UTAMU WA MABOSS?????? 5
Michael alimcheka sana Alex alimwambia Linda ndo mwanamke pekee watakaewezana naye???????? Alex alichukia sana..
"Sijui hata wewe ni rafiki gani ambae hata haujali kama rafiki Yako yuko katika matatizo,badala unipe pole ndo kwanza unanicheka na kumsifia huyo mwanamke ????????"
Kwanza umefuata nini ofisini kwangu??Michael alimwambia Alex nimekuja kwa sababu Bi Brown alisema anahitaji kuletewa bidhaa" okay aliitikia Alex..
Alifunga laptop yake mara moja akakumbuka alikuwa na mkutano na miss Kate.
"Labda nimfukuze tu Linda, hana faida. ananiletea shida tangu aanze kufanya kazi hapa.
Hata ratiba yangu ya leo siijui hawezi hata kunikumbusha vitu muhimu badala yake ananisahaulisha tu????????????..
"Ninapaswa kumchunguza,Alisema Alex kisha
Akasimama na kwenda ofisini kwake linda na kitu cha kwanza alichokiona kilimshtua????????
Alex Alifika ofisini kwa Linda akakuta Linda amelala muda wa kazi!,
Oh nilisema msichana huyu hayuko tayari kufanya kazi. Anafikiri ni rahisi kufanya kazi katika kampuni ya Fan star Ltd????????????
Aliwaza kumwamsha akaghaili kuna wazo lilimjia Alex akatabasamu..alimsogelea Linda akaanza kusokota nywele zake taratibu na kuzifanya ziwe rafu sana...
"Nina hakika itakuwa ngumu sana kwake kuzichana, akawaza Alex na baada ya hapo
Alichukua ufunguo wa gari lake na kuiacha kampuni huku akitabasamu...
Alifika kwenye mgahawa ambapo yeye na miss Kate walikubaliana kukutana.
Aliingia kwenye mgahawa huo na kumuona kate akiwa amekaa sehemu yenye ubaridi huku akibonyeza simu yake...
"Hi, miss Kate" Alex alisema mara moja akiwa anaelekea sehemu aliko kate na Kate akatabasamu.
"Halo Alex, unaonekana nadhifu sana kama kawaida yako" alisema Kate huku akiachia tabasamu lake la kupendeza..
"Unapaswa kuwa makin na usinitege, si unajua baba yangu ataniua ikiwa nitajaribu kufanya ujinga na mshirika wake wa biashara" akasema Alex...
Kate alitabasamu tu huku akimkumbatia Alex..
Bas Alex alimwita mhudumu ambaye walimuagiza vitu wanavyovitaka.
Na muhudumu akaenda mara Moja kuwaletea vinywaji na vyakula walivyoagiza.
Huku ofisini Linda Akiwa amelala hodi ikamuamsha na akatabasamu kidogo kuona ni Ella, sekretari wa Alex.
"Halo Linda" alisalimia na Linda akajibu "Halo"
"Subiri...huo ni mtindo wa nywele wa aina gani" aliuliza ella na Linda akamtazama kwa mshangao.
"Unamaanisha nini kusema mtindo wa nywele gani? Maana nywele zangu nimezibana tu kawaida ella alicheka tu akamwambia
"Hata hivyo nimekuja kukusalimia TU ndio nikakutana na nywele zako ambazo haziko kwenye mpangilio mzuri, unakaaje hivo ofisini bado Linda hakumuelewa.
"Mbona sikuelewi" Linda Alisema kwa sababu hakuwa anaelewa ella anasema nini "
"Labda uangalie nywele zako. Bye" Alisema ella na kuondoka ofisini kwa linda.
Linda alichukua simu yake na kujitazama kupitia kamera na akashtuka sana.
Nani amenifanya hivi?????????nahisi huyu ni Alex ndo amefanya huu ujinga
"Naapa Alex ni anataka kuuww Leo maana Nina uhakika YEYE ndio kazivuruga nywele zangu..
Alisimama kwa hasira na kwenda ofisini kwa Alex lakini hakumkuta, akaamua kumsubiri.
Dakika 30 baadaye, Alex aliingia na alionekana kuwa na wasiwasi sana mara baada ya kumuona Linda..
"Nini.....unafanya nini ofisini kwangu" alisema na Linda akamuangalia kwa dharau.
"Sikujua kuwa wewe ni msusi . kwa hivyo mtindo uliotengeneza kwenye nywele zangu unaitwaje" akasema Linda????????
"Unaongea nini? mimi nitakuwaje msusi? umerukwa na akili wewe Alisema Alex
"Kwahiyo unasema kuwa si wewe uliyefanya hivi kwenye nywele zangu" Linda alimuuliza Alex huku akizinyoosha nywele zake zilizovurugika.
"Hapana. Sijawahi hata kufikiria kukugusa Toka nje ya ofisi yangu miss Linda" Alisema Alex na linda akamtazama kwa hasira...yani hili????????
"Nimeingia hapa peke yangu kwa hiyo nitaenda nje mwenyewe," Linda alisema na kuendelea kusimama.
"Huyu jamaa ananikera kila siku, ngoja nitamtafutia dawa yake, akawaza linda..
Hata hivyo aliondoka na kumuacha Alex ofisini kwake kazi ziliendelea ikafika jioni muda wa kutoka..
Siku hiyo Linda hakuwa na pesa ya nauli hivyo akaamua kutembea kwa miguu..
Mara gari lilipita lakini likasimama mbele ya Linda na kurudi nyuma.
Linda alilitambua gari hili ni gari la Alex,..
Gari lilisimama pembeni yake na Alex alitoa kichwa nje akamtazama.
"Nini" aliuliza linda
"Utasimama tu hapo na kuendelea kunitazama au utapanda kwenye gari" Alisema Alex..
" Hapana. usijali, nitatembea tu" Linda alisema akijaribu kuringa kidogo alidhan Alex atambembeleza na kumuambia 'tafadhali ingia kwenye gari nikurudishe nyumbani' lakini badala yake, akampa ishara dereva wake aendelee na safari kheee Linda alishangaa????????akaanza kupiga kelele kabla hawajaenda mbali
"Subiri!!!!!" Linda alipiga kelele na gari likasimama mara moja.
" Nini " akauliza Alex
"Nitaingia kwenye gari" Linda alisema na kukimbilia siti ya nyuma alipokaa Alex alikaa pembeni yake kisha akamwambia dereva sehemu anakoshukia????????????"
Itaendeleaaaaaa
Full 1000
WhatsApp 0742133100.