Story......................MISS TANZANIA
Mtunzi...................Zooper
Sehemu..ya...........30(FINAL)
Whatsapp..............0613083801
ilipoishia......
Diana alifika mpaka nyumbani na kumfanya Mr.James ashangae kwa ujio wa binti yake tena wa bira kutoa tarifa zozote zile..............
ENDELEA NAYO.......
Diana alifika mpka nyumbani kwao na kukaa kwenye kochi huku akilia na haikupita mda driver tax aliingia akiwa na mabegi
yake na kumuomba kiasi cha pesa alichokuwa anakidai ila Mr.James aliweza kumlipia mwanae na ndani akabaki yeye na binti yake baada ya driver tax kuondoka.
Kiufupi Diana aliumia sana kufika na kukuta Albert ameshaoa tena aliyemuoa ni mdogo wake ambae ni Angelina alichukia sana na kujikuta akitengeneza kisasi na ndugu yake kwa mara nyingi tena,machozi ya binti yake yalimfanya Mr.James amsogele,
"Diana mwanangu tatizo nini binti yangu?",Mr.James alimuuliza binti yake na hakupendezwa kumuona yupo kwenye hali aliyonayo kwa wakati huo.
"Baba ina maana na wewe ulikuwa hujui kama Albert anafunga ndoa tena mtu mwenyewe aliyeolewa ni mdogo wangu?",Diana aliongea na kumfanya Mr.James aelewe ni kipi kilichomfanya alie.
Kwanza alimfata mchozi binti yake na kumkumbatia mana ndiyo mtoto wa pekee aliyekuwa nae,
"Mwanangu utawalaumu bure wale hawana makosa mwenye kosa ni mimi na wewe, Albert alikuwa anakujali sana na kuna siku alikuja kwangu akitaka kujua hali yako na mimi ndiye niliyempa ruhusa atafute mke mwingine, naomba nikili kuwa bira mimi kumwambia Albert huenda mpaka sasa ivi angekuwa bado anakusubiri wewe", Mr.James aliongea na kumfanya mwanadada Diana apate mwanga kidogo ya kipi kilichosababisha mpaka Angelina kuolewa na Albert alijiona yeye ndio chanzo cha yote yaliyotokea.
Mr.James alikumbuka kitu cha mhimu sana alichokuwa amemwandalia binti yake na alikuwa akimsubiri siku atakayo kuja Tanzania aweze kumpatia kitu hicho,
"Mwanangu nifate kuna sehemu nataka nikupeleke"
"Wapi baba?",Diana alihoji lakini Mr.James hakutaka kujibu kitu zaidi ya kuondoka na kwenda kupanda kwenye gari huku Diana nae akimfata nyuma ambae nae alienda kupanda kwenye gari alilo panda baba yake mzazi huku gari likiondoka maeneo hayo.
Safari ya Mr.James na binti yake iliwafikisha mpaka kiwandani kulipokuwa na kiwanda kipya kabisa cha nguo huku watu mbalimbali wakiendelea na kazi na kila mtu akiwa bize,
Mr.james anamjua binti yake ni mtu wa kuuliza maswali kila mara ilibidi yeye ndiyo aanze kumwambia kabra hajaulizwa na binti yake,
"Ndoto yako uliyowahi kuniambia mwanangu ilikuwa ikinisumbua mno, ata kulala nilikuwa silali vizuri kwa mawazo ya kukufungulia kiwanda ila namshukuru mungu nilifanyikiwa nakuikamilisha ndoto yako Diana hichi unachokiona hapa ni kiwanda chako, nilifungua kwa ajili yako",Mr. James aliongea.
Baada ya kumaliza kuongea tu binti yake alimkumbatia kwa furaha baba yake kwa kuweza kukamilisha ndoto aliyokuwa akiitamani,Diana alizunguka na kukikagua kiwanda chake na alilizika nacho kwa asilimia mia moja na hakuacha kumshukuru baba yake kwa kutumiza ndoto zake.
Stewart na Manka waliamua kufunga ndoa na tarifa zilimfikia Angelina ambaye nae alifurahi kuona rafiki yake anafunga ndoa na Stewart walipanga tarehe ya ndoa na siku ilipofika ndoa iliweza kufanyika huku Mr.John na mke wake wakifurahi kuona mwanao kapata mke na ameamua kuishi maisha ya kiutu uzima na ata Angelina pamoja na Albert walihudhulia katika ndoa hiyo na kutoa zawadi kemkemu kwa wanandoa hao.
Stewart na Manka walianza maisha mapya wakiwa kama mke na mme.
Mr.James aliamua kumuita Angelina na Diana akiwa maeneo yale nakuwakalisha ili wamalize tofauti zao,na aliwakumbusha kuwa wao ni ndugu hawatakiwi kuwa na uadui.
Diana aliamua kumsamehe ndugu yake na kumuomba msamaha mahali alipokuwa amekosea na Angelina naye alifanya ivyoivyo,
Angelina na Diana wakawa kitu kimoja na kutokana na Angelina kuwa Miss Tanzania aliamua kufanya matangazo kwa kuvaa nguo zilizokuwa zikitengenezwa na kampuni ya Diana na hii ilifanya kampuni hiyo iliyokuwa ikiitwa DCL(Diana Company Limited) kukuwa kwa kasi na kuwa moja ya kampuni yaliyokuwa yakiingiza kiasi kikubwa cha pesa ndani ya Tanzania.
Mr.James,Mr.John na Mwanamama katalina waliamua kumaliza tofauti zao hasa Mr.James na Mwanamama katalina waliamua kuishi kiutu uzima na kuacha yapite mambo ya miaka ya nyuma kila mmoja alimsamehe mwenzake.
Baada ya mwaka mmoja kupita Diana alipata mwanaume mwingine waliyefunga nae ndoa huku ndoa yao ikihudhuliwa na karibu kila mtu na ata mwananadada Angelina nae alikuwepo kwenye ndoa ya ndugu yake,huku Albert akimpongeza Diana kwa kumpata mwenza wa maisha yake.
MWISHOOO.
Ahsanteni sana???????????? kwakuweza kufatilia simulizi hii mpaka hapa inapofika tamati nawapenda sana ndugu zangu,MUNGU awatie nguvu kwenya kazi za mikono yenu... Mwisho wa simulizi hii ndio mwanzo wa simulizi nyingine..