PENZI LA MHALIFU 26
Niliamua kumwambia Afande Joel "Asante kwa kunipenda Afande Joel ila naomba heshima ichukue nafasi yake sababu tayari nipo kwenye ndoa nazani wewe mwenyewe unafahamu"
Niliongea nikiwa na uhakika Afande Joel nimwelewa na nitofauti na alivyokuwa Afande Davi.
"Naelewa kuwa upo kwenye ndoa ata mimi pia nipo kwenye ndoa Angel, nipo tayari kukupa mshahara wangu wote nitakaoupata ila naomba walau mara moja tu unipe penzi lako" Afande Joel aliongea kwa msisitizo.
"Sipo tayari kuzagamuliwa na wewe Afande Joel na siku nyingine ukiniita kwa ajili ya kuniambia ujinga wa aina hii sitaitikia wito wako" niliongea na baadae niliamua kuondoka.
Afande Joel alibaki akiniangalia huku akiwa hamini kama nimeweza kukataa ombi lake.
"Huyu mwanamke mbona anaonekana mgumu sana huyu!?" Afande Joel aliongea baada ya kubaki mwenyewe.
Mimi niliweza kufika nyumbani baada ya kuachana na Afande Joel huku nikiwa na mawazo yangu baada ya kuanza kutongonzwa na Afande Joel.
Siku zilizidi kwenda huku Afande Joel akizidi kunitongoza na kiukweli alikuwa na maneno matamu ya ushawishi na kuna mda alianza kuigeuza akili yangu. ilifika kipindi nilikuwa naogopa kumpa nafasi ya kuongea mbele yangu sababu ya maneno yake yalikuwa na ushawishi sana na kama angekuwa mwanamke mwingine asiyejielewa tayari angekuwa ameshafanya sex na Afande Joel.
Upande wa Cyborg alifanikiwa kupata kazi na ndani ya mda mfupi alikuwa ameshajulikana sehemu alipokuwa akifanyia kazi na ajabu boss wa Cyborg alikuwa ni hawala wa Afande Joel.
Siku hiyo Afande Joel alienda kumtembelea mchepuko wake kwenye kituo chake cha kazi na alishangaa kumkuta Cyborg akiwa pale. hakutaka kuonesha kuwa anamfahamu Cyborg zaidi ya kumpa salamu ya kawaida.
Afande Joel alimuuliza mchepuko wake ni mda gani wafanyakazi wake huwa wanatoka kazini kwani alikuwa na mpango wake baada ya kumuona Cyborg. mchepuko wake alimpa ratiba kamili na Afande Joel aliondoka huku akiwa na mpango wake.
Nakumbuka ilikuwa ni siku ya ijumaa na siku hiyo tulitoka mapema kazini, nilifika nyumbani na Cyborg alikuwa bado hajarudi.
Nikiwa ndani nilisikia sauti ya Afande Joel nje ya nyumba yetu na kunifanya niende kumfungulia mlango.
"Karibu Afande" nilimkaribisha na Afande Joel aliingia mpaka ndani.
Nilishindwa kuelewa ni kitu gani kilichomleta na ukizingatia tumetoka kazini mda sio mrefu na mfanyakazi wangu wa ndani hakuwepo mda huo.
"Afande Joel kuna tatizo gani!?" nilimuuliza sababu niliona haongei kitu kilichomleta.
"Ndio Afande tatizo lipo, tena sio dogo"
Alinijibu na mimi niliamua kumuuliza.
"Lipi hilo!?"
Baada ya kumuuliza Afande Joel alitoa bahasha aliyokuja nayo na baadae alitoa pesa zilizokuwa ndani ya bahasha nakunisogelea.
"Hizi ni million 4 nilipata dili sehemu Angel... aliniambia na kabra sijamuuliza aliendelea kuongea mwenyewe....nimeamua kuja kukupatia wewe ila naomba ukubali kunipatia penzi lako walau mara moja Angel" aliniambia na alizidi kuongea maneno mengi ya kunishawishi huku akinikabizi milion 4 kwenye mkono wangu.
Kiukweli niliona utakuwa ujinga wa kukataa pesa kwani ata ningefanya nae mapenzi bado kitumbua changu atakiacha na hataondoka nacho na Cyborg ataendelea kukila kama kawaida.
"Sawa nimekubali ila inatakiwa tufanye upesi" nilijikuta nikimjibu na hakutaka kupoteza mda kwani pale pale alianza kunipapasa na mimi nilianza kufungua mkanda wa suruali yake kwa ajili ya kumvulisha maana sikutaka mambo yawe mengi.
Tukiwa kwenye maandalizi ya kuzagamuana tulisikia mtu akifungua mlango na hakuwa mwingine bali alikuwa mfanyakazi wangu wa ndani akiwa pamoja na mtoto wangu, kiukweli nilijisikia aibu baada ya yeye kutufuma.
ilibidi tusitishe kile tulichotaka kukifanya na nilimwambia Afande Joel aende kwake kwani mazingira hayakuwa rafiki tena.
Afande Joel alikubali na kuondoka huku pesa akiziacha kwenye mikono yangu.
Niliamua kumfata mfanyakazi wangu na kumwambie asije akajaribu kumwambia Cyborg kile alichokiona, na ili kumpoza nilimpatia elfu hamsini ya kumshawishi zaidi asije kutoboa siri.
Nilienda chumbani kujipumzisha huku nikiwa siamini kama nilitaka kuliwa na Afande Joel japo sikutaka kuzirudisha pesa alizonipatia na nilikuwa nimeshafanya maamuzi ya kufanya mapenzi na Afande Joel walau mara moja ili milion 4 zibaki kwenye mikono yangu.
Mda wa Cyborg kurudi nyumbani ulifika na aliporudi alishangaa kuona pesa ndani ya chumba chetu.
"Malaika hizi pesa umezitoa wapi!?" aliniuliza na mimi niliamua kumjibu.
"Nimezipata kwenye dili mme wangu bira kufanya madili maisha hayaendi kabisa"
"Mmmh sawa ila asije kuwa mwanaume kakuhonga ili aje akuzagamue!! siku nikimjua akianane nitakata kichwa chake na nitarudi kwenye maisha yangu ya zamani ya kuvuta bangi" Cyborg aliongea na mimi nilishituka sababu ndiyo ukweli uliokuwepo.
Cyborg aliniambia kuwa alibadilika kwa sababu ya penzi langu na ndilo lililomfanya aache tabia aliyokuwa akiifanya kipindi cha nyuma.
Aliniambia kama nikija kumsaliti basi atarudi kwenye maisha aliyokuwa akiishi zamani ya uharifu.
Nilimkubalia huku nikiwa na langu kichwani, siku hiyo ilipita na kesho yake Afande Joel alitafuta gest na alinipa taarifa nimfate ili tukamalizane kutokana na pesa alizokuwa amenipatia.
Nilibaki njia panda kwani maneno ya Cyborg yalikuwa yakizunguka kwenye kichwa changu na mbaya zaidi kila ninapofanya mapenzi na mwanaume yoyote yule ni lazima anogewe na penzi langu.
Kiukweli nilikuwa njia panda na nilishindwa kufanya maamuzi je? niende kwenye gest kwa ajili ya kuzagamuana na Afande Joel ili milion 4 ziendelee kuwa kwenye mikono yangu au niache kwenda kwa ajili ya kulinda heshima ya ndoa yangu na Cyborg.
Unajua nilifanya maamuzi gani!? usikose sehemu ijayo ili upate kujua..