Story......................MISS TANZANIA
Mtunzi...................Zooper
Sehemu..ya...........01
Whatsapp..............0613083801
Anza nayo...
Tarehe husika ya usajili ilitangazwa kwa wadada wote wenye sifa ya kuweza kushindana kwenye mashindano ya Miss Tanzania au wengine hupenda kuita mrembo wa taifa,wadada mbalimbali na warembo waliwasili katika kampuni ya FNF iliyopewa haki ya kusimamia mashindano hayo ndani ya mwaka huo husika,si wenye rangi nyeusi, weupe na ata wenye mwonekano wa maji kunde wote walionekana ndani ya kampuni hiyo kwa ajili ya kujisajili.
Kulikuwa na wadada wa kutosha na karibu kila mtu aliamini ataweza kunyakua taji hilo ndani ya mwaka huo.
Nje ya jengo la FNF kuna magari mawili ya kifahali yanawasili maeneo ya jengo hilo na kwenye gari la kwanza anatelemka Mwanamama pia gari la pili anatelemka kijana mweupe na mtanashati aliyevaa kinadhifu, waliingia ndani ya jengo hilo wakielekea moja kwa moja mpaka walipo kinadada waliokuja kwa ajili ya usajili katika kampuni hilo, karibu kila mwanadada aliyekuja kwa ajili ya usajili macho yao yalikuwa kwa watu wale wawili walionekana ni watu wakubwa ndani ya ile kampuni.
Mwanamama pamoja na kijana yule waliwasogelea warembo waliokuwa maeneo yale na hii kuwafanya wote waliokuwa pale wakae kimya na wasitishe mazungumzo waliyokuwa nayo baada ya kuwaona watu wale wakija upande wao,
"Hi ladies,I'm katalina nitakuwa pamoja na nyinyi, na mimi ndiye msimamizi wenu mkuu mpaka pale tutakapofika tamati ya haya mashindano, mnakalibishwa wote katika kampuni hii ya FNF na mjisikie kama mpo nyumbani", Mwanamama aliyejitambulisha kwa jina la katalina aliongea.
Baadhi ya wadada walitoa sauti za kumshukuru kwa kumfahamu Mwanamama aliyejitambulisha kwa jina la katalina na mda huo wakiwa na mazungumzo kijana aliyeongoza na mwanamama katalina nae pia alitoa salamu kwa wanadada wote waliokuwa pale kisha alimsogelea karibu mwanamama katalina nakumwambia,
"Mama namazungumzo na wewe,naomba tuongee pembeni kidogo",kijana yule aliongea
"Okay my son,ila ngoja kwanza nikutambulishe na litakuwa ni jambo jema kwa wao kukufahamu", Mwanamama katalina aliongea,basi aliwaambia wanadada wote kuwa anataka kufanya utambulusho mwingine mbele yao na hii iliwafanya wote kutega masikio yao vizuri ili kumsikiliza,
"Huyu mnayemuona hapa anaitwa Albert ni mwanangu wa peke, mtakapo mwona popote pale basi mjue ni yeye pekee aliyenifanya niitwe mama na anafanya kazi katika kampuni hii ya FNF tutakuwa naye bega kwa bega kwa baadhi ya mambo mpaka pale tutakapohitimisha mashindano yetu",Mwanamama katalina alimaliza kuongea.
Wanadada walipiga makofi kumfahamu Albert mtoto wa msimamizi wao na kilichowavutia zaidi ni mwonekano aliokuwa nao kijana huyo uliowavutia wengi waliokuwa pale.
Baada ya utambulisho huo mama na mtoto walisogea pembeni kwa ajili ya maongezi,
"Mama mda tayali wa kwenda kumpokea Diana airport umefika,nahisi tayali atakuwa ameshawasili hapa Tanzania na nilimuahidi nitafika mda mwafaka kumpokea"
"Albert mwanangu kwani Diana amekupa Nini mpaka ushindwe kufata ratiba zako za kazi unajua kabisa wewe ndiyo utakayekuja kuwa mlithi wangu badae lakini haiwezi pita siku hujamtaja Diana",Mwanamama katalina aliongea kuonyeshwa kutokupendezwa na maneno aliyotamka mwanae.
"Najua mama wewe Huwa humpendi Diana na sijui ni kwanini ila yule ni rafiki yangu na kaniambia ata yeye atakuja kushuriki mashindano haya ya Miss Tanzania, I will see you later mom( nitakuona badae mama)", Albert aliongea Huku akiondoka na kuelekea kwenye gari kwa ajili ya kwenda airport.
"Huyu mtoto ana matatizo Gani huyo Diana kwani kampa Nini na mbaya zaidi aje kushuriki haya mashindano hiyo haiwezekani labda sio Mimi katalina, sema hajui ni kitu gani kinachonifanya nimchukie Diana ila ipo siku atajua",
Mwanamama katalina aliongea na ilionekana hapendi Diana kuona akiwa Karibu na kijana wake Albert.
Ndani ya mgahawa mkubwa na maarufu ulio katika ya mji wanaonekana waudumu wawili mmoja ni mwanadada anayefahamika kwa jina la Anjelina akiwa amekaa na rafiki aliyefamika kwa jina la Manka na hii ni baada ya kumaliza kutoa hudumia kwa wateja wao huku wakisubiri wateja wengine waje, na story mbalimbali zilichukua nafasi,
"Anjelina kuna habari mpya zinazosamba, umezipata izo habari?", Manka alimuuliza rafiki yake.
"Habari gani tena?"
"Mashindano ya Miss Tanzania sio mda yataanza kwa jinsi ulivyo mrembo rafiki yangu na unavyo tembea kimiss, mimi naona yanakufaa kabisa na inatakiwa uende ukashiriki"
"Eeeh!!,yani jinsi ulivyoanza kuongea Manka nikajua utaongea kitu cha mana mimi tangu lini nikafaa kuwa Miss Tanzania?, acha tu niendelee na kazi yangu ya kuwa mhudumu wa mgahawa na uzuri ninachopata kinanitosha",Angelina alimjibu Manka.
Manka hakupenda kile alichozungumza Angelina na aliona rafiki yake ana kila sifa za kushiriki mashindano hayo,
"Yani wewe ndio mana Huwa sikupi madili kila kitu ninachokwambia Huwa unasema ivyoivyo, tangu tumemaliza chuo mwaka uliopita madili mengi ya maana nakupa lakini unapuuzia tu, yani basi tu kwakuwa mimi sina sura kama yako na bahati mbaya tena umbo langu halieleweki ningeenda kushiriki huenda ningekuwa mtu mashuhuli kwenye hii nchi, mambo ya kufanya kazi za ajabu na malipo yenyewe ni ovyo tu hapa",Manka alilalamika na kuondoka maeneo Yale.
Angela alibaki anacheka tu mana ameshamzoea rafiki huyo hakosi maneno na viugomvi vidogo visivyo na sababu na alinyenyuka nakuendelea na kazi baada ya wateja wengine kuanza kuongezeka katika mgahawa huo.
Albert anafika katika uwanja wa ndege na gari lake kwa ajili ya kumpokea mtu ambae kamfanya awe hapo ila anakuta ndege bado haijawasili ilibidi akae kusubiri mpaka itakapo wasili, haikuchukua mda ndege iliweza kuwasili,
Abiria walianza kushuka kwenye ndege na moja ya abiria hao ni mwanadada mrembo naye anaonekana akitelemka kwa madoido huku usoni akiwa kavaa miwani na nyuma yake kulikuwa na kijana waliyeshuka nae wote kwenye ndege ila kijana huyo alikuwa akimtazama mwanadada aliyekuwa mbele yake na alivutiwa na jinsi alivyokuwa akitembea, ilibidi amuwahi akaongee nae,
"Excuse young lady, is this your country?",kijana alimuuliza baada ya kumsogelea.
"Yes ofcourse,nini ulichotaka kusema"
"Ooh kumbe ni mtanzania mwenzangu samahani sana nilijua ni mtu wa kutoka taifa jingine ndio mana nilikuuliza kwa kingeleza ,mimi naitwa Stewart sijui mwenzangu unaitwa nani",Stewart alijitambulisha lakini mwanadada huyo hakutaka kumjibu zaidi ya kuendelea na safari yake mpaka sehemu ya mapokezi.
Albert alikuwa yupo makini kuangalia kila mtu aliyekuwa anapita pale Ili asije kupotezana na mtu aliyemfanya kuwa maeneo yale, kwa mbali anamuona mtu aliyekuwa akimsubiri kwa hamu ila akiongozana na kijana mmoja aliyekuwa nyuma yake,
"Yule nani aliyeongozana na Diana?,anyway ngoja nikampoke tu",aliongea kana kwamba kuna mtu anayeongea nae, akiwa kama mwanaume alijikuta akipata wivu baada ya kumuona Diana akiongozana na kijana mwingine.
Albert alisogea mpaka pale alipo Diana na ata mwanadada Diana alivyomwona Albert alimkimbilia na kumkumbatia huku kila mtu akiwa na furaha ya kumuona mwenzake,
"Umebadilika sana Diana unazidi kuwa mrembo zaidi"
"Ata wewe Albert unazidi kuwa handsome zaidi ya nilivyokuacha"
"uliyekuwa umeongozana nae yuko mbona simuoni hapa?", Albert aliuliza.
"Nani tena!"
"Mmmh nimewaona kuanzia kule mmeongozana ila mwenzako nashangaa gafra kapotea tu"
"Hahahaha yule ata sijuani nae kabisa tumeshuka wote kwenye ndege",Diana alianza kumwelezea jinsi ilivyokutana na kijana aliyekuwa anamwongelea hali iliyomfanya Albert amwelewe vizuri na waliamua kuondoka maeneo yale.
Kipindi wao wanaongea kumbe kijana Stewart aliyejitambulisha mbele ya Diana alisikia kila kitu walichozungumza mana alikuwa amejibanza mahali akiwasikiliza.
"Huyu mwanamke lazima nimtafute na lazima nitampata tu", yalikuwa ni maneno ya Stewart aliyeamua kuondoka maeneo hayo.
Wakiwa ndani ya gari baada ya kutoka uwanja wa ndege Diana alivyotazama kwa nje aliona kuna mgahawa wa kisasa hali iliyomfanya amuongeleshe Albert,
"Albert naomba usimamishe gari mara Moja".
Albert alifanya kama mwanadada alivyokuwa anataka na gari ikawa imesimama.
"I miss Tanzanian coffee, twende kwanza tukanywe kahawa kisha baada ya hapo tuendele na safari", Diana aliongea na wakati huo wakiwa wanatelemka kwenye gari,moja kwa moja walielekea mahali kulipokuwa na mgahawa.
Walipofika Diana aliagiza kahawa na mhudumu aliyeenda kwa ajili ya kuwahudumia hakuwa mwingine bali alikuwa Angelina aliyeenda kuwafatia kahawa,Diana na Albert waliendelea kuongea huku wakisubiri kahawa iletwe.
Angelina alibeba vikombe vya kahawa ila alipofika karibu na meza waliyokuwa wamekaa na akijianda kwa ajili ya kuweka vikombe vile vya kahawa mezani bahati mbaya alijikwaa na kumwaga kahawa iliyoenda kuwalowanisha Albert pamoja na Diana, kilikuwa ni kitendo kilichomkela Diana.
Diana alinyenyuka kwa hasira na kumfata Angelina Kisha kumpiga Kofi,
"Unaakili wewe, unashindwaje kuwa makini mpaka unachafua watu kiasi hichi",aliongea kwa sauti ya juu iliyomfanya ata boss wa mgahawa ule asogee kuangalia tatizo nini?.........ITAENDELEA.
Sina msaada na Angelina nini ambacho kinamkuta karibu katika sehemu ya pili ya mkasa huu wa kusisimua.
NB: Story hii NIYAKUTUNGA na haina ukweli wowote ule unaoendana na taratibu za nchi yetu????????.
Pata Story hii mpaka mwisho kwa Tsh 1000 za k???????????????????????? lipia kupitia namba,
0613083801 HALOPESA,John Bugumba.
.