Story......................MISS TANZANIA
Mtunzi...................Zooper
Sehemu..ya...........07
Whatsapp..............0613083801
Ilipoishia.......
"Unaweza kuniambia ni kwanini unamchukia sana yule binti",swali la Mwanamama katalina lilimfanya Albert ajutie kile alichokiuliza......
ENDELEA NAYO.....
Swali la Mwanamama katalina lilimfanya Albert ajutie kile alichokiuliza.
"Mama mimi yule simwamini tu na sio kwamba ety namchukia hapana simwamini kabisa yule binti",Albert aliongea.
"wewe humwamini ila mimi namwamini na ninampenda kama mwanangu na pia kumbuka yule ni mtoto wa rafiki yangu namchukulia kama mwanangu na kilichonivutia zaidi na kunifanya nimpe nafasi ya kushiriki ni kuwa yule binti ni mzuri sana sio kisura tu ata kitabia yupo tofauti na wengine na mabinti kama hao ni wachache sana", Mwanamama katalina aliendelea kushikilia msimamo wake wa kumuamini Angelina.
Albert hakutaka tena kuendelea kuongea na mama yake aliondoka pale sebleni na kuelekea chumbani kwake kupumzika lakini alichukua simu yake na kumtafuta Diana alipiga lakini simu iliita bira kupokelewa mpaka ikakata yenyewe,
"Nimekaa mda mrefu sana nikisubiri huu mda ufike hapa ni lazima nije niweke wazi hisi zangu kwa Diana, kiukweli nampenda sana kesho lazima nimwambie kama nampenda",Albert aliongea na chumba chake mwenyewe akikili kumpenda Diana aliamua kuzima simu yake baada ya Diana kushindwa kupokea simu yake.
Nyumbani kwa Mr.James palikuwa hapakaliki kabisa na hii ni baada ya kufika mpaka saa 7 usiku pasipo binti yake kuonekana nyumbani,
"Nimefanya ujinga gani mimi sikutakiwa kumfanyia vile binti yangu na sijui atakuwa kwenye hali gani mda huu",Mr.James aliendelea kujilaumu kwa kitendo cha kumpiga binti yake Diana.
Licha ya kuwa ni usiku sana alitoka mpaka nje na kwenda kwa mlinzi wake,
"Shika kiasi cha laki moja hiki kama malipo ya kazi ambayo nakupatia sasa ivi", Mr.james aliongea.
"Kazi gani boss?"
"Nenda kamtafute Diana na hakikisha unarudi nae hapa nyumbani sasa ivi",Mr.James aliongea Huku akiondoka hakutaka kusubiri jibu kutoka kwa mlinzi wake.
"Jamani mbona tanenepa mwaka huu Yani kumtafuta mtu napewa laki, safi sana akirudi nitamwambia atoloke tena nipewe laki nyingine",Mlinzi aliongea huku akitoka na kwenda kumtafuta Diana.
Mlinzi alifurahi baada ya kupewa kiasi kile cha pesa pasipo kutegemea tena kazi yenyewe ni kumtafuta Diana, alizunguka karibu kila pande usiku huo lakini hakuafanyikiwa kumpata Diana usiku huo.
Ni siku nyingine mpya sauti za ndege zilimwamsha na kumfanya aamke lakini kichwa kilikuwa kikimuuma sana na alipotazama mazingira ya chumba alichokuwa amelala alishangaa kuona sehemu ile ni ngeni kwake,
"Mmmh hapa nipo wapi tena na nimefikaje?",hakuwa mwingine bali ni mwanadada Diana aliyeamka kutoka usingizini.
"Gari langu,simu yangu...", Alinyenyuka haraka baada ya kumbukumbuku kumrudia za wapi alipokuwa siku ya Jana, alitoka na kufunga mlango wa kile chumba.
Alianza kutembea ndani ya nyumba asiyoijua na mazingira ya mle ndani yalimvutia zaidi hasa alipokuwa akiyatazama,aliendela kuzunguka mle ndani ili aone kama atakutana na mwenyeji ya ile nyumba.
Stewart nae mda huo ndiyo alikuwa akiamka kutoka chumbani kwake alitoka na kukutana na mwanamke ambae alifanya amtazame mara mbilimbili kuhakikisha kama ni yeye,
"Weweee..."
"Wewee nim...."
wote walijikuta wanaongea kwa pamoja.
"Niambie nimefikaje hapa na kwanini umenileta hapa kwako bira ruhusa yangu", Diana aliongea na akimshutumu Stewart.
"Unaongea nini wewe, mimi ndiyo nikuulize umeingiaje humu ndani?",Stewart nae alikuja juu.
Yalikuwa ni mabishano kati ya Stewart na Diana kila mtu akitamani kujua hasa Diana ambae alimkomalia kwa kumlalamikia Stewart kumleta kwake bira ridhaa yake.
Majibishano yale mama Stewart aliyasikia na kuamua kutoka na kuwafata,
"Ooh binti umeshaamka", sauti ya mama Stewart ilimfanya Diana aache kuzungumza na kugeuka nyuma kuangalia mtu anayemuongelesha.
"Mama wewe ndio umemleta huyu?,mana hapa lawana napewa mimi sasa ivi",Stewart aliongea baada ya kumuona mama yake mzazi.
"Kwani mnajuana au mmeshawahi kuonana?",Mama Stewart aliamua kuwauliza.
"Hapana hatujuani",Diana aliamua kumuwahi Stewart kabra hajalopoko.
Mama Stewart alimuelezea Diana jinsi ilivyokuwa jana yake mpaka wao kuchukua maamuzi ya kumsaudia na kumleta pale,baada ya maneno yale Diana alijikuta anamwaga machozi na hii iliwashangaza Stewart na mama yake.
"Binti mbona unalia?"
"Kwa uliyonisimulia sikutegemea kama mimi ndiyo wa kufanya yale mambo, nipende kuomba samahani kwa usumbufu niliowapatia siku ya jana naombeni niondoke nikaangalia usalama wa gari yangu mana niliiacha katika ile klabu".
Mama Stewart alimruhusu Diana huku akimsititiza awe makini zaidi lakini Stewart aliamua kumpeleka kwa kutumia gari lake.
Ndani ya gari Diana alikuwa ni mwenye mawazo na Stewart alilitambua hilo.
"Hupaswi kuwa na mawazo Diana, nyakati za wanadamu siku zote zinatofautiana huwezi kuwa na furaha kila siku leo utakuwa na mawazo kesho utakuwa na furaha ni moja ya jaribu unalopaswa kulipitia kwa wakati huu Diana, japo najua kuna kitu kilichokufanya mpaka ukachukua maamuzi uliyoamua kuyafanya", Stewart aliongea lakini Diana hakumjibu kitu mpaka pale walipofika na yeye kushuka kwenye gari na kwenda kwenye gari yake na bahati ilikuwa kwake kwani gari yake aliikuta ikiwa salama kabisa na alimuaga Stewart na yeye akaelekea nyumbani kwao.
Mwanamama Katalina asubuhi hiyo alijiandaa mapema sana kwa ajili ya kuondoka,Albert alivyotoka chumbani kwake alishangaa kumkuta mama yake yupo kwenye maandalizi ya kuondoka,
"Mama leo mbona mapema sana unasafari ya wapi?"
"Leo kuna zoezi kubwa linatakiwa lifanyike la washiriki wote kuonyesha kile walichonacho na tutawagawia namba kabisa watakazokuwa wakitumia", Mwanamama katalina alijibu.
"Nimekuelewa mama lakini mara ya mwisho kuwasiliana na baba ilikuwa lini?"
"Albert naona unataka kuharibu siku yangu asubuhi hii,baba yako tangu aende marekani mpaka sasa ivi hakumbuki kama ameacha familia huku atakama kampuni ni yake lakini familia pia ina umhimu mkubwa sana, wewe umeshakuwa sasa ivi unaweza kumtafuta baba yako mwenyewe na kuongea nae", Mwanamama katalina hakupendezwa na kila kilichoulizwa na Albert aliondoka pale nyumbani na kumuacha mwanae akimtazama tu.
Palepale Albert alichukua simu yake na kumpigia Diana ambae mda huo alikuwa akiendesha gari akielekea nyumbani kwao, aliamua asimamishe gari pembeni ili apokee simu, na temu hii upande wa Albert ilikuwa tofauti na jana usiku kwani simu ilipokelewa,
"I'm sorry Albert niliona missed call zako na mda huu ndiyo nilikuwa najiandaa kukupigia sema umeniwahi my dear",Diana aliongea.
"Jambo la kawaida ila jiandae huku leo kuna kitu cha mhimu mnachotakiwa kukifanya nazani unafahamu Diana"
"Ndio naielewa ratiba nzima",Diana alimjibu.
"Mwisho wa yote leo nahitaji unipe mda wa kuongea na wewe jioni ya leo kuna kitu mhimu ninachotamani kukwambia", Albert alimuomba Diana waonane.
"Albert naanzaje kukataa kuonana na wewe my dear,ata mimi pia na mengi yakuongea na wewe na umefanya jambo la maana sana kufanya tuonane"
Simu ilikatwa na kumfanya Diana awashe gari na kuendelea na safari na ndani ya mda mfupi aliweza kuwasili nyumbani kwao na kumkuta baba yake amesimama nje.
Mr.James aliitazama gari ya binti yake kwa umakini wa hali ya juu akimshuhudia binti yake akitelemka ndani ya gari lake hilo,
"Jana ndiyo ukaona ukalale nje ya nyumba kisa kukwambia ukweli?"
"Nisamehe baba ni makosa yangu nakili nilikosea", Diana aliamua ajishushe mbele ya baba yake.
"Ivi unajua nilipata tabu kiasi gani kukulea Diana na umeshawahi kujiuliza mama yako yupo wapi?", maneno ya Mr.James yalifungua akili ya mwanadada Diana baada ya kutamkiwa neno mama.
"Baba, mara zote nilikuwa naitafuta hii nafasi ya kuongea vizuri na wewe baba yangu,uniambie kuhusu mama yangu mzazi yupo wapi?...ITAENDELEA.
Nyie mbele ya hii simulizi kuna vipande ambavyo hutakiwi kuvikosa kabisa yani utakuwa umepitwa utamu ???????????? kabisa, karibu katika sehemu inayokuja.
NB: Story hii NIYAKUTUNGA na haina ukweli wowote ule unaoendana na taratibu za nchi yetu????????????????.
Pata Story hii mpaka mwisho kwa Tsh 1000 za k???????????????????????? lipia kupitia namba,
0613083801 HALOPESA,John Bugumba..