Story......................MISS TANZANIA
Mtunzi...................Zooper
Sehemu..ya...........09
Whatsapp..............0613083801
ilipoishia........
Kabra hajawafikia alishika simu yake na kuanza kutabasamu kwa kile alichokiona kwenye simu aliwasogelea huku akiwa anakitu cha kuongea kwa Angelina..........
ENDELEA NAYO.....
Albert alifika maeneo yale na kumuangalia Angelina kwa dharau,
"Diana unaongea na mtu atakayeenda kulitia taifa kwanye aibu mda sio mrefu, kwakuwa ulikuwa hujui ngoja nikuonyeshe yani tukio ulilolifanya leo ndani ya mda mfupi tu video yako imesambaa mitandaoni na hongera kwa hilo umekuwa superstar gafra tu",Albert aliongea baada ya kufika pale.
Angelina hakuamini ikabidi achukue simu yake nakuangalia ni kweli karibu kila mtandao wa kijamii habari zilikuwa ni za yeye kuanguka na sauti za watu kumcheka ndizo zilizokuwa zikisikika katika video hiyo.
"Hapana hii haiwezekani hauwezi kunifanyia ivi Albert nani katuma hii video mtandaoni?", Angelina alikuwa kama kichaa palepale alimfata na kumkaba shati lake Albert bira kujali kama ni mtoto wa Mwanamama katalina.
"Unakichaa wewe binti unaanzaje kumshika Albert unamjua huyu ni nani katika hii kampuni?", Diana aliongea kwa kufoka.
Albert aliitoa mikono ya Angelina na kujipangusa sehemu aliyoshikwa na Angelina kama ishara ya kuchafuliwa na Angelina.
"Huyu kachanganyikiwa naona, yani umesahau kama mlikuwa mnachukuliwa video na tukio lilikuwa live mitandaoni mpaka uje unikabe mimi, Diana emu tuondoke haina haja ya kuendelea kuongea na mtu aliyechanganyikiwa hapa", Albert alimchukua Diana na wakaondoka wakimuacha Angelina maeneo yale akiendelea kuangalia video na kusoma comment za watu,wapo waliomuonea huruma na wengine kumponda hii ilimkasilisha sana Angelina na kushindwa kuzuia hasira zake aliibamiza chini simu yake na kuondoka maeneo hayo huku simu ikiwa pale chini.
Upande wa mwanadada Mary akiwa na rafiki yake Faith walikuwa wakipongezana tu baada ya kusambaza clip zao fupi mitandaoni zikiwaonyesha wakitembea kimadaha nakupongezwa na watu wengi hali iliyomfanya Mary azidi kufurahi zaidi,
"Shoga umeona vitu ivyo huu mwaka ni wangu nakwambia angalia like na comment, haahhaahahaha huu mwaka uMiss Tanzania huo nauona",Mary aliongea.
"Bora sisi yule aliyeanguka sijui huko aliko ana hali gani sasa ivi"
"Wewe sindio ulikuwa unamsifia kuwa ni mzuri sasa ivi kikowapi yani kwenye mazoezi tu anaanguka je? siku yenyewe ya mashindano itakuwaje?",Mary alimjibu Faith .
"Kwanza tuachane na izo story, hujaniambia kinachoendelea kwa kijana wa boss", Faith aliamua apindishe mada baada ya kuona rafiki yake amemgeuzia kibao yeye.
"Umefanya jambo la mhimu kunikumbusha ngoja nimtafute mida hii".
Mary alichukua simu yake nakumpigia Albert lakini simu ilikuwa haipatikani mda huo ikamlazimu amwandikie ujumbe .
Upande wa Albert na Diana walielekea sehemu tulivu kwa ajili ya kufanya maongezi yao na temu hii Albert alipanga kumwelezea Diana kile alichothamilia kumwambia na ata simu yake aliamua kuizima kabisa ili asipatiwe usumbufu wa aina yoyote ile,
"Albert tayali tumeshafika sehemu husika naomba uanze wewe kuniambia kitu ulichotaka kuniambia",Diana alitoa nafasi kwa Albert na hii kumfanya avute pumzi kwanza kabra ya kuanza kuzungumza huku Diana akitega masikio yake vizuri kumsikiliza.
"Diana wewe ni rafiki wa mda sana kwangu, tangu tulipofahamiana shuleni kwenye shule tuliyosoma wote na mpaka hii leo bado ni marafiki tu,kuna jambo lililo ndani ya moyo wangu ningependa kukwambia"
"Jambo gani hilo Albert?", Diana alibidi aulize.
"Diana,jambo lenyewe ni...Nakupenda Diana naomba uwe mke wangu",Albert aliamua kufungua kile kilichokuwa moyoni bira kujali kuwa Diana atafanya maamuzi gani baada ya kumwambia vile.
Diana hakuamini kusikia neno nakupenda kutoka kwa Albert ilibidi amuulize kwa mara nyingine lakini bado Albert alisisitiza kuwa amemaanisha kwa kile alichokisema.
Diana alikumbuka ahadi aliyowekeana na baba yake au Mr.James mpaka kusainishana karatasi ulikuwa ni wakati mgumu sana kwa Diana kufanya maamuzi,
"Hapana Albert hatuwezi kuwa pamoja ", Diana aliamua kuongea japo alijua Albert atajisikia vibaya ila hakuwa na kingine zaidi ya kufanya yale maamuzi.
"Kwanini Diana isiwezekane?, kama tatizo ni wazazi wetu nipo tayali mimi kwenda kuishi mbali na wewe ili tuwe mbali nao najua mama yangu hakupendi wewe na ata baba yako pia hanipendi mimi, lakini mimi nakupenda wewe Diana".
"I'm sorry Albert,sio kwa sababu hiyo nataka nikamilishe kwanza jambo langu la haya mashindano sihitaji kuingia kwenye mahusino kwa sasa naomba unielewe Albert", Diana aliongea.
"Diana sielewi hatima yangu ni ipi, nisubiri mpaka mashindano yatakapoisha? au nifanye kitu gani?",Albert ilibidi aulize kwa mara nyingine.
Diana alifikilia nakuona hatakiwi kumkataa Albert moja kwa moja kwani bado anamalengo ya kumtumia ili aibuke mshindi wa mashindano ya Miss Tanzania yaliyokuwa yamebakiza miezi miwili tu yafanyike.
"Albert nipe mda tafadhali nifikilie kuhusu hili", kidogo maneno ya Diana yalimpa matumaini Albert na kumfanya arudishe tabasamu lililokuwa limepotea na maongezi mengine yakiendelea.
Mwanamama Beatrice akiwa amekaa alishangaa kumuona binti yake Angelina akiwa analia tena alimpita pasipo ata kumsalimia na kuelekea chumbani kwake moja kwa moja, mbaya zaidi alifika na kufunga mlango wa chumbani kwake,
Mama yake ilibidi anyenyuke na kumfata,
"Wewe Angelina fungua mlango mwanangu umepatwa na nini?",Mwanamama Beatrice aliongea lakini ni sauti ya kilio tu kutoka kwa mtoto wake ndiyo aliyokuwa akiisikia.
Aliendelea kumwita bira mafanyikio na Angelina aligoma kabisa kufungua mlango.
Manka alishangaa kuona picha za rafiki yake Angelina imesambaa mtandaoni ikimuonyesha jinsi alivyoanguka na watu wakimcheka,
"Dah masikini Angelina atakuwa kwenye kipindi kigumu sana, ngoja nikamuangalie nyumbani kwao alitoka nakuelekea nyumbani kwa rafiki yake.
Ndani ya mda mfupi tu aliweza kufika na kubisha hodi na Mwanamama Beatrice alikuja kumfungulia.
"Mama Angelina yuko wapi?", ndio swali la kwanza alilokutana nalo Mwanamama Beatrice pasipo ata kusamiliwa na binti huyo.
"Bora ata umekuja rafiki Yako kajifungia chumbani hataki ata kufungua mlango yumo analia tu na sijui tatizo gani limempata huko"
Manka hakutaka kuanza kumwelezea zaidi ya kuchukua simu yake na kumwonyesha kile kilichokuwa kikiendelea mitandaoni, Mwanamama Beatrice nae hakuamini baada ya kuangalia ilimuumiza sana kuona mwanae alivyozalilika mbele za umati.
"Binti yangu atakuwa kwenye kipindi kigumu sana na anaweza kufanya jambo litakalomlea matatizo,Manka naomba tusaidizane kuuvunja mlango".
Wazo la Mwanamama Beatrice liliungwa mkono na Manka, kazi ilibaki moja tu ya kuvunja mlango.
Walitafuta kitu kizito na kuanza kuvunja mlango mpaka pale walipofanyikiwa kuuvunja na kumkuta Angelina amekaa huku akilia,
"Angelina mwanangu hupaswi kujilaumu izo ni changamoto naomba usiwe mnyonge kiasi hicho"
"Mama nisiwe mnyonge huoni kinachoendelea mitandaoni, na mimi kuanzia leo sitakanyaga tena katika ile kampuni na hayo mashindano siyataki tena mtaenda kushiriki wenyewe", Angelina alikuwa kamaanisha kile alichokizungumza na hakutaka kurudi tena kwenye kampuni ya FNF.
Mwanamama Katalina nae pia aliiona video ile mitandaoni lakini lawama zote alizipeleka kwa mtu aliyekuwa akirecord kwa kushindwa kumsitili Angelina.
lakini palepale simu yake iliita na kuipokea,
"Tunajivunia sana kuingia mkataba na kampuni yenu katalina", sauti ya mpigaji ilisikika.
"Unamaana gan Mr.?"
Tukio la binti yule kuanguka kwetu imekuwa kama faida mana ile video imesambaa kwa wingi na chapa ya kiatu chetu ilionekana kitendo kilichowafanya watu waangalie ni kampuni gani hilo lililotengeza viatu vilivyomfanya binti anguke,hiyo ni faida kwetu kwani followers kwenye mitandao yetu hivi ninavyokwmabia wameongezeka kwa kasi sana na hii imekuwa faida kwetu japo ni fedhea kwa binti wa watu,
Aliendelea kuongea.....
Nazani kesho Kuna zawadi yake sisi kama kampuni tutakuja kumpa na kumtia moyo aendelee kushiriki kwenye mashindano japo najua watu wengi watashangaa sana",alikata simu baada ya kumpa tarifa zile.
Baada ya simu kukatwa Mwanamama Katalina aliamua kunyenyuka kwenye kiti alichokuwa amekaa na kwenda kwenye gari lake tena akiliondoa kwa kasi na haikufahamika ni wapi anapoelekea.....ITAENDELEA.
Wapi ambapo Mwanamama Katalina anaenda?,mashindano bado miezi miwili tu na Angelina amegoma kushiriki tukutane katika sehemu inayokuja.
NB: Story hii NIYAKUTUNGA na haina ukweli wowote ule unaoendana na taratibu za nchi yetu????????????????.
Pata Story hii mpaka mwisho kwa Tsh 1000 za k???????????????????????? lipia kupitia namba,
0613083801 HALOPESA,John Bugumba..