PENZI LA MHALIFU 30
Cyborg alianza kumwambia mambo mengine mengi aliyokuwa akiyajua yeye na kumbe kipindi wao wanaongea boss wao alikuwa nyuma yao akisikiliza mazungumzo yao.
Baadae alikohoa na kuwafanya wageuke nyuma na kusitisha kile walichokuwa wakikizungumza..
"Endeleeni tu na maongezi yenu" boss wao aliwaambia ambae ni mchepuko wa Afande Joel na Cyborg hakutaka kusitisha mazungumzo yao zaidi ya kuendelea kuongea.
Mda wa kazi ulipoisha Cyborg alirudi nyumbani na alipofika alinisimulia kila kitu kilichotokea kazini kwao.
Sikutaka kujali kile alichoniambia kwani niliona ni mambo ya kawaida tu.
Basi Cyborg alipoenda kazi siku iliyofata alishangaa kuona akichangamkiwa na boss wake ambae ni mchepuko wa Afande Joel au kwa jina alikuwa akiitawa Salome na siku iliyofata hivyohivyo napo alichangamkiwa.
Cyborg nae aliamua kujiachia na kutengeneza mazoea na boss wake.
Mimi huku nilikuwa sina habari zozote ya kilichokuwa kikiendelea, siku hiyo nilishuhudia Cyborg akija nyumbani na gari hivyo niliamua kumuuliza.
"Cyborg na hii gari umeitoa wapi!?"
"Hii ni ya boss wangu, sasa ivi napatana nae balaa na ananiamini sana" Cyborg aliongea na mimi niliishia kuguna kwa kile alichokiongea.
Basi siku hiyo ilipita na siku iliyofata Cyborg alikuja na gari kwa mara nyingine kama siku iliyopita.
Niliona kuna kitu hakipo sawa hivyo niliamua kumuuliza Cyborg ni kipi kinachoendelea lakini Cyborg alinitoa wasi wasi nakuniambia hamna chochote kile zaidi ya ukaribu alionao kwa boss wake.
Siku hiyo usiku tukiwa tumelala kwa mara kwanza tangu Cyborg anioe hakunigusa yani hakutaka tutiane kabisa.
Nilishangaa sana sababu haikuwa kawaida ya Cyborg na ata siku ambazo tulikuwa hatufanyi mapenzi basi ilikuwa ni lazima anikumbatie.
"Cyborg kuna tatizo gani mbona leo hutaki ata kunishika!?" ilibidi nimuulize sababu uvumilivu ulinishinda kabisa.
"Malaika leo nimechoka balaa na kingine sijisikii kufanya mapenzi kabisa"
Cyborg alinijibu na kuendelea kulala, nilishindwa kumwelewa kiukweli kwani haikuwa kawaida ya Cyborg. Basi usiku huo ulipita.
Siku iliyofata nikiwa kazini mimi pamoja na asikari wenzangu nilimuona Afande Joel akiwa bize kuongea na simu na baadae aliondoka bira kumuaga mtu yoyote yule.
Sikutaka kufatilia mambo yake ila baada ya mda kupita nilipigiwa simu huku namba ikiwa ni ya mme wangu na sauti iliyosikika haikuwa ya Cyborg bali ilikuwa ni sauti ngeni kabisa ya mwanaume mwingine kwenye masikio yangu.
"Njoo ushuhudia ugomvi ulioko huku wa mme wako" aliongea na kukata simu bira ata kujitambulisha kwangu.
Nilishindwa kuelewa sababu sikujua nisehemu gani ninayotakiwa kwenda na kingine kilichonichanganya zaidi ni baada ya yeye kuniambia kuna ugomvi.
Niliamua kujiongeza mwenyewe kwa kuelekea sehemu aliyokuwa akifanyia kazi Cyborg. ilibidi nichukue usafiri na kuwahi sehemu husika.
Sikuamini kile nilichokikuta kwani niliwakuta baadhi ya watu wakiwa wanahangaika kuwatuliza Cyborg pamoja na Afande Joel na nilipoangalia kwa umakini nilimuona kijana aliyekuwa ameshika simu ya Cyborg na nilipata uhakika wa karibu asilimia zote kuwa ndiye aliyenipigia simu na kunitaka nifike pale haraka na upesi.
Afande Joel alikuwa akiongea maneno ya kila aina akimtuhumu Cyborg kuwa anatembea na mchepuko wake ambae ni Salome huku akimtishia lazimi ampeleke gerezani na upande wa Cyborg kama ilivyokuwa kawaida yake huwa hatuogopi kabisa sisi maasikari aliamua nae kumpolomoshea kila aina ya maneno na matusi kama msenge tu, utanifanya nini wewe fala na mengineyo.
kwanza niliishiwa nguvu kwa ugomvi uliokuwa ukiendelea pale na nikiwa najiandaa kusogea karibu yao ili Cyborg aweze kuniona alitokea boss wao ambae ni mchepuko wa Afande Joel anayeitwa Salome na kuongea.
"Joel mimi na wewe tumeshamalizana sihitaji ulete ugomvi kwenye ofisi yangu bira kuwa na sababu za msingi na ukizingatia wewe ni asikari polisi tena hapo ulipo umevaa uniform za kazi, naomba uondoke" Salome aliongea na baadae Afande Joel niliona akiondoka huku akiwa ni mwenye hasira na alikuwa akitamka matusi ya kila aina.
Sikutaka tena kusogea alipo Cyborg niligeuka kwa ajili ya kuondoka lakini tayari Cyborg alikuwa ameshaniona, aliamua kuja nilipokuwa mimi na alianza kuongea mwenyewe bira ata kumuuliza.
"Malaika hamna chochote kile kinachoendelea ni wivu wa huyo Afande Joel" Cyborg aliongea huku akiwa ni mwenye mashaka.
"Tutaongea tukiwa nyumbani" nilimjibu na kuamua kuondoka nakumuacha mwenyewe.
Sikujua tena kilichokuwa kikiendelea baada ya mimi kuondoka na kiukweli sikuwa na hamu kabisa ya kurudi kituoni ila sikuwa na namna zaidi ya kwenda na kusubiri mpaka pale mda wa kazi utakapoisha ndipo nitakaporudi nyumbani kwa ajili ya kumuuliza vizuri Cyborg.
Mda wa kazi ulipoisha nilirudi nyumbani na kumsubiri Cyborg kwa hamu.
Siku hiyo Cyborg hakurudi na gari la boss wake na alikuja peke yake tu. Aliingia mpaka ndani na baada ya kumuona kitu cha kwanza nilichomuuliza ni kile kilichotokea kazini kwao......ITAENDELEA..