PENZI LA MHALIFU 15.
Nakumbuka ilikuwa siku ya jumatano, siku hiyo nilikuwa kazini kwenye ofisi niliyokuwa nikikaa mimi pamoja na Afande Neema. Kwenye chumba hicho cha ofisi yetu Afande Neema hakuwepo zaidi ya mimi peke yangu nilikuwa nimekaa mwenyewe tu.
Nilisikia mtu akigonga mlango na kabra sijaenda kufungua aliingia Mkuu wetu na moja kwa moja alinifata mpaka nilipokuwa nimekaa.
Mkuu baada ya kunifikia alianza kunikumbatia huku akitumia nguvu, kitu kilichoanza kuniogopesha kwani mlango hakuufunga baada ya yeye kuingia kwenye ofisi yetu na mtu yoyote kama angetuona basi lazima angehisi natoka nae kimapenzi.
"Unakichaa mkuu!?" nilimwambia lakini bado alizidi kunikumbatia huku akiniziba nisiweze kuona mlangoni.
Baadae niliamua kutumia nguvu kwa kumsukuma. aliamua kujitoa kwenye mikono yangu nakuondoka mwenyewe huku akiwa anatabasamu.
Sikujua ni kwanini aliamua kufanya vile ila mimi niliachana nae na kuendelea na kazi zangu.
Siku hiyo ilipita na siku iliyofata nyumbani kwangu niliona mabadiliko makubwa kutoka kwa Cyborg kwani alipunguza kunichangamkia na alionekana ni mtu mwenye mawazo.
Nilijaribu kumuuliza Cyborg tatizo nini mpaka awe kimya kiasi hicho ila Cyborg hakutaka kuniambia.
Siku tatu zilipita huku Cyborg akiwa hana raha kabisa.
Nilizidi kushangaa kwani alikuwa hataki kufanya mapenzi na mimi, na kila tulipokuwa kitandani Cyborg alikuwa akigeukia upande mwingine kabisa kwa kifupi alikuwa hataki tugusane.
Siku hiyo usiku niliamua kumuuliza.
"Cyborg tatizo nini mme wangu mbona sio kawaida yako!?" nilimuuliza ila Cyborg aliniangalia kwa hasira na kuamua kutoka nje bira kunijibu chochote, Kiukweli nilishindwa kuelewa tatizo nini.
ilipita wiki tukiwa hatuna maelewano ndani ya nyumba na Cyborg hakuwahi kufanya mapenzi na mimi.
Ilibidi nimtafute kaka yake na Cyborg na kwenda kuongea nae ili ajaribu kuongea na Cyborg na amuulize tatizo nini. Shemeji aliniambia ataongea na mdogo wake na atayaweka mambo sawa hivyo alinisihi niendelea kuwa mvumilivu na nisichukue maamuzi ya kuachana na mdogo wake.
Maisha hayo niliyazoea japo yalikuwa yananiweka kwenye wakati mgumu kwani nilipoteza tabasamu hasa nilipokuwa kazini, nakumbuka nilikuwa ofisini mimi pamoja na Afande Neema.
Alikuja mkuu wetu wa kazi akiwa kakunja sura na ilionesha ni mtu mwenye hasira.
Alipofika kwenye meza yangu ya kazi alianza kuipiga piga kwa kutumia mikono yake huku akiongea.
"Nenda ukamwambie mme wako aache kutembea na mke wangu lasivyo nitamfanyia kitu kibaya" aliongea na kugeuka kwa ajili ya kuondoka ila niliamua kumuuliza.
"Mme wangu aachane na mke wako!!!?" nilimuuliza lakini hakutaka ata kunijibu zaidi ya kuondoka na kutuacha mimi pamoja na Afande Neema tukimushangaa.
Afande Neema ilibidi aniulize tatizo nini ila nilimjibu sijui chochote kile kilichokuwa kikiendelea.
Nilitamani mda wa kazi uishe haraka ili niweze kwenda nyumbani kwa ajili ya kumuuliza Cyborg.
Hatimae mda wa kazi uliisha na mimi nilirudi nyumbani na kitu cha kwanza nilichotamani kujua nikumuuliza Cyborg ili nifahamu kile kilichokuwa kikiendelea.
Nakumbuka siku hiyo Cyborg alirudi nyumbani mida ya saa 5 usiku, kwanza niliona anataka kunizoea kwa kukaa kimya mbele yangu bira kuniambia sababu inayomfanya akae kimya, nilimfata na kwenda kumkaba.
"Malaika achia shati langu!" Cyborg aliongea akinitaka nimuachie shati lake ila mimi sikutaka kufanya kile alichokuwa akikisema.
"Siwezi kukwachia mpaka uniambie kitu gani kinachoendelea na nani kakupa ruhusa ya kwenda kufanya mapenzi na mke wa mkuu wangu!?" nilimuuliza huku nikiwa namtazama machoni.
Macho yake yalionyesha kuwa ni kweli ameshamzagamua mke wa mkuu wetu sababu hakutaka kuniangalia baada ya kumuuliza vile.
Cyborg aliongea baada ya mimi kumuuliza "mbona wewe umefanya mapenzi na huyo boss wako ila mimi sijakuuliza kitu chochote" Cyborg aliongea kitu kilichonishitua na kunifanya nishangae.
"Mimi Cyborg! lini hiyo nimemvulia chupi yule mpuuzi!?" nilimuuliza na Cyborg hakutaka kuongea sana zaidi ya kuchukua simu yangu nakunionesha picha zilizokuwa kwenye simu yake.
Picha alizonionyesha zilionyesha mimi nikiwa na mkuu wangu wa kazi huku akiwa kanikumbatia na ndipo nilipoikumbuka ile siku mkuu wa kazi aliyokuja ndani ya ofisi yangu nakuanza kulazimisha kunikumbatia.
Ilibidi nimuulize Cyborg "Nani kakutumia izi picha!?"
"Huyo huyo mpuuzi wako na mimi nataka nitembee na mke wake mpaka ajute kufanya mapenzi na wewe haiwezekani ale utamu ninaokula mimi" Cyborg aliongea.
"Niombe msamaha haraka Cyborg kabra sijafanya maamuzi magumu hapa" nilimwambia maana nilikuwa nimeshachukia tayari kwa kitendo cha Cyborg kufanya mapenzi na mke wa boss wangu huku akihisi analipiza kisasi.
Lakini Cyborg alikataa kabisa na kudai yupo sahihi na anafanya vile kwa ajili ya kulipiza kisasi.
Nilimwambia Cyborg kuwa sijafanya chochote kile na mkuu wangu ila hakutaka kunielewa zaidi ya kuendelea kukomalia kuwa nilishafanya nae mapenzi ndiyo maana nilimpa ruhusa ya yeye kunikumbatia.
Nilijikuta nikipata hasira na sikutaka tena kuendelea kukaa nyumbani kwangu.
Niliamua kumchukua mwanangu nakuondoka nae nikibeba na nguo zangu baadhi huku nikimuacha Cyborg pamoja na dada wa kazi nyumbani.
Safari yangu ilinipeleka kwenye nyumba ya wageni, nilienda kuchukua chumba kwa ajili ya kupumzika huku nikiwa na mawazo kutokana na ugomvi uliokuwepo wa ndoa yangu.......ITAENDELEA.
Inapatikana kwa Tsh 1000 tu.
Namba za malipo.????????????????
0613083801 HALOPESA Jina John Bugumba.
0755271203 M-pesa Jina John Bugumba..