PENZI LA MHALIFU 23.
Siku kadhaa zilipita, nakumbuka ilikuwa ni siku ya jumamosi na ilikuwa ni mida ya saa moja jioni, siku hiyo nilikuwa nikitembea peke yangu huku nikiwa nimevaa nguo za kawaida tu na kwakuwa nilikuwa bado sijayazoea vizuri mazingira nilifika kwenye uchochoro na kukutana na kundi la vijana waliokuwa wakivuta bangi.
Japo nilikuwa asikari ila niliogopa baada ya kuwaona vijana waliokuwa wakivuta bangi na ukizangatia nilikuwa kwenye mazingira hatarishi kidogo.
Sikutaka kuwasemesha zaidi ya kuendelea na safari yangu ila kijana mmoja aliniita na mimi nilijifanya kama sijamsikia.
Kijana aliyekuwa akiniita alikasirika baada ya kuniona nikiendelea na safari yangu bira kuitikia wito wake, aliamua kunifata na aliponifikia aliyashika makalio yangu nakuniambia.
"Oya sister nakuita alafu wewe unajifanya usikii sio?" Aliongea huku mdomo wake ukitoa harufu ya bangi.
Sikutaka kuwa mnyonge mbele yake na ukizingatia mimi ni asikari.
"Ivi unajua mimi ni nani!?" niliamua kumuuliza.
"Wewe si malaya kama malaya wengine tu sister, twende nikakutie" kijana alinijibu.
Baada ya kuniambia maneno yale niliona anataka kunizoea kwani nilimpiga teke lililompeleka mpaka chini.
"Kuwa na adabu mjinga wewe" niliongea na kuondoka huku nikimuacha akiugulia maumivu.
Baada ya mimi kuondoka wenzake walianza kumcheka na kumwambia kakubali kupigwa na mwanamke kizembe hivyo na yeye hakutaka kukubali.
Nikiwa natembea kuelekea kwangu kumbe alikuwa akinifatilia bira mimi kujua. nilifika mpaka kwangu na kabra sijaingia ndani nilisikia kijana aliyekuwa akinifatilia akiongea kwa sauti ya juu.
"Kumbe wewe malaya unakaa hapo lazima nije nikutie siku moja" aliongea na sauti yake waliisikia mpaka majirani zangu.
Cyborg mda huo alikuwa ndani na alitoka baada ya kuisikia sauti ya kijana mvuta bangi aliyekuwa akiniongelesha.
Cyborg baada ya kumuona kijana aliyekuwa akiniongelesha hasira zilimshika na kumsogelea na kijana huyo kutokana na bangi alizokuwa amevuta alijiamini na alikuwa na uhakika kuwa Cyborg hawezi kumfanya kitu chochote kile.
Cyborg alianza kuongea maneno ya kila aina baada ya kumfikia.
"Nani amekupa ruhusa ya kumuita mke wangu malaya!?"
"Huyo Malaya tu na lazima nije nimtie siku moja, atakuja kukupa habari zangu" aliendelea kuongea kwa kujiamini.
Cyborg alishikwa na hasira na kuanza kupigana nae, na kutokana na nguvu alizokuwa nazo alimzidi na kwa bahati mbaya alimsukuma chini na kwenda kuanguka kwenye jiwe na kusababisha apate jeraha kwenye kichwa chake.
Ilibidi nimfata kwa ajili ya kumzuia sababu niliona anaelekea kumuua.
"Malaika mwache nimuue huyu mpumbavu yani anakuita malaya na anabahati nimeacha kuvuta bangi leo ningemtusua na baadae ningeita masela wamzibue kabisa huko nyuma" Cyborg aliongea huku akiwa na hasira na majirani walitoka kwenye nyumba na kusogea kwenye nyumba yetu kwa ajili ya kuangalia ugomvi uliokuwa ukiendelea.
Ilikuwa ni aibu kwangu nikiwa kama asikari ugomvi kutokea ndani ya nyumba yangu, na kwakuwa kijana aliyepigwa na Cyborg alikuwa bado akiugulia maumivu niliingia ndani na kuchukua pingu yangu kisha baada ya hapo nilitoka na kwenda kumfunga kijana aliyekuwa akiniita Malaya na kunitukana kila aina ya matusi.
Kijana alishangaa kuona na mfunga pingu na kuanza kumvuta kumpeleka kituoni huku Cyborg akinisindikiza kwa ajili ya usalama wangu kwani yalikuwa ni majira ya usiku.
"Wewe Malaya mbona umenikamata peke yangu na huyo Malaya mwenzako umemuacha?" aliongea akimaanisha kuwa Cyborg ni Malaya mwenzangu.
Cyborg alimpiga kofi lililomfanya apige kelele kama mwizi aliyeshikwa na wananchi wenye hasira kali. kidogo ilisaidia na kumfanya apunguze kupiga kelele.
Nilimfikisha kituoni na asikari waliokuwa zamu walimchukua na kwenda kumuweka selo.
Afande mwenzangu aliniuliza kilichotokea na mimi niliamua kumsimulia kila kitu.
"Hawa vijana wanazidi kuongezeka siku hadi siku na bahati mbaya bangi zao wakishavuta wanawaza kufanya ngono na kuiba, hamna kitu cha maana wanachowaza" asikari mwenzangu aliongea na mimi nilikubaliana na maneno yake.
Mimi na Cyborg tuliamua kurudi nyumbani na Cyborg hakuacha kuniuliza ilikuwaje mpaka kibaka akanifatilia na ukizingatia kuwa mimi ni asikari.
Nilimsimulia kila kitu kilichotokea na Cyborg alinisihi nisije kurudia tena kupita kwenye vichochoro vya wavuta bangi.
Basi siku hiyo ilipita na siku kadhaa zilipita, na upande wa mme wangu Cyborg nilishangaa kumuona siku hiyo akijiandaa na kuvaa kichungaji hivyo ilibidi nimuulize.
"Mme wangu unaenda kanisani au?"
Baada ya kumuuliza Cyborg aliniangalia na kuniambia.
"Naenda kuhubiri watu waache maovu na wamrudie mungu"
Nilimshangaa baada ya kuniambia vile sababu ata yeye tu alikuwa bado hajaacha tabia yake yakutoa kila aina ya maneno wakati wa kufanya sex......ITAENDELEA.