Story......................MISS TANZANIA
Mtunzi...................Zooper
Sehemu..ya...........16
Whatsapp..............0613083801
ilipoishia.........
haikumfanya apunguze upendo wake na hii ilimfanya ata Mr.James aone utofauti wa kijana Albert na kijana Stewart aliyepunguza mazoea ya kuja kumuona Diana kama ilivyokuwa hapo kabra na hii kumfanya aanze kupunguza chuki alizokuwa nazo kwa Albert.........
ENDELEA NAYO.....
Upande wa kijana Stewart akiwa amekaa na ameshika simu yake macho yake yalikuwa yakitazama picha za Miss Tanzania ambae ni Anjelina hakumkumbuka tena Diana kwa wakati huo na akili zake zilikuwa kwa mwanadada Angelina,
"rafiki yako anaendeleaje?", sauti ya mama yake mzazi ilisikika na kumfanya aweke simu pembeni ili ajibu kile alichoulizwa.
"Rafiki gani mama?"
"Mtu wa ajabu sana wewe kwani Diana sio rafiki yako, wewe sindio ulitukulupua hapa usiku twende tukampe hamasa Diana ya kushinda taji la Miss Tanzania?", mama yake aliongea.
"Aaah kumbe Diana yupo anaendelea vizuri tu japo hataweza kutembea tena na anatumia kiti kutembea sasa ivi"
"Masikini binti bado mdogo na ni mrembo kweli lakini kapatwa na matatizo ya ukilema mapema sana,nafikiri familia yake itakuwa kwenye majonzi sana",mwanamama aliongea.
"Mama ngoja mimi nitoke mara moja", Stewart hakutaka kuka pale nakuendelea kusikiliza story za mama yake mzazi tena zinazomhusu Diana, kiujmla alitaka kusahau jina la Diana ndio mana hakutaka ata kulisikia kwenye masikio yake.
Upande wa Mary akiwa na rafiki yake Faith walikuwa ni watu wakulaumiana hasa Faith alimulaumu sana Mary,
"Mimi nilijua utatengeneza mipango ya maana kumbe hamna kila kitu bora ata mimi nilikuwa kwenye kumi bora",Faith aliongea.
"Albert anajifanya mjanja nilimtisha kwa kumuigizia tu kuwa nitamuua mama yake kama nisipokuwa Miss Tanzania nasikuwa na mpango wa kumuua kabisa,sasa temu hii nitamuonyesha kama mimi ndio Mary", Mary aliongea.
Hasira zake za kushindwa kuwa Miss Tanzania aliamua kuzimalizia kwa Albert na alipanga kutimiza kile alichomwambia Albert.
Faith alishangaa kumsikia rafiki yake akitamka vile,
"Mimi naona unaenda kuwa kichaa yani unataka mpaka umue mtu kisa kutokuwa Miss Tanzania?,emu achana na hayo mambo rafiki yangu yameshaisha tuangalie michongo mingine maisha yaende",Faith aliongea kama kumshauli Mary.
"Huwa sipendi dharau kwenye maisha yangu kwakuwa Albert kanionyesha dharau acha nimuonyeshe mimi ni mtu wa aina gani, na wewe pia kama huna stori zingine unaweza kupotea hapa na usikanyage tena kuanzia leo"
"Heeeeeh!!, makubwa yamekuwa hayo tena aya mimi naondoka ila nilichokwambia kizingatie utaingia matatizoni kwa kufanya kitu ambacho hakina faida yoyote ile",Faith aliongea nakuondoka.
Hasira alizokuwa nazo Mary za kukosa taji la Miss Tanzania zilimfanya mpaka avunje urafiki na Faith akiapa kufanya kile alichomwambia Albert kuwa atamuangamiza mwanamama katalina.
Upande wa Miss Tanzania Angelina aliingia mkataba na makampuni tofauti tofauti na moja likiwa ni kampuni kubwa la uigizaji Tanzania, maisha ya Angelina yalibadilika kwa mda mfupi tu na hakuishi tena uswahilini yeye pamoja na mama yake kwani aliweka mashariti kwenye moja ya kampuni aliloingia nalo mkataba ya wao kumnunulia nyumba.
Akiwa amekaa na mama yake mzazi Miss Tanzania alipata wazo,
"Mama ni mda mrefu leo inatakiwa twende gerezani tukamsalimie baba", Angelina akiwa na mwanamama beatrice aliona ni mda mwafaka wa kwenda kumsalimia baba yake aliyekuwa gerezani.
"Huwa najihisi ni mwenye hatia kwa kumuona baba yako akiwa gerezani bira mimi huenda asingekuwa gerezani, huwa nashindwa kumtazama baba yako usoni",mwanamama beatrice aliongea na kumfanya Angela amsogele na kumkumbatia mama yake kama ishara ya kumtoa wasiwasi.
Mwanamama beatrice alikubali kuongozana na binti yake mpaka gerezani na walianza safari mda huohuo kuelekea gerezani.
Ndani ya gereza anaonekana baba wa makamo aliyekondeana na kuchokeana na hii ni kutokana na maisha ya gerezani yalivyo,akiwa ameka ndani ya gereza asikari alifika,
"Mfungwa namba 12"
"Nipo afande",ilikuwa ni namba ya baba huyo wa makamo aliyefahamika kwa jina Gerald, alisimama na kumfata afande.
Mbele ya macho yake hakuamini kumuona mwanamke aliyempenda kwa dhati na pembeni yake kukiwa na binti mrembo,
"Unawafahamu hawa watu?",ni swali lililotoka kwa afande akimuuliza Gerald.
"Ndio afande ni mke wangu na huyo ni binti yangu na mtoto wangu wa peke",Gerald alijibu na kumfanya afande ampe ruhusa ya kufanya maongezi na watu waliokuja kumtembelea katika gereza hilo maarufu.
"Angelina mwanangu, umekuwa binti mkubwa sasa",Gerald alimwambia binti yake huku akiwa na furaha iliyoambatana na machozi.
"Ndio baba mwanao niko hapa".
Mda wote mwanamama beatrice alikuwa kimya aliwaacha baba na mtoto waonge.
"Nilipata bahati ya kupunguziwa kifungo cha kukaa gerezani nimebakiza miezi 6 tu ya mimi kuwa gerezani sio mda nitaungana na nyinyi tena uraiani",Gerald aliongea na kuifanya familia yake ifurahi baada ya kupata tarifa zile mpya.
Waliongea mpaka pale asikari alipokuja kumchua Gerald na kumrudisha gerezani huku Mwanamama Beatrice na mwanae wakiondoka, Angelina akiwa na furaha kwa alichokisikia kutoka kwa baba yake baada ya kuwaambia mda aliobakiza wa miezi 6 atoke gerezani.
Ni siku ya mapumziko siku hii mwanamama katalina hakwenda katika kampuni ya FNF aliamua kubaki nyumbani na kufanya mambo mengine, na ata mwanae Albert hakuwepo nyumbani siku iyo.
Baada ya mda mrefu pasipo kumpigia mke wake temu hii aliamua ampigie mwanamama katalina tena kwa video call na ata mwanamama katalina alishanga kuona baba yake na Albert amempigia simu ilibidi apoke na wakaanza kuongea huku kila mtu akiwa anamuona mwenzake.
Upande wa nje wa nyumba hiyo mwanadada Mary alienda kukusanya vijana wa mtaani nakuja nao maeneo ya nyumba ya mwanamama katalina, akiwa ndani ya gari lake na kazi aliyotaka kuifanya niyakumteka mwanamama katalina,
"Sikilizeni nimebadilisha mawazo msimuue kwanza tupige pesa alafu mengine badae", Mary aliongea na vijana wake.
"Eleweka Mary kwahiyo tunambeba na kumleta huku nje au anafia hukohuko ndani", moja ya kijana aliongea.
"Punguza bangi jamaa yangu kwani hujamsikia sister Mary alivyosema emu twendeni ndani tukambebe huyo mama na kama tukikuta kuna wengine nikipigo tu nakumchukua mtu wetu sisi hatujali", moja ya kijana aliongea.
Walikubaliana na walisogea mpaka sehemu ya geti nakubisha hodi na haikupita mda alifungua mlinzi ila alipigwa na kitu kizito kilichomfanya aanguke chini na kuzimia palepale.
Mwanamama katalina alikuwa hana habari akiwa bado anaongea na mme wake alishanga kuona vijana wakiingia ndani na ata mme wake aliweza kuwaona kupitia simu ya mke wake,
"Nyie ni kina nani?", mwanamama katalina aliwauliza akiwa na wasiwasi wa hali ya juu.
"Hatuna mda wa kupoteza hapa kamateni twende nae", moja ya kijana aliongea.
Mwanamama katalina alijaribu kuleta ubishi ila hakuwa na nguvu za kuwazuia kwani walimchukua na kumpeleka mpaka kwenye gari lao tena akipewa vitisho vya hali ya juu kama tu atajaribu kunyenyua mdomo wake na kupiga kelele kifo kitakuwa halali yake.
Mary alifurahi kuona vijana wametekeleza agizo lake aliondoa gari kwa speed na mwanamama katalina akiwa ndani ya lile gari.
Upande wa Albert alikuwa hajui kilichokuwa kikiendelea nyumbani kwao akiwa amekaa na Diana akiendelea kumfariji alipowasha data kwenye simu yake alishangaa kukutana na sms nyingi zikiingia na zilionyesha zimetoka kwa baba yake na ndani ya mda huohuo baada ya kuwa online baba yake alipiga simu,
"Fanya unachojua uende nyumbani mama yako hayupo salama", alianza kumwelezea jinsi ilivyokuwa.
"Diana nakuja sasa ivi tu",Albert aliondoka upesi akimuacha Diana kwenye maswali mengi.....ITAENDELEA
Albert atafanyikiwa kumpata mama yake?,na Mary kapanga kufanya nini kwa Mwanamama Katalina?,sehemu ijayo ina majibu zaidi.
NB: Story hii NIYAKUTUNGA na haina ukweli wowote ule unaoendana na taratibu za nchi yetu????????????????.
Pata Story hii mpaka mwisho kwa Tsh 1000 za k???????????????????????? lipia kupitia namba,
0613083801 HALOPESA,John Bugumba..