PENZI LA MHALIFU 14
Asikari wengi wa kike na baadhi ya wanawake waliokuwa wanakuja pale kwa ajili ya kuleta kesi zao, wengi wao walikuwa wameshafanya mapenzi na mkuu wetu na alikuwa akitumia cheo chake kwa ajili ya kuwazagamua.
Siku moja yakiwa ni majira ya usiku, nikiwa ndani nikiangalia tv pamoja na mfanyakazi wangu tulisikia sauti ya mwanamke nje akibisha hodi.
Mfanyakazi alienda kufungua na baadae aliingia binti mwenye miaka isiyopungua 27 akiwa kabeba mkoba mdogo begani kwake.
Binti huyo alinisalimia na baadae aliniuliza kama hapo ni nyumbani kwa Cyborg na mimi nilimjibu hajakosea kwani ndiyo kwake hivyo nilishangaa kumuona akikaa pasipo kukaribishwa.
"Ulikuwa na shida nae au sababu mimi ni mke wake!?" nilimuuliza lakini alinijibu kuwa anashida na Cyborg na angependa kuongea mbele ya Cyborg mwenyewe na sio mimi.
Nilishindwa kuelewa anashida gani na nilikuwa na hamu ya kujua kilichomleta hivyo wote tuliamua kumsubiri Cyborg.
Baada ya mda kupita Cyborg aliweza kufika nyumbani, naye alishangaa kumuona binti huyo ndani ya nyumba yetu.
"Sarah umeijia nini hapa!?" Cyborg alimuuliza na ndipo nilipomtambua kuwa anaitwa Sara.
"Nimeijia mahitaji ya mtoto, mda wote nahangaika kumlea mtoto mwenyewe alafu wewe unakula raha huku na mkeo" Sara aliongea na mimi nilishituka baada ya kusikia hivyo.
Cyborg alienda kumnyenyua Sara na kuanza kumvuta akimpeleka nje. kulikuwa na kila dalili za kumuumiza binti wa watu hivyo niliamua kumuwahi na kwenda kumzuia.
"Acha usimvute hivyo utamuumiza, pia unatakiwa uniambie huyu mwanamke anachokisema ni ukweli au uongo!?" nilimwambia Cyborg lakini hakutaka ata kusikia zaidi ya kuendelea kumpeleka nje Sara.
Alimfikisha nje na Cyborg alimwambia hataki kuiona sura yake nyumbani kwetu, hakuishia hapo kwani pia alimkataa mtoto na kusema sio wake amtafute baba halisi wa mtoto.
Sikutaka kuingilia mambo yao ila nilitaka wamalize mazungumzo yao na mimi nimuulize vizuri Cyborg aniambie juu ya habari hizo.
Baadae Sara aliondoka huku akilia na kudai lazima aende polisi kufungua kesi ya Cyborg kukataa kumhudumia mtoto.
Baada ya Sara kuondoka Cyborg alirudi ndani na mimi niliona ndiyo nafasi yangu ya kumuuliza vizuri.
"Naomba uniambie bira kunificha chochote kile Cyborg juu ya mwanamke aliyeondoka mda mfupi uliopita" nilimwambia na nilichokuwa nikisubiria ni jibu kutoka kwa Cyborg.
"Malaika siwezi kukudanganya, yule manzi kweli aliwahi kuwa demu wangu ila hakuwa wangu peke yangu alikuwa ni demu wa masela, yani kiufupi kila mvuta bangi kipindi hicho alikuwa akitembea nae, nashangaa anang'ang'ania nakusema mtoto ni wangu utafikiri alilala na mimi peke yangu!!" Cyborg aliongea.
"Una uhakika gani kuwa mtoto sio wako!? maana yeye ndiye anayefahamu baba wa mtoto ni nani!?"
Cyborg alicheka baada ya mimi kumuuliza vile nakunijibu "Yule alikuwa anaelewa show yangu na ata ujio wake hapa itakuwa ni kwa sababu ya kukumbuka penzi langu na sio mtoto"
Cyborg alinijibu na mimi nilifikiria kwa mda nakuona anachoongea ni cha kweli kwani ni ngumu kwa mwanamke yoyote yule kusahau penzi la Cyborg
Alikuwa na ufundi wa kipekee kitandani na kama angetembea na mwanamke aliyekuwa hamjui basi lazima angeamini Cyborg ni mcheza X.
Siku hiyo ilipita na ilipofika asubuhi nilipigiwa simu na kuambiwa niende na Cyborg kwenye kituo changu cha kazi huku ikisemekana kuna kesi inayomhusu ya kukataa kulea mtoto.
Nilimwambia Cyborg kuhusu taarifa ile na aliongea huku akiwa na hasira.
"Unaona mipango ya huyo mwanamke kwanini asingeenda kwenye kituo kingine cha polisi mpaka kaamua kwenda kwenye kituo unachofanyia wewe kazi!?, hii ni mipango yake na subiri ataona" Cyborg aliongea ila nilimwambia ni mambo madogo hayo na haina haja ya kuwa na hasira.
Tuliondoka kwa kuongozana pamoja mpaka kituoni na Mkuu alivyo na dharau baada ya kusikia kesi inamhusu mme wangu aliniambia nichukue maelezo mwenyewe kutoka kwake ya kumuuliza kwanini kakataa kulea mtoto.
Nilimuuliza ilimradi ili ionekana kama nafanya kazi, na Cyborg aliniambia tukapime DNA na kama mtoto atakuwa wake basi atakubali kumlea ila kama sio wake kamwe hawezi kumlea.
Makubaliano yaliwekwa kati ya Cyborg na Sara ya kwenda kupima DNA na baadae majibu yalionesha mtoto sio wa Cyborg.
Sara alibaki ni mwenye aibu kwa majibu yale na Cyborg aliamua kumwambia.
"Mimi nilijua tu umekumbuka show yangu ndiyo maana ukaamua kuja na mbinu hii, sasa ivi nimebadilika sio Cyborg yule wa zamani sababu nimeshaoa. sitaki kukuona ukijitokeza tena mbele yangu Sara" Cyborg alimwambia Sara nakunishika mkono kisha baada ya hapo tuliondoka huku tukimuacha Sara akituangalia.
Tukiwa njiani Cyborg aliamua kuniuliza.
"Umeamini kile nilichokuwa nakwambia Malaika!?"
"Kipi hicho mpenzi!?" ilibidi nimuulize.
"Kuhusu mtoto wa Sara kuwa sio mtoto wangu"
"Ndio mme wangu nimeamini" nilimjibu na tulijikuta tukikumbatiana bira kujali kama tupo barabarani.
Kiujmla ningekuwa kwenye wakati mgumu kama mtoto angekuwa ni wa Cyborg kwani nilitamani Cyborg asiwe na watoto wengine wa nje zaidi ya mtoto mmoja tuliyekuwa nae......ITAENDELEA.
Inapatikana kwa Tsh 1000 tu.
Namba za malipo.????
0613083801 HALOPESA Jina John Bugumba.
0755271203 M-pesa Jina John Bugumba..