KISURA WA DAMPO 11
(nilizaliwa na kichaa nikazaa na ceo)
Mwandishi HURU MEDIA
Basi akaagiza chakula na wakati huo sikuwa na hamu ya kula kabisa yaan, basi nikawa nasikia raha kumuona namna ambavyo anatafuna chakula, akaniuliza “ vipi nikuletee na wewe chakula?...
“ hapana ww kula tu mimi nimeshiba, nikajibu na mack akataka kuagiza kitu ila nalipoona nimekazia kuwa sitaki kula akakubali, akala pale na baada ya hapo muda ulikuwa umeshaenda, akanichukua tukapanda kwenye gari na safar ya kwenda kisongo ikaanza,…
Tulipanda ndege ndogo ambayo ilikuwa inabeba watu sita tu, ila kabla sijapanda ndege nikaanza kuusikia ule mngurumo sijui wasiwasi ulitoka wapi, maana mara zote huwa tunasikia ndege zikipita, ila sijui ni kwakuwa zinakuwa mbal hivyo sauti haiwi kali, ila siku hio niliona kama ndege inaningurumia masikioni, mack aliona wasiwasi wangu, akanishika mkono kisha akasema “ usiogope mamaa, basi kwa tabu tukapanda ndege, nilikuwa natetemeka muda wote na muda wote mack alikuwa amenikumbatia kuniondolea hofu, nikaanza kusikia kichefu chefu, nikamtapikia mack…
Ikabidi mack aite wahudumu wa ndege kisha wakaja na kunisaidia kunisafisha, na sijui mack alijua maana alibeba nguo mbili yangu na yake, kisha akanipa kidonge akanambia nimeze ili nijisikie vizuri, basi nikameza akawa anasema “ nisamehe nilisahau kukupa mapema ili kukuzia kutapika mamaa, naomba nisamehe sana…
Sikuona kosa lake, basi tuliubadilisha nguo hapo hapo kwenye ndege na baada ya hapo mack akawa amenituliza mpaka tulipofika uwanja wa mwalimu nyerere ambapo tulishuka na likaja gari flani kali sana kisha likatuchukua na baada ya hapo tukaanza safari ya kwenda kwenye nyumba ambayo alikuwa anaishi mack….
Tulienda mpaka osterbay, na wakati huo sijawah klufika dar kuanzia nimezaliwa nikaanza klushangaa ile jam mno, maana arusha na mpanda hakunaga jam ya namna ile, ikabidi niulize, maana kuuliza sio ujinga kuwa “ kwa hio dar ndio magari yanatembea kibibi harusi, aisee mack akaanza kiucheka, na dereva wake ni kama alikuwa anajizuia kucheka ila alitaka kucheka maana hakuna mtu hata mmoja ambae alitegemea kama nitauliza swali kama lile…
,mack akacheka kidogo kisha akajikausha maana yakutaka kuniona nalia, na kunambia, “ magari hayatembei kibibi harusi bana, hapa kuna foleni, magari ni mengi sana, hivyo yanashindwa kupishana ndio maana yanaenda taratibu sana…
Sasa hapo nikamuelewa na siku hio sikulia, nikaanza kushangaa zile flyover, nikajikuta naropoka na kusema “ ona ona magari yanapaa, ila dar bana kuna mambo ya ajabu sana mpaka magari yanapaa…
Mack akacheka na safari hii hata dereva wake akashindwa kujizuia nay eye akacheka na mack akacheka kidogo kisha akatulia na kusema “ mke wangu sio kwamba magari yanapaa, ila hizo zinaitwa barabara za flyover, hizo barabara zimejengwa mahususi kupunguza foleni ya jiji hili, kwa hioo ni barabara kama ambavypo zilibvyo barabara nyingine, akaendelea kusema….
“ ahaa sawa, niajibu kisha nikatulia…
Basi safari ikaendelea tukaenda mpaka nyumban kwa akina mackmill ikabidi niulize na mimi “ kwa hio na leo umenileta kwenye hotel nyingine ila unapenda kuchezea hela, kila siku tunaenda hotelini tu…
“ hii ya safari hii mke wangu sio hotel, hapa ni sehemu ambayo mimi na wewe tutakuwa tunaishi mamaa, na tutaishi hapa kwenye maisha yetu yote, labda kama usipende kukaa hapa ndio naweza kukutafutia nyumba nyingine umesikia mamaa…
NAKUJA….
KISURA WA DAMPO 12
Nilizaliwa na kichaa nikazaa na ceo
Mwandishi HURU MEDIA
Basi tukiwa tumekaa pale, mara akapita mdada wa kazi, akiwa amebeba mikate ambayo ilikuwa inatoa fungus akaenda kuiweka kwenye sehemu ya uchafu, aisee nilikimbia kisha nikautoa ule mkate na kusema kwa ukali kuwa “ wewe kwanini unatupa chakula…
Kila mtu ambae alikuwa pale akaanza kunishangaa, ndio ni chakula ila ule mkate tayar ulikuwa umeshaharibika hivyo haukuwa unapaswa kuliwa zakdi ya kutupwa tu…
Nikakaa chini nikaanza kula, mack ikabidi anifate kisha akaniambia “ kiuna chakula kingi sana ndani mamaa, sidhan kama unapaswa kula chakula kama hiki, huu mkate umeshaharibika hivyo usile utapata madhara…
“ yaan matajiri bana, yaan ingawa semeni simpendi ila ningempa huu mkate angenishukuru bana, embu niacheni nile, mimi siwez kuangalia chakula kinatupwa alafu nikakubali, basi wakataka kunizuoa ila nikaanza kuleta vurugu ikabidi waniache, nikaanza kula, yaan nilikula mpaka nikaumializa, nikaomba maji nikashangaa naletewa maziwa, nikajikuta naropoka na kusema “ yaan kuwa tajiri rah asana, badala ya kunywa maji unakunywa maziwa….
Wafanyakazi wakawa wananishangaa, nilipomaliza kula macxk akanichukua akanipeleka chumban kwake, sas aile nimefika tu chumban kwake, akaniangalia kisha akasema “ kwanini ulikuwa unakula mkate ulioharibika mamaa, kuna chakula kingi sana humu ndani, ila hata sikumjibu maana niliona kama anajifagharisha kwa chakula chake…
Basi nikaingia bafuni nikaoga, na mara baada ya kumaliza kuoga, nikatoka mack akataka kunipa mafuta aiseee nilishtuka kisha nikasema “ wewe yaan unataka kunishika ili unifanyie tabia mbaya, sitaki mimi, aisee mack alicheka kisha akasema “ ni kweli nakutaman kila nikikuona na ukizingatia namna ambavypo ulivyo na joto ndio kabisa, ila naona kama unateseka sana, maana unaliona kabisa tumbo lako namna ambavyo lilivyokubwa, kuna vitu siwez kukuruhusu ufanye kwa usalama wa mtoto wetu…
Akiwa anaongea pale mara nashangaa anakuja kuingia daktari, na alipoingia akaanza kunipima joto, si akataka kunichoma sindano, nikakataa, ikabidi mack amuambie huyu anaogopa sana sindano hivyo mpime joto na umuangalie choo maana huenda kikawa na shida, maana amekula chakula chja ajabu, sasa Yule baba akanipa vikopo viwili akasema “ kimoja utaweka kinyesi, na kingine utaweka mkojo, mimi sawa, nikaenda chooni, aiseee nikaanza kujisaidia kwenye kile kibobo, mkojo niliuweka kweli ila kinyesi kikajaa kibobo kizima, Yule nikanawa alafu nikaaanza kuona kinyaa sasa…
“ mimi siwez kubeba bana, ikabidi mack aje kule uwani, akachukua kile ncha mkojo akatoka nacho kisha akamuomba docta kibobo kingine akaenda kuchota kinyesi, kisha akarudi chooni, maskin akaanza zake kusafisha…
Kweli narudi chooni nakuta kile kibobo ni kisafi kinanukia, utasema kimemwagiwa pafyumu na wala hata hakuniuliza kitu…
Basi maisha ya kwenye kasri yakaanza, sasa kuna muda nasikia raha kulala ndani kuna mjuda namiss maisha yangu, yaan kuna siku mvua inaweza ikanyesha, ukashangaa unanikuta nje, nimelala pemben ya nyumbna nimejifunika maboksi…
Mack akawa akiamka anaanza kunitafuta, mwanzo alikuwa anapata shida ila mwisho akawa anajua nalala nje, akawa ananizuia ila sikuwa nataka namuambia aniache na maisha yangu, akawa anakuja kisha analala na mimi pale nje, yaan mwamba alinipenda kweli, licha ya kuwa mtoto wa mtaani, ila alinipenda na kutaka kunipa maisha ambayo nahitaji kuishi na haikuwa kazi sana, maana alikuwa anaishi na mimi kwa namna nilivyo hakuwa hata anataka kunibadilisha, nbaada ya kujua hjivyo vyakula havinidhuru akawa anafanya na kuniletea kabisa, na nakula, ingawa yeye hakuwa anataka kula ila sikuwa namjali kabisa…
Siku moja tukiw achjumban mack alinifata kisha akanambia “ nataka ukishajifungua nikuoe, naomba niambie nitapeleka wapi posa…
Hapo kwa kupeleka posa nikajikuta naanza kulia, maana ndugu zangu ni wale wenzangu wa mtaani, sasa tukiangalia kweli atapeleka wapi posa, ikabidi aanze kufanya kazi ya kunibembeleza sasa na akajua ni kile kisirani changu cha mimba, hivyo kwa upole akaniuliza “ unataka nini mamaa, sipendi kukuona unalia, utakachokitaka nitaenda kukuletea sasa hivi…
“ mimi sina wazaz wala sina familia hivyo sidhan kama utaweza kunioa, nikasema…
NAKUJA…
KISURA WA DAMPO 13
(nilizaliwa na kichaa, nikazaa na ceo)
Mwandishi HURU MEDIA
Usiseme hivyo mke wangu husqer embu nambie maisha uliyoyapitia nataka kukusaidia, akasema kwa sauti ya upole mpaka nikajikuta naanza kumuonea huruma na mimi..
Najua ulishasikia kuhusu mimi kuzaliwa na mama kichaa, nikasema ila sikuwa na uhakika kama amesikia kweli au laa, ila nilikuwa naaamin kila mtu ananijua na anajua maisha yangu, ila mack akasema ndio najua, ila kwani haukuwah kujaribu kutafuta ndugu zako? Akauliza…
Embu nambie naanza kuwatafutiwa wapi na wakati hata mama yangu hawezi kuongea na hawakuwah kumtafuta hata mara moja, kiukwel kama umenipenda sana naomba posa yangu ukawasaidie watoto wa mitaan, hata kama utaweza kuwachukua wenye nia ya kusoma uwa someshe, utakuwa umenisaidia sana..
“ usijal mke wangu, kuanzia umekutana na mimi ndio mwisho wa mateso yako, nitahakikisha nakupenda na nakulinda kwenye siku zote za maisha yetu, nitahakikisha kuwa unakuwa mmoja wa wanawake bora sana dunian, hata kama ulikuwa na mama mwenye maisha magumu ila angalau ujivunie mume ambae umempata na utaishi nae maisha yako yote, akasema mackmill mpaka nikajikiuta natabasamu…
Basi siku moja mama yake akaja na mdogo wake wa kiume mack, alikuwa anaitwa Andrew, yaan huyu shemeji yangu alikuwa ni mtu flani poa sana, yaan hana makuu kabisa, na alikuwa ananiheshimu sana, sasa hapo nina mimba yangu kubwa, mama akaagiza kuwa tuletewe supu, kumbe matajiri kabla hawajaletewa chakula huwa wanaanzaga kuletewa kwanza supu kuchangamsha tumbo wakiwa wanasubiri supu…
Kweli baada ya muda ikaletwa supu, kiukweli sikuwa najua ni supu ya nini, ila baadae nikaja kujua ni supu ya pweza, na kama mnavyojua mimba yangu haichagui haibagui, ilipokuja nilishangaa maana sikuwah kuiona, ila nilipoonja jilikunywa supu yote pekee yangu, maana hawakuwa wanataka kunikera, na baada ya kumaliza hapo hata sikuongea na mtu na badala yake nikanyooka zangu nje nikaenda kukaa kwenye garden, sasa siku hio kulikuwa na wafanyakazi wawili walikuwa kama wanaongeza ongeza mauwa pale, nikamfata mmoja na kumuambia “ usipande hilo uwa hapo, njoon upande karibu na mlangoni…
“ madam hapo mlangoni kuna bati ua halitakuwa vizuri maana halitapata jua la kutosha, akasema Yule kijana na mimi nikaitikia ndio tu, kana kwamba nilikuwa nimemuelewa, ila kiukweli nilimuona kama amenidharau, yaan mimi natoa wazo alafu ananipinga…
Basi kijana wa watu akawa anaendelea zake na kupanda zake mauwa, alipopanda ile sehemu ambayo sikuwa nataka apande sijui hata kwanini nilijisikia vibaya sana, nikaanza kulia, aiseee nililia mpaka mack na mama yake wakatoka nje kutaka kujua nina shida gani?...
“ yaan nawambia asipande ua pale hanisikii anapanda tu, mimi nataka lipandwe hapa, nikawa nasema kwa sauti ya kilio, na mama yake mack akacheka kisha akasema “ haya nenda kalichukue upande mwenyewe umpe Baraka mjukuu wangu, kweli nikalichukua na kwenda kupanda sehemu ambayo nilikuwa naitaka, kisha hapo ndio moyo wangu ukatulia sasa, maana nilikuwa na hasira vibaya mno….
Watu wote walipoona nimetulia wakaanza kucheka na mama yangu mkwe akaanza kusema “ naomba anachosema huyu binti mtu yoyote Yule hana haki ya kumpinga, watu wote wakaitikia kwa ishara ya kukubali…..
NAKUJA
KISURA WA DAMPO 13
Mwandishi HURU MEDIA
Basi maisha yakawa yanaendelea, na mimba yangu kwenye msosi tu si haba, yaan nilikuwa nakula kama nakimbizwa, yaan sijawah kuvimbiwa wala kuumwa tumbo, yaan chakula kikibaki siwez kuruhusu kitupwe, nitakikalia chini nile mpaka nihakikishe nimekimaliza, maana kwanza unatupaje chakula na wakati kuna watu wengi wanalala njaa…….
Mack alikuwa ananitaman sana ila alikuwa ananioena huruma, nilikuwa namuona mara nyingi namna ambavyo alikuwa anajikaza ili asinitese tu, ila haikuwah kuwa rahisi kabisa kwake, alikuwa mara nyingi ananikumbatia kwa nguvu na nilikuwa nauhisi kabisa mtalimbo wake namna ambavyo unapata tabu…
Siku moja akanifata kisha akanambia “ husqer mke wangu nataman sana kukiupeleka kwenye kampuni wakujue, aisee nikajikuta naanza kulia, akaniouliza nini wewe…
“ nilijua tu unataka kunidhalilisha, umeshindwa kusubiria mpaka nijifungue unataka kunipeleka na mimba ili watu waanze kunicheka najua hauna mipango mizuri na mimi, nikawa nalalamika hapo…
“ nimekuambia nakupeleka ila sijakuambia nakupeleka lini, nilikuwa hata na mimi nataka kukupeleka ukijifungua maana siku zilizobaki ni chache sana, akasema mack…
“ siku ni chache sana ndio maana hutaki kunipeleka , yaan wewe mwanaume najua hautaki mahawara zako wanione nikiwa na mimba ndio maana hautaki kuniupeleka sasa hivi, yaan nashangaa kila siku unasema kuwa unataka kunioa ila hautaki watu wanijue, na hautaki watu wajue kuwa nina mimba yako, kwanini sasa ulilala na mimi, nikazidi kulalamika…..
Mack akanisogelea kisha akanikumbatia kwa mahaba makubwa sana kisha akasema “ unataka nini mke wangu kipenzi, si unajua kila unachokita nitahakikisha nakutimizia…
“ nataka unikumbatie nikaongea kwa sauti ya madeko, aisee hapo sasa uvumilivu ukamshinda mack, akaanza kujinywea juice yangu ya asili, yaan nilipewa kiss moja matata mpaka nikatulia nikawa hata siwez kusema neno, akanikiss [pale kisha akanmabia “ hio ndio adhabu yako kwa kunibania sauti unajua kabisa mumeo sijiwezi kwako, kwanini unanitega na wakati unajua kabisa uvumilivu wangu ni mdogo sana…
Nikajicxhekesha chekesha pale maana hata mimi sio siri nilikuwa nasikia rah asana…
Basi bana maisha yakawa yanaendelea na nikawa nalelewa kama malkia vile, muda ukaenda, siku moja nipo zangu ukumbini nakula makande, maana siku hio niliwaambia kuwa nimemiss kula makande, nikaanza kusikia tumbo linaniuma, yaan kiuno chote kimekaza balaa, nikavbunga nikajua ni hali ya kawaida, ila haikuwa hali ya kawaida, mara nikashangaa naanza kutapika, aiseee nilitapika sana, kumbe ndio nilikuwa navunja chupa kwa kutapika….
Ikabidi mama yake mack aitwe maana macvk siku hio alikuwa mbali, amekjuja nilikuwa hoi, akanikimbiza hospital, yaan ile nafika tu hospital nikawa nasikia kama nataka kutoa haja kubwa, madaktar sasa wakaniwahi, nikabebwa mzobe mzobe mpaka leba, yaan walipotaka kunipima tu, wakashangaa mtoto huyo anatoka zake…
Basi nikazaa mtoto wa kiume kafanana na mack copi right yaan ukimuona unajua kabisa ni mack amejizaa tu, maana kuanzia masikio , mdomo, pua mpaka rangi ni mack mtupu, yaan hauwez kubisha kabisa…
Mack alifurahi sana, na akawa anataka baada ya mimi kujifungua ndio tufunge ndoa, basi nikarudi nyumban, yaan hii familia ni zaidi ya familia maana waliunilea kama yai, sio mama mkwe sio mack, wote walikuwa wanahakikisha kuwa nakuwa nafuraha na Napata kitu chochote ninachokitaka tena kwa wakati bila kero wala bughudha yoyote ile….
Basi nikamaliza miezi mitatu, mwili wangu ukaanza kukaa sawa, yaan nilikuwa namuona mack namna ambavyo alikuwa anateseka sana kihisia, muda ni mrefu na ukizingatia kipindi cha ujauzito alikuwa anaogopa sana kunikera na ananionea huruma ndio kabisa yaan…
Siku moja nimemuacha mtoto kitandani, maana alikuwa amelala baada ya kunyonya, nikasema niingine bafuni maana nilikuwa nasikia joto balaa, ile nimeingia bafuni nashangaa mack huyo, akaja na yeye, akawa anasema kuwa anataka kuniogesha kumbe mwamba kazidiwa bana…
Anajitia kuniogesha ili aanze kunitega ale mzigo, sasa namna ambavyo alikuwa ananipaka sabuni ni ntafrani tu, mimi mwenyewe nikasahau kama nina mtoto mchanga nikajikuta nimemvamia, maana tayari nilikuwa nimeshazoea, na yeye hakutaka kulaza damu, ukizingatia amejitunza sana kwaajili ya kunivumilia mimi, basi shughuli bin shughulati ikaanza taratibu bila jasho…
NAKUJA…………..
KISURA WA DAMPO 14
(nilizaliwa na kichaa nikazaa na ceo)
Mwandishi HURU MEDIA
Basi kila mmoja alikuwa na hamu na mwenzake, maana mimi nilikuwa nimemmiss nay eye ni balaa, yaan ilikuwa ni shoo juu ya shoo, hatukujua hata tulienda masaa mangapi, tumekuja kushtuliwa na kilio cha mtoto akiwa analia, kwa maana ameamka, nikajimwagia chap nikaenda kumuona, nakuja kuangalia saa ni saa tisa na nimeingia bafuni saa sita….
Basi na mackmill nay eye akaoga pale, na mara baada ya kuoga akaja kunisaidia kubembeleza mtoto, akataka nitumie na kinga nisije kubeba mimba ya pili na wakati mtoto alikuwa bado mdogo, akaniletea vidonge kiukweli sikuwa najua hata ni vidonge gani, nikameza na maisha yetu yakawa yanaendelea kama kawaida…
Sasa mtoto alipofikisha mwaka mmoja mack akataka kwanza tufunge ndoa na mwisho akataka kwenda kunisomesha na kunitambulisha kazin kwake, maana sikuwa najua kusoma wala kuandika, sasa mke wa mkurugenzi kama mackl natakiwa kuwa na hadhi flani na sio kuishi maisha ya kichokoraa kama ambavyo nilikuwa nimeyazoea…
Cha kwanza tukaanza mikakati ya ndoa, na nikamuomba mack kuwa tualike watu wote wenye maisha magumu na mayatima ndio tule nao, maana hao matajiri wenzake kwanza wanauwezo mkubwa sana wa kujilisha chakula chochote kile wanachokitaka hivyo kuwaalika ni kama kutumiza wajibu, ila kuna watu ambao chakula kizuri kukipata ni kama bahati kwao, na akanielewa, yaan akaanza kuweka matangazo kuwa yoyote anaetaka kuja kula kwenye harusi anaruhusiwa na akatafuta usafiri ukawa unazunguka mijini, nikaomba akawachukue na machokoraa wenzengu wa arusha na mpanda hakubisha, ingawa machokoraa wengi huwa na tabia ngumu ila nilimuomba avumilie, ila watafurahi sana…
Basi tukachukua na watoto yatima, sikuwa najua kama mack alijiandaa vilivyo, na mni mtu mwenye pesa yaan alikuwa na uwezo wa kliulisha hata jiji zima la dar es salam, basi tukafunmga ndoa ya kihistoria, na watu walikula wakasaza, baada ya ndoa mack akatoa tamko kuwa atawasaidia watoto wa mitaani, sio wote ila wenye maadili kidogo kwa maana atawasomesha, na kuwatafutia nyumba…
Basi akajenga nyumba kubwa sana, akawaweka huko, ili angalau wasiwe wanalala majalalani, na mwenye nia alimuwezesha, niliona kama amenifanyia kitu kikubwa sana, ambacho binafsi sikuwah kufikiria kama kuna mtu anaweza kukifanya kwaajili yangu….
Baada ya hapo akaanza kunitafutia mwalimu, ambapo nilisoma ile elimu ya watu wa zima, nikasoma masomo ya darasa la kwanza mpaka la saba kwa miaka miwili, na baada ya hapo nikaafanya mtihani wa darasa la saba nikafaulu, kama mnavyojua ukisoma kwa malengo huwezi feli, baada ya hapo nikaingia kwenye QT, ambapo nilisoma kitado cha kwanza mpaka cha nne kwa miaka miwili na baada ya hapo nikatakiwa kwenda kusoma kidato cha tano na cha sita kwenye shule ambazo nilikuwa nimepangiwa na serikali, ilikuwa ngumu sana kwa mack, maana alikuwa ananipenda sana nalikuwa ameshanizoea, ila alikuwa anataman sana kuona kuwa na mimi siku moja nimefikia ndoto zangu, ila kabla sijaenda kusoma akanambia kuwa anataka kwenda kunitambulisha kwenye kampuni yake, na kiukweli sikuwah kuwa mbishi, nikakubali haraka haraka pale….
Kuanzia nimezaliwa sikuwah kupanda lift, sasa ile tunafika kwenye hilo jengo nikashanga mack anabonyeza ukutani mara mlango ukafunguka, nikajikuta naropoka, “ doh kuwa na pesa ni raha mpaka milango inajifungua yenyewe, mack hakunijibu zaidi ya kutabasamu tu…
NAKUJA…
KISURA WA DAMPO 15
Mwandishi HURU MEDIA
Sasa lift ilipoanza kutembea nilipatwa na hofu nikajua ni tetemeko la ardhi, nilimshika mack kwa uoga, sasa sikuwa naangalia namshika wapi, maana nilikuwa tayar nimeshapanic, kumbe nimemshika suruali naishusha chini, mack akawa anapamba kunituliza , ila sikuwa namuelewa, namuambia “ tumetekwa mack tumetekwa tunafanyaje tutoke hapa kwenye tetemeko la ardi, mack ananielewesha ila sikuwa hata namuelewa kabisa yaan, niliona kama anajiongelea zake tu na sikuwa namuelewa kitu hata kimoja, lift inakuja kufunguka wote tumetokwa na jasho mpala la pua na mack amabaki na boksa tu, kwa maana suruali ilikuwa chini…
Wafanya kazi walioona wakajifanya hawajaona na kugeuka, mack akaniangalia kisha akasema “ ona sasa ushamba wako umenifanya mpaka nimedhalilika husqer, kwani ulikuwa na shida gani, na nilikuhakikishia kuwa upo salama, hio ni lift tu, na hatukuwa tumetekwa wala hatukuwa kwenye tetemeko la ardhi, akazidi kusema mack…
Kiukweli niliona aibu sana, ila sikuwa na namna zaidi ya kumuomba mack masamaha, maana ushamba wangu umesababisha mpaka nikamshalilisha mume wangu kipenzi, mack hata hakuwa na hiyana, na ukizingatia alikuwa ananipenda vibaya mno, hivyo kumuomba msamaha kulimfanya ajisikie vizuri sana, ila akanipa onyo kuwa nisije nikarudia tena, na nikakubali pale…
Basi tumefika pale nashangaa kila mtu akimuona mack anainamisha kichwa, sijawah kuona kitu kama kile nikajua labda wanamuogopa mack, sijui hata niliwaza nini, yaan nilihisi labda wanajua mack ni mtu mbaya, kumbe hawez kuwafanya kitu nikajikuta naropoka na kusema “ nyie msiiname iname huyu hana shida na sio katili, yupo kama nyie tu mimi ndio namjua, hivyo msipate shida ya kuinama inama maana maana mtamfanya ajisikie vibaya na wakati ni mtu kama nyie, si ndio mume wangu, nikasema na mack akaniangalia kisha akatabasamu, kisha akasema “ ni kweli msiwe mnainama inama mnaponiona bana mimi nipo kama nyie..
Kumbe walichokuwa wanakifanya ni kumpa heshima kama boss mimi nikaona kama wanateseka tu, ila hakuna kitu kilichobadilika sasa mackl akaita wafanyakazi wale viongozi kwenye sehemu kama ofisi kubwa akawaambia jambo kisha tukaenda kwenye sehemu kama liukumbi, wakaja wagfanyakazi wote wa ile kampuni, hapo sijui kama natakiwa kutambulishwa nipo tu natoa macho, yaan kwa namna ambavyuo mack alikuwa amenikarabati, nilikuwa kama mdada wa kishua kumbe ni mshamba kupita maelezo ya kawaida…
Basi kweli watu wlaipokuja wote mack akanitambulisha pale kama mke wake, watu wakawa wanipa pongezi pale, na baada ya hapo nikashangaa naona mwanga kwenye ukuta kisha nikaanza kuona maandishi yanatokea alafu yanatembea, nikajikuta naropoka, “ yaan kuishi mjini raha maana mpaka maandishi yanatembea yenyewe, yaan watu walicheka sana, ila mack alikuwa ameshazoea vimbwanga vyangu, wala hakuona kama nitamtia aibu maana ndio alikuwa amechagua kuwa na mimi, na alichagua kuishi na mimi kwa namna nilivyo, kwa hio alijua gfika hawez kunifundisha kila kitu, na mambo mengine nitajifunza wakati nakutana navyo, ndio akaninong’oneza na kunambia kuwa ile ilikuwa ni projector nay ale maandishi hayapiti ila yamewekwa hivyo akataka nitulie na mimi nikamuelewa…
Kuna mtu alikuwa anatakiwa kuwasilisha presentension flani ndio maana aliwasha projector baada ya hapo, watu wakaanza kumpigia makofi, na mack akachukua mic na kusema “ hii kampuni kuanzia leo ipo chini ya mke wangu, naomba mtakapomuona mumpe ushirikiano na mumuheshimu kama ambavyo mnaniheshimu mimi, kwa maana kumkosea mke wangu kipenzi ni kama kunikosea mimi akasema, sio siri nilijihisi kuthaminiwa, nikajisikia vizuri sana, nikajikuta nashindwa kuvumilia na kumsogelea mack mume wangu kisha nikamkiss, na mtu mwenyewe namjua nikimgusa tu imo, nusu tuzidishe dozi ndio mc aliekuwa pale akakohoa ndio kushtuka kuwa tupo mbele za watu mack sasa hapo akaniachia kisha akaniuliza “ kwanini umefanya hivi na wakati unajua kabisa mimi ni maharage ya mbeya kwako…
Nilitaka kukushkuru nikaona kama unazidisha dozi, nikajibu mack hakuwa na cha kufanya zaidi yua kucheka tu, maana hata asipocheka atafanya nini na wakati ameshatia aibu mbele za watu…
NAKUJA.