PENZI LA MHALIFU 25
Cyborg aliamua kutumia nguvu na sikutaka kumzuia zaidi ya kumuacha anizagamue japo nilikuwa sina hamu kabisa ya kufanya sex na yeye.
Baada ya kumaliza kunizagumua aliniambia.
"Malaika ina maana utaendelea kununa mpaka lini au umenichoka na unataka tuachane!?"
"Sijakuchoka ila umekuwa ukirudia makosa yale yale karibu kila siku, ina maana nisingewakuta wewe pamoja na huyo mwanamke ulikuwa unamzagamua sindio!?"
nilimuuliza na Cyborg alikiri kweli ningechelewa kidogo tu ningekuta tayari wameshaanza kuzagamuana.
Nilimwambia kuanzia siku hiyo aache kazi ya kuhubiri na atafute kazi nyingine kwani ata kuhubiri kwenyewe ilikuwa ni ilimradi tu ili aweze kujipatia sadaka.
Cyborg alinikubalia, na kwakuwa alikuwa ni mpambanaji alipanga kutafuta kazi nyingine ya kufanya.
Siku iliyofata nilivaa nguo zangu za kiasikari na kwenda kwenye nyumba ya jirani yangu kwa ajili ya kumpiga mkwala, nilienda huku nikiwa nimeshika bastora mkononi.
Nilimwambia jirani yangu asirudie tena kumuwekea mitego Cybrog lasivyo asije kunilaumu kwa maamuzi nitakayoyachukua, jirani aliogopa na baadae aliniahidi hatarudia tena kumtega Cyborg.Tangu siku hiyo jirani alikaa mbali na sisi na hakutufatilia tena.
Siku moja tukiwa tumelala usiku, tulisikia sauti ya mawe yakipondwa kwenye madirisha ya nyumba yetu na kwakuwa madirisha yalikuwa ya vyioo yaliweza kupasuka baada ya kupondwa na mawe.
Mimi na Cyborg tuliamka na kwenda kuangalia mtu aliyefanya tukio hilo ila hatukubahatika kumuona.
"Huyu mjinga gani anayetaka kutuletea michezo ya ajabu!?" Cyborg aliuliza huku akiwa na hasira ata mimi pia nilikuwa kwenye hasira kwani ilikuwa ni hasara kwetu kwa madirisha kupasuliwa.
Usiku huo ulipita na siku iliyofata majira hayo hayo ya usiku tulisikia mtu akilusha jiwe batini, na kutufanya tuamke kwa mara nyingine tena kwa ajili ya kwenda kuangalia.
Tulifika nje lakini hatukuona mtu yoyote yule zaidi ya kukutana na ukimya wa hali ya juu.
"Malaika wewe nenda ukalale mimi nitajificha kwa ajili ya kuangalia ni nani anayetufanyia huu mchezo" Cyborg aliongea na mimi niliamua kurudi ndani nikimuacha Cyborg nje mwenyewe.
Alikaa kwa mda mrefu bira kumuona mhusika. na kwakuwa kulikuwa na kaubaridi Cyborg aliingia ndani na alipofika alinisogelea na kunikumbatia huku akiniandaa kwa ya kufanya sex usiku huo. ile tumeanza kuzagamuana tulisikia jiwe kwa mara nyingine na temu hii halikutupwa moja bali yalitupwa zaidi ya mawe matatu kwa mkupuo.
Cyborg hakutaka kujali kama yupo uchi, alinyenyuka na kuchukua kitenge changu nakutoka mpaka nje, na alipofika alisikia kishindo cha mtu kukimbia.
Cyborg hakutaka kumuacha alianza kumkimbiza huku akiwa ameshika kanga na baadae aliona kanga inamfanya asikimbie vizuri hivyo aliitupa nakuanza kumkimbiza hivyo hivyo akiwa uchi, bahati mbaya hakufanikiwa kumpata.
Cyborg alirudi akiwa uchi na mimi nilipomuuliza aliniambia kuwa hajabahatika kumuona.
"Niachie mimi hiyo kazi mme wangu kesho lazima tumshike na atatueleza vizuri" nilimjibu Cyborg na wote tuliamua kulala.
Siku mbili zilipita bira ya mtu aliyekuwa akituletea usumbufu kuja hivyo tuliamua kuifanyia ukarabati nyumba kwa kuweka vyioo vingine.
Baada ya siku kadhaa kupita tuliweza kupata usumbufu tena na safari hii tulikuwa tumeshajiandaa, mimi na Cyborg tulitoka nje haraka nakuanza kumkimbiza mtu aliyekuwa akileta fujo kwenye nyumba yetu na bahati nzuri Cyborg alifanikiwa kumshika.
Kumbe alikuwa ni yule kijana mvuta bangi niliyempeleka selo wiki kadhaa zilizopita.
"Kumbe wewe ndiyo unayetuletea usumbufu kwenye nyumba yetu?" Cyborg alimuuliza baada ya kumshika.
"Na bado sitaishia hapa tu mpaka malaya wako akubali kunipa kitumbua chake" aliongea na kwakuwa alikuwa ameshajiandaa alichomoa kisu na kumkata Cyborg kwenye mkono ili amwachie na apate nafasi ya kukimbia.
Mimi ilibidi nichukue siraha yangu na kumpiga risasi ya kichwani kijana aliyemshambulia Cyborg na kufariki hapo hapo.
Sikuwa na wasi wasi wowote ule sababu nilijua nitajitetea vipi kwenye mikono ya sheria.
Nilimuwahi Cyborg na kwenda kuangalia jeraha alilokuwa amelipata.
"Pole mme wangu, huyu mpuuzi ameshakufa tayari" niliongea huku nikijaribu kumpatia huduma ya kwanza Cyborg.
Ilibidi niwapigie simu polisi wenzangu na walipokuja niliwaeleza kila kitu kilichotokea na hakukuwa na kesi tena zaidi ya mwili wa kijana niliyemuua kuchukuliwa na kupelekwa kwa ajili ya kwenda kufanyiwa uchunguzi.
Afande Joel alinipa pole kwa kilichotokea ila aliniambia kuwa ana maongezi na mimi ya private na angeomba tuonane siku nikiwa na mda. sikutaka kumkatilia sababu alikuwa ni mfanyakazi mwenzangu tuliyekuwa tunaheshimiana.
Tulipanga siku ya kukutana kwa ajili ya maongezi kama akivyokuwa akihitaji.
Basi hali ya Cyborg ilitengemaa na siku niliyomuahidi Afande Joel kwa ajili ya kuonana ilifìka.
Nilienda kuonana nae na Afande Joel aliniambia sababu iliyomfanya atake kuonana na mimi.
"Angel utanisamehe kwa hichi nitakachoenda kukwambia" Afande Joel aliongea na nilianza kuhisi kuna kitu alichopanga kuniambia ambacho sio kizuri kwa upande wangu.
Afande Joel aliniambia kuwa ametokea kunipenda na angetamani tuwe kwenye mahusiano ya siri, nilishindwa kuelewa ni kitu gani nilichonacho cha mhimu mpaka ifike hatua karibu kila mwanaume atamani kuwa na mimi huku wakiwa wanajua nimeolewa na nipo kwenye ndoa......ITAENDELEA.