Story......................MISS TANZANIA
Mtunzi...................Zooper
Sehemu..ya...........03
Whatsapp..............0613083801
ilipoishia sehemu iliyopita.......
Albert bira kujali kama yupo barabarani na barabara sio yake peke yake aligeuza gari pasipo kutazama vizuri ili........
ENDELEA NAYO......
Albert bira kujali kama yupo barabarani na barabara sio yake peke yake aligeuza gari pasipo kutazama vizuri, ilibaki kidogo tu apate ajari na bahati ikawa upande wake mana mtu aliyekuwa anaendesha gari lililotaka kuigonga gari alikuwa akiendesha kwenye mwendo wa kawaida na alipoona gari ya mbele yake imegeuza ilimlazimu kusimamisha gari yake ili asisababishe ajari,
"Wewe jamaa vipi hujui sheria za barabarani wewe",aliongea kwa sauti juu akimwambia Albert lakini aliyekuwa akiongea nae ni kama alikuwa hasikii kile anachoambiwa kwani gari la Albert lilitokomea tena kwa speed kali.
Ndani ya hospital alipo Mwanamama katalina,
"Wewe ndiyo mhusika wa mgonjwa aliyeletwa?",Nesi alimfata mwanamama katalina na kumuuliza.
"Ndio nesi ni mimi"
"Nifate huku".
Katalina alinyenyuka na kumfata huku akiomba mtu aliyemgonga asiwe kwenye hali mbaya itakayo mfanya awe na kesi kwa kile kilichotokea,alipelekwa moja kwa moja mpaka kwa doctor kwa ajili ya kupatiwa majibu ya mgonjwa wake,alifika na kuketi huku hofu ikiendelea kumtawala mwanamama Katalina,
"Mgonjwa wako hajapata majeraha makubwa sana, sema alianguka vibaya hali iliyompelekea apate jeraha mdomo lililosababisha damu kumtoka,na pia alipata mshituko uliomfanya azimie", doctor aliongea.
"Anaendeleaje kwa sasa doctor?"
"Nazani atakuwa ameshaamka na unaweza kwenda kumuona pia unaruhusiwa kwenda nae nyumbani na kuna dawa nitakuandikia anazopaswa kutumia kwa ajili ya kuondoa majeraha madogo aliyoyapata",doctor aliongea na hii ilipunguza hofu kwa mwanamama katalina alinyenyuka na kutoka kwenye chumba Doctor na aliende moja kwa moja kumuona mgonjwa.
Albert alifika hospital na kushuka haraka na kazi ya kwanza aliyokuwa nayo nikumpigia mama yake simu ili ampe maelekezo ni wapi alipo na na Mwanamama Katalina alimwelekeza mwanae ni wapi alipo kwa wakati huo.
Katalina tayali alikuwa ameshafika katika chumba alicholazwa Angelina na kumkuta amekaa kitanda akiwa ni mwingi wa mawazo mwanadada huyo,
"Pole sana binti kwa kilichotokea na pia nisamehe sana sikuthamilia kufanya kile nilichokifanya, naomba nikili kwako ilikuwa ni bahati mbaya tu mimi kukugonga wewe", ", Mwanamama katalina aliongea.
"Usijali mama yale yalikuwa nimakosa yangu mimi, mawazo niliyokuwa nayo yalinifanya nipoteze umakini wa kutembea barabarani", Angelina aliongea.
Na mda huohuo Albert aliweza kufika na kumkuta mama yake akiongea na mgonjwa aliyekuwa pale,
"Mama kimetokea nini?", ndio swali la kwanza aliloongea bira kujali mama yake anazungumza na mtu mwingine.
"Usijali mwanangu nitakuelezea badae mhimu ni kumshukuru mungu mana hamna kilichohalibika zaidi"
"Na huyu mgonjwa ni....", Albert alisita baada ya kuiona sura ya Angelina alikumbuka ndiyo mtu akiyewamwagia kahawa na kumpiga Diana,pia alikumbuka alivyomuahidi kuwa atamfanya kulipa kwa kile alichokifanya ila kwa wakati huo Albert hakutaka kuongea chochote.
"Binti naomba nikuchukue nikupeleke nyumbani kwenu na pia kuna dawa utatakiwa kuzitumia zitakazo kufanya hali yako iwe sawa", Mwanamama katalina aliongea.
"Usijali mama nitaenda mwenyewe tu haina haja ya wewe kijisumbua na kupoteza mda wako", Angelina alijibu kwa unyenyekevu.
"Wewe umeambiwa upelekwe mbona unaanza kuleta malingo tena hapa", Albert aliamua kuingilia mazungumzo yale na maneno aliyotamka yalimfanya mama yak3 akasilike kidogo.
"Albert maneno gani hayo unayomwambia mgonjwa, emu naomba uondoke nitakuja nyumbani tuongee vizuri".
"Sawa mama endelea kumbembeleza mgonjwa wako",Albert aliongea na kuondoka.
Hali ile ilimshangaza Mwanamama katalina kwa kitendo alichokionesha mwanae ila upande wa Angelina yeye alifahamu ni kwanini Albert alikuwa vile mana alimuahidi ni lazima atamkomesha kwa alichowafanyia masaa kadhaa yalipita.
Mwanamama katalina alimbembeleza Angelina ambae alikubali kupelekwa nyumbani kwao na wote walielekea kwenye gari lililoanza kundoka maeneo yale ya hospital.
Nyumbani kwa Mr. James aliamua kumuita binti yake Diana ili amuulize vitu vya msingi,
"Mwanangu najua wewe umeshakuwa sasa ivi na ata ukiniletea tarifa za wewe kutaka kuolewa siwezi kukataa mana najua tayali umeshafikia umri wa kuwa na mwenza kwa sasa Diana, emu naomba uniambie Albert ni mpenzi wako?", Mr.James alimuuliza binti yake.
"Yule ni rafiki yangu tu baba kama walivyo marafiki wengine na wala sio mpenzi wangu".
"Mimi nimtu mzima Diana nimepitia mengi zaidi yako ndio mana nakuuliza kwa mara nyingine tena,Albert ni mpenzi wako?", Mr. James aliuliza tena.
"Kiukweli baba ngoja nikwambie ukweli huenda utanielewa, kwa sasa sina malengo ya kuolewa ila malengo yangu mimi nikuwa Miss Tanzania na hiyo ndiyo sababu iliyonifanya niwe karibu na Albert ili iwe vyepesi kwangu kukamilisha ndoto zangu na uzuri ni kuwa kampuni yao inasimamia mashindano haya kwa miaka ya ivi karibuni", Diana aliongea.
"Kwa maana hiyo unataka kumfanya Albert kuwa daraja la wewe kufika unapotaka kufika",Mr.james alimuuliza mwanae kwa mara nyingine.
Beatrice hakutaka kujibu zaidi ya kutikisa kichwa tu na hii kumfanya Mr. James alelewa.
Mr.James alifikilia kitu alichoona ni sahihi kufanya kwa upande wake,
"Nimekuelewa binti yangu ni subiri nakuja sasa ivi tu kuna kitu lazima tukubaliane",Mr James alinyenyuka nakuondoka na haikupita mda alirudi akiwa na karatasi pamoja na pen.
"Baba pen na karatasi vya nini tena!!!",Diana aliuliza kwa mshangao.
"Subiri utaona tu".
Mr.James alimpa karatasi na pen binti yake na Diana alichukua akiwa bado hafahamu ni kipi ambacho baba yake anataka kufanya.
"Aya andika haya maelezo nitakayokuwa nakwambia", Mr. James aliongea.
"Baba maelezo gani?"
"Nisikilize kwa umakini kisha uandike,andika ivi MIMI DIANA NAWEKA MAKUBALIANO NA BABA YANGU MZAZI AU MR.JAMES YA KUWA SITAKUJA KUWA NA MAHUSIANO YOYOTE YALE YA KIMAPENZI NA KIJANA ALBERT NA ATABAKI KUWA RAFIKI YANGU KWENYE MAISHA YANGU YOTE, NA IKITOKEA TUKAWA WAPENZI, MAHUSIANO KATI YANGU NA BABA YANGU YATAKUWA YAMEKUFA.", Mr.James alimaliza kuongea.
"Baba kwanini lakini umeshindwa kuamini kile nilichokwambia, basi na kwakuwa huamini ngoja niandike kile unachokitaka",Diana aliongea na kuanza kuandika maelezo yale pia aliweka na sahihi kumaanisha kuwa ata yeye hana kipingamizi na kile alichokisema baba yake.
"Vizuri binti yangu hiyo karatasi ilete hapa nitaenda kutoa copy na wewe nitakupatia copy na mimi nitabaki na hii original"
"Lakini baba mbona ni jambo dogo hilo ila wewe unataka kulifanya liwe kubwa kweli"
Mr. James hakutaka kuongea zaidi ya kuichukua ile karatasi na kuondoka.
Mwanamama katalina akiwa na Angelina walifika katika nyumba iliyo maeneo ya uswahilini hali iliyomshangaza Mwanamama katalina kuona mazingara anayoishi Angelina na hii kumhuzunisha zaidi,
"Pale unapopaona ndio nyumbani kwetu naishi mimi na mama yangu mzazi", Angelina aliongea na wakiti huo akiwa anashuka kwenye gari.
Katalina nae aliona haitakuwa vyema kuondoka pasipo kwenda kumuona mama wa mtu aliyemgonga, alishuka nakuongozana na Angelina mpaka nyumbani kwao na kumkuta mama Angelina kalala kwenye kochi dogo akiendelea kuuchapa usingizi.
Sauti ya mwanae iliyomtoa usingizini na kumfanya amke,
"Angelina umeshafika kumbe mwanangu"
"Ndio mama nimekuja na mgeni hapa alitaka kukuona na msalimiane", Angelina aliongea na kumfanya mama yake amtazame Mwanamama katalina kwa umakini zaidi.
"wewe sio katalina, mbona sura yako sio ngeni kwenye macho yangu?",Mama Angelina aliongea kwa kumaanisha na ilionyesha anamfahamu katalina na ata katalina alivyomtazama vizuri mwanamke aliye mbele yake na yeye alimukumbuka.
"Beatrice ni wewe?"
"Ndio ni mimi katalina",Mama Angelina alijibu.
Sio Beatrice ambae ni mama wa Angelina na wala sio Mwanamama katalina wote walijikuta wakikumbatiana kwa furaha huku Angelina akiwa bado haelewi kilichowafanya watambuane na kukumbatiana kwa furaha kiasi kile aliamua kumuuliza mama yake,
"Mama kwani mmeshawahi kuonana hapo kabra ?"
Ni stori ndefu binti yangu nitakusimulia siku moja na utaelewa tu.
Mwanamama katalina na Beatrice waliongea mengi siku hiyo na ata Angelina alimweleza mama yake kuwa alipokuwa anafanya kazi tayali ameshafukuzwa na sasa anajukumu la kutafuta kazi sehemu nyingine,lakini mwanamama katalina aliahidi kumpatia kazi katika kampuni lao la FNF,
na alimweleza siku inayofata asubuhi na mapema anatakiwa afike katika kampuni iyo ya FNF kwa ajili ya kuanza kazi na hiyo ikawa kama bahati nyingine kwa mwanadada Angelina...ITAENDELEA.
Mambo ndio kwanza yameanza hii niya moto tukutane sehemu ijayo.
NB: Story hii NIYAKUTUNGA na haina ukweli wowote ule unaoendana na taratibu za nchi yetu ????????.
Pata Story hii mpaka mwisho kwa Tsh 1000 za k???????????????????????? lipia kupitia namba,
0613083801 HALOPESA,John Bugumba.
.