MPANGAJI 04 ๐๐ซ ยฐยฐยฐยฐ Asubuh na mapema Sele aliamka na kufanya mazoezi kiasi kama ilivyokuwa kawaida
โla haulaa!โ alijisemea sasa akivuta begi lake na kuchukua ufunguo mezani na kutokomea nje
Alimkuta Esta akiwa mlangoni na begi lake tayri kwa safari..
Mama Mwajuma nae alikuwepo kumsindikiza mwanae
Baada ya Salamu sele alichukua begi la Esta na kulivuta taratibu kutokea nje Mama Mwajuma tayari alishahisi kuna jambo linaendelea kati ya watu hawa wawili hata hivyo kwa upande mwingine alifurahi kwani pamoja na mambo mengine ya Sele, alikua ni kijana mtanashati, mwenye adabu na asiyekuwa na makuu, kuhusu anafanya kazi gani mama mwajuma hilo halikumuumiza sana kichwa isipokuwa ni namna ambavyo uhusiano huu utaishia
โpotelea pote hawa ni watu wazimaโ aliwaza mama Mwajuma sasa wakipiga hatua kutoka nje ya nyumba, tayari wapangaji wengine waliokuwepo walishaagana na Ester na wengine tayari walikua wameshamzoea
โsasa Mama wewe ishia hapa mimi nitamsindikiza Esta mpaka ubungo na kuhakikisha anapanda basi la Lindi kabisa mama!โ alisema Sele huku akitabasamu,
โitakuwa vizuri kabisa Basi mimi niishie hapa, Sasa Esta, nikuage Mwanangu alisema mama Mwajuma huku akipunguza mwendo kidogo Sele alikuwa ameshaelewa hapa ni โmausiaโ ndio ambayo yanafuata
โMwanangu usinifiche kitu mimi ni mtu mzima, niambie una uhusiano na Sele?โ mama Mwajuma aliuliza huku akimtazama mwanae usoni
โhapana mama, Ni tumezoeana tu yaani, hivyoo tu!โ alisema Esta huku akiwa kama anataka kusitisha mzungumzo
โila Sele anakupenda maana hajawahi kuwa na ukaribu na mtu yoyote , sasa mpaka anafikia hatua ya kukusindikiza hadi stendi?โ alisema mama Mwajuma
โungejua sio kunisindikiza tu, kanaipa hadi laptop!โ alijisemea moyoni Esta
โhaya mama uwe makini huko shuleni, kaa vizuri na walimu wenzako, na mkuu wako wa shule na usisahau kuniletea mzigo wangu likizo ya mwezi wa 6โ alisema mama Mwajuma akimuaga mtoto wake kwa mbali alimnyooshea mkono Sele ambaye alikua sasa ameweka begi chini akimsubiri Esta ambaye alifika na kisha safari ikaanza. Hawakupiga hadithi sana kwani kila mtu alikua anawaza mambo yake kichwani, walipofika Kimara Mwisho Esta alilalamika kuwa kuna kitu aliagizwa na shoga yake amnunulie na alisahau kununua,
โyaani Nikifika bila hicho kitu Shoga yangu hatanielewa kabisa yaaniโ alisema Esta akimweleza Sele
โokay tushuke kwanza unaweza kukipata hapo nje hicho unachokitafuta halafu tukachukua bajaji tu kwenda stendi bado ni mapemaโ alisema Sele huku akisogea mlangoni
Walishuka pale Kimara mwisho ambapo wengine walipenda kuita darajani
Na kuvuka upande wa pili
sele alijua bila shaka ni vitu vya wanawake ambavyo shoga yake huyo alimuagiza
โwanawake wana vitu vingi sana yaani!โ alijisemea sele huku sasa akivuta begi la Esta
Walisogea kabisa pembeni ya barabara na kuingia mtaani walikaribia sehemu kulikua na bajaji kadhaa zimepaki Esta akamwambia Sele asubiri yeye aende kuuliza hicho kitu
Alisogea pale na kabla hajafika alishadakwa na madereva kadhaa alichagua mmoja kisha wakaongea halafu baada ya muda kidogo Esta alimnyoshea mkono Sele amfuate
Sele alimfuata na kuingia kwenye bajaji ya Yule kijana
โvipi tena?โ aliuliza Sele akiwa ameduwaa
โnakumbuka wakati nakuja nilikuambia unizunguushe nione mji kwahiyo leo ni zamu yako kaa utulie mwanaume wewe na usiongee kitu!โ alisema Esta kwa utani
โhaya langu jicho Esta, ila kwa hali safari labda kesho unapajua Lindi wewe?โ Sele aliongea sasa akiwa haelewi nini kinatokea
โhata hapa Dar nasikia kuna sehemu inaitwa Lindiโ alisema Esta Sele hakua na namna isipokuwa kucheka tu walipita sehemu kadhaa na baadae wakatokea mbele ya jengo moja zuri sana โLOTHA EXECUTIVE LODGE & RESTAURANTโ maandishi makubwa yalisomeka kwenye kibao cha jengo hilo
*************************
โpacheki sista kama hapafai nikupeleke nyingine ipo kati hapo nayo barida tu kama hii!โ alisema Yule kijana wa bajaji akiwa amesimama tayari kutoa mizigo
Esta alishuka kwa kujiamini huku Sele akiwa hajui kama anatakiwa kupiga kelele za shangwe au kilio ama anatakiwa kufanya nini,
Esta alifika ndani na baada ya muda alirudi
โasante kaka pako vizuri bei gani vile ulisema?โ alisema Esta kifungua pochi yake na kutoa elfu tano
โah buku mbili tu sista, kama vipi chukua minamba nini ili kama niaje niaje nini fresh tuu!โ alisema Yule kijana mpaka Esta alicheka
โhahaha usijali, sasa namba yako nitaisave niaje niaje bajajiโ aliongea huku Sele sasa akishuka kwenye bajaji na mizigo
โkiuhalisia nataka niende Lindi nikiwa sina deni na mtu Seleโ
Alisema Esta huku akiwa anatangulia ndani, Sele alifuata kama kondoo aliyekuwa mafichoni walipita mapokezi na mhudumu akawapokea na kuwapeleka kwenye chumba ambacho tayari Esta alishachagua, kilikua ni chumba kizuri sana, Esta alitua mizigo yake na kuipanga vizuri sele alikaa kwenye sofa lililokuwa pale chumbani na kukunja nne huku akimkodolea macho Esta kama mtu anayesubiri kupewa muongozo
โsele nikuambie kitu!โ alianza Esta kwa upole sana, yeye kama mwalimu alijua namna ya kuweza kueleza somo lake likaeleweka kwa mwanafunzi wake huyu aliyekuwa mbele yake
โmimi nina miaka 26 sasa hivi, nina vitambulisho vyote kuanzia cha kupigia kura cha kazi hadi cha Taifaโ alianza Esta
โunataka kusemaje?โ aliuliza Sele
โnaona kama mwenzangu umejaa hofu kana kwamba umeingia na mwanafunzi wa form one hapa kwahiyo muda wowote utakamatwa!โ alisema Esta huku akicheka
โHapana mwalimu mimi sijawa na hofu, ila nashangaa tu, ubungo imekuwa hii, sasa sijui hicho kitanda ndio basi au!โ alisema Sele kwa utani
โkwahiyo huna hofu kabisa?โ aliuliza Esta
โkwahiyo nikuogope wewe au!โ aliuliza Sele
Esta hakujibu alisogea mpaka kwenye meza na kupiga simu mapokezi ambapo aliagiza supu ya kuku na chapati
โ Sele safari yangu ni kesho, kwahiyo leo nimeamua rasmi nibaki na wewe hapa, kuna mambo inabidi nikuambie Sele ka aujuavyo kule nyumbani hakuna uhuru sana na tusingeweza kuongeaโ alisema Esta
โ kwakuwa leo ni siku ndefu kwanza nikushukuru sana kwa zawadi Sele yaani nikifika pale shule nitaosha kweli!โ alisema Esta akiitoa ile komputa kwenye begi lake
โooh usijali Estaโ alisema Sele
โnielekeze elekeze basi ujue mimi sio mtundu sana kwenye komputaโ alisema Esta akienda pale kwenye Sofa alipokaa sele,
โooh, wewe mwalimu tena si mmespma ICT chuoni jamani!โ alisema Sele
โtumesoma lakini theory nyingiii!โ alisema
โmh tuanze na niniโฆโ sele alikatishwa na sauti ya mhudumu aliyekuwa anagonga mlango na alifungua , na mhudumu akaweka mizigo mezani,
โkaribuniโ alisema mhudumu
โtuletee maji makubwa ya Kilimanjaro na glass mbiliโ alisema Esta sasa akisogea pale mezani na kuanza kupiga msosiโฆ
Walimaliza kula na kisha Sele akamuelekeza vitu kadhaa kwenye komputa katika hali ambayo Esta alishikwa na bumbuwazi,
โsele mbona unaijua komputa hivi? Na wakati huo umesema hutumii kabisa mitandao ya kijamii?โ aliuliza esta akiwa ameduwaa
โah kumbe nilikua sijakuambia kazi yangu hadi leo! Hahaha alisema Sele akichekaโ
โMimi ni IT nimejiajiri binafsi, kazi yangu ni kufunga mifumo mbali mbali katika ofisi, majengo ya watu binafsi n. kama vile kuweka software za cctv camera, ama za ulinzi n.k, mwakani inshallah Mungu akipenda nitakuwa na ofisi yangu rasmi sasa hivi nafanya deiwaka tu na kampuni moja hivi inaitwa TAAโ alisema Sele huku akiwa ametulia kabisa
โwaooh kumbe, niko na IT hapa, kwahiyo kumbe ninyi ndio mnahack akaunti za watu insta, eeh?โ aliuliza Esta kwa utani na sasa muda wa kubadili mada uliwadia โleo afe kipa afe bekiโ aliwaza..
Itaendelea.. ๐
full 1000
0784468229
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi






Maoni