Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  never give up harmonize

*MY FOREVER MAN 💘* *1-5* *__________________________________* *SEHEMU YA KWANZA*

26th Aug, 2025 Views 11



Ilikuwa majira ya saa moja jioni kamila alikuwa amekaa kwenye jumba lake la kifahari katika seble yake iliyopambwa na vitu vya thamani aliendelea na kazi zake za ofisini huku pembeni kukiwa na grass ya juice ya passion.
Akiwa anaendelea na kazi zake mara mlango Mkuu wa kuingilia ndani ulifunguliwa kwa nguvu akaingia mpenzi wake kijo.
Kijo alisimama mbele yake akawa anamuangalia huku akiyumba yumba.
" Inamaana hunioni mpenzi. Kijo aliuliza
Kamila alivua miwani yake ya macho akamuangalia vizuri alafu akasimama.
" Kijo umerudi tena ukiwa umelewa na unaweza kuniambia ulikuwa wapi kwa siku tatu?
Kijo alitoa tabasamu dogo lenye dharau.
" Yani wewe bwana hujui kabisa mahaba baada ya kunipokea kwa shangwe na furaha , unipetipeti unanipokea kwa maswali kwanza ushukuru nimerudi kama isingekuwa nimeishia na pesa nisingerudi hapa.
Sasa mpenzi naomba unipe laki tano hapo marafiki wananisubiri.
" Sikiliza kijo nimechoshwa na mambo yako najua huko uliko ulikuwa na wanawake zako sasa nasema hivi sina hela za kuchezea
" Kwahiyo hunipi au?
" Sina hela za mchezo.
" Wewe ni atm yangu huwezi kukosa hela.
" Basi atm yako leo imeishiwa hela.
" Siku hizi umekuwa jeuri sana lakini sawa tu nitajua nini cha kufanya .
Wakiwa wanaendelea kuzozana Abby gateman wa hiyo nyumba aliingia .
" Na huyu mfungua geti wako, mkaa getini ndio anakutia kiburi nina uhakika huyu mwanaume unalala nae.
Abby alisimama huku akiwa anashangaa anaingizwa vipi kwenye ugomvi wao?
" Madam mimi nimeleta hii karatasi kuna mtu kanipa pale getini.
" Naona na wanaume wa nje wanaanza kuleta vibarua wewe mwanamke malaya sana na mimi siwezi kuendelea kuwa na wewe. Na wewe gateman unaejifanya una kifua cha mazoezi unawavutia wanawake za watu siku nikikukamata nakuchinja.
" Kijo naomba uende ndani .
" Niende ndani saizi kwani mimi kuku? Au una mahamu yako unataka .... Kijo hakumaliza kuongea akaondoka huku Abby akimsindikiza kwa macho wakati huo kamila alikuwa anajisikia vibaya kwa kudhalilishwa .
" Madam mzigo wako huu.
Kamila alipokea ile karatasi.
" Samahani Abby kwa kile kilichotokea.
" Usijali ila pole.
" Asante. Abby alionekana kumuonea huruma kamila lakini hakuwa na msaada.

" Yani nina kila kitu, kazi nzuri, pesa, nyumba , magari lakini kitu kimoja tu nimekosea kupata mpenzi wa kweli. Nampenda sana kijo lakini siku zote amenifanya Chumio lake na suruhisho la matatizo yake hana mapenzi ya kweli kwangu yupo kwangu kwa sababu. Kamila aliongea kwa uchungu
" Pole madam ninaona unachopitia lakini ipo simu Mungu atakupa wa kuendana nae.
Kamila alitoa tabasamu dogo.
" Tatizo nampenda sana na sijui kama naweza ku move on.
" Basi unatakiwa kumuomba sana Mungu waweze kumbadilisha na awe kwenye mstari unaotaka wewe.
" Nahisi kukata tamaa juu yake .
" Kumbuka ni vibaya kukata tamaa na Mungu ndio kimbilio letu na suruhisho letu kwa kila kitu ,niombe sana akionyesha kipi bora kwako.
Abby alijaribu kumfariji kwa maneno baada ya hapo alirudi getini kuendelea na kazi zake.

Siku ya pili Mida ya saa mbili usiku kamila alipiga simu ya kijo ikawa haipokelewai. Alikaa na kufikiria sana badae aliamua kuchukua koti lake na kutoka nje.
Alipokuwa kwenye maeneo ya bustani alisikia sauti ya kike ukiongea kwa ukali.
" Unashangaa nini nimekuja kuchukua hela.
" Latifa mpenzi wangu hela sasa hivi nitapata wapi na unajua mwisho wa mwezi bado haujafika?
" Mimi sitaki kujua , hivi unajua kuwa mimi ni mwanamke mzuri sana?
" Ndio najua mpenzi wangu wewe ni mrembo.
"Basi kama unajua hilo ndio nahitaji huduma sitaki unifuje .
" Mbona najitahidi sana mpenzi wangu kukupa vi elfu kumi kumi...
" 😀😀😀 Ongea taratibu wewe watakucheka watu sasa elfu kumi si hela ya maandazi tu. Na nasema hivi kama huniwezi bora tuachane.....
" Usiseme hivyo mpenzi wangu .
" Basi ukitaka kuwa na mimi tafuta hela kijana kabla wenye nazo hawajapata nafasi na mwaka huu usipotimiza ninachotaka mimi na wewe byebye.
" Nionee huruma Latifa.
" Wakukuonea huruma ni mama yako mzazi mimi sicheki na wowote, eti nakosa hata hela ya kununulia chu* alafu nasema na mimi nina mpenzi.
" Basi nusu ya mshahara wangu nitakupa ukafanye mambo yako.
" Nipe hela ya nauli niondoke boda ananisubiri hapo nje.

Abby aliingiza mkono mfukoni akatoa noti ya shilingi elfu kumi akampa.
" Hii inatosha nini sasa?
" Si nauli .....
Latifa aliingiza mikono kwenye mifuko ya Suruali akachukua hela yote aliyokuwa nayo.
" Hizi una mbakishia nani?
" Hiyo ni hela yangu ya kula kesho, ukichukua mimi nitaanzia wapi kesho?
" Hizo sio shida zangu.
Latifa alichukua hela zote hakubakisha hata mia mbovu kisha akaondoka.

Kamila alitingisha kichwa.
" Nilijua ni mimi tu napitia haya kumbe tupo wengi huyu mwanamke hana tofauti na kijo.
Kamila aliingia ndani huku akiwaza haya mapenzi ni kitu gani mpaka yanaburuza watu kiasi kile.

Siku zilienda siku moja Mida ya saa kumi jioni akiwa chumbani kwake amesimama dirishani alimuona yule mwanamke wa Abby siku hiyo alikuwa na furaha walikumbatiana na Abby alionyesha upendo kwa yule mwanamke alikuwa akimtengeneza nywele.
" Leo ndio ile siku ya furaha kwako .
" Siku ya mshahara si ndio?
" Ndio yani unapenda pesa wewe.
" Hakuna asiyependa hela.
Abby waliingiza mkono mfukoni akatoa hela na kumpatia. Yule mwanamke alifurahi na kumbusu, Abby alitoa mfuko uliokuwa na zawadi akampatia furaha ilizidi kwa Latifa .

Mambo aliyokuwa anafanya Abby yalikuwa yanamvutia kamila alitamani mpenzi kwake kijo aweze kuwa kama yeye angalau awe na furaha nae ajione anaishi na mwanaume halisi na sio kivuli cha mwanaume.


MY FOREVER MAN 💘 2

Kamila kumtazama Abby na Latifa kupitia dirishani. Moyoni mwake alijawa na hisia tofauti wivu , mshangao na heshima aliyokuwa akionyesha Abby kwa Latifa.
“Yani mlinzi wangu anaweza kuwa na upendo hivi, hata kama hana mali lakini moyo wake ni safi Kijo angekuwa robo yake tu, ningekuwa na furaha isiyoelezeka.

Usiku ulipofika, Kamila alipokuwa anajiandaa kulala alipigiwa simu na rafiki wa kijo.
" Hallow
" Kamila kuna tatizo limetokea.
" Tatizo gani? Kijo kafanya nini tena huko?
" Kijo kugombana kampiga mtu chupa ya kichwa na kumuumiza vibaya maeneo ya kichwani
" Kwahiyo inakuwaje?
" Kakamatwa na polisi yupo kituo cha kati.
Kwakuwa ilikuwa muda umeenda kamila aliamua kulala kesho yake asubuhi aliwahi kituoni kwenda kujua kinachoendelea.

Alipofika kituoni aliongea na mkuu wa kituo na badae kijo akaachia lakini kwa sharti la kumtibu mgonjwa aliemjeruhi. Gharama zote za kumuhudumia mgonjwa ilikuwa ni juu ya kamila.

Wakiwa wanarudi nyumbani kamila alipigiwa simu na mama yake.
" Iko wapi?
" Nipo njiani naenda nyumbani.
" Naomba uje nyumbani haraka sana nina maongezi na wewe.
" Sawa.
Alipokataa simu alimgeukia kijo.
" Mama kaniita natakiwa kwenda nyumba.
" Kwahiyo.
" Na kushusha hapo mbele utachukua usafiri wa kukufikisha nyumbani.
" Kwanini usinifikishe kwanza nyumbani alafu wewe ndio uendelee na mambo yako.
" Haitawezekana.
" Kwahiyo huko ni bora kuliko mimi?
" Kumbuka alieniita ni mama yangu.
" Kwani mama kitu gani bwana.
Kamila hakujali maneno ya kijo alifika sehemu akasimamisha gari.
" Shuka.
" Nipe hela ya nauli.
Katika alitoa elfu kumi akampa.
" Usichelewe kurudi nyumbani leo nina hamu ya kuwa na wewe mpenzi wangu. Alisema kijo huku akishika kwenye gari.
Kamila aliwasha gari na kuelekea nyumbani kwa mama yake.
Alimkuta mama yake akimsubiri kwa hamu.
" Shikamoo mama.
" Marahaba. Mbona leo haujaenda kazini?
" Kijo mama...
" Huyo ujinga , mwanaume mpumbavu asiethamini uwanaume wake?
" Kapinga mtu akawekwa ndani.
" Nimesikia hizo habari ndio maana nikataka uje tuzungumze. Kamila mwanangu najua kila kitu unachopitia kwa huyo mwanaume mpuuzi, asije na kazi anachojua yeye ni kukunyonya tu, hakuna mapenzi ya kweli kati yenu na wala hawezi kubadilika . Kwanini usiachane ukafanya mambo yako mengine? Acha kuishi kimazoea huku ukijua moyoni atabadilika.
Kamila akimsikiliza mama yake kwa makini kisha akashusha pumzi
"Unachosema ni kweli mama lakini naomba unipe muda kwanza.
" Nakuonea huruma mwanangu.
" Najua mama ila nitalimaliza hili.

Baada ya kamila kumaliza kuongea na mama yake aliondoka alipofika nyumbani hakumkuta kijo alimuuliza Rehema dada wa kazi.
" Kijo yupo wapi?
" Alipokuja hakika sana akaondoka.
" Kweli sikio la kufa halisikii dawa.

Ilifika usiku Mida ya saa nne kijo alikuwa bado hajarudi.
Kamila alipanda kitandani kwaajili ya kulala lakini usingizi ulipotea alijigeuza pale kitandani huku mawazo yakimrudisha kwa Abby mara kwa mara. Sauti yake tulivu, maneno yake ya faraja, hata tabasamu lake lilikuwa linampa tumaini jipya.
aliamua kushuka kitandani na kwenda mpaka . Abby alipomuona alishtuka .
“Madam! mbona upo hapa muda huu kuna tatizo ?”
Kamila alitabasamu
“Hapana hakuna tatizo nimekosea usingizi Nimeona nitembee mpaka hapa.”
"Ni vizuri lakini huku nje kuna baridi.
" Bora huku kuliko kakaa mwenyewe nikiandamwa na msingi wa mawazo
"Pole kwa msongo wa mawazo.
Kamila alimuangalia
“Abby napenda kujua zaidi kama hautojali.

Abby alinyamaza kwa sekunde chache, akashusha pumzi.
“Madam… mimi ni mtu wa kawaida sana natoka kwenye familia ya kawaida sana ila nashukuru wazazi wangu walipambana kunipatia urithi wa elimu nimesoma mpaka chuo kikuu lakini changamoto ni ajira.
Kamila alishangaa.
" Wewe unanitania ama? Umesomea nini?
" Uchumi
" Khaaaa na uchumi wako umeukalia hapa getini kwangu?
" Ajira ni ngumu madam.
" Kesho utanipatia cv zako nitakufanyia kazi.
" Nitashukuru sana madam.
" Na kipi kingine ambacho sikufahamu kuhusu wewe abby?
Abby alitabasamu alafu akasema
"Sina cha maana ukilinganisha na maisha yako. Ila najua mwanamke anachohitaji siyo gari wala nyumba, bali ni mtu wa kumjali kwa moyo wote.”

Maneno hayo yalimgonga Kamila mpaka akajikuta machozi madogo yanamtiririka. Aliwahi kuyafuta haraka kabla Abby hajagundua.
Wakati huo huo, mlio wa honi ukasikika.
" Ni nani huyo muda huu? Kamila aliuliza na Abby alinyanyuka haraka akaenda kuchungulia .
" Ni boss kijo. Alijibu Abby kisha akafungua geti na
Gari jeusi liliingia kwa kasi na kusimama. Kijo alishuka akiwa na uso wa hasira na dalili zote za pombe.
Kijo alimwangalia Kamila
“Wewe ni mke wangu au ni mwanamke wa mlinzi wako?
" Kijo unanikosea adabu.
" Mwanamke wa mtu muda huu unashuka unakuja kufanya nini getini unajifanya mnong’onezana, mnatafuta nini hapa?”
“Kijo, unazidi kunichosha. Mimi nimeshuka tu kuja kuongea sina kosa. Naomba usinihukumu kwasababu ya kuficha makosa yako.
Kijo alimgeukia Abby “Na wewe chunga sana, usije ukaanza kufikiria mengine zaidi ya kufungua geti!”

Kijo aliondoka akaingia ndani huku akifunga mlango kwa nguvu. Kamila alimtazama Abby na kutabasamu kidogo.
“Usijali maneno yake, Watu kama yeye hawawezi kuelewa maana ya upendo.
“Nipo sawa, madam.”
" Uwe na usiku mwema.
" Nawe pia madam. Kamila aliondoka akaingia ndani huku Abby akiwa anamsindikiza kwa macho.
moyoni mwa Abby kulianza kuchomoza kitu ambacho hakuwahi kukihisi mvuto kwa Kamila, mwanamke ambaye kwa kawaida hakuthubutu hata kumwangalia mara ya pili.
" Sasa yani kuna watu wana bahati sana ila wanashindwa kuzitumia.
Kamila ni mwanamke mrembo sana na anajua maana ya mapenzi lakini kijo bure kabisa akili zake kama za kuku.


MY FOREVER MAN 💘 3

Abby alimuona kijo ni mwanaume mwenye bahati lakini alishindwa kuitumia vizuri nafasi yake.

Kamila alifika chumbani akamkuta kijo kajilaza kitandani akiwa na hajavua viatu.
Kamila hakumuongelesha alisogea aliinama na kumvua viatu taratibu , alimfungia vifungo vya shati ili amvue lakini kijo alimgeukia upande kama kwamba hataki.
'" sasa utalalaje hivyo na nguo?
" Ukichoona ni nguo tu yani wewe mwanamke umeshindwa kujiheshimu kabisa.
" Kivipi? Mbona unanihukumu kwa mambo ambayo sioni kosa alafu usijisahaulishe kuwa wewe ndio kwenye makosa hapa na unajaribu kuficha makosa yako.
" Achana na mimi nenda kaendelee kukaa na huyo gateman wako.
" Yamekuwa hayo, huna dogo.
" Sitaki ujinga. Na usiniongeleshe.
" Sawa.
Kamila alipanda kitandani akajifunika duvet lakini kijo aliendelea kulalamika .
" Unaniona fala ila ipo siku utajua umuhimu wangu yani wewe ni wakunisaliti na yule mlinzi? Hili nilishitukia mapema sana ndio maana tangia mwanzo sikutaka mfanyakazi wa kiume hapa ndani.
" Ulitaka wa kike ilipite nae maana mashine yako ukiona mwanamke haiwezi kujizuia kabisa.
" Alafu angalia kauli zako , Mbona Rehema yupo na sijawahi kumgusa.
" Mmmh najua kila kitu na Rehema ni mtu mwenye misimamo yake ndio maana umeshindwa.
" Sawa kama unataka kushindana na mwanaume, tutaona mwisho wake. Unafikiri kunipa hela na kila kitu ndio unaweza kunipangia kila kitu mimi bado ni mwanaume ninahitaji heshima yangu. Nahitaji kuheshimiwa kama kichwa cha familia ....
Kamila alipuuzia maneno yake akatafuta usingizi.

Asubuhi ilipokucha kijo aliamka alikuwa bado na hangover nzito. Alikaa kitandani akiwa anamuangalia kamila ambae bado alikuwa amelala alafu akashuka kitandani na kwenda
Kusimama kwenye dirisha la chumbani, macho yake moja kwa moja yalielekea getini ambapo Abby alikuwa anafanya mazoezi ya viungo alikuwa alinyanyua vyuma kama kawaida yake.
" Hicho ndio anachokijua kutunisha misuli ili amvutie na kuchukua wanawake wa watu. Ngoja nimtokee huko nje .

Kijo kutoka chumbani alipofika nje alimtazama Abby kwa jicho la chuki huku akavuta sigara kisha akatembea taratibu mwishowe alimkaribia.
“Ehee bwana mdogo… wewe ni nani hasa kwenye hii nyumba? Kijo aliuliza kwa sauti ya dharau huku akimuangalia usoni
“Ni mlinzi, bosi,” Abby alijibu kwa heshima.
“Mlinzi wa nyumba au mlinzi wa mke wangu? Kijo aliongea alafu akavuta sigara na kumpulizia moshi wa sigara uso kwa Abby.
Abby aligeukia pembeni kisha akashusha pumzi, akaendelea kusimama kwa utulivu.
“Bosi, naomba usiniseme vibaya kuhusu madam. Mimi nafanya kazi yangu ya kulinda mali zako na familia yako. Hakuna kingine zaidi ya hapo, swala la madam ni kwamba namuheshimu sana ....
Kijo akacheka kwa kejeli, kisha akamshika Abby kwenye kola ya shati.
“Usijifanye mtakatifu. Nimekuona jana usiku ukimnong’onezea maneno mwanamke wangu. Kwanza unapata wapi ujasiri wa kukaa na kucheka na mwanamke wa Boss wako? Unaonaje nikufundishe somo kidogo ujue kuwa hii nyumba mimi ndiye simba?
Abby alimuangalia huku moyoni akijisemea .
" Huna hadhi ya kuwa simba wewe ni fisi tu.
" Eti dogo umesahau mimi ni nani hapa ndani?
Kabla Abby hajanyanyuka mdomo wake kujibu Kamila alitokea ghafla, akiwa na hasira.
“Kijo! Acha mara moja kumshutumu Abby kama una hasira naomba uzimalizie kwangu tafadhali.
Kijo akamgeukia Kamila huku akishindwa kudhibiti hasira.
“Kwa nini unamkingia kifua mlinzi wako kila mara? Kweli Kamila? Yaani mwanaume wa hadhi kama mimi unataka kunichanganya na mtu wa getini ambae haeleweki mbele wala nyuma.
Kamila ni mara mia uwe na mwanaume alienishihda vigezo na mwenye muonekano mzuri nitakuwa na shaka sana nitajua kuna kitu umefuata ila sio huyu asiye na kitu ni kuishushia heshima.

Kamila alinyamaza kwa sekunde, kisha akasema kwa sauti yenye msisitizo:
“Kijo, tatizo sio Abby. Tatizo ni wewe na tabia zako. Abby hajakosea chochote ila wewe kila siku umekuwa mzigo kwangu.”
Yale Maneno yalimchoma Kijo kama msumari ndani ya moyo wake
Akamuachia Abby taratibu, lakini akatoa onyo kali:
“ Dogo Usijisahau hii nyumba huna uhuru nayo kiivyo wewe ni mlinzi tu, naweza kukufukuza muda wowote. Na wewe Kamila, usije ukajaribu kunichezea akili yangu wewe ni mali yangu, mali yangu pekee yangu.
Baada ya hapo kijo aliondoka , Abby alimwangalia Kamila kwa macho ya upole, akasema kwa sauti ndogo:
“Asante kwa kunitetea, madam.”
Kamila akamgeukia, akatabasamu kidogo lakini macho yake yalijaa hofu. Alihisi dhoruba kubwa inakuja na Kijo anaweza kufanya chochote.
" Usijali Abby siku zote nitakuwa mtetezi wako na usijali sana maneno ya kijo ni mtu wa hasira .
" Sawa lakini kwa upande mwingine ana haki ya kujionea wivu wewe ni mwanamke wake.
" Abby najua unajua mengi kuhusu mimi na kijo lakini kuna mengine hujui.
" Pole ila ndio mwanaume wako.
Kamila alitoa tabasamu dogo alafu akasema.
" Yeye sio moyo kusema niliacha na nao itakuwa mwisho wa maisha yangu. Ipo siku na muda usiojulikana nitaendelea na maisha yangu maana hata mimi natamani kitu kinachoitwa furaha na amani.
Abby nadhani tuna mambo mengi ya msingi ya kuongea mimi na wewe .
Abby alikuwa akimuangalia tu
" Acha niende ila wakati ukifika utaelewa ninachokiwaza akilini mwangu.
Safari hii kamila alitoa tabasamu mwanana lilileta nuru usoni mwake kisha akageuka na kutembea taratibu akirudi ndani.


MY FOREVER MAN 💘 4

.Kadri siku zilivyokuwa zinaenda kamila alijikuta anakuwa karibu sana na Abby . Usiku kijo akiwa hayupo kamila alitoka nje walikaa pamoja na kupiga story.

Siku moja Mida ya saa mbili usiku kamila alitoka ndani akiwa na vikombe viwili pamoja na chupa ya chai iliyojaa chai nzuri ya viungo.
" Kuna baridi sana nimeandaa chai nzuri tunywe pamoja .
" Ooooh kwanini ujisumbue madam
" Sio kujisumbua nimependa kufanya hivi.
" Unataka kijo akija anichinjie hapa getini kwako? Abby aliongea kama utani.
" Achana na kijo ni wivu wake tu unamsumbua.
Waliendelea kunywa chai huku Abby akiendelea kusifia chai kwa utamu .
" Madam umejifunza wapi kupika hii chai tamu?
" Mwalimu wangu ni mama yangu.
" 👌 Hongera ziende kwake.
Kamila alicheka
" Una utani wewe.
" Yani mimi ndio ningekuwa kijo nisingekuwa naenda kunywa pombe kinywaji changu ingekuwa ni hii chai.
Kamila alikuwa anacheka tu.
Mara kengele ya getini nililia , kijo aliweka kikombe chini kisha akaenda kufungua , hamadi akakutana na sura ya Latifa.
" Vipi mama mbona saizi tena bila taarifa?
" Mbona maswali nje ya geti kwani hapo ndani upo na nani?
" Yupo madam.
" Tusipoteze muda nimefuata hela ya matumizi mpenzi wangu.
" Latifa juzi tu nimekupa hela leo tena unataka?
" Kama ile uliyonipa imeisha mimi nifanye nini?
" Lakini unajua hali yangu mimi sina hela kwa sasa. Abby aliongea taratibu ili kamila asisikie.
" Yani wewe ni bure kabisa mwanaume gani unakosa hela yangu wenzangu wote wamepata wanaume mimi namilikiwa na kibwengo jamani najuta kukufahamu wewe kaka na kuanzia sasa mimi na wewe tusijuane yani sikutaki na sitaki hata kukuona.
" Latifa, Latifa..... Abby aliita lakini Latifa hakutaka kumsikiliza aliondoka huku akiendelea kuongea maneno ya kumkashifu. Kamila alinyanyuka na kumfuata abby pale alipokuwa kasimama akamshika begani.
" Kuna tatizo gani na huyo mwanamke wako?
" Acha tu madam ni mambo ya kawaida.
" Sio kweli, hebu njoo ukae tuongee.
Walirudi kukaa Abby akawa amejiinamia.
" Umasikini ndio sababu ya haya yote kama ningekuwa na pesa basi ningelikuwa na mwanamke ninaempenda.
" Usiseme hivyo Abby mapenzi sio kitu wa la pesa bali mapenzi ni ule upendo wa dhati kutoka moyoni na kuyakubali mapungufu ya mwenzio pamoja na kuelewana.
" Kwangu hayo yote hayapo.
" Wewe huna tofauti na mimi. Nadhani unajua kila kitu ninachopitia na kijo.
" Kwa nilipofika basi acha niweke mapenzi pembeni niwe yatima wa mapenzi naamini hakuna atajaenipenda nikiwa sina kit.......
Kabla Abby hajamaliza kuongea kamila alimziba mdomo Abby akageuka kumuangalia japo kulikuwa kuna Mwanga hafifu lakini waliweza kuonana , kila mmoja alimkazia macho mwenzie.
Kwa sauti ya chini kamila akasema
" Usiseme hivyo unajua kuna wengine tunatamani sana hiyo nafasi. Abby kuna muda natamani wewe ndio uwe unanimiliki.
Maneno ya kamila yalifanya Abby aduwae hakutegemea kusikia maneno mazito vile ya kutetemesha moyo wake kutoka kwa boss wake binti mrembo na tajiri.
Abby alikohowa kidogo na kumfanya kamila azinduke na kukaa sawa.
Walikaa kimnya kwa muda kila mtu akiangalia pembeni .
Baada ya muda kamila alinyanyuka .
" Naenda kupumzika uwe na usiku mwema.
" Nawe pia.
Kamila alipiga hatua mbili akasimama na kumgeukia Abby.
" Abby usiumize kichwa sana kwa kilichotokea huenda ikawa ndio heri yako.
Abby aliitikia kwa kichwa akiwa na maana kukubaliana na maneno ya kamila

Kamila alienda chumbani kwake akajirusha kitandani huku akionekana mwenye furaha. Alivuta mto na kuukumbatia kwa nguvu.
" Kuondoka kwa yule msichana mjinga huenda ikawa ni nafasi nzuri kwangu ya kuwa na Abby .
"Abby your my own. Nataka nikifanya uwe mwanaume wangu wa maisha. My man forever.


MY FOREVER MAN 💘 5

Kulipokucha asubuhi kabla kamila hajaenda kazini alimfuata Abby.
" Habari za asubuhi madam.
" Salama unaendeleaje?
" Nipo sawa madam.
" Jioni naweza kuziona CV zako?
" Bila shaka madam.
" Basi ziandae .
" Sawa.
Kamila alienda parking akapanda kwenye gari yake , aliendesha mpaka getini akasimama.
" Uwe na kazi njema Abby.
" Nawe madam uwe na kazi njema na Mungu alitangulia kwenye safari yako.
" Amina.
Kamila aliwasha gari akaondoka huku nyuma Abby alianza kuchambua matukio kuanzia jana usiku na yaliyotokea dakika chache zilizopita.
Alijikuta anatabasamu
" Baada ya kuvurugwa bahati malaika amekuja kuituliza moyo wangu na kunipa nguvu mpya . Mmmmh..... Sijui nini kinataka kutokea acha nikupe muda nione.

Baada ya Siku chache kupita kamila alipigiwa simu na kupokea habari kuhusu Kijo amejeruhiwa vibaya baada ya ugomvi mkali kutokea bar. Alidaiwa kumwaga meza za watu na kutupa glasi ovyo mpaka kundi la vijana likamvamia na kumpiga hadi akapoteza fahamu. Alilazwa hospitali kwa siku tatu.
Lakini Kamila hakwenda hospitali kumuangalia . alipokea simu kutoka marafiki wa Kijo wakitaka aende hospitali jibu lake lilikuwa
“Mimi nimeshachoka na vituko vyake. Hawezi kubadilika acha akae huko akitoka atajua jinsi ya kujiheshimu .

Siku Kijo alipotoka hospitali, alifika nyumbani akiwa amefungwa bandeji kichwani. Alimkuta Kamila sebuleni akiwa na laptop yake. Alienda kukaa kwenye kochi huku akiugulia maumivu, alimuangalia kamila lakini kamila hakuonesha kujali ujio wake.
“Kwa hiyo mwanamke hukujali ninachopitia hata kuja hospitali hapo kinafikia umeshindwa?
" Ukiona hivyo nimechoshwa na mambo yako kijo.
" Umenichoka si ndio?
"Yani ni zaidi ya kuchoka.
" Hiyo ndiyo heshima ninayostahili mimi?” Kijo alifoka.

Kamila akafunga laptop taratibu, akamtazama kwa macho ya hasira.
“Kijo nimevumilia vya kutosha. Ulevi wako, ugomvi wako, fedheha zako. Mimi si mama yako wa kukulea au kufuatilia maisha yako. Hii sio ndoa tulikuwa tunaishi tu, umekuwa mzigo kwangu Nimechoka!”
Kijo akabaki mdomo wazi.
“Una maanisha nini Kamila?”
“Na maanisha sikupendi tena, na siko tayari kuendelea kuishi maisha ya mateso na wewe. Nimekuchoka kabisa!” Kamila akainuka, akaenda chumbani huku akimwacha Kijo akipiga mayowe kwa hasira.
" Wewe piga kelele ukimaliza beba virago vyako uondoke hapa .
Kijo alinyanyuka kutoka nje.
" Fungua geti.
Abby alinyanyuka na kufungua geti dogo na kiko akatoka huku akiwa anavuta mguu wake

Usiku huo, kamila aliwa amejawa na maumivu moyoni, Kamila alifungua chupa za mvinyo akanywa sana mpaka macho yakawa mekundu. Akahisi pumzi nzito na upweke mkubwa. Akajikuta akitembea kuelekea getini.
“Abby… Abby!” aliita kwa sauti iliyokuwa ikitetemeka.
Abby alimfuata haraka
“Madam, kuna shida?”
Kamila akamshika mkono, akasema kwa sauti ya upole
“Naomba usiniite Madam sasa hivi niite Kamila.”
Alimvutia ndani wanapandisha mpaka chumbani kwa kamila .
" Kaa hapo.
" Kitandani?
" Hicho sio kitanda cha mkweo Abby kaa.
Abby alikaa kwa uwoga na kamila akakaa pembeni yake. Kamila alichukua grass yenye mvinyo akampa.
" Shika kunywa.
" Madam...
" Shhhhh...... Kamila alimzuia asiingie chochote kisha akapeleka grass ya mvinyo kinywani kwa Abby, Abby alifungua mdomo wake na kunywa kidogo baada ya hapo alichukua ile grass na kunywa mwenyewe taratibu.
" Madam ,kijo akinikuta hapa itakuwa balaa.
" Achana na kijo. Hapa ni mimi na wewe tu.
Waliangaliana Macho yao yalipokutana, kulikuwa na kitu ambacho kilijijenga kwenye akili zao. Abby alijaribu kujizuia, lakini Kamila alimkaribia zaidi.
“Abby… nimechoka kuumizwa. Nimechoka kuishi na mtu ambaye hajui nataka nini. Lakini wewe… wewe unafanya niamini bado kuna upendo,” Kamila alisema huku machozi yakimdondoka.
Abby alinyamaza sekunde chache, moyo wake ukidunda kwa kasi.
" Kamila....
" Abby.... Nahitaji faraja kutoka kwako tafadhali usinitupe nipe ninachokihitaji.
Hatimaye, Abby akamvuta taratibu na kumbusu Busu dogo likageuka hisia zisizoelezeka miili yao ilifukuta, hisia zilizofichwa kwa muda mrefu zikafichuka usiku huo walijikuta wakianguka taratibu kitandani na kuzama kwenye mahaba mazito ambayo hakuna hata mmoja wao alitarajia.

Full 1000
0784468229.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

*MY FOREVER MAN 💘* *1-5* *__________________________________* *SEHEMU YA KWANZA*  >>> https://gonga94.com/semajambo/my-forever-man-1-5-__________________________________-sehemu-ya-kwanza

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
profile
mjukuu 26 Aug 2025 22:06
*MY FOREVER MAN 💘*
*1-5*
never give up harmonize
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest