Story......................MISS TANZANIA
Mtunzi...................Zooper
Sehemu..ya...........21
Whatsapp..............0613083801
ilipoishia....
Waliekea kwenye ndege Diana akiwa na Mr.James na ata nyumba yao iliachwa chini ya uangalizi wa Angelina na Mwanamama Beatrice.......
ENDELEA NAYO......
Angelina na mama yake waliamua kurudi mpaka nyumbani huku wakiwa na matumaini ya Diana kurudi Tanzania akiwa ameshatibiwa tatizo la miguu linalomsumbua na kurudi katika hali yake kama zamani.
"Griiigriiigriiii",ni mlio wa simu wa mwanadada Angelina aliyeamua kupokea baada ya kuona namba ngeni iliyompigia,
"Hello, Miss Tanzania unaongea na Big Don", sauti ya mwanamziki huyo mashuhuli ilisikika masikioni mwanadada Angelina.
"Unashida gani na mimi na nilikataa kufanya kazi na wewe Big Don",Angelina aliongea kwa kujiamini bira kuogopa umaarufu aliokuwa nao Big Don hali iliyomkasilisha msaani huyo ila hakutaka kuonyesha hasira zake mbele ya mwanadada Angelina.
"Angelina hii ni kazi ambayo unatakiwa uifanye kwa lazima mana tayali nimeshaweka makubaliano na kampuni unayofanya nayo kazi na pia kumbuka una mkataba na kampuni iyo... kama huamini basi nenda ukaonge na manager wako atakupa maelezo zaidi, lazima utekeleze makubaliano yenu yalivyokuwa", Big Don aliongea kitu kilichomchanga Angelina.
"Unaongea nini wewe?"Angelina aliongea lakini simu tayali ilikuwa imeshakwatwa.
"Nani huyo tena", Mwanamama beatrice aliuliza.
Angela alimweleza kila kitu mama yake alichoambiwa na Big Don.
"Mimi naamini mwanangu huyo msanii anataka akutumie tu ni bora uangalie namna ya kuvunja mkatana na hilo kampuni"
"Mama sio msanii tu ata ninapo fanya kazi Manager naye anatabia hiyohiyo ya kuharibu ndoto za mabinti wengi",mwanadada Angelina aliendelea kulalamika.
Aliamua kutoka pale nyumbani na kuelekea katika kampuni ili apate habari kamili na siku hiyo alienda peke yake bira ya rafiki yake Manka, alifika na kumkuta manager akiwa anaendelea na majukumu yake kama kawaida,
"Manager makubaliano yetu ya mkataba yalikuwaje?",Angelina alifika na kuhoji swali mbele ya manager huyo.
"Nayakumbuka sana makubaliano yetu ni lazima ukafanye kazi kwa Big Don na iyo pia ni kazi ya kampuni yetu ukikataa utakuwa umeenda kinyume na makubaliano yetu", Manager aliongea huku akiwa anaendelea na kazi zake hakutaka ata kumuangalia Angelina.
Angelina aliona sasa wanataka kumtania aliamua kutoka na kwenda nyumbani kuchukua mkataba alioingia na kampuni hilo huku kichwani akipanga kufanya kitu kitakacho msaidia.
Mwanadada Mary milion 100 alikuwa ameshatumia na alikuwa amebakiza pesa kidogo sana na kwakuwa milion 100 alizipata kirahisi kutoka kwa Albert sasa aliamua kuja na mpango mwingine utakaomfanya apate pesa nyingine.
Akiwa amekaa na rafiki yakr Faith ambao urafiki wao ulirudi upya na ukawa kama zamani,
"Pesa zimeisha ngoja niende kwa mjinga wangu temu hii nafilisi kila kitu",Mary aliongea.
Mwanadada Faith hakuongea lolote lile zaidi ya kusikiliza maneno ya rafiki yake.
Mary alipanga mipango na vijana wake ya kwenda kumkamata Mwanamama katalina yani wafanye kama walivyofanya mwanzo ili aweze kujipatia pesa,lakini temu hii Faith aliamua kufanya kitu alichoona ni sahihi kwa upande wake alitafuta namba ya Albert na akafanyikiwa kuipata nakumpigia simu,
"Albert huu ni msaada kwako na kwa familia yako haina haja ya kujua mimi ni nani, ila kaa ukijua tu mama yako inatakiwa awe kwenye uangalizi mkubwa sana mda wowote Mary anaweza kumteka",Faith alikata simu baada ya kuongea na Albert.
"Utanisamehe rafiki yangu Mary sitaki uingie sehemu ambayo sio nzuri ya kunyanganya mali za watu", yalikuwa ni maneno ya mwanadada Faith.
Albert baada ya kupatiwa tarifa na Faith aliamua kutafuta walinzi wa kuweza kumlinda mama yake popote pale atakapokuwa.
Siku iliyofata mwanamama katalina alikuwa bize na kazi kwenye kampuni yake ya FNF na alikuwa na ulinzi wa kutosha aliotafutiwa na mwanae Albert kwa ajili ya usalama wake.
Upande wa nje wa kampuni hiyo alifika Mary akiwa kwenye gari yake na vijana wake wa kazi waliokuwa ndani ya gari hiyo na alipaki kwa mbali kidogo ambapo ni ngumu watu kuweza kugundua kama kuna tukio linalosubiliwa kufanyika.
"Leo inatakiwa muwe faster kuliko siku zote hapa tunasubilia gari yake ikitoka tunaizibia njia na nyie mnashuka haraka kwenda kumchukua na kumleta kwenye hii gari",Mary aliongea na vijana wake ambao kwake ni zaidi ya makomando,
Walikubaliana na kusubiri mpaka mda ulipokaribia kufika.
Gari ya mwanamama Katalina ilionekana akiwa anaendesha na ilipofika karibu na gari ya Mary, kitendo cha haraka kilifanyika cha Mary kuziba njia kwa mbele kwakutumia gari lake hali iliyofanya mwanamama katalina ashindwe kupita na kusimamisha gari yake, mda huohuo vijana wa Mary walishuka ili wakamchukue mwanamama katalina.
"Kwa usalama wako telemka haraka sana wewe mama", kijana mmoja aliongea alipofika kwenye gari la Mwanamama katalina.
Mlango wa gari ulifunguliwa na wakatalemka wanaume wawili tena wakiwa wameshika siraha za moto,Mary alivyoona ivyo aliliondoa gari haraka maeneo yale bira kujalia kama kulikuwa na vijana wake.
Ata wale vijana nao kila mtu alitafuta njia yake ya kuokoa maisha hakuna aliyebaki maeneo yale,
"Huyu binti anataka kunizoea kukoswa kwake taji la Miss Tanzania hasira anataka azimalizie kwangu, na huu ni mwanzo tu nitampeleka gerezani akiendelea kunifatilia",Mwanamama katalina aliongea na safari iliendelea ya kuelekea nyumbani huku vijana wa Mary hakuna aliyebaki maeneo yale ata mmoja.
Mwanadada Diana na Mr.James walikuwa tayali wameshafika nchini Canada na walichokuwa wakikisubiri kwa wakati huo ni kupata majibu ya kuhusu matatibu,
"Mwanangu naamini utarudi kwenye hali yako na ningependa kujua una malengo ya kufanya kitu gani kwa sasa", Mr.James alitamani kujua malengo ya binti yake.
"Baba, mimi natamani nije niwe na kiwanda cha kuchakata nguo siku moja na kiujmla napenda mambo ya fashion ndio mana ndoto yangu ilikuwa ni kuja kuwa Miss Tanzania ili niweze kuyatangaza mavazi yangu mimi mwenyewe",Diana aliongea.
"ila bado hakijaalibika kitu bado ndoto yako imeshaanza kutimia na imebakiza kidogo iweze kutimia"
"Unamaana gani baba?"
"Angelina ni mdogo wako na ni binti muelewa ivyo anaweza kukutangazia biashara yako ukimwambia",Mr.James aliongea.
"Sizani kama atakubali baba", Diana hakuwa na matumaini kama Angelina atakubali kufanya kile alichokisema baba yake.
Wakiwa bado na maongezi tarifa ziletwa za wao kupatiwa majibu ya tatizo linalomsumbua Diana.
Na tarifa walizopatiwa ni kuwa itamchukua karibu mwaka mzima mwanadada Diana kurudi katika hali yake ya kawaida japo uwezekano wa kupona sio mkubwa kiasi hicho, mwanadada Diana alihuzunika sana na ata Mr.James ila hakukuwa na njia nyingine zaidi ya kukubaliana na hali halisi.
"Mwanangu mimi siwezi kukaa huku mda wote lazima nirudi Tanzania nikasimamie biashara yetu ili nisije kukuta mambo yameharibika, na nitaajiri mtu atakaye kuwa anakuangalia na kila baada ya mwezi mmoja kuisha nitakuwa nakuja kukujulia hali mwanangu",.
Mr.James aliongea mengi na binti yake na alipanga kurudi Tanzania baada ya siku kadhaa tu kuendelea na majukumu yake.
Stewart sasa aliamua kuitafuta namba ya Mwanadada Angelina na mtu aliyempatia namba hiyo ni Manka mwenyewe rafiki wa Angelina,
Angelina akiwa ameshika mikataba yake aliyoingia na kampuni hilo la uigizaji
akiisoma na kuipitia upya, kuna ujumbe uliingia lakini hakutaka kuusoma kwa mda huo bali aliendelea na kile alichokuwa akikifanya,
"Huu mkataba nimeusoma wote mbona sioni sehemu ikiniambia kuwa natakiwa nifanye kazi nje ya kampuni...... mimi sio mjinga kiasi hicho", Angelina alijihakikishia kuwa mikataba iko upande wake na kile alichokisema manager wake ilikuwa ni uongo aliirudisha mahala pake ili kesho asubuhi afikishe tarifa ile mahakamani.
Alishika simu yake kwa ajili ya kuangalia ni nani akiyetuma ujumbe katika simu yake,
"Najua utajiuliza sana kwanini imekuwa mapema Angelina lakini ukweli siku zote huwa haubadiliki na utabaki palepale, nakupenda Angelina nakupenda sana",ulikuwa ni ujumbe kutoka kwa Stewart na namba ilikuwa ngeni kwa Angelina kitu kilichomfanya acheke kuona mtu ambae ata hamjui alafu anamtumia ujumbe wa kumwambia anampenda ila kwa kuwa ni Miss Tanzania wa mwaka huo jumbe kama zile aliona ni kitu cha kawaida tu kutumiwa. ..ITAENDELEA.
Stewart atafanyikiwa kumpata Angelina?.
Pata Story hii mpaka mwisho kwa Tsh 1000 za k?????? lipia kupitia namba,
0613083801 HALOPESA,John Bugumba..