๐๐ MPANGAJI 05 โขโขโข Sasa Esta alitafuta namna ya kuanza mazungumzo yake yale aliyoyaita rasmi, Aliweka komputa
โSele, naomba kwanza nisamehe sana ila sina namna nyingine isipokuwa hiiโ alisema akianza
Alimsimulia Sele kuhusu historia yake ya maisha, elimu yake na mapenzi na kisha akamsimulia kuhusu mama Mwajuma na hadithi nyingine ambazo hakuona umuhimu wa kuzificha
โ mama Alikuja kutafuta maisha Dar miaka wakati huo aliniacha na bibi, kwa uhalisi mama alipata ujauzito akiwa darasa la saba, na mara baada ya kujifungua na mimi kuacha kunyonya ndio akaja huku Dar, alikuwa kila mwaka anakuja na kuniletea nguo na pesa za matumizi na hatimaye nikamaliza darasa la saba na kuchaguliwa kidato cha kwanza, wakati nikiwa likizo mwezi wa sita nakumbuka mama alikuja kijijini kwetu Moro goro akiwa na mtoto mwingine mdogo akasema anaitwa Mwajuma na ndio mama akatutambulisha rasmi kuwa ameolewa na mwanaume muislamu na kuamua kubadili na yeyeโ alisema Esta,
โkuna kitu nakiona kwako Sele, nilivyokuja nilisikia habari nyingi sana kuhusu wewe ndio maana hata siku ile nikasubiri kuonana na wewe , nimeona unahitaji msaada Sele ,na mimi ndio wa kukupa huo msaada Sele, tafadhali kama ulikua huna imani na mimi naomba sana uniamini, naomba sana Sele, naahidi kukutunzia siri yako yote kabisa utakayoniambia kuna kitu naona kabisa hakiko sawa Sele na mbaya zaidi hata wewe mwenyewe huna furaha na maisha haya unayoishi!โ alisema Esta sasa na machozi yakaanza kumtoka
โtafadhali niambie sele, wewe ni nani hasa, umetokea wapi na familia yako iko wapi, sele, tafadhali nimeangalia mpaka usajili laini yako umeandika โsele sele seleโ yaani majina yote matatu ni sele tu,โ esta alizidi kumbananisha Sele
Sasa Sele machozi yalikua yanamelenga lenga tayari kabisa kutoka
Lakini alijikaza kiume na kuuondoa mkono wa Esta,
โkwanini nikueleze hayo yote Esta kwanini?โ alingโaka sele
โah kwasababu, ah kwasababu.. nimekupenda Seleโ alimalizia Esta huku akisimama na kuweka mikono mdomoni kama mtu aliyesema jamboa ambalo hakutakiwa kusema,
Sele alipigwa na mshangao sasa , ndio hata yeye alishikwa na bumbuwazi na kujikuta sasa anatamani kuona kama yuko ndotoni ili aamke kutoka usingizini
โEsta wewe ni mwanamke pekee ambaye umeyabadili maisha yangu na nakupenda pia, lakini kuhusu historia Yangu, mimi ni nani nisingependa kukueleza Esta, kwakuwa inaniumiza mimi mwenyewe na itakuumiza wewe pia lakini kukueleza wewe ni hatari zaidi ya unavyofikiri weweโ alisema Sele,
โkumbukuka nimekuambia kila kitu Sele, na naapa kabisa Sele, nitatunza siri yako yoyote ile kuanzia leo hii na hata kama itakuwa ngumu kiasi gani basi siwezi kuachana na wewe Seleโ
โEsta unajua wewe ni mzuri, una macho mazuri sana, lakini baada ya kusikia hayo yote hutakuwa hivi ulivyo Esta, tafadhali usitake kujua haya!โ alisema Sele kwa kumsihi sana Esta
โnakuahidi Sele usiponiambia basi hata Lindi siwezi kwenda Tenaโ alisema Esta
โEsta sikiliza kwa umakini, na naomba sana unisikilize nitakuambia kila kitu ila kwa mashartiโ alisema Sele
โmasharti yoyote Sele niko tayariโ alisema Esta akikaa vizuri sasa kusikiliza hadithi ya Sele
โokay, kwanza hutamwambia mtu yoyote kwa namna yoyote ile, kwasababu yoyote ile utaendelea kuniita Sele , na hutanipigia simu popote mpaka mimi nianze kunitafuta, na hivyo hivyo kwenye mesejiโ alisema Sele
โhakuna shida Seleโ nitaweza yote hayo
โokay sasa Esta mimi jina langu halisi ni GiFT Lukas Tupaโ
Alisema akiweka kituo huku akimtazama vizuri Esta, ambaye hakuonyesha kustukaโ
โnarudia naitwa Gift Lukas Tupa estaโ alisema tena akimwangalia Esta machoni na sasa Esta akili zake zilielewa haraka
โwhaaat! Unasemaje Sele? Unataka kusema baba yako ni Mheshimiwa Lukas Tupa, the President?โ aliuliza esta huku akiweka mikono mdomoni Sele alitingisha kichwa tu kukubali
โbado hadithi haijaanza Esta nilikuambia mapema !โ alisema Sele sasa akimhurumia Esta
โSele noo ,โ
โokay sasa kwa mzee tuko wawili mimi na dada Yangu Doreen ambaye yeye yuko Italy ameolewa huko na alibadili kabisa na uraia, kwa ufupi iko hivi mzee Tupa alikua Mhadhiri mwandamizi pale udsm kabla hajateuliwa kuwa mbunge na Raisi aliyepita kama unakumbuka
Sasa mama yangu alikua ndio kwanza assistant lecturer pale kitengo cha sheria huko na huko akawa na mahusiano na mzee Tupa na ndio akazaliwa dada Doreen, na mimi ndio nikafuatia, mzee tupa alipoteuliwa kuwa Mbunge na hatimaye kuwa waziri wa Fedha akatupangia nyumba maeneo ya mikocheni, na mama alituambia wazi wazi kuwa mzee alikua na mke wake mkubwa na yeye alikua mke wake mdogo! Dada Doreen yeye alienda Kenya kusoma na mama akakataa mimi kwenda nje ya nchi kusoma na badala yake akasema nisome hapa hapa Tz ili niwe nae karibuโ Sele aliendelea na story yake kisha akanywa maji kidogo na kuendelea
โmzee akikua anakuja kwa mwezi mara mbili, na kila siku aliyokuwa anakuja basi angeniletea zawadi mbali mbali, kiuhalisia tulikua na maisha mazuri sanaโ
โhata hivyo hatuweza kukutana na ndugu zetu wengine wa mama mkubwa na hatukupewa habari zao kabisa, nakumbuka kuna siku mama alisema kuwa mahusiano yao bado hajawa rasmi na endapo tungetambulishwa basi mzee angeweza kukosa kazi, na uteuzi wake ukaishia hapo kwakua ni kashfa ambayo ingeweza kumkosesha kibarua chake, unajua tena waziri haipendezi kuwa na mchepuko!โ alisema Sele,
Maisha yaliendelea vizuri tu na dada Doreen akamaliza shule kule na mimi nikamaliza sekondari na nikaendelea na kidato cha tano na kumaliza vizuri kabisa kidato cha sita na kufaulu vizuri kwenye vyeti vyangu Jina langu ni Gift Jonathan Charles ambalo ndilo jina la babu yake mama, na hii ilifanyika makusudi ili k uficha ubini wangu, kumlinda mzee,
Hakukua na tatizo lolote kwani wakati ambao nilitaka kuongea na baba niliongea nae na hakuna kitu ambacho ningekosa
Nakumbuka siku hiyo nilikua najiandaa kwenda chuo kikuu majira ya saa moja usiku nilishangaa kuona gari la baba nje, nilistuka kidogo kwakuwa ilikua ni siku chache tu zimepita alikua pale,
โlabda amekuja kuniagaโ nilisema huku nikishuka ngazi haraka kutoka nje kumpokea baba,
Uso wake haukuwa na furaha kama siku zote lakini alionyesha bashasha,
โmama yako yupo?โ alisema haraka akiingia ndani
โndio yupo chumbani kwakeโ nilisema nikirudi zangu โjuuโ kupanga mizigo yangu kwani nilikuwa miongoni mwa wanafunzi watano tuliopata ufadhili wa masomo kusoma nje ya nchi
โmzee alipitiliza ndani huku walinzi wake wakibaki nje, namkumbuka mmoja aliitwa Joshua โ
Baada ya masaa mawili hivi niliona baba akiondoka zake na mimi niliamua kushuka chini kumfuata mama na kumkuta Sebuleni analia
Sikujua hata pa kuanzia lakini mama aliniita na kuniambia yaliyojiri
โbaba yako anateuliwa kuwa Raisi kwenye chama chake mwaka ujao, kutokana na ushindani uliopo kwenye Chama ni yeye na Waziri mkuu wa sasa ndio wanapewa nafasi kubwa sana hata hivyo mheshimiwa Raisi anataka kumuachia yeye kijitiโ
Alisema mama
โsasa mbona unalia?โ nilimuuliza mama
โiko hivi, mimi ni mchepuko tu mwanangu, mimi ni mchepukooo!โ alisema kwa hasira akitupa glass ya maji sakafuni
โah sijaelewa mamaโ
โiko hivi mwanangu Gift kuanzia sasa hivi baba yakao hatakuja tena hapa! Kwa ufupi hutakutana nae popote sio wewe tu lakini hata mimi piaโ alisema akilia
โmama kwanini Lakini?โ nilisema nikiwa sielewi
โmwanangu wewe ni msomi sasa unajua, Raisi hatakiwi kuwa na makando kando, kuanzia keshoa anaanza kufuatiliwa hata akienda chooni, anayetakiwa kuwa nae bega kwa bega ni mke wake wa ndoaโ alisema mama
โnaelewa mama, sasa bado nashindwa kuona kwanini unalia!โ nilisema
โleo amekuja kutupa tahadhari kuwa mkewe amejua tunapoishi hivyo tuwe makini na ikibidi tuhame kabisa hata nje ya nchi mapaka uchaguzi upiteโ alisema mama kwa uchungu
Sasa nilielewa uzito wa lile jambo, na sikuona namna ya kufanya, mama yangu hakuwa na ndugu tuliyeweza kumfahamu zaidi alituambia tu kuhusu baba yake ambaye alifariki alipokuwa mdogo na mama yake alifariki wakati akijifungua, na akaenda kulelewa katika kituo cha watoto Yatima cha Samaritan Morogoro ambapo alisomeshwa na wamisionari mpaka alipofika UDSM na kukutana na baba yangu,
Hata hivyo kwa macho na kwa vitendo baba yangu alinipenda sana na alimpenda mama yangu pia alishamfungulia miradi mikubwa sana na kumuachia pesa nyingi kabla ya uchaguzi na alimuahidi kuwa nae bega kwa bega
Wakati naondoka pale sebuleni mama alinipa barua ambayo ilikua imetoka kwa mzee
๐ ...itaendelea !!
full 1000
0784468229
Makala nyingine zinazocheza na ladha yako
Mapendekezo haya yanatokana na kile unachosoma sasa + Endelea kugundua zaidi






Maoni