PENZI LA MHALIFU 43 (FINAL).
Bahati nzuri Cyborg aliweza kupitiwa na usingizi na nilikuja kushituka mida ya saa 11 asubuhi na nilipoangalia niligundua kuwa umeme bado umekatika.
"Mmmh hapa inatakiwa niamke walau nikazuge kufanya mazoezi huko nje, huyu akishituka lazima atataka kuninyandua" nilijiwazia mwenyewe na sikutaka tena kurudi kitandani sababu nilimjua Cyborg hachelewi kuniomba cha asubuhi.
Basi bhana japo kulikuwa na kaubaridi ila niliamua kwenda kufanya mazoezi kwa ajili ya kupoteza mda ili paweze kukucha ile nimefika nje na kuanza kufanya mazoezi Cyborg alifika.
"Mmmh!!!! Malaika, wewe tangu lini ukafanya mazoezi asubuhi ivi tena na baridi hii!?" Cyborg aliniuliza na mimi sikutaka kumuonesha kuwa nachenga mizagamuo.
"Umesahau kama mimi ni asikari!?" niliongea huku nikiendelea kufanya mazoezi yangu.
"Basi twende ndani nikakufanyishe mazoezi mke wangu" Cyborg aliniambia na mimi nilijua lengo lake nikutaka nimpe cha asubuhi.
Nilimkatilia na kuanza kumpa elimu ya jinsi mazoezi yalivyo mhimu kwenye mwili wa binadamu. Cyborg ilibidi akubali na yeye aliamua kukumbushia kwa kupiga pushapu kadhaa.
Moyoni nilijipongeza kwa kuweza kumchenga ila sasa mawazo yote yalikuwa pale mama atakapoamka, sikujua ataniambia kitu gani.
Nilifanya mazoea mpaka saa 12 na Cyborg aliniambia twende tukaoge wote.
"Wewe nenda tu mme wangu mimi nakuja huko mda sio mrefu" niliongea maana sikutaka kwenda kuoga nae pamoja kwani nilazima tungenyanduana huko huko bafuni.
Cyborg alishindwa kunielewa ila aliamua kwenda kwa ajili ya kuoga.
Cyborg alipomaliza kuoga na mimi nilienda kuoga na baada ya kumaliza nilivaa haraka nguo zangu za kazini.
"Angel leo mbona una haraka hivyo unawahi wapi!?" Cyborg ilibidi aniulize maana siku hiyo akili yangu nilikuwa naijua mwenyewe.
Nilimwambia kuna kazi mhimu hivyo ni lazima niwahi.
Baada ya kumaliza kuvaa nilitoka chumbani na kukutana na mama mlango.
"Mmmmh" mama aliguna baada ya kuniona.
"Mama shikamoo" ilibidi nimsalimie.
"Marahaba mmeo anaonekana yupo vzuri ila mwambie awe anapunguza sauti usiku na kutukana hovyo" mama aliongea na mimi nilijua hakuna siri tena kwani kila kitu kilikuwa wazi.
Niliamua kumkubalia kuwa nitaongea nae na baada ya hapo nilimuaga kwa ajili ya kuondoka ila mama aliniambia siku inayofata ataondoka.
Nilienda kazini siku hiyo na siku iliyofata mama aliondoka na sisi tuliendelea na maisha kama kawaida.
Siku iliyofata kwakuwa ilikuwa ni siku ya mapumziko niliamua kwenda kwenye duka la Cyborg.
Nilimkuta Cyborg akiwa kakaa na mwanamke mnene aliyejaza mchina kwenye makalio yake na alionekana ni mteja waliyezoeana kwani niliwakuta wakipiga story huku wakicheka. basi niliamua kuungana nao na kupiga story.
Baada ya mda mwanamke tuliyekuwa tukipiga nae story aliaga na kuondoka na kutuacha sisi wawili.
Dekika kadhaa zilipita tukiwa sisi wawili dukani na Cyborg aliamua kuniambia.
"Malaika kuna sehemu naenda kuangalia mzigo mara moja naomba uniangalizie hapa" Cyborg aliongea nakunipa maelekezo ya bei husika ya bidhaa zake.
Nilibaki mwenyewe na baada ya dekika kadhaa alikuja kijana aliyetokea kwenye duka la jirani na kunisalimia.
"Sister samahani wewe ni mke wa jamaa anayeuza hapa!?" aliniuliza na mimi niliamua kukubali kuwa ni mke wa Cyborg ila bado nilikuwa njia panda sababu sikujua thamila yake.
"Kwanini umeniuliza hivyo kwani kuna tatizo!?"
Baada ya kumuuliza aliamua kunijibu.
"Ndio tatizo lipo jamaa yako ni kitombi sana kwa mademu za watu"
"Mmmh" ilibidi nigune baada ya kusikia kuwa Cyborg anatembea na wanawake wa watu.
"Huenda umekosea mme wangu hayuko hivyo" nilipingana na kile alichoniambia ila aliniambia kama siamini basi nimpe namba zangu ili aweze kunionesha ushahidi.
Nilimtajia namba zangu kisha baada ya hapo aliondoka na kuniambia atanitumia ushahidi.
Nilibaki mwenyewe huku nikiwa natafakari maneno aliyoniambia kijana aliyeondoka mda sio mrefu na kuna mda niliamini maneno yake hasa baada ya kukumbuka jinsi nilivyomkuta Cyborg akiongea na mteja tena wakiwa wanacheka kabisa.
Niliendelea kukaa kwenye duka la Cyborg na baada ya masaa kadhaa kupita Cyborg aliweza kurudi.
Sikutaka kumuuliza Cyborg juu ya kile nilichoambiwa na nilipanga kuanza kufanya uchunguzi mwenyewe.
Baada ya kukaa kwa mda mrefu niliondoka na kurudi nyumbani na kumuacha Cyborg mwenyewe.
Siku mbili zilipita na siku ya tatu nikiwa kazini kwangu niliweza kupigiwa na namba ngeni na nilipoipokea ilisikika sauti ya mwanaume na alijitambulisha kwa jina la Oscar na alinikumbusha vizuri kuwa ndiyo yule kijana niliyempatia namba siku niliyoenda kumtembelea Cyborg dukani kwake.
Oscar aliniambia niende kwenye duka lake ili anioneshe jinsi mme wangu Cyborg anavyochepuka.
Niliamua kuondoka nikiwa na nguo zangu za kazi na sikutaka kutumia gari langu kwenda sehemu niliyoelekezwa.
Nilifika mpaka kwenye duka alilokuwemo Oscar na alishituka baada ya kuniona nikiwa na sare za kiasikari.
"Aya niambie yupo wapi mme wangu!?" ilibidi nimuulize baada ya kuona duka la Cyborg limefungwa ila nilishangaa kumuona Oscar akizidi kuniogopa zaidi.
"Sinakuuliza mbona upo kimya!?" nilimuuliza kwa mara nyingine na aliamua kuongea.
"Samahani umechelewa kwani ameondoka mda sio mrefu mme wako akiwa na mchepuko wake" alinijibu huku akiendelea kuwa na wasiwasi.
Baada ya kuniambia vile niliona kama ananipotezea mda hivyo niligeuka kwa ajili ya kuondoka lakini kuna kijana mwingine aliyekuwa duka la jirani aliamua kuniita.
Kipindi naenda kuonana na kijana mwingine akiyeniita nilimuona kijana aliyekuwa akiitwa oscar akifunga duka lake na kuondoka huku akionekana ni mtu mwenye wasiwasi.
Nilifika mpaka kwa kijana aliyeniita aliyenisalimia baada ya mimi kufika pale kisha baada ya hapo aliniambia.
"Afande samahani, yule kijana alitaka kukuchonganisha wewe na mme wako na siku ile alikuambia vile ili aweze kupata namba yako ya simu na siku ya leo alipanga kufanya mapenzi na wewe kwenye duka lake" aliongea na alinifafanulia zaidi kuwa yeye na kijana yule hawapatani kwani walikuwa na ugomvi na ndiyo maana ameamua kuniambia ukweli.
Dah kweli kila mwanaume ananjia zake za kutongoza niliongea mwenyewe baada ya kugundua kuwa ilikuwa ni mipango ya yule kijana Oscar ili aweze kufanya mapenzi na mimi. nahisi kilichomwogopesha ni baada ya kuniona nikiwa na sare za kiasikari.
Nilirudi kazini kwangu na baadae nilipata uhakika mwenyewe kuwa Cyborg hanisaliti kwani upendo uliongezeka mara dufu kwenye ndoa yetu.
Kidogo usumbufu wa kutongozwa ulipungua hasa kutoka kwa asikari wenzangu na ata mtoto wa mbunge aliacha kunifatilia baada ya kugundua kuwa ni mwanamke mwenye msimamo na nilikuwa mgumu kugawa kitumbua changu hovyo.
Basi tuliendelea na maisha mimi pamoja na Cyborg huku nikiwa bado na watoto wangu wawili na sikuwa na mpango kabisa wa kuacha kazi yangu ya uasikari.
Pia mme wangu Cyborg nae biashara yake ilizidi kuimalika na mpaka sasa tuna miliki magari mawili na tumejenga nyumba nyingine ya kisasa.
Upande wa mdogo wangu Anna alibahatika kuolewa na mwanaume mwingine na alibahatika kupata mtoto mmoja.
Bira kusahau mtoto wa Cyborg aliyezaa na dada wa kazi bado aliendelea kumhudumia na kutoa matumizi ya msingi yaliyokuwa yakihitaji.
Ninachoshukuru kwa Cyborg mpaka namaliza kusimulia mkasa huu hakuwa kuuchoka mwili wangu na kila siku nilikuwa mpya kwake japo ni mwanaume aliyekuwa na udhaifu wake lakini siku zote wanasema hakuna binadamu aliyekamilika kila mtu anamadhaifu yake.
Asanteni sana kwa kufatilia mkasa huu naamini mtakuwa mmejifunza mengi kwenye story hii nawapenda sana ?????
MWISHOOO.