Ingia

Sema Jambo

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94

MISS TANZANIA Mtunzi...................Zooper Sehemu..ya...........04

18th Apr, 2025 Views 32

Story......................MISS TANZANIA
Mtunzi...................Zooper
Sehemu..ya...........04
Whatsapp..............0613083801

ilipoishia sehemu iliyopita........
Na alimweleza siku inayofata asubuhi na mapema anatakiwa afike katika kampuni iyo ya FNF kwa ajili ya kuanza kazi na hiyo ikawa kama bahati nyingine kwa mwanadada Angelina......

ENDELEA NAYOO....
Baada ya kukaa kwa mda mrefu Mwanamama katalina aliamua kumuaga Beatrice nakuondoka akiwaacha mama na mtoto wakiwa kwenye maongezi hasa Angelina aliyetamani kujua mama yake amefahamianaje na Mwanamama katalina,
"Mama naomba unipe stori ya wewe kumfahamu katalina", Angelina aliongea,nae Beatrice hakutaka kumficha mwanae,
"Mwanangu mimi na katalina tulikuwa marafiki wakubwa sana kipindi tunasoma na wote tulisoma shule moja na kipindi cha ujana wetu rafiki yangu Katalina alibahatika kumpenda kijana mmoja aliyekuwa akiitwa James aliyekuwa akisoma shule ya jirani na kiukweli walipendana sana, pia urafiki kati yangu na katalina uliongezeka na Sasa hatukuwa marafiki wawili bali tulikuwa watatu yani Mimi,katalina na James......

Beatrice alisita nakuendelea kuongea.....

Baada ya mahusiano Yao kudumu kwa mda mrefu, nakumbuka tulikuwa kitado cha nne kuna kijana mpya alihamia pale shuleni kwenye darasa letu na alikuwa na uwezo darasani hali illiyotufanya Karibu kila mtu pale shuleni kutamani kufundishwa na kijana yule na baada ya mda mrefu kupita yule kijana alitengeneza mazoea na rafiki yangu Katalina na wakawa wanaongozana Karibu kila sehemu waliyokuwa wakienda.

Upande wa James  aliona mabadiliko makubwa kwa katalina mana hakuwa na mda wa kukaa nae tena kama mwanzo ndipo alipoamua kufatilia kiundani zaidi na aligundua kila kitu kilichokuwa kikiendelea kati ya Katalina na yule kijana kwa kumbukumbu zangu alikuwa anaitwa John",Mwanamama Beatrice aliongea.

Angelina alishanga  kuona mama yake anakaa kimya,
"Ehee nini kiliendelea mbona umeishia njiani mama"

Mwanamama Beatrice ilibidi amwangalie binti yake,
"Ndio naendelea kuongea nilikuwa nameza mate mwanangu eeh,basi baada ya James kugundua kuwa katalina yupo karibu na John, siku moja James alikuja pale shuleni kwetu na kuanzisha  ugomvi kati yake yeye na John hali iliyosababisha katalina na John wapigwe suspension(wasimamishwe) na wote kuambiwa waje kufanya mitihani tu ya kidato cha nne, kuanzia siku hiyo mahusiano kati ya katalina na James yalikufa na kila mtu alikuwa na chuki na mwenzake mpaka hii Leo ninavyoongea sizani kama James akikutana na Katalina atamsalimia na katalina nae ivyoivyo ", Beatrice alimaliza kusimulia na kumfanya mwanae aelewe.

Upande wa Mwanamama Katalina alifika nyumbani kwake na kumkuta mwanae Albert ametulia akitazama tv,
"Mgonjwa wako yupo katika hali gani mama?",Albert aliongea.
"Ni maajabu niliyokutana nayo huko leo,yule sio mgonjwa tu bali ni mtoto wa rafiki yangu tuliyesoma nae miaka ya nyuma", Mwanamama katalina alianza kumsimulia mwanae kwa kifupi kunzia alipomgonga na gari Angelina na kumpeleka kwao na ata Albert  mwenyewe alishanga kwa kile alichoambiwa na mama yake.

Bado Mwanamama katalina aliendelea kuongea mbele ya mwanae,
"Na sio ivyo tu, bali yule binti kesho atakuja kuanza kazi kwenye kampuni yetu na nimepanga kumpa kazi ya kusambaza vivywaji kwa warembo wote watakao kuwa pale"
"Mama hapana hapo umekosea yule hana sifa za kufanya ile kazi hana umakini yule binti",Albert aliongea na alionyesha kabisa hajapendezwa na maamuzi ya mama yake ya kumpa kazi Angelina.
"Kwani unamjua yule binti mpaka ukatae yeye kuja kufanya kazi kwenye kampuni yetu?"
"Hamna mama sio ivyo ila anaonekana tu hawezi ile kazi ", Albert hakutaka kuongea kitu kinachomfanya apinge mana ni lazima jina la Diana angelitamka mbele ya mama yake asiyetaka kulisikia hilo jina.
"Basi kama humjui maamuzi tayali nimeshayafanya haina haja ya kupingana na maamuzi ya mama yako", katalina aliongea na kuondoka akielekea chumbani na kumuacha mwanae aliyekuwa akimtazama.
            
Upande wa Mary akiwa na rafiki yake Faith nao walikuwa na mipango Yao ili wakamilishe kupata kile walichokuwa wakikitaka,
"Rafiki yangu hapa usajili tayali tumeshamaliza, kinachofata ni karibu kila siku kwenda kwenye ile kampuni ili nipate nafasi ya kuwa na yule kijana na ole wake akae kwenye kumi na nane zangu, uMiss Tanzania huo kama nauona", Mary aliongea.
"Nilijua tu malikia wa mipango nakukubali, kesho asubuhi na mapema inatakiwa tuwe tumeshafika katika ile kampuni",Faith aliongea.

Maongezi mengine yaliendelea ya marafiki hao wawili kuweka mipango Yao sawa.

Ni asubuhi na mapema Angelina aliamka nakujiandaa kwa ajili ya kwenda kuanza kazi yake mpya kama alivyoambiwa na Mwanamama katalina, alipokuwa akianza safari kutoka nyumbani kwao mama yake alikumbuka kitu na kumwita binti yake kabra bado hajafika mbali ambae nae alirudi kwa ajili ya kumsikiliza,
"Mwanangu naomba uwe makini sana usije kuniaibisha huko unakoenda",Beatrice aliongea.
"Aya mama nakuahidi temu hii sitasababisha tatizo lolote lile na nitafanya kazi kwa umakini zaidi",Angelina alimpa ahadi mama yake nakuondoka kwenda kuanza majukumu yake ya kazi mpya pia alivaa mavazi ya kawaida tu siku hiyo.

Kama walivyopanga siku ya jana na ndivyo ilivyokuwa asubuhi ya leo kwani Mary na rafiki yake Faith walijiandaa asubuhi na mapema na kwenda  kwenye kampuni ya FNF.

Angelina alifika kama alivyoambiwa ila bahati mbaya  mwanamama Katalina alikuwa bado hajawasili ilimlazimu kutafuta sehemu nzuri ya yeye kukaa na kumusubiria,
ndani ya mda mfupi tu alianza kushuhudia magari ya kila aina ya kiingia na wadada warembo wakishuka kwenye magari hayo, haikupita mda Mary na Faith nao waliwasili,
"Mmmh mwone yule mdada aliyekaa kule",Faith alimuonyesha Mary sehemu aliyokuwa amekaa Angelina.
"Eee namuona kwani amefanyeje",Mary alijibu.
"Yule ni mzuri ila hajui kujitunza angalia ata mavazi tu aliyovaa nitofauti na sisi wote hapa".
"Nilijua tu yani ndiyo tatizo lako hilo kwani mimi sio mzuri mpaka umsifie mwanamke ambaye hata hujawahi kumuona umenikera sana Faith",Mary ni binti asiyependa kuona mwanamke mwingine anasifiwa na hii ilimkera sana kumuona Faith akimsifia Angelina.
"Basi Mary yaishe nilikuwa nakutania tu ndugu yangu alafu tazama kule magari ya watu wako yanawasili".Faith aliongea.

Mary alivyogeuka aliona magari mawili yakiongozana na hawakuwa wengine bali ni gari ya mwanamama katalina iliyokuwa mbele na nyuma yake ikifuatiwa na gari ya kijana wake Albert yalienda mpaka sehemu ya parking.

Mwanadada Angelina baada ya kuiona gari ya mwanamama katalina alisimama na kwenda kuifata kabra hata mhusika mwenyewe hajatelemka katika gari lake, ile anafika tu alikutana na mwanamama Katalina aliyekuwa anashuka kutoka kwenye gari yake, kipindi yote hayo yakiendelea Mary na Faith walikuwa wakishuhudia kila kitu,
"Angelina umeshafika tayali?", mwanamama katalina aliongea baada ya kumuona Angelina.
"Ndio mama shikamoo",Angelina alitoa salamu kwa heshima mbele ya Katalina aliyeipokea na kuelekea nae sehemu husika na kumtambulisha kwa wafanyakazi wenzake ambao nao walifurahi kuongezewa mtu mana kulikuwa na majukumu mengi katika kampuni hiyo,
"Angelina mwanangu"
"Abee mama",
"Wewe kazi yako itakuwa ni kusambaza vinywaji kwa wadada na warembo mbalimbali watakao kuwa wanafika maeneo haya, pia kazi yako asubuhi ni kujumuika na wenzako kufanya usafi na kingine ambacho sikukwambia hapo awali ni kuwa, hawa wadada wote unaowaona mmoja wao atakuwa Miss Tanzania wa mwaka huu umakini unatakiwa uwe nao, pia tutakuwa na semina za mda mfupi na nyakati ambazo semina zitakuwa zinafanyika kazi yako ni kuhakikisha vinywaji havikosekani kwenye semina hizo na ni jukumu ninalo kupatia wewe binti yangu", Mwanamama katalina alimaliza kuongea.
"Aya mama nimekuelewa na nakuahidi nitafanya kazi kwa bidii".

Kazi mpya ya Angelina ilikuwa ni hiyo na aliingia kwenye majukumu yake ya kazi mda huohuo kwa kuanza kuzunguka ndani ya jengo hilo kutekeleza kile alichoambiwa na mwanamama katalina.

Tarifa ilitolewa ndani ya kampuni hilo kuwa kutakuwa na semina fupi kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa washiriki wote waliojisajili huku wengine pia wakiendelea kujisajili kwa ajili ya mashindano.

Kijana Albert akiwa anaelekea kwenye ofisi yake Mary na Faith walimuona,
"Nisubiri hapa nakuja sasa mpango wangu lazima utimie",Mary alimwambia Faith huku akiondoka na kumfata Albert.
Kutokana na mazingira kuwa mageni kwa Angelina alijikuta akiwa bize kushangaa kuliko kuangalia mbele anakoelekea bahati mbaya aligogana na mtu mtu aliyekuwa mbele yake na kuanguka chini...ITAENDELEA.

Nani aliyegongana na Angelina na kipi kitakachotokea?,karibu katika sehemu ya tano

NB: Story hii  NIYAKUTUNGA na haina ukweli wowote ule unaoendana na taratibu za nchi yetu????????.

Pata Story hii mpaka mwisho kwa Tsh 1000 za  k???????????????????????? lipia kupitia namba,
0613083801 HALOPESA,John Bugumba.
 .

Za hivi punde ni za 🔥🔥🔥 | Sema Jambo
Your settings were saved successfully!
Something went wrong!
You're not logged in
Click here to login and post your story

Welcome gonga94 Continue reading the various stories available here. Click here. Are you an artist then create an account here Signup/Login


mjukuu rewards 100
 

NASEMA KWA MAMA SEHEMU YA 10*

mjukuu rewards 100
 

NITAKUPA USINIROGE (1)

mjukuu rewards 0
 

SHANGA TISA EP: 19

mjukuu rewards 0
 

SHANGA TISA EP: 18

mjukuu rewards 0
 

SHANGA TISA EP: 17

mjukuu rewards 0
 

SHANGA TISA EP: 16

mjukuu rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 42

mjukuu rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 41

mjukuu rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 40

mjukuu rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 39

mjukuu rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 38

mjukuu rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 37

mjukuu rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 36

mjukuu rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 35.

mjukuu rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 34

mjukuu rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 33.

mjukuu rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 32

mjukuu rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 31

majario rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 30

majario rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 29

majario rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 28

majario rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 27

majario rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 26

majario rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 25

majario rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 24

majario rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 23.

majario rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 22

majario rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 21

majario rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 20

majario rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 19.

majario rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 18

majario rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 17.

majario rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 16

majario rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 15.

majario rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 14

majario rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 13.

majario rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 12

mjukuu rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 11.

mjukuu rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 10

mjukuu rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 09

mjukuu rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 08

mjukuu rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 07.

mjukuu rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 06

mjukuu rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 05.

mjukuu rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 04.

mjukuu rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 03

mjukuu rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 02

mjukuu rewards 0
 

PENZI LA MHALIFU 01.

mjukuu rewards 0
 

RUNGU LA KIPOFU 22.

mjukuu rewards 0
 

NASEMA KWA MAMA **** 3--4

mjukuu rewards 0
 

SHANGA TISA EP: 15

mjukuu rewards 0
 

SHANGA TISA EP: 14

mjukuu rewards 0
 

WIFI KHAA 04

mjukuu rewards 0
 

NASEMA KWA MAMA* 1-----2

mjukuu rewards 0
 

KIJIJI CHA WAGENI! 04

mjukuu rewards 0
 

MKE WA MGANGA ( 1——5 )

mjukuu rewards 0
 

SHANGA TISA EP: 13

mjukuu rewards 0
 

RUNGU LA KIPOFU 21.

mjukuu rewards 0
 

RUNGU LA KIPOFU 20.

mjukuu rewards 0
 

RUNGU LA KIPOFU 19.

mjukuu rewards 0
 

RUNGU LA KIPOFU 18.

mjukuu rewards 0
 

RUNGU LA KIPOFU 17.

mjukuu rewards 0
 

RUNGU LA KIPOFU 16.

mjukuu rewards 0
 

RUNGU LA KIPOFU 15.

mjukuu rewards 0
 

RUNGU LA KIPOFU 14.

mjukuu rewards 0
 

RUNGU LA KIPOFU 13.

mjukuu rewards 0
 

RUNGU LA KIPOFU 12.

mjukuu rewards 0
 

RUNGU LA KIPOFU 11

mjukuu rewards 0
 

WIFI KHAA 02 #Tulipoishia

mjukuu rewards 0
 

RUNGU LA KIPOFU 10

mrindia rewards 0
 

RUNGU LA KIPOFU 09

mjukuu rewards 0
 

*MY CHUNUN* 01

mjukuu rewards 0
 

SHANGA TISA EP: 09

mjukuu rewards 0
 

SHANGA TISA. EP: 08

mjukuu rewards 0
 

SHANGA TISA EP 07

mjukuu rewards 0
 

SHANGA TISA EP 06

mjukuu rewards 0
 

SHANGA TISA EP 05

mjukuu rewards 0
 

SHANGA TISA. EP: 4

mjukuu rewards 0
 

SHANGATISA EP: 3

mjukuu rewards 0
 

SHANGA TISA EP: {02}

mjukuu rewards 0
 

SHANGA TISA. EP: 1

mjukuu rewards 0
 

RUNGU LA KIPOFU 08

mjukuu rewards 0
 

RUNGU LA KIPOFU (06 & 07)

mjukuu rewards 0
 

RUNGU LA KIPOFU 05

mjukuu rewards 0
 

RUNGU LA KIPOFU 04

mjukuu rewards 0
 

RUNGU LA KIPOFU 03

mjukuu rewards 0
 

RUNGU LA KIPOFU (01& 02)

mrindia rewards 0
 

RUNGU LA KIPOFU 01

mjukuu rewards 0
 

MTOTO WA GETI KALI 1 - 6

mjukuu rewards 0
 

MIMI SIO KICHAA

mrindia rewards 0
 

SITOMWACHA HATA IWEJE

mjukuu rewards 0
 

BINTI MCHAWI

Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest