Story......................MISS TANZANIA
Mtunzi...................Zooper
Sehemu..ya...........10
Whatsapp..............0613083801
ilipoishia......
Baada ya simu kukatwa Mwanamama Katalina aliamua kunyenyuka kwenye kiti alichokuwa amekaa na kwenda kwenye gari lake tena akiliondoa kwa kasi na haikufahamika ni wapi anapoelekea........
ENDELEA NAYO..
Mwanamama katalina alienda moja kwa moja mpaka nyumbani kwa mwanadada Angelina,na aliwakuta wakimbebeleza binti Anjelina aliyegoma kabisa kurudi kufanya kazi kwenye kampuni ya FNF,
"Anjelina unajua ni kipi kilichonileta hapa?",mwanamama katalina aliuliza baada ya kufika.
"Hapana mama sijui",Angelina alijibu kwa unyenyekevu wa hali ya juu.
"Kesho jitajidi sana uje kuna zawadi imeandaliwa kwa ajili yako na kampuni tuliloingia nalo mkataba wa nyie kuvaa viatu vinavyotengenezwa na kampuni hilo", Mwanamama katalina aliongea.
"Zawadi ya kuaibika mama na sura yangu nitaiweka wapi", Angelina bado hakukubaliana nae kabisa mwanamama katalina.
Uwepo wa wao watatu kuwa pale yani mwanamama katalina,Manka na mama yake mzazi walifanya ushawishi mkubwa uliomfanya mpaka Angelina akubali kwenda.
Baada ya maongezi ya mda mrefu kati ya Albert na Diana wakiwa bado wanaendelea kuongea, kijana Albert alichukua simu na kuiwasha na baada ya simu yake kuwaka alikutana na ujumbe huku namba iliyotumika kutuma ujumbe huo ikiwa ni ngeni,
"Mama mzazi ni mmoja tu duniani sijui kwanini umesahau kile nilichokwambia kwamba mama yako yupo kwenye hatari Albert",
Ni ujumbe uliosomeka kwenye simu yake na ulimtoa kwenye mudi ya kuendelea kuongea na Diana, ata Diana aliliona hilo.
"Albert kuna tatizo?",Diana ilibidi amuulize baada ya kumuona ameishiwa raha na tabasamu kufutika usoni.
"Ndio diana naomba niende tutaongea siku nyingine", Albert hakutaka kusubiri kuona Diana ataongea nini aliamua kuondoka maeneo yale akimuacha Diana kwenye maswali yasiyokuwa na majibu.
"Huyu itakuwa kuna kitu kinachomsumbua sio bure lakini mimi hayanihusu mambo yake nikipata ninachokitaka ata urafiki kati yangu na yeye lazima ufe, sina kingine cha kufanya zaidi ya kuheshimu makubaliano niliyoweka na baba yangu", Diana aliongea kuonyesha kuwa yupo na Albert kwa sababu flani.
Nae palepale simu yake iliita ilimlazimu aipoke,
na mtu aliyempigia hakuwa mwingine bali ni Stewart,
"Diana nipo nyumbani kwenu nakusubiri nimepiga stori na baba yako mpaka amechoka nakuondoka",Stewart aliongea.
"Ivi unakichaa Stewart nani aliyekuelekeza nyumbani kwetu unawezaje kuja bira kuwa na ruhusa yangu na ulipajuaje?",Diana aliongea maneno ya kutosha na upande wa Stewart hakuwa ata na wasiwasi wowote zaidi ya kumuimiza awahi kurudi nyumbani yupo anamsubiri.
Albert baada ya kuachana na Diana alimtafuta Mary kwenye simu ili ajue ni kwanini amemtumia ule ujumbe na majibu aliyopatiwa ni waonane sehemu tulivu ili waweze kuongea vizuri,
Albert hakujali kama tayali giza limeshaanza kutanda mda huo aliitaji kujua atafanya nini kumsaidia mama yake mzazi alienda mpaka sehemu aliyoitwa na Mary na kufanyikiwa kumkuta akimsubiri,
"Nilijua huwezi kuja",Mary aliongea baada ya kumuona Albert.
"Mama yangu ni mhimu kuliko kitu chochote kile na ndiyo mana nipo hapa nahitaji uniambie nani aliye nyuma ya haya yote unayoniambia", Albert aliongea na mda huo alikuwa bado kasimama.
"relax Albert kwanza unatakiwa ukae ili unisikilize kwa umakini zaidi",Mary aliongea tana akiwa hana wasiwasi wowote ule.
"Aya nimekaa nani anayetengeneza mipango ya kumuangamiza mama yangu kama akishindwa kuwa Miss Tanzania?",Albert kwa mara nyingine tena aliuliza.
"Unataka kumjua huyo mtu?"
"Ndio tena sasa ivi tu"
"Aliyekaa mbele yako ndiyo anamipango ya kumuua mama yako kama tu akikoswa uMiss Tanzania",Mary aliongea.
"Unamaanisha wewe ndiyo una hiyo mipango ya kumuangamiza mama yangu kama usipokuwa Miss Tanzania?".
Albert alinyenyuka kwenye kitu alichokuwa amekaa na kumfata Mary ambae hakuwa na wasiwasi wowote ule.
"Nitakuua nakwambia ukijaribu kumuua mama yangu ole wako umguse na kuanzia sasa ivi nitafanya juu chini usiendelee na mashindano labda sio mimi Albert", Albert aliongea huku mboni za macho yake zikibadilika na kuwa nyekundu.
"Wewe ndio unatakiwa uniogope mimi na sio mimi kukuogopa, naitwa Mary na unachotakiwa kufanya kwa sasa nikunisikiliza kile ninachokitaka, una usiku wa leo tu wakujiuliza uwe upande wangu au ufanye kile unachoona ni sahihi ili mama yako afe, na kaa ukijua sipo peke yangu kwenye hilijambo na ole wako upeleke tarifa polisi usije kunilaumu kwa kitakacho mtokea mama yako Albert, kesho asubuhi nahitaji jibu langu upo upande gani wangu au upande wako?", Mary baada ya kumpiga mkwala Albert alinyenyuka na kuondoka maeneo yale.
"Huyu mwanamke mbona anajiamiani sana, subiri nitamwonyesha",ni maneno yaliyotoka mdomo mwa Albert baada ya Mary kuondoka.
Upande wa Diana alifika nyumbani mida ya usiku na kweli alimkuta Stewart akiwa pale tena wanaongea na baba yake vizuri hali iliyomshangaza kidogo,
"Mwenzako kakusubiri sana na ametoka uingeleza kwa ajili yako", Mr.James aliongea na kumfanya Diana ashangae ni lini Stewart alienda uingeleza ila hakutaka kumwambia baba yake ukweli.
Mr.James ilibidi awapishe kwa ajili ya mazungumzo,
"Stewart ndio ujinga gani huu ulioamua kuufanya?",diana alimuuliza Stewart tena akiwa hana utani ata kidogo.
"Umesahau kama na wewe ulilala nyimbani kwetu Diana?, ata mimi leo nilitamani kuja kulala nyumbani kwenu na uzuri nilikufatilie ile siku bira wewe kujua ndiyo mana imekuwa vyepesi mimi kuja kwenu",Stewart aliongea.
Diana hakuwa na kingine tena zaidi ya kukubaliana na hali na stori mbalimbali ziliendelea lakini Stewart alikuwa tofauti na Albert kwani ni mtu mwenye matani mengi na hii ilimfanya Diana atabasamu na mpaka ulifika mda wa kula wote wakapata chakula kisha baada ya hapo Stewart alionyeshwa chumba anachotakiwa kulala usiku huo.
Upande wa Albert baada ya kufika nyumbani hali haikuwa nzuri kutokana na kile alichoambiwa na Mary aliwaza sana ni kitu gani anatakiwa afanye ili mama yake awe salama mana kwa maneno aliyoambiwa na Mary yalimfanya aanze kuamini kuwa Mary alikuwa anamanishe kile alichokisema.
"Huyu inatakiwa niende nae kwa akili lasivyo nitampoteza mama yangu na ata nikisema niende kutoa tarifa polisi bado haitasaidia kitu zaidi ya kuongeza matatizo zaidi, ngoja nikubaliane nae alafu nione kapanga kufanya nini",Albert akiamua kufanya maamuzi ya kukubali ili aone atakachoambiwa na Mary ni kipi, alipanda kitandani na kulala.
Siku mpya ilifika na Albert asubuhi hiyohiyo alimtumia ujumbe Mary na kumtarifu kuwa yupo tayali kuwa upande wake ili mama yake awe salama,
Ata upande wa Mary baada ya kuupata ujumbe ule alilukaluka kwa furaha nakuona sasa mipango yake inaenda vizuri na amebakiza hatua chache tu afikie kile alichokuwa akikitaka, kwanza alimtarifu Albert wanapaswa kukutana jioni ya siku hiyo na amueleze kiundani zaidi ya kipi anachohitaji,
Angelina nae aliamua kwenda kwenye kampuni ya FNF kama alivyoambiwa na mwanamama katalina na alipofika alishangaa akiitwa ofisini kwa mwanamama huyo,
"Angelina unakumbuka nilichokwambia jana", ndicho alichoongea mwanamama katalina.
"Ndio mama nakumbuka"
"Hii ni zawadi yako imeletwa na hatukutaka washiriki wengine wajue mana ingeonekana jambo la ajabu sana kwa kile kilichotokea jana, yakupaswa uchukue naamini utaipenda".
Angelina aliichukua na kuangalia ndani ya box lile alikutana na simu ya garama na ndio zawadi aliyopatiwa na kampuni ile ya viatu.
"Hutakiwi kukata tamaa tuna miezi miwili tu imebaki fanya mazoezi ya kutembea na viatu vya aina ile na inatakiwa uniahidi kuwa kesho tutakapofanya mazoezi kwa mara nyingine hutoniangusha Angelina".Mwanamama katalina aliongea na kumfanya Angelina kutafakari kile alichoambiwa.
"Nakuahidi na temu hii nitafanya kwa jitihada zangu zote, sitakubali tena kudhalaulika mbele za watu, kuanzia leo mimi nitakuwa mshindani wa kweli kwenye mashindano hayo ya Miss Tanzania".Angelina aliongea kwa kujiamini na ata mwanamama katalina hakuamini kusikia maneno yale kutoka kwa angelina.
Hii ilimaanisha kuwa ameapa kuwa mshindani na sio msindikizaji kwa wenzake kauli aliyozungumza ilimfurahisha sana mwanamama katalina...ITAENDELA.
Nyie bado tunaendelea na simulizi yetu ngoja tuone kama kweli Angelina ataweza kushindana na Mary pamoja na Diana.
NB: Story hii NIYAKUTUNGA na haina ukweli wowote ule unaoendana na taratibu za nchi yetu????????????????.
Pata Story hii mpaka mwisho kwa Tsh 1000 za k???????????????????????? lipia kupitia namba,
0613083801 HALOPESA,John Bugumba..