Story......................MISS TANZANIA
Mtunzi...................Zooper
Sehemu..ya...........13
Whatsapp..............0613083801
ilipoishia.........
"Mama hii ni lazima naomba tuondoke lasivyo nitakupoteza mama yangu naombe uelewe hiki ninachokwambia"
"Utanipoteza kivipi Albert", Mwanamama katalina alimuuliza mwanae...
ENDELEA NAYO.....
Albert baada ya kuona mama yake hamwelewi anachoongea aliamua kumshika mkono na kumtoa maeneo yale huku watu wengine wakiwaangalia tu.
Upande wa Angelina alikuwa akiendelea kupiga picha na washiriki walimwomba wapige nae picha kwa ajili ya kutunza kumbukumbu, Diana aliamua kuondoka na kuelekea kwenye gari lake huku akilivua taji alilokuwa amepewa kama mshindi wa pili na kulitupa chini kwa hasira na kupanda kwenye gari lake, akiwa anajianda kuwasha na kugeuza gari ili aondoke baba yake alifika,
"Binti yangu, naomba ushuke kwenye hiyo gari", Mr.James aliongea.
"Baba niache kwa sasa nahitaji kubaki peke yangu, utanikuta nyumbani baba",Diana aliongea tena bira kumuangalia baba yake usoni.
Diana hakutaka kumsikiliza baba yake aliwasha gari na kuondoka maeneo hayo tena gari ikiwa kwenye mwendo usiokuwa wa kawaida.
Mr.James alishangaa kuona binti yake ameshindwa kumsikiliza,
"Huyu mtoto mbona hataki kunisikiliza kile ninachomwambia na wasiwasi na huo uendeshaji wake wa gari",Mr.James alikasilishwa na kitendo cha mwanae kukataa kumsikiliza.
Albert yeye alikuwa bado amemshika mama yake mkono akimhimiza watoke eneo hilo haraka sana na wakati huo walikuwa wameshafika nje ya ukumbi,
"Una matatizo gani mbona unanikokota tu bira kunisikiliza mimi mama yako?", Mwanamama Katalina aliamua kuwa mkali baada ya kuona Albert anampelekesha tu bira kumfafanulia vizuri.
"Mama kuna watu wamepanga kukuua,ndio mana nakutoa kwenye hili eneo",Albert hakuona sababu ya kuficha tena aliamua kuongea mbele ya mama yake.
"Watu wamepanga kuniua!!, ni kina nani hao?"
"Mama nitakwelezea tukufika nyumbani naomba tuondoke hapa mana sio sehemu salama kabisa".
Hakuna asiyependa kuishi baada mwanamama Katalina kusikia maneno ya mwanae aliamua kukubali kuongozana nae mpaka nyumbani.
Upande wa Stewart alitoka na kuwaacha wazazi wake akiwa na lengo la kumtafuta Diana, huku baba yake mzazi au Mr.John ilibidi amchukue mke wake waende nyumbani na wakimuacha kijana wao aendelee kula ujana usiku huo, Mr.John akiwa na mke wake walielekea mpaka sehemu ya parking na kuingia kwenye gari lao.
Mr.John aliwasha gari na kuirudisha nyuma kidogo ili aiondoshe ila bahati mbaya alipokuwa akiirudisha nyuma aligonga gari iliyokuwa nyuma yake,
"Nani wewe unayerudisha nyuma gari bira kutazama vizuri mpaka umegonga gari yangu?", sauti ilimfikia Mr.John aliyegonga kwa bahati mbaya na ikamlazimu kushuka na kumuacha mke wake kwenye gari.
Ata mwenye gari iliyogongwa naye alishuka kuangalia ni nani huyo aliyeigonga gari lake na hakuwa mwingine bali ni Mr.James na wote walijikuta wakikutana,
Japo kuwa ilikuwa ni usiku na mwaga ukiwa ni hafifu uliokuwa maeneo yale ila Mr.James aliitambua vizuri sura ya Mr.John.
"Ni wewe mpuuzi", Mr.James aliongea na kumfanya Mr.John ashangae ni nani huyo anayemwita mpuuzi.
"Kwani we nani unayeniita mpuuzi?, na nipende kukuomba samahani mana ilikuwa bahati mbaya tu", Mr.John aliongea kiupole.
Mr.James alikumbuka enzi zile za ujana alivyokuwa akimpenda mwanamama Katalina na mtu aliyemfanya atengane na mwanamke aliyekuwa akimpenda ni Mr.John aliyekuwa maeneo yale.
"Unajifanya umenisahau na alafu unauliza mimi nani?, hukumbuki ulichowahi kunifanyia miaka ya nyuma au unafikili sura yako siikumbuki?", Mr.James aliongea.
"Kwani wewe nani mbona sikuelewi"
"Hunielewi leo utanielewa tu,wewe sindio John?"
"Yes, ni mimi"
"Unamkumbuka katalina?", Mr.James alimuuliza.
Mr.John alianza kuvuta kumbukumbu ndipo sura ya katalina ilipoanza kuja kwenye kichwa chake na kumkumbuka vizuri.
"Najua huwezi kusema kwakuwa upo na mkeo kwenye gari ila unatakiwa ulipe taa ya gari langu uliyoiharibu", Mr.James aliongea tena akiwa hana utani ata kidogo.
Mr.James alichomoa mfukoni kadi iliyokuwa na namba zake nakumpa Mr.John,
"Milion 4 nikifika nyumbani kwangu ziwe zimeshaingia kwenye simu yangu ya matengenezo ya taa ya gari yangu uliyoipasua", hakutaka kuongea mengi alienda kupanda kwenye gari na kuondoka.
Alimuacha Mr.John akimtazama bira kummaliza nae pia alikumbuka jinsi walivyowahi kupigana enzi za ujana wao kisa katalina na hii kumfanya acheke ila aliamua kuingia kwenye gari na kuondoka akiwa na mkewe.
Diana baada ya kutoka kwenye ukumbi wa akiwa na hasira baada ya kuibuka mshindi wa pili na sio wa kwanza kama alivyokuwa anataka yeye, alikuwa bado akiendesha gari kwa kasi usiku huo kuelekea nyumbani kwao, lakini siku hiyo ilikuwa ni mbaya kwake kwani alifika sehemu yenye kona na ilitakiwa akate kona kwa umakini lakini alijikuta akipoteza umakini hali iliyosababisha kwenda kugongana na gari lililokuwa likija upande wake na gari ya mwanadada Diana ilienda kuangukia pembeni huku Diana akiwa ndani ya lile gari, na ata lile gari jingine lilokuwa na watu zaidi ya watano nalo lilienda kugonga mti uliokuwa pembeni hali iliyowafanya wote waliokuwa kwenye gari ile kuumia vibaya sana huku wengine wakifariki hapohapo.
Kwakuwa ilikuwa ni majira ya usiku watu wachache walifika pale kwenye ajari na kuanza kuwasaidia watu waliopatwa na ajari na Diana akiwa ni miongoni mwao, huku vijana wengine wakiichukulia kama bahati kwao kwa kuiba vitu vilivyokuwa ndani ya ile gari.
Diana alikimbizwa hospital kwa ajiri ya matibabu, huku kwenye hospital hiyo wakiwa na kazi ya kumtafuta ndugu yoyote yule wa Diana mana ata wale waliomleta waliezea jinsi ilivyokuwa nakuwaachia mzigo wauguzi wa hospital ile,
Waliamua kumpiga picha Diana na kusambaza tarifa zake mtandaoni kuwa ndugu yoyote anahitajika,
Baadhi ya watu walianza kufananisha picha iliyotumwa mitandaoni ya mtu aliyepata ajari na picha ya mshindi wa pili kwenye mashindano ya Miss Tanzania, na kweli tarifa zilisambaa kwa wingi kuwa mshindi wa pili wa mashindano ya Miss Tanzania yaliyomalizika mda mfupi uliopita amepata ajari.
Upande wa Mr.James alikuwa ameshafika nyumbani kwake lakini alishangaa kutokumwona binti yake ila haikichukuwa mda simu yake ilianza kuita,
"Nani tena huyu anayepiga simu usiku huu",aliangalia mpigaji na kukuta namba ni ngeni ila aliamua kuipokea ili ajue ni nani anayempigia,
"Mr.James tarifa ninazo ziona mitandaoni zina ukweli wowote ule?",alikuwa ni mfanya biashara mwenzake aliyekuwa akiongea upande wa pili.
"Tarifa gani?"
"Kata simu nakutumia picha hapo haraka sana".
Mr.James alikata simu na huwa sio mpenzi wa kutumia mitandao sana ndio mana mpaka wakati huo alikuwa bado hajapata tarifa juu ya kile kilichokuwa kikiendelea kwenye mitandao ya kijamii.
Aliwasha data nakuangalia picha alizotumiwa na mfanyabiashara mwenzake hakuamini kuona sura ya binti yake Diana tena akiwa kwenye hali mbaya na tarifa zikisema za kumtafuta ndugu yoyote wa binti huyo,
"Huu ni uongo mwanangu Diana hawezi kuwa kwenye hii hali", Mr.James alipingana na kile alichokiona lakini haikubadilisha ukweli wowote kuwa ni mwanae Diana.
Mda huohuo alitoka na kwenda kwenye hospital kuhakikisha kama ni binti yake kweli.....ITAENDELEA.
Karibu katika sehemu inayokuja tujue hali ya Diana
NB: Story hii NIYAKUTUNGA na haina ukweli wowote ule unaoendana na taratibu za nchi yetu????.
Pata Story hii mpaka mwisho kwa Tsh 1000 za k?????? lipia kupitia namba,
0613083801 HALOPESA,John Bugumba..