Story......................MISS TANZANIA
Mtunzi...................Zooper
Sehemu..ya...........11
Whatsapp..............0613083801
ilipoishia......
Hii ilimaanisha kuwa ameapa kuwa mshindani na sio msindikizaji kwa wenzake kauli aliyozungumza ilimfurahisha sana mwanamama katalina...
ENDELEA NAYO....
Baada ya Angelina kuamua kutokukata tamaa na kuipambania nafasi ya kuwa Miss Tanzania mambo yalibadilika kwani alianza kuonyesha ushindani wa hali ya juu na ata baadhi ya washirika wenzake walianza kuona mabadiliko kutoka kwake hali iliyowafanya wasahau ata lile tukio la kuanguka na video yake kusambaa, huku Albert akimuahidi Mary kuwa lazima awe Miss Tanzania.
Siku nazo zilisogea sasa zilibaki siku mbili tu kwa ajili ya mashindano kufanyika.
Makampuni mbalimbali ya mavazi na wafanyabiashara wakubwa walitoa uthamini kwa washiriki mbalimbali kutumia bidhaa za mavazi yao ili waweze kujitangaza kibiashara zaidi, na kila mshiriki alisubiri kwa hamu siku iweze kufika.
Mary alimua amtafute Albert,
"Albert unakumbuka makubaliano yetu yalivyokuwa", alikuwa ni Mary aliyekuwa akiongea na hii ilimfanya Albert kukaa kimya huku akimsikiliza mwanadada huyo.
"Nakumbuka lakini mimi nitafanya nini ikiwa sipo sehemu ya watu watakao husika kupiga kura kwa ajili ya kumchagua mushindi?",Albert alijibu kiutaratibu na kiukweli alikuwa ameshikwa na kushikika na mwanadada Mary.
"Namba yangu ya ushiriki unaijua nenda kaongee na mama yako awashawishi majaji wawe upande wangu siku hiyo, mimi ninachotaka niushindi tu tumia njia yoyote ile unaoijua wewe ilimradi niwe Miss Tanzania vinginevyo utampoteza mama yako mzazi, naondoka Albert tukutane siku ya mashindano",Mary aliongea nakuondoka.
Albert alibaki mwenye mawazo asijue cha kufanya kwa kile alichoambiwa na Mary,
"Huyu asinifanye mimi mtoto mdogo ngoja tuone baada ya mashindano nini atafanya kwa mama yangu,sitafanya kile anachokitaka na mama yangu hatopata tatizo lolote lile", Alibert sasa aliamua kushikilia msimamo wake kama mwanaume.
Siku mbili ziliisha na siku ya tukio ya kumchagua mrembo wa taifa ilifika na kila mtu aliusubiri usiku huo kwa hamu kila mwanadada alikuwa na uhakika wa kuibuka mshindi mbele ya wenzake.
Mwanadada Diana mawasiliano na Stewart yaliongezeka zaidi siku hadi siku na ilifika mda ata Mr.James mwenyewe alitokea kumkubali kijana Stewart na hii ikamfanya Stewart awe na uhuru wa kwenda nyumbani kwao Diana mara kwa mara na ata siku hiyo aliamua kuja kwa ajili ya kufanya maongezi na Diana,
"Diana leo ni siku uliyokuwa ukiisubiri kwa hamu sana naamini usiku wa leo lazima utaibuka mshindi na utakuwa Miss Tanzania wa huu mwaka",Stewart aliongea.
"Nashukuru kwa kunitia moyo ila kuna mtu nilitegemea ndiyo atakuwa msaada wangu wa kuifanya kazi hii iwe nyepesi lakini nae naona kama hajali kabisa",Daina aliongea akimaanisha Albert.
"Mtu gani huyo?"
"Sio lazima sana umjue, kikubwa nahitaji uwepo wako usiku wa leo hakikisha unakuja kuniunga mkono", Diana aliamua abindishe mada hakutaka kuongea kiundani zaidi.
"Tena sio mimi tu nitakuja na wazazi wangu Mr.John na Mrs.John"
"Hahahahaha, mtoto wa mzee John unamaneno".
"Eheee vip kuhusu Mr.James atakuwepo kwenye siku hii mhimu Diana?",Stewart alimuuliza akimaanisha baba yake mzazi.
"Ndio mzazi niliyenae lazima aje atake asitake".
Walikuwa wameshazoeana kwa kiasi kikubwa sana na utani kwao kilikuwa ni kitu cha kawaida kati ya Diana na Stewart.
Upande wa Albert mawazo yalikuwa kwa mama yake mzazi na alisahau ata kumtafuta Diana siku hiyo alipokuwa nyumbani kwao macho yake yote yalikuwa kwa mwanamama katalina.
"Leo mbona unaniangalia ivyo shida nini Albert mwanangu?"
Mwanamama katalina alimuuliza mwanae.
"Hapana mama ila najiuliza leo nani atakayeibuka mshindi na natamani pia mwaka kesho kampuni letu lipewe hii tenda ya kusimamia tena mashindano yajayo",Albert aliongea.
"Albert kweli umekuwa sasa ivi mwanangu na unaongea mambo yenye kujenga tofauti na zamani lakini inakupaswa ujiandae na wewe hatuna mda wa kupoteza",Mwanamama katalina aliongea na kuelekea chumbani kwake.
"Yani leo siwezi kukaa mbali na wewe mama ata dekika moja nitakuwa na wewe kila sehemu kuhakikisha unakuwa salama", Albert aliongea baada ya mama yake kuondoka.
Angelina nae alikuwa kwenye maandalizi makubwa siku hiyo na alimchukua rafiki yake Manka amfanyie make up itakayomfanya apendeze zaidi ya wengine,
"Angelina sioni mtu wa kukushinda amini maneno yangu na baada ya masaa machache yajayo utakuja kuamini hichi ninachokwambia", Manka aliongea.
"Manka tafadhali acha maneno yako nakujua vizuri ukianza kuongea hapa utaifanya ata hii make up ukiyonipaka ifutike mana unajua kunipa plesha wewe", Angelina aliongea.
Walipokuwa wakiendelea kuongea huku Manka akimpamba rafiki yake mwanamama Beatrice alifika na kumsogelea binti yake,
"Mwanangu leo hakikisha unashinda na pia kuna jambo la mana nitakwambiwa siku ya leo", maneno ya mwanamama Beatrice yalimfanya mwanae Angelina amtazame mama yake nakumuuliza,
"Jambo gani hilo mama?"
"Sio wakati wake sasa ivi kukwambia nenda kwanza ukashinde kisha baada ya hapo nitakweleza kila kitu",Mwanamama Beatrice hakutaka kumwambia mwanae kwa wakati huo.
Angelina alikubali kishingo upande na kuendelea na maandalizi.
Usiku uliokuwa unasubiliwa kwa hamu uliweza kufika wanahabari walijazana kwenye ukimbi huo maarufu kwa ajili ya kuchukua habari na matukio mbalimbali,
Washiriki wote walikuwa wameshawasili sehemu ya tukio na kila mwanadada siku hiyo alipendeza isivyo kawaida,
"Mary unauhakika lakini umeweka mipango sawa isije kuwa unaniambia tu hapa kuwa lazima ushinde ukaja kushindwa",Faith aliongea.
"Acha ujinga yule tayali nimeshamvuluga akili yake tena unatakiwa unyamaze kabisa watu wasije kukusikia ukaharibu mipango yangu bure na hapa kuna waandishi wa habari wa kutosha sitaki uivuluge siku yangu Faith",
"Mmmmh haya sisi washindi wa pili ngoja tusogee", Faith aliongea.
Baada ya kuhakikishiwa na Mary kuwa atakuwa mshindi wa pili na yeye atakuwa mshindi wa kwanza alianza kusogea sehemu ya tukio husika.
Majaji zaidi ya watano walifika kwa ajili ya kuanza zoezi na mmoja wao akiwa ni mwanamama katalina akiwa na majaji wenzake.
Washiriki walisogea na zoezi lilianza lasimi.
Washiriki wenye namba za mwanzoni kila mmoja wao alianza kupita kwa kutembea kimadoido nakuongea kingeleza mbele ya umati uliokuwa pale na ilifika zamu ya mwanadada Mary ambae aliamini kabisa pale anaenda kutekeleza wajibu tu wa kufanya kama washiriki wenzake wanavyofanya ila hamna atakaye kuwa mshindi zaidi yake yeye, hii ilimpunguzia umakini na hakutembea vizuri kama wenzake walivyofanya na ata alipoanza kuongea bado aliongea ilimradi tu hali iliyofanya ata majaji waliokuwa wamekaa pale wengi wao hawakufurahisha na kile alichokifanya na ata rafiki yake Faith nae alijitahidi kwa kiasi chake akiamini ushindi ni wa kwao.
Zamu ya mwanadada Diana ilifika,
Mr.James alifurahi kumuona mwanae lakini alivyotazama majaji walipokuwa wamekaa alimuona mwanamama katalina hii ikazidi kumkasilisha zaidi.
Stewart nae alikuwa amekaa pamoja na wazazi wake walipomuona Diana wote walipiga makofi ishara ya kuwa wapo pamoja nae.
Diana alisogea mpaka kwenye stage nakuanza kutembea kimadoido na hii kuwafanya majaji wengi wafurahishwe na kile alichokifanya kwani alikuwa anajiamini sana ila ilikuwa tofauti kwa mwanamama katalina ambae yeye kwake hakuona maajabu yoyote Diana aliyoyaonyesha na ata Diana alivyoanza kuongea kiingeleza bado kilikuwa kimenyooka na kuzidi kuwafurahisha wote waliokuwa pale.
Majaji wengi walishika kalamu zao nakumpa marks za juu Diana karibu wote walimpa marks za juu.
"Mimi naona huyu ndiyo atakuwa mshindi wetu japo ni mzunguko wa kwanza tu ila sizani kama kuna mtu atakuja kumfikia",Jaji mmoja aliongea aliyekuwa amekaa karibu na mwanamama katalina aliyeyasikia yale maneno.
"Bado kuna washiriki wengine Mr na mizinguko bado ipo mingine kuna watakao fanya vizuri kuliko ata huyo aliyepita", Mwanamama katalina aliongea ili kusitisha mazungumzo yao kumuongelea Diana.
Na mda huo Diana alikuwa akiondoka huku watu wengi wakimpongeza, na washiriki wengine walipita mpaka pale ilipokuja kufika zamu ya mwanadada Angelina ambaye naye temu hii alikuwa tofauti kwani alijiamini isivyo kawaida.
Alivyotokeza mbele ya umati karibu kila mtu alishangaa kuona tabasamu la mwanadada Angelina na utembeaji wake uliokuwa wa kitofauti na hii kuwafanya watu wote ukumbini wakae kimya...ITAENDELEA.
Nani atakaye nyakua taji la Miss Tanzania karibu katika hatua inayofata.
NB: Story hii NIYAKUTUNGA na haina ukweli wowote ule unaoendana na taratibu za nchi yetu????????????????.
Pata Story hii mpaka mwisho kwa Tsh 1000 za k???????????????????????? lipia kupitia namba,
0613083801 HALOPESA,John Bugumba..