asubuhi nimemuacha kalala narudi nakuta hayupo!"
"Dah sijui atakuwa wapi tu, twende kwa yule binti wa jirani anayependa kumsuka"
"Poa poa!"
Waliongozana na walipofika huko binti alisema hajui ni wapi Bibiana alipo.
Hali ilikuwa sio shwari kwa Niko baada ya kumkosa Bibiana, miezi ilikatika pasipo kumpata na cha kushangaza Mama Mkwe wake hakuwahi kumpigia simu kwa ajili ya kumuulizia, siku moja Niko na Ben walichukuana na kuelekea ukweni na kumkuta Mama mkwe.
"Mama shikamoo!"
"Marahaba!"
"Umeshapata taarifa za Bibiana!?"
"Msahau na usiendeleee kumtafta tena!"
Mama Mkwe aliongea.
"Kwanini Mama!?"
"Wewe elewa nilichokwambia"
"Kwani Bibiana yupo wapi!?"
"Ivi huelewi nilichokwambia au!?"
"Oya Niko tuondoke"
Ben alimvute akimtoa ili asizidi kuharibu zaidi.
"Bora wewe nimwelewa kuliko mwenzako na kama ningejua nisingekubali mwanangu aishi na kudume suruali kama huyu ambaye hakuwahi hata kutoa ile shingi mia kama mahali"
Mama mkwe baada ya kuongea alirudi ndani.
"Huna chako hapa jamaa yangu tuondoke tu"
"Siamini kabisa Bibiana ndiyo wakunifanyia ivi!?"
"Nyie mnanipigia kelele!"
Sauti ya Mama mkwe iliwakulupua na kuwafanya waondoke na baada ya mda Niko alifika kwenye gheto lake akiwa pamoja na Ben.
"Kaza roho jamaa yangu wewe ni mtoto wa kiume!"
"Nipo fresh mbona"
"Basi poa tutachekiana!"
Macho ya Niko yalimtazama Ben aliyegeuka na kuondoka na baada tu ya kutoweka aliingia ndani na kukitazama kitanda alichokuwa akikitumia kulala na Bibiana.
Kitanda kilimkumbusha mbali hasa siku ya kwanza aliyombikir..i na kumkaribisha kwenye ulimwengu wa mahaba, mambo mazito aliyakumbuka Niko aliyofanya na Bibiana na kusogea zake kilipokuwa kitandani na kujilaza huku akiwaza na kuwazua.
"Kumbe ukapuku mbaya ivi yaani ufundi wote ule kwa Bibiana ila bado kanikimbia tu duh, sijui atakuwa wapi sasa ivi ila fresh tu haya yatapita!"
Mawazo yakujifariji yalipita kwenye kichwa cha Niko akimuwaza Bibiana.
Miaka miwili ilikatika na Niko aliyasongesha maisha pasipo kuwa na uwepo wa Bibiana, bahati mbaya kwake mambo badala ya kunyooka yalikata kona na kupinda balaa, kila kitu kiligoma na mambo yalikuwa hayaendi kabisa. Akili ya Niko iliwaka moto baada ya kazi aliyokuwa akiifanya kufa na hakukuwa na kazi tena ila Ben alipata wazo na kushauriana naye kitu gani wafanye.
Makubaliano yaliyopita ni wao kwenda kujifunza ufundi wa kuendesha magari makubwa kwa madogo walau waweze kupata dili za hapa na pale za kuyafanya maisha yao yasogee, walijichanga na kwenda kwenye mafunzo na baada ya mda walimaliza na kilichokuwa kimebaki kwao ni kila mtu kupambana kivyake kutafta madili ya kazi.
Bahati kwa Niko alipata kazi kwa moja ya don mkubwa aliyemwahidi kumlipa mshahara mnono tu, alibeba kile kilichokuwa chake na kuhamia kwenye nyumba ya tajiri yake iliyokuwa mbali na yeye alipokuwa akiishi.
"Kijana karibu sana hapa ndiyo kwangu!"
"Asante boss!"
"Nadhani nimeshakupa maelezo kuhusu kazi yako!?"
"Ndio boss"
"Utakuwa unalala kwenye chumba cha nje anacholala mlinzi na usisahau kila siku asubuhi kuamka na kuyafanyia usafi magari yangu"
"Nimekuelewa boss!"
"Oky, kazi yako ya kwanza ni kwenda kumchukua mke wangu yupo safarini na sio mda atafika kwenye kituo cha magari!"
Niko alikubali na kuondoka kwenda kuianza kazi yake kwa mara ya kwanza, alipanda moja ya gari la boss wake na kuanza kuendesha lakini ndani ya gari aliongea kimoyo moyo kuwa watu wanapesa na wanajua kuzichezea hasa, inakuaje mtu anashukia kituo cha magarii kilichokuwa karibu tu ambacho angeweza kuchukua boda boda kwa bei ya chini itakayomleta sehemu husika mpaka yeye ahangaike kumfata na gari? lakini haikumfanya aache kufanya kazi iliyomleta.
Aliendesha gari taratibu ili asije kuharibu mambo na ukizingatia ndiyo siku yake ya kwanza kazini na baada ya mda alifika na kupaki gari yake pembeni na kushuka ndani ya gari, macho ya watu yalikuwa kwake kutokana na gari ya gharama aliyokuwa nayo kitu kilichomtia kiburi Niko baada ya kuona watu wanamwangalia kila mara na alipokuwa amesimama yeye alipita binti aliyekuwa kafungasha balaa na kumfanya Niko ameze mate na kumwita.
"Unaniita mimi kaka!?"
Binti aliongea na kugeuka nyuma kuangalia kama kuna mtu mwingine aliyekuwa akiitwa na Niko.
"Ndio wewe!"
Angeanzaje kulinga baada ya kuitwa na Niko aliyekuwa kasimama nje ya gari la thamani.
"Abee kaka!"
Niko alimtazama kuanzia chini mpaka juu na kuongea.
"Nimeku..penda nipe namba zako"
"Mmmmh aya andika!"
Alitoa kimeo chako nakutaka kumpa ila alisita ili maswali yasije kuwa mengi kwa binti ya kwanini yupo na gari ya gharama ya kifahari alafu anakimeo kilichochokeana.
"07.....
Binti alimtajia na baada ya kumaliza aligeuka na kuondoka na Niko aliisave namba yake lakini pale pale simu yake iliita na kuipokea.
"Hello!"
Sauti ilimwacha hoi Niko kwani haikuwa ngeni kwake.
"Hello!"
Alimjibu kwa hofu kubwa huku moyo wake ukienda mbio.
"Upo wapi nimeshafika tayari na nimepewa maelezo na mme wangu utakuja kunichukua!"
"Nipoo...
"Acha tu nimeshakuona nakuja hapo!"
Simu ilikatwa lakini Niko bado aliendelea kuiweka simu yake sikioni akiwa haamini baada ya kuisikia sauti ya mtu ambaye hakumtegemea kabisa............ITAENDELEA..