Story......................MISS TANZANIA
Mtunzi...................Zooper
Sehemu..ya...........26
Whatsapp..............0613083801
ilipoishia......
Mary alivyosikia anataka kuchomwa sindano yanye sumu alitaka kukimbia lakini alikuwa ameshawekwa katikati na sindano ililetwa kwa ajili ya Mary kuchomwa......
ENDELEA NAYO........
Sindano ililetwe na baba mzazi wa Albert akaishika na kumsogelea Mary,
"Usinichome nakuomba bado napenda kuishi tafadhali,nitamtoa mtoto wako na kesi nitaifuta,na kingine nakuahidi sitaisogelea tena familia yako", maneno yalimtoka Mary akijijitetea lakini haikusaidia kitu mzee alizidi kumsogea na kuamlu vijana wamshike ili amchome sindano.
Vijana walimshika na sindano ililetwa Mary akachomwa,
"Hii sindano ina masaa 6 tu wewe kuweza kuendelea kuishi unachotakiwa kufanya ni kwenda polisi kwa miguu yako mwenyewe ukaongee vile unavyojua wewe ila mwanangu siku ya leo hakikisha anatoka,na wewe utakuja nyumbani kwangu kwa ajili ya kuchomwa sindano ya kuondoa iyo sumu....vijana mwachieni na tuondoke kazi kwake ibaki kwake", Mzee aliongea na kuondoka akiwa na vijana wake.
Mary alihisi kuchanganyikiwa kwanza alianza kukimbia kuelekea kituoni ili aendane na mda kama alivyoambiwa alivyofika kituoni alidanganya kumsamehe Albert na pia atalipia garama zote za usumbufu aliotoa kwa jeshi la polisi na mda huohuo Albert aliweza kuachiwa.
Aliachiwa na kumkuta mbaya wake ambae ni Mary ila hakutaka kuongea chochote zaidi ya kuondoka na kwenda nyumbani kwao huku akimuacha Mary akisubili kupatiwa bill ya kwenda kulipa kwa usumbufu aliotoa kwa jeshi la polisi,
"Binti hii hapa bill yako lakini siku nyingine unatakiwa uwe makini usije ukaleta usumbufu tena kwa jeshi la polisi lasivyo selo itakuhusu"
"Sawa Afande nimeelewa"
Afande aliongea na Mary alipewa bill nakuondoka huku kichwa kikiwa kinawaka moto sehemu ya kuipata pesa na kulilipa jeshi la polisi.
Albert aliweza kuwasili nyumbani na kumkuta baba yake kitu kilichomfarahisha sana hakujalia kama alikuwa gerezani alisogea na kumkumbatia baba yake na ata mzee nae alifurahi kumuona kijana wake,
"kijana wangu umekuwa sana inatakiwa tukutafutie mwanamke wa kuoa ndiyo mda wenyewe huu",baba mtu aliongea na kumfanya Albert acheke akiwa na mama yake mzazi.
"Albert ingekuwa vyema ukienda kuoga kwanza mwanangu....
lakini kabra Mwanamama Katalina hajamaliza kuongea aliingia Mary pasipo ata kubisha hodi kama vile ameingia nyumbani kwake,
"Tayali mwanao nimeshamtoa Mzee wangu nichome sindano ya tiba nisije kufa mimi angalia yamebaki masaa mawili tu ili nife nakuomba baba ufanye ivyo"
Weeee usiniite baba mimi siwezi kuwa na binti mwenye tabia ya kijinga ivi, usiyekuwa na huruma na binadamu wenzako, yani kijana wangu unampakazia kosa mtu ambae hana hatia, watu kama nyinyi hamtakiwi kuishi kwahiyo mimi siwezi kukuchoma iyo sindano ya kukutibu na inatakiwa uondoke hapa kwangu",Mzee aliamua kumgeuka mwadada Mary nakuvunja makubaliano waliyowekeana.
Mary alihisi kuchanganyikiwa sababu alijaribu kumuomba msamaha baba mzazi wa Albert lakini bado aliweka mkazo hali iliyomfanya amfate mpaka Albert ambae kidogo aliingiwa na huruma.
Albert alisogea mpaka alipo baba yake,
"Baba naamini atakuwa ameshajifunza binadamu tunajifunza kutokana na makosa tunayofanya, na hii itakuwa fundisho kwake na kwa watu wengine inabidi umchome iyo sindano na aondoke akaendelee na maisha mengine",Albert aliongea akimtetea Mary.
"Binti umeona binadamu anavyotakiwa kuwa huyu ulitaka kumfunga kabisa lakini yeye amekusamehe tena kwa moyo mmoja unabahati angekuwa mtu mwingine sasa ivi usingekuwa kwenye hii dunia"
"Nakuahidi sitarudi tena na wala sitafanya kitendo kama hicho kwa mtu mwingine",Mary aliongea kuonyesha kuwa kathamilia kubadilika.
"Kwakuwa umekili mwenyewe simama na uondoke",Baba Albert aliongea.
"Na sindano je, hunichomi?", Mary ilibidi aulize baada ya kumuona Baba Albert anamwambia aende bira kumchoma sindano.
"Hakuna cha sumu wala nini nilicheza na akili yako tu sisi tumepitia ayo mambo kabra ya wewe kuzaliwa, ile sindano niliyokuchoma ilikuwa na maji", alimaliza kuongea nakuelekea chumbani akimuacha Mary asiamini kile alichokisikia.
Licha ya yote bado alimuomba msamaha Albert na aliahidi kuanzia siku hiyo watakuwa marafiki wenye kujaliana bira kujali ni kipi kiliwahi kutokea kipindi cha nyuma,na tofaut zao wakawa wamezimaliza huku Mary akiondoka nyumbani kwa Mwanamama katalina.
Baada ya miezi 6 Mr.Gerald au baba mzazi wa mwanadada Angelina leo alikuwa akiachiwa huru na siku hiyo Angelina alikuja akiwa na Mwanamama Beatrice kwa ajili ya kumpokea Mr.Gerald,
"Baba Karibu uraiani, tulikukumbuka sana na atimae leo tunaenda kuishi pamoja",Angelina aliongea.
Macho ya Gerald yalikuwa kwenye gari waliyokuja nayo familia yake na uvumilivu ulimshinda ikabidi awaulize Mwanamama Beatrice alimweleza kila kitu Mr.Gerald kwamba binti yake ni Miss Tanzania na maisha aliyoyaacha yamebalika kwa kiasi kikubwa hayapo kama mwanzo,
"Siamini kama binti yangu umeweza kuyabadilisha maisha ya familia yetu kitu ambacho ata mimi nilishindwa mpaka kuingia kwenye kazi za wizi zilizonifanya nikawa gerezani",Mr.Gerald aliongea.
"Baba hayo yameshapita sasa ivi tugange yajayo na wewe sio mwizi tena kuanzia sasa baba".
Walimchukua Mr.Gerald na kwenda nae nyumbani na hii ni baada ya kukaa gerezani kwa mwaka mmoja na sehemu kutokana na kosa la wizi alilowahi kulifanya kipindi cha nyuma.
Nchni Canada baada ya mda mrefu kupita hali ya mwanadada Diana ilianza kutengemaa na sasa alikuwa na uwezo wa kutembea peke yake japo kwa shida ila ilitia matumaini ya kuja kupona mda wowote, huku penzi lake na Doctor Tayler likizidi kuchanua siku hadi siku.
Diana akiwa amekaa na mwenza wake Doctor Tayler alishangaa kumuona mwanadada mrembo mwenye asili ya kihindi akiingia maeneo hayo na kwenda kumkumbatia Doctor Tayler kitendo kilichomfanya Diana apate wivu ila aliamua kunyamaza kimya tu.
Doctor Tayler aliona asipokuwa makini anaweza kugonganisha magari aliamua kunyenyuka na kuondoka na yule mwanadada huku Diana akiwatazama tu jinsi wanavyoondoka.
Doctor Tayler alimfika mpaka nje na mwanadada huyo,
"Naisha mbona unakuja bira tarifa hujui kama na kazi ya kukaa karibu na mgonjwa kipenzi?",Doctor Tayler aliongea akiwa na hasira kwa kumwona Naisha maeneo yale mana aliona mipango yake itavulugika kwa uwepo wa mwanadada huyo.
"Mimi sio mtoto Tayler inaonyesha kuna kitu kinachoendelea kati yenu, kwakuwa upo bize na mgonjwa basi ukiniitaji utanitafuta mweyewe",Naisha aliondoka na kumuacha Doctor Tayler akimtazama.
Mda huo Daina nae alikuwa akija maeneo hayo alimkuta Doctor Tayler kasimama peke yake,
"Mgeni wako yuko wapi mbona ameondoka au umemfukuza?",lilikuwa ni swali kutoka kwa Diana lililomtoa kwenye mawazo Doctor Tayler.
"Aaah yule tulisoma nae na kuna sehemu anaenda sema alipita hapa kunijulia hali tu, lakini nani kakwambia utembee peke yako bira uwepo wangu Diana hii ni hatari kwako emu turudi ndani",Doctor Tayler aliamua kukatisha yale mazungumzo kwa kumwambia Diana arudi ndani.
Naisha alivyotoka kwa Doctor Tayler alienda moja kwa moja kwa rafiki wa Doctor Tayler ili amuulize kile kinachoendelea kati ya Doctor Tayler na mwanadada Diana....ITAENDELEA.
Naisha ataambiwa ukweli wa kinachoendelea kati ya doctor Tayler na Diana? Karibu katika sehemu ijayo.
Pata Story hii mpaka mwisho kwa Tsh 1000 za k???????????????????????? lipia kupitia namba,
0613083801 HALOPESA,John Bugumba..