PENZI LA GANGSTAR
(sio lazima unipende nikikupenda mimi inatosha ) 1
HUSQER BALTAZAR
Kuna vitu unaweza usiamin kama vinaweza kumfanya mtu akakupenda sana mpaka akapagawa, muda mwingine huyo mtu ambae hatukutegemea kabisa kama anaweza kumpenda mtu kama wewe…
Siku moja nilikuwa natoka zangu nyumban, hapo nimegombana na mama yangu wa kambo, kanitukana sana na hata usiku wake hata sikula hivyo wakati naamka asubuh akanambia kuwa anataka nibandike chai na nioshe vyombo, hata sikumjibu maana hata usiku sikula, yaan wale wao alafu vyombo nioshe mimi wewe kuweza, nikaondoka akawa ananitukana ila hata sikumtilia maanani, maana kwanza siku hio nilikuwa natakiwa kwenda kwenye interview, maana nilikuwa nataman sana kuhama nyumban,maisha ya mama wa kambo mwenye roho mbaya kama huyu ninaeishi nae sio poa kwa kweli……
Sasa nikiwa njian si ndio nikamuona mdada anasutwa balaa, akawa amekaa chini analia, nikasogea mpaka pale alipo kisha nikamnyanyua na kumuambia aondoke, si ndio binti mmoja akadakia na kusema “ unajua huyu katufanyia nini, embu acha kuingilia mambo yasiokuhusu wewe mchawi mwingine…
“ ndio nimeshaingilia sasa utanifanya nini, nikaongea kwa sauti ya ukali kidogo, nikashangaa wanacheka kinafki na mmoja akasema “ na huyu tumuingize ili ajute kuingilia mambo yasiyomuhusu maana anajishaua sana, akasema mmoja wa wale mabinti, ila hata sikumjibu nikamuinua Yule bint na kutaka kuanza kuondoka nae…
“ wewe changudoa ulielaaniwa muache huyo muasherati hapo chini haujui alichotufanya, mwanamke mnafki kama nini, unajifanya unaingilia unajua sisi ni akina nani mpaka unaingilia ngoma zisizokuhusu, akasema bint mwingine na mimi nipo kimya naanza kuondoka zangu maana sikutaka kubishana na watu, ila sikuona sawa kumuona mtu anaonewa tena barabaran kabisa, niliona sio ustaarabu hata kama amefanya makosa kiasi gani….
Wale mabint walipoona kuwa siongei nao naondoka na yule waliokuwa wanamchamba kimya kimya wakawasha vile vispika vyao na kuanza kuimba zile nyimbo za mafumbo wakaanza kusema “ na yeye yumo nay eye yumo matako hana anakalia kiuno, wakiwa wanamaanisha kuwa yule dada hana makalio anachotumia kukalia ni kiuno sie kimya …
Mara wakabadilisha nyimbo wakaanza kuimba “ ngedere nipe sura yangu nimtishie mwanangu, ngedere nipe sura yangu nimtishie mwanangu, huyu nae vipi mbona sura ngumu ni ngedere nyani, sikujua walikuwa wanamlenga nani, maana hakukuwa na yoyote kati yetu ambae alikuwa ana sura mbaya, maana ni kweli Yule dada ambae walikuwa wanamuimba, hakuwa na shepiu ila sura mashallah…
Sasa mmoja akajichanganya akaja kunizodoa, aiseee nilimshika mkono nikamkunja, hakuamin macho yake, wenzake wakataka kuingilia wakahisi wananiweza, sijui hata zile style za shaulin soka nilizotoa wapi, maana niliwatembezea kichapo kama jakchain, yaan ni mwendo wa kuruka nao tu, mpaka nakuja kutulia wote wamekimbia na watu wametuzunguka wanashangilia, Yule dada ambae nilikuwa namsaidia akanifata kisha kwa sauti ya upole akasema “ nisamehe sana kwa kukuingiza kwenye ugomvi wangu ila nashkuru sana kwa kunisaidia….
“ usijal, ni jukumu langu kumsaidia kila anaeonewa, nikasema na Yule binti akatabasamu kisha akanambia kuwa yeye anaitwa angel na mimi nikamuambia kuwa naitwa scholastica ila anaweza kuniita tu skola, basi tukaagana pale kumbe zile harakati zote zile kuna mwamba alikuwa ananiangalia tu, akawa anaangalia namna ambavyo niligeuka john cena dakika za kuhesabu ila sikumuona, nikaendelea zangu na safari yangu…
Nikakuta nimechelewa kwenye interview kwa hio hata sikuweza kuingia ndani, nikawa najiambia kuwa mungu hawez kuniacha maana anajua kuwa nilikuwa natenda msaada hivyo lazima atanisaidia, ingawa nilikuwa najipa moyo ila nafsi yangu ilikuwa inaniuma sana, maana kukaa na mama yangu wa kambo sio jambo rahisi maana ana vituko zaidi ya vituko vya jini yaan, nikiwa natembea tembea mara mvua ikaanza kunyesha, kikawaida huwa natembea na kikoi, sasa nikakitoa kikoi changu na kujifunika, nikafika eneo moja ambapo hakukuwa mbali sana na sehemu ambayo nilikuwa nimeenda kuombea kazi, kwa maana ni yale majengo ambayo ni maghorofa tu hakuna nyumba za kawaida, hivyo kumetulia sana…
Nikatafuta sehemu nikasimama maana mvua ilikuwa kubwa kidogo, mara nikashangaa namuona mtu anakimbia kuja upande niliokuwepo, aliponiona akaingia ndani ya kikoi changu kisha akavua vuatu na suruali yake akaweka ndani ya mkoba wangu akabaki na boksa, akanilaza chini, yaan mambo yote yalikuwa yanaenda haraka sana kiasi kwamba sikuwa naelewa hata ni kitu gani kilikuwa kinaendelea…
“ anza kuguna, anza kuguna haraka sana, akasema nikawa sielewi, nikashangaa ametoa kisu kisha akasema utaguna huguni, tena uniite majina matamu, sikuwa na namna zaidi ya kufanya kile ambacho alikuwa anataka nikaanza kusema “ auchi ahhhhh mume wangu, tamuuu ahhhhh tamuuu shiiit, nikashangaa anaanza kunikiss, ghafla wakawa wanapita watu na ilikuwa mchana, ila Yule kijana alikuwa amejifunika kikoi changu akawa anapanda juu na kushuka chini kana kwamba ananikula kumbe sio kweli, na kwa aina ya lile eneo lilivyo ni ngumu watu kupita pita, hivyo hata wale ambao walikuwa wanapita walipoona kuna muhuni anakula uroda wakaona wasimkatishe utamu mwanaume mwenzao wakaendelea zao kukimbia kana kwamba kuna mtu walikuwa wanamtafuta….
Walipopita Yule mwanaume akaamka haraka sana kisha akaanza kuvaa nguo zake haraka haraka kisha akasema “ ni mara ya pili tunaonana na tumai tutaonana mara nyingine nyingi zaidi, kisha akaniachia business card yake na kusema “ kesho mapema sana naomba ufike kwenye kampuni ya Nuresh campany nitakulipa kwa wema ulionifanyia leo kisha akaondoka zake…..
Nilibaki nimetoa macho ila kwenye swala la kulipwa ndio nilipopaelewa, maana sikuwa nataka kabisa kurudi nyumban, maana kukaa na yule mama ni bora hata kukaa na mzimu, basi sikutaka hata kurudi nyumban, nikajiambia kuwa nitaenda kwa shoga yangu na kutakapo pambazuka niende kwa kwa huyo mwanaume aliposema huenda nikapata hata mtaji wa kuchoma mahindi…
Kweli nilikuwa na rafiki yangu mmoja alikuwa amepangisha na alikuwa anafanya kazi ya mama ntilie tu, nikamfata na kuomva kulala kwake, maana nilishaapa kuwa sitakaa nirudi nyumban tena mimi, na kweli akakubali, basi nimelala ila akili mwangu nawaza namna ya kufika kwenye hio nuresh kampan…
Basi asibuh kulipopambazuka mimi ndio nikawa wa kwanza kuamka na haraka haraka nikaanza kujiandaa kisha nikachukua simu yangu na kuanza kupiga kwenye ile namba ambayo nilikuwa nimepewa, ilikuwa ni asubuh sana hivyo nilikuwa naongea kwa sauti ya utulivu sana wakati ambapo simu ilipokelewa…
“ hallo nani mwenzangu, upande wa pili uliongea mara baada ya kupokea ile simu ambayo niliipiga…
“ mimi ndio Yule dada ambae ulinambia kuwa nikutafute jana kwa kuwa nilikusaidia, sasa sijajua kampuni yako ilipo hivyo kama hautajali naomba kujua ilipo nije, nikasema kwa sauti ya utulivu sana, nikasikia upande wa pili unasema “ kum*mak*, kumbe wewe Malaya unasauti tamu hivi, yaan hapa nilipo mpaka nimesimamisha aiseeee, guna basi kidogo nitakuongezea malipo, akasema Yule mwanaume, nikashangaa huyu mwanaume vipi, yaan mimi nilikuwa nataka msaada kuhusu msaada nilioutoa alafu mtu anakuja kunambia maswala ya kuguna guna weee kuweza…
“ samahan kama hauwez kunisaidia basi, naomba nikutakie asubuh njema nikasema ila kabla sijakata simu nikasikia upande wa pili unasema “ hauna mamlaka ya kunikatia simu mimi, guna kidogo nitakupa pesa yoyote unayotaka mamaaaa, akasema…
Nikaona huu upuuzi, nikaanza kuhisi labda nimekutana na muhuni tu, na huenda nisilipwe nikakata zangu simu na kuanza kuona hakuna cha msaada wala kitru gani ambacho ningeweza kukipata….
Basi pozi lote la kwenda kwenye kampuni kulipwa likakata, shoga yangu yeye akajiandaa zake kisha akaenda kwenye mihangaiko yake, sasa ile natoka tu nashangaa magari mawili meusi yanakuja kupaki pemben ya nyumba ambayo nilikuwa naishi, tena zilikuwa ni range nyeusi, mara nikasikia mlango unagongwa nikajua ni wageni wa shoga yangu, nikaenda kufungua nikashangaa nakutana na sura ya Yule mwanaume ambae nilimsaidia, nikiwa bado nashangaa shangaa pale akapitiliza mpaka ndani kisha akawa kama anakagua kagua kisha kwa akanisogelea na kusema “ hii sio sehemu sahihi kwako..
“ unataka nini na kwanini unafatilia maisha yangu, naomba uondoke, nikasema..
Akacheka sana kisha akasema “ kuondoka, unahisi kuwa nitaondoka hapa, yaan leo umenifanya nimesimamisha kirahisi rahisi lisaa lizima alafu unaniambia maswala ya kuondoka, mwanamke wangu hawez kukaa sehemu kama hii, embu jiandae tuondoke, akaongea kwa sauti ya mamlaka….
Nikajikuta nimetoa macho maana sikuwa najua nimeanza kuwa mwanamke wake lini……..
NAKUJA…….
Likes zikifika 2000 napst kiande kingine, hakikisha unasharebkwa kadri yabuwezo wako.