Story......................MISS TANZANIA
Mtunzi...................Zooper
Sehemu..ya...........05
Whatsapp..............0613083801
Ilipoishia.......
Kutokana na mazingira kuwa mageni kwa Angelina alijikuta akiwa bize kushangaa kuliko kuangalia mbele anakoelekea bahati mbaya aligogana na mtu mtu aliyekuwa mbele yake na kuanguka chini......
ENDELEA NAYO......
Ulikuwa ni mgogano uliompeleka mpaka chini Angelina na alinyenyua uso wake kumtazama mtu aliyegongana nae,
"Nilijua tu, mtu kama wewe hufai kufanya kazi kwenye hili kampuni sijui umempa nini mama mpaka akakupatia iyo nafasi", alikuwa ni Albert aliyegongana na Angelina na kumfanya mwanadada huyo kuanguka.
"Samahani ilikuwa ni bahati mbaya kaka angu sikuzamilia kabisa", Angelina alijibu kwa upole.
"Emu nyenyuka huko unitokee hapa", Albert aliongea kama vile anaongea na mtoto wake, Albert alinyenyuka na kuondoka maeneo Yale.
Tukio lile Mary aliliona na kumfanya asite kidogo kumfata Albert na kufanya kile alichopanga kukifanya.
"Mmmh, kumbe yule kaka ni mkali kiasi hicho,Leo sitakiwi kufanya nilichopanga kufanya ngoja nitafanya siku nyingine ngoja ",Mary aliongea na kuamua kuondoka maeneo yale hakutaka tena kufanya kile alichopanga kufanya.
Albert baada ya kumfukuza Angelina alichukua simu yake nakumpigia Diana,
"griiii,griiiii,griii", Diana aliitazama simu yake na kukuta mtu anayempigia ni Albert,kabra hajaipokea alikumbuka maeno ya baba yake pia makubaliano waliyowekeana aliamua aipoke,
"mambo vip Diana ",sauti ya upande wa mpigaji ilisikika.
"Niko poa dear hofu kwako Albert"
"Njoo katika kampuni yetu ujisajili leo zimebakia siku chache tu usajili ufungwe na pia semina zimekaribia kuanza yakupaswa ufanye haraki kipenzi", Albert aliongea na kumpa tarifa Diana.
"Sasa ivi tu nakuja na pesa za usajili nitakuja nazo hapo",Diana alikata simu na kwenda kujianda ili aende sehemu husika.
Siku zilizidi kusogea huku ikiwa imebaki siku moja tu usajili uweze kufungwa na mwanadada Diana alifanyikiwa kujisajili baada ya kupata msaada kutoka kwa Albert licha ya mwanamama katalina kupinga lakini Albert alilazimisha mpaka akafanyikiwa kumsajili Diana.
Angelina nae alikuwa ameshazoea yale mazingira ya kazi licha ya zalau alizokuwa anapata kutoka kwa baadhi ya wanadada waliokuwa wakija pale lakini alichukulia kama changamoto tu ya kazi,
Siku hiyo alipeleka kinywaji ofisini mwa Mwanamama katalina aliyemkuta kakaa kwenye kiti chake akiaw bize na kuhakikisha usajili wa washiriki,
"Mama ulisema nikuletee cocoa hii hapa", Angelina aliongea huku akiweka kikombe kile cha cocoa katika meza ya mwanamama katalina.
"Ahsante sana mwanangu alafu emu kaa hapo uniambie, historia ya elimu yako ikoje mwanangu?",Mwanamama Katalina.
"Mama mimi nimesoma mpaka chuo kikuu pia na shahada ya biashara na nilimaliza mwaka Jana ila kutokana na ugumu wa maisha imenilazimu nijichanganye mtaani", Angelina aliongea.
"So,you can speak English?"(kwahiyo unaweza kuongea kiingeleza?),Mwanamama katalina alimuuliza Angelina.
"Yes, I can speak (ndio ninaweza kuongea)", Angelina alijibu.
"Safi kabisa mwanangu jiandae na wewe jina lako naliingiza kwenye mashindano ya uMiss Tanzania ", katalina aliongea nakumfanya Angelina atoe macho kwa kile alichokisikia.
"Lakini mama mimi sizani kama nitaweza naomba ubadilishe maamuzi yako",Angelina aliongea.
"Beatrice alikuwa rafiki yangu sana na wewe ni kama mwanangu ndio mana unaniita mama ivyo nisingependa upinge kile ninachokisema, garama zote nitasimamia mimi unatakiwa ufanye kile ninachotaka na usiogope kuhusu kazi yako utakuwa unafanya na kushiriki pia semina zitakazokuwa zikiendelea", mwanamama katalina aliongea.
"Lakin......"
"Mmmh Angelina nimeshamaliza kuongea licha ya ivyo wewe ni mzuri sana ndiyo mana nimeamua kuliweka jina lako kwa watu watakao shiriki",Mwanamama katalina alimaliza kuongea na kumfanya Angelina atoke katika ofisi yake akiwa na mawazo juu ya kile alichoambiwa.
Mda wa kazi uliisha alirudi nyumbani na kumwelezea mama yake kile alichoambiwa na Mwanamama katalina,
"Mimi nina kubaliana na maneno ya rafiki yangu Katalina, mwanangu kushiriki sio dhambi ata Kama ukishindwa halitakuwa tatizo lakini ukishinda unaweza kuyabadilisha maisha yako kabisa, mimi kama mama yako naomba ukashiriki hayo mashindano", Beatrice alimwambia mwanae na kumfanya akubali kushiriki kishingo upande kwa ajili ya kumlizisha mama yake na Mwanamama katalina.
Upande Mwanadada Diana leo aliamua kwenda supermarket na alifika nakuanza kununua vitu vilivyo mfanya awe pale lakini alishituka baada ya mtu kumgusa mgongoni na kumfanya ageuke,
"Tumekutana tena kwa mara nyingine, vip unanikumbuka ?", Sauti ya mwanaume ndiyo iliyosikika katika masikio yake.
"Hapana sikukumbuki kabisa", Diana alijibu na kumfanya mwanaume huyo kucheka.
"Naitwa Stewart, na tulikutana airport nikajitambulisha kwako Diana", Stewart aliongea.
"Umelijuaje jina langu na nani aliyekwambia?",Diana aliongea wakati huo wakitembea pamoja katika supermarket hiyo huku akiendelea kuangalia vitu mbalimbali vilivyomfanya awe pale.
"Umesahu kama plate namba ya gari lako imeandikwa kwa jina lako",Stewart aliongea kwa kujiamini.
Kipindi Diana anawasili pale supermarket Stewart aliweza kumuona akishuka kwenye gari lake na yeye alikuwa maeneo hayo ya nje ndipo alipoamua kumfata mpaka ndani.
Diana hakuwa na kingine tena sababu ni kweli plate namba ya gari lake kuna jina lake,
"Okay,Nini unataka kutoka kwangu?"
"Namba yako Diana, sina kingine zaidi ya kuhitaji namba yako",Stewart aliongea kuonyesha kweli anauhitaji wa namba ya Diana.
"Kama shida ni namba lipia vitu vyote nilivyonunua hapa utaipata namba yangu",Diana aliongea akijua amemkomesha Stewart .
"Mbona vichache ulivyo chukua ongeza vingine mpaka utakapolizika".
Maneno ya Stewart yalimfanya Diana akili kuwa amejikologa kumpa sharti lile ila hakuwa na pingamizi tena zaidi ya kutimiza ahadi yake, alinunua vitu alivyovitaka na kweli Stewart alilipia na wakabadilishana namba za simu.
Ndani ya kampuni la FNF Semina na mafunzo mbalimbali yalianza kutolewa kwa warembo wote waliosajiliwa kwenye mashindano hayo husika kwa kufundishwa namna ya kutembea kimiss ili wasije kulitia aibu taifa siku ya tukio ,Diana akiwa ameka siku iyo akifatilia mafunzo waliyokuwa wakipatiwa alishangaa kumuona Angelina maeneo hayo tena akiwa kama mshiriki wa mashindano,alikuwa na kisasi na Angelina kwa kosa la kumwagia kahawa na kumpiga kibao,
"inawezekanaje huyu binti aliyetumwagia kahawa na kunipiga kibao awe ni moja ya washiriki?, kwani Albert hajui kama yupo hapa?",ni maswali aliyokuwa akijiuliza yasiyokuwa na majibu ila palepale aliamua kumtumia ujumbe Albert.
Upande wa Albert alipata ujumbe kutoka kwa Diana uliomshitua kidogo,
"Yule binti aliyetumwagia kahawa na kunipiga kibao nimoja ya washiriki wenzetu katika mashindano haya ulikuwa unalijua hili Albert kama yupo hapa na anashiriki haya mashindano?",Albert ata yeye alishituka kuuona ujumbe ule.
Licha ya kufanyakazi kwenye ile kampuni alikuwa hajui kama Angelina na yeye ni moja ya washiriki.
"Ina mana mama ameona kumpa kazi haitoshi akaamua kabisa ampe nafasi ya kushiriki mashindano ya Miss Tanzania!!",ni mawazo ya kijana Albert aliyoyapata kutokana na ujumbe aliotumiwa na Diana.
Alinyenyuka na kutoka ndani ya ofisi yake Moja kwa moja alielekea sehemu ambayo semina inafanyikia ili ajihakikishie kwa macho yake mwenyewe.
Ndani ya dekika kadhaa tu alifika nakuanza kuangaza kama atafanyikiwa kumuona Angelina maeneo yale na kweli katika kuangaza alimuona akiwa kama moja ya washiriki lakini wakati yeye anamtazama Angelina, Faith alimuona na kumjulisha rafiki yake Mary,
"Wewe Mary yule kule mtoto wa kiongozi",Mary alitazama nakumuona Albert kasimama kwa pembeni kabisa akimtazama Angelina.
"Shoga yangu nakuja Sasa ivi tu",Mary alitoka nakumuacha rafiki yake huyo na bira kumwambia ni kipi anachoenda kufanya.
Alienda mpaka alipo Albert nakumgusa begani na hii kumfanya ageuke kuangalia ni nani huyo, alikutana na sura ngeni na hakuwahi kuiona hapo kabra,
"Naomba unifate",Mary aliongea pasipo ata kumpa nafasi Albert ya kuongea.....ITAENDELEA.
Mary anatamwambia nini Albert inakuja sehemu ya 6
NB: Story hii NIYAKUTUNGA na haina ukweli wowote ule unaoendana na taratibu za nchi yetu????????.
Pata Story hii mpaka mwisho kwa Tsh 1000 za k???????????????????????? lipia kupitia namba,
0613083801 HALOPESA,John Bugumba.
.