MPANGAJI 02
๐๐๐๐๐
Ilipita wiki moja na hali ikawa shwari kabisa kwa wapangaji wa mzee Mhina, siku hiyo usiku Sele alikua anarudi zake na kwa bahati mbaya siku hiyo alikua amechelewa kupita siku zote na hivyo ilibidi agonge geti na kusubiri kidogo, alikua amevaa begi lake kama kawaida na mkononi akiwa na mfuko wa chipsi na soda yake tayari kabisa kuingia ndani, mara nyingi alikua akichelewa alifunguliwa mlango na kaka Ephraim au mzee Ngoda,
siku hiyo ilikua tofauti sana kwani wakati geti linafunguliwa Aliona sura ngeni kabisa machoni pake ya msichana mrembo umri wa miaka 25-28 hivi, Sele alijikuta akishikwa na kigugumizi na akili yake ikasimama kidogo akiwa ameduwaa pale getini.
โingia ndani kaka Sele!โ alisema Yule msichana nae akiduwaa
โah ah, bila Shaka wewe ni Ester?โ alisema Sele sasa akiingia ndani
โumejuaje?โ aliuliza Ester akimalizia kufunga geti.
โah mama yake alisema utakuja wiki iliyopita kwahiyo nimeona wewe ndio mgeni tu hapa vipi mbona hujalala mpaka sasa hivi!โ aliuliza Sele akieleka mlangoni kwake.
โah kuna tamthilia naangalia kwahiyo niliposikia unagonga nikaona nikufungulie na nikuone maana nasikia tu sele! Sele!โ alisema akitabasamu
โohoo ushasikia umbeya tayari!โ alisema sele sasa akiingia chumbani kwake,
Sele aliingia ndani kwake huku mawazo yake yakiwa kwa Ester ni kweli alikua anakutana na wasichana wengi kila siku, na hata hapo walikuja wapangaji wengi tu wa kike na kuondoka lakini haijawahi kutokea msichana aliyeubamba moyo wake kama ilivyokuwa kwa Ester,
โsiamini kama nimekamatika hivi!โ alijisemea Sele akifungua soda yake na kunywa,
Pamoja na kuwa ilikua ni mara ya kwanza wanaonana na binti Yule Sele alijiapiza kabisa Yule binti ameushika moyo wake.
Ester nae kwa upande wake aliona kitu cha tofauti kwa sele, kwanza zile hadithi alizokuwa amesikia kwa mama yake pamoja na wapangaji wengine kuhusu sele alitaka kuthibitisha kwa macho yake, na hivyo baada ya kusoma ratiba ya sele na kukosa kumuona mara kadhaa ndipo sasa siku hii akaamua kujitahidi kuwahi nafasi ya kufungua mlango ili amuone sele.
Haikua sababu ya mapenzi wala nini Ester alitaka tu kuona huyo Sele ni mtu wa namna gani, ni jini kweli? Au ni mtu wa namna gani! Na pengine akirudi kazini kwake Lindi basi angekuwa na kitu cha kusimulia walimu wenzake au pengine hata wanafunzi wake.
Ester alikua mwalimu wa sekondari ya kata ya kibaoni akifundisha Kiswahili na Historia, ni mwaka mmoja tu ulikua umepita toka aajiriwe katika shule hiyo baada ya kumaliza chuo cha aualimu huko Butimba Mwanza , kulikua na tetesi kuwa mama Mwajuma alikua amemficha mtoto wake huyo kwa mume wake baada ya yeye kuja Dar, na ndio maana hakuwahi kufika hapo nyumbani, na baada ya kukusumbuliwa sana na Ester mwenyewe ndipo sasa hakuwa na jinsi isipokuwa kumleta Ester amuone mama yake na baba yake wa Kambo,
Hivyo ester alitumia likizo ile ya pasaka kuja kumtembelea mama yake na ndipo sasa akasikia kuhusu Sele,
โkwakweli huyo Sele ni kama jini mwanangu yaani hapa pengine anatusikia!โ ester alikumbuka maneno ya mama yake mchana huo na kisha akatabasamu tu akivuta shuka kulala katika chumba cha mwajuma,
Siku hiyo sele Alijikuta anachelewa makusudi kutoka ili tu amuone Ester ni kweli alimaliza kujiandandaa kabisa na kisha akawa anasikiliza huko nje kama atasikia sauti ya wanawake na ester akiwemo ndipo akatoka na begi lake na kuangaza huko na huko.
โza asubuhi shemeji!โ alikuwa aisha akimsalimia Sele
โah poa tu vipi hajambo kaka!โ alisema sele akiangaza macho huko na huko na hatimaye akamuona Ester akitoka.
โkaka Sele za asubuhi! Nataka leo twende huko mjini na mimi niangaze macho jamani, si unajua nimetokea kijijini jamani!โ alisema Ester huku akiongeza mwendo kuelekea kule Sele aliko.
โdah Litakufa jitu leoโ aliwaza Sele.
โooh twende basi nikutembezeโ alisema sele nae akiwa siriasi
Wapangaji wengine walitoka kuchungulia kwani hakuna aliyewahi kuongozana na Sele hata siku moja!
โkweli mtu na mtuwe!โ alisema mama Mwajuma akiwa ameshika mdomo
โmama baadae jamani natoka na kaka Sele!โ ester alisema kwa sauti..
โsele unafanya nini ?โ alisikia sauti ikimwambia kwenye hisia zake.
โunafanya makosa Seleโ.
โACHA UF..LA SELE wewe ni mwanaume!โ sauti nyingine ilimwambia.
Hakujali aliendelea kupiga hatua akiwa sambamba na Ester ambaye alikua na mkoba wake na simu yake ya Samsung galaxy.
โmh kwahiyo tunaanzia wapi? Kazini kwako au mtaani kwanza?โ aliuliza ester!
โwewe umesemaje kwani?โ Sele nae aliuliza
โnilisema tukaangalie mjiโ alisema ester
โBasi sasa leo nitakutembeza mpaka miguu iume!โ alisema Sele
โkwahiyo kazini kwako hatufiki?โ aliuliza Ester
โhapana mama, leo utembee uone mji kama ulivyotaka!โ alisema Sele kwa upole
โkwahiyo kaka Sele nimesababisha wewe usiende kazini jamani!โ aliuliza Ester
โmh mbona umekazania kazi! Kaz! Kwani umeambiwa nafanya kazi gani! Hahaha?โ Sele aliulizahuku akimtazama Ester.
โhamna Bwana, si unajua tu mjini hapa kazi ni muhimu sana!โ alisema Ester.
โbasi kama ulivyosema hapa ni mjini sio kila kazi lazima uendeโ alisema Sele na sasa walikaribia kufika Stendi
โkariakoo, posta, kivukoni!โ ilikua sauti ya konda akinadi dala dala.
โtwende zetuโ alisema Sele kisha wakaingia kwenye gari
Njiani walipiga hadithi za hapa na pale na Sele alijisikia vizuri sana na wakati mwingine alicheka hadi abiria wengine waligeuza shingo zao kuwatazama, kwa yoyote aliyewaona hakika alijua tu hawa ni wapenzi wapya ama wanandoa ambao wanakwenda kula fungate, kwani wakati mwingine Ester alimlalia mabegani sele,
Ester alimkumbuka mpenzi wake Ima, ambaye alianza nae mahusiano akiwa chuo cha ualimu , walikua na ndoto nyingi za kuishi pamoja bila kujua ima alikua na mpenzi wake mwingine aliyekuwa nae, siku ya mahafali yao Msichana huyo alikuja chuoni na kisha Ima Akamtambulisha mbele yake kuwa ni mchumba wake, ni bahati tu rafiki zake Ester waliwahi kumuweka โchini ya ulinziโ vinginevyo siku ile ingekuwa ya mwisho kwa ester,
Na kutoka pale Ester alijiapiza hatakuja kupenda tena mwanaume katika maisha yake, na ndio maana walimu wenzake pamoja na maafisa elimu aliwatolea nje mchana kweupe na hakutaka mazoea na yeyote, sasa alipopata habari za Sele kidogo zilimstaajabisha hususani aliposikia hajawahi kutembelewa na mwanamke yoyote,
Ester alikuwa anakumbuka hayo yote sasa wakiwa karibu kabisa kufika kariakoo
Walifika na kushuka na kuanza kutembea huko na huko, na kununua vitu vidogo vidogo,
Baadae walifika kwenye mgahawa na kuagiza supu, walimaliza kisha wakaedelea na mizunguuko kutoka kariakoo hadi posta na kuendelea na mizunguuko mpaka kufika saa 7 mchana Ester alikuwa hoi taabani wenyewe wanasema aliomba poo.
โhahaha hapa ujue nataka tuunge mpaka Temeke tushuke taifa tukaangalie mechi ya taifa starzโ alisema sele
โno no no Sele nimechokaโ alisema Ester.
โokay tumchukulie mama Mwajuma zawadi basi tugeuke ila mimi nitakuacha home siwezi kubaki nyumbani sasa hivi! Ujueโ alisema Sele
โhaya bhana turudi tuuโ alisema Ester kisha wakarudi kituoni na kupanda dala dala,
โkweli leo nimetembea mjini, ila Dar ni nzuri kwakweli!โ alisema Ester huku akishushia na fanta yake
โyeah mzee baba Kajitahidi kuweka mji vizuriโ alisema Sele
โhivi una mishe gani Lindi!โ aliuliza Sele
โmimi ni mwalimu jamani Sele si nilikuambia!โ alisema Ester
โ ah kweli asee nakumbuka, kwahiyo unakula likizo sio!โ
โyeah, wewe ndio umegoma kabisa kuniapeleka kazini kwako!โ alisema ester
โhahaha si upo bhana tutaenda siku moja!โ alisema Sele sasa akichukua mizigo na kushuka!..
.. ๐ itaendelea
FULL TSH 1000
NAMBA YA MALIPO NI 0657774735
JINA MKEGANI MPONDA MTANDAO NI TIGO.