Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  artist

SIMULIZI YA MAISHA: NILIMUUA MAMA YANGU MZAZI ILI NIOLEWE NA BABA | EP 44

7th Jun, 2025 Views 62

SIMULIZI YA MAISHA: NILIMUUA MAMA YANGU MZAZI ILI NIOLEWE NA BABA | EP 44

Na Sam Darfur 0717255498

RECAP: SEHEMU ILIYOPITA
Ilikuwa ni kauli ambayo hakuna ambaye angetarajia kama ningeitoa kwa wakati ule, hata Betrice mwenyewe hakujua kama ningesema kwamba nahitaji kampuni. Alinitazama huku akiniuliza kwa ishara ya mikono nami nilimuonesha ishara kwamba kila kitu kipo sawa. Nikamwambia.
“Nipe kampuni yangu. Mwisho wa kikao tunaweza kuondoka sasa” maneno yangu tisa yaliwaacha watu katika sintofahamu lakini nilimaanisha kile ambacho nilikuwa nimekiongea…

SEHEMU YA 44
Mmepunguza kuweka Like, msiww hivyo jamani... Ebu Like twende pamoja.

Nilimuona mjomba akisimama, kijasho kilikuwa kinamtoka huku misuli ikisisimka katika mwili wake. Alinitazama kuanzia juu hadi chini kisha akamtazama Mzee Jawan ambaye alipigwa na butwaa.

Kwa upande wake hakuwa anaelewa kwanini nilichukua maamuzi kama yale tena kwa ghafla mno. Aliniuliza.
“Alvila kuna nini?”
“Muulize huyo Loy anajua anachokifanya juu yetu, anakula samaki halafu anamsingizia paka kisa anapenda shombo?”” Nilisema huku nikimnyooshea kidole Loy ambaye alizidi kutetemeka.
Alijikuta anataka kuongea lakini maneno yalikuwa yakimporonyoka sio moja wala mbili ambalo lilikuwa likija akili mwake.
“Loy kuna nini ambacho unakifanya hadi
Alvila achukue maamuzi haya?” Mama
Brandina aliuliza
“Loy mchawi anataka kuwauweni ninyi nyote” alisema Betrice kwa sauti kidogo
“Unasemaje wewe mpumbavu?” Loy alikuja juu
“Umesikia, ebu usinichoshe bwana” Betrice alijibu kwa nyodo huku akitingisha kichwa chake.

Mama Brandina alitafakari kwa muda, ndani ya kichwa chake kulikuwa na maswali juu ya kile ambacho kilikuwa kikiendelea lakini alikosa majibu mwisho aliamua kufunguka ili kujua ukweli.
“Nini kinaendelea Alvila?”
“Loy utasema au niseme mimi?” nami nilimuuliza Loy “Kusema nini?”
“Ulichozungumza na mke wako mara baada ya mimi kukupigia simu kisha kukupa habari za kifo cha Brandina”
“Hakuna, hakuna kitu ambacho niliongea zaidi ya kusema kwamba nakuja hospital lakini kwa bahati mbaya ratiba ziliingiliana” alijibu huku akiwa anatetemeka mno.

Nilitingisha kichwa changu kutoka kulia kwenda kushoto kuharishia kwamba kile ambacho alikuwa akikiongea hakikuwa na ukweli ndani yake, niliamua kumtwanga swali la pili.
“Kikao cha mwisho ambacho tulizungumza kuhusu kampuni, mke wako alipandikiza nini katika shingo ya Brandina?”
“Hilo halinihusu labda yeye angekuwepo”
“Linamhusu la kula kuku, kuku, kuku” Betrice akidakia kwa kukumbushia kauli ya Loy baada ya kupa taarifa ya msiba
“Nawe kelele” Mama Brandina alisema kwa hasira mno.
“Muache anaajua anachokisema” Nilimtetea
Betrice

Betrice ilibidi akae kimya, alinitazama na kunikonyeza huku akinisisitizia kwamba niendelee na maswali yangu. Nami niliona nina kila sababu ya kufanya hivyo nikauliza.
“Fine, achana na hilo swali nakuuliza lingine. Jana wakati tumeweka kikao cha nani ambaye atakalala katika chumba cha maiti. Mke wako alitakiwa kulala katika kile chumba?”
“Hapana haikuwa hivyo lakini pia halinihusu”
Alijibu Loy
“Kwanini sas alikuja kulala?” Betrice aliuliza
“Nimesema kelel wewe binti” Mama naye alikuja huu huku akimtazama Betrice “Unachekesha na unatia hasira, anyways la mwisho. Kwanini mke wako aliondoka hapa mara baada ya kukucha tu?” nilimuuliza Loy
“Anasema kwamba anaumwa”
“Unajua anachoumwa ni nini?” nilimuuliza
Swali hili lilimfanya awe kimya haswa, hata kujibu kwake kulikuwa ni kugumu zaidi ya kigugumizi ambacho kilimkumba.
“Hah, hapa, ndio hapana” alisema
“Ok, sisi hata hatuna shida na mke wako, wala hatuna shida na wewe ila tunataka kampuni yetu” nilisema haya huku nikitoa simu yangu tayari kwa ajili ya ku-play sauti yake ambayo alikuwa akiongea kuhusu kufurahia kifo cha Brandina.

Nilimtazama Betrice nilimuona akiweka tabasamu. Nikamtazama Mzee Jawan niligundua kwamba alikuwa haelewi nataka kufanyaje na mwisho kabisa nikamtazama Mama nikasema.
“Kila kitu uzaliwa kikiwa na sababu ndio maana wanaosema Mungu yupo watakuambia kwamba yupo kwa sababu kuna vitu ambavyo ameviumba na haviwezi kujizalisha tena, mfano mlima.
Kikawaida chuki huzaa chuki, upendo huzaa upendo, huruma huzaa huruma hata huzuni pia itazaa huzuni. Nilitokea kumpenda Loy kama sehemu ya familia yangu, nilitokea kum’heshimu na kumfanya kuwa namba moja ya watu ambao nitawaondoa kutoka katika umasikini hadi kuwa Tajiri na kutambulika hapa Dar es salaam lakini kwake hakutaka upendo wetu badala yake alituonesha chuki.

Chuki hii sijui alipandikizwa au aliitengeneza mwenyewe lakini leo hii inatufanya au inanifanya hata mimi niwe na chuki. Betrice ni miongoni mwa marafiki zangu wakubwa sana, hakuna ambacho sijamshirikisha kuanzia kumwambia kwamba tunataka kwenda kwa mganga ili kumtibu Brandina ila chakushangaza mjomba alikataa hadi kumpanga mpango wa kwenda Kenya
Kumbe katika kurupushani na pirika pirika za kutaka kuokoa maisha ya Brandina, kuna watu ambao walikuwa wanatuchora, wanatuchota nyota. Wakati sisi tukiamini kwamba Brandina alikuwa anaumwa maradhi ya kawaida ambayo yalitokana na msongo wa mawazo kumbe nyuma yake kulikuwa na uchawi.

Naomba ni play hii sauti mpate kusikia” niliweka kituo cha mazungumzo yangu, nika-play ile sauti.
“Mke wangu tayari mmoja katangulia! Leo tunakula kuku, kuku, kuku”
“Uwi! Si nilikuambia dawa mimi naijua sasa ngoja nikaandae nyingine ili nimpe Alvila naye atakufa siku si nyingi”
“Mungu wangu simu sijakata” nilisimamisha sauti kisha nikasema.
“Nina kila sababu ya kukuua na kukufaya jambo lolote baya ila naheshimu nimeona nilichokifanya kwa Mama yangu hapo kabla kinatosha sitaki nikuue. Unaweza nipa funguo na vitu vyangu vingine”
Mjomba alitetemea, alikuwa kama kuku ambaye amemwagiwa maji. Akili yake ilishindwa kufanya kazi, hakuamini kama kweli anayoyasikia ni maongezi yao.
“Nisame, nisamehe” alisema
“Too late, huwezi hata kurudisha maisha ya
Brandina hapa” Betrice alisema “Nimekusamehe mbona mjomba, tena nimekusamehe sana tu.

Sikutaka hata kukuua maana ningeamua ningefanya hivyo. Mke wako nahisi ingawa sina hakika sana kachukua nywele zangu au Betrice kamwambie kwamba sisi ni minabii hawezi kutuua nipe hizo gunguo” nilisema kwa jazba na kumpokonya Mjomba funguo za kampuni ambazo alikuwa ameshika mkononi.
“Hata akienda kwa mganga ataambiwa tumeshakufa” Betrice alisema huku akifunga mtandio kiunoni ili kuweka kijora chake sawa.

Sio Mama Brandina wala Mzee Jawan ambaye alishindwa kuungana na mimi katika maamuzi ambayo niliyachukua. Niliona wakinipigia makofi kisha Mama Brandina akasema.
“Loy kama umasikini umeutaka mwenyewe, sidhani kama kuna mtu ambaye anaweza kukufanyia hivi kiustarabu. Umeondoa maisha ya Brandina ambaye alikuwa na ndoto zake, alikuwa na shauku ya kufanikiwa nenda tu hata mimi sina cha kukutetea”
“Kweli, kama alivyosema mke wangu hapo. Mie ndio kabisa maana natamani hata kukuua fanya kuondoka tu.”
“Yaani hana hata aibu ona aliposimama pale na lisuruali lake, kama kuroga si wangeroga hawa ambao wapo hapa ila wewe kha” Betrice aliangua kichambo cha kufa mtu.
“Uzuri ni kwamba nyaraka zote niko nazo, nyumba, kesho narudisha kwa wenyewe hata kama nilipanga kwa miaka mitatu, kuhusu gari nitalifuata na vikorokoro vingine vyote” nilimwambia Mjomba.

Mfano nikikuambia tunayoisoma ni season ya kwanza ambayo naiuza kwa 3000Tsh utanielewa...!? Mbele bado season nne yaani season 1,2,3,4 na zote nauza kwa 3000Tsh kwa kila moja. Lakini, leo ukipia 2500Tsh nakupa season zote. Njoo WhatsApp namba ni 0717255498..
   

SIMULIZI NA SAUTI
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork

HONGERA WEWE NDIO MSHINDI WA VOCHA YA LEO VOCHA NAMBA (499712343590381) MTANDAO VODACOM TUMA NENO NIMESHINDA KWENDA NAMBA 0768304821


mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MSHANGAZI EPISODE 1

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MIMBA YA BESTMAN 13

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MIMBA YA BESTMAN 10

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

YAMENIKUTA

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MIMBA YA BESTMAN 9

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

JINSI YA KUTUNZA UKE

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

PART 5 MY HEART

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MY HEART 03--04

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

*MY HEART* *1---2 *

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MIMBA YA BESTMAN 7

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

ANIPHA 6--7.

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

MIMBA YA BESTMAN 05

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

side chick episode 3

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

SIDE CHICK EPisode 2

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 18

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 17

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 16

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 8

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

CAREEN Sehemu ya 1

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

RATIFA Sehemu ya 32

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

JINA LANGU SHAMSA EP3

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

JINA LANGU SHAMSA EP2

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

JINA LANGU SHAMSA EP1

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

BOYCHILD PART 3

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

DRAMA OF LOVE part 4.

mjukuu rewards 100 Comments 0
 

DRAMA OF LOVE part 3

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest