. Nilipokuwa mdogo, nilipenda sana kompyuta. Wakati watoto wengine wanacheza nje, mimi nilikuwa nikiandika programu kwenye kompyuta. Nilianza kujifunza lugha ya programu nikiwa na umri wa miaka 12 tu.
Nilipofika shule ya Sekondari, nilitengeneza programu ndogo ndogo kwa ajili ya burudani, baadhi zikiwa za muziki na michezo. Vipaji vyangu vilionekana wazi mapema, na wazazi wangu waliniunga mkono sana.
Mwaka 2002, niliingia katika Chuo Kikuu cha Harvard, ambako nilisomea sayansi ya kompyuta. Hapo ndipo ndoto kubwa ilianza. Niliona fursa ya kuunganisha wanafunzi wa vyuo kwa njia ya mtandao. Wazo likawa rahisi.
Tovuti ya kijamii ambayo watu wanaweza kuwasiliana, kushare picha, na kujifunza kuhusu wenzao.
Mnamo Februari 4, 2004, nilizindua Facebook iliyokuwa inaitwa awali TheFacebook nikiwa na rafiki zangu wa karibu Eduardo Saverin, Andrew McCollum, Dustin Moskovitz, na Chris Hughes. Tovuti ilianza ndani ya Harvard tu, lakini ndani ya muda mfupi ilienea kwa vyuo vingine kama Yale na Stanford.
Facebook ilikua haraka sana. Nikachukua uamuzi mgumu: kuacha masomo Harvard ili kuifanyia kazi kikamilifu. Nilihamia Palo Alto, California, na hapo ndipo ndoto ilianza kuwa biashara kubwa.
Leo hii, Facebook (sasa Meta) ni moja ya kampuni kubwa zaidi duniani, ikimiliki pia Instagram, WhatsApp, na Threads. Licha ya changamoto za faragha na ukosoaji mwingi, Facebook imeleta mapinduzi makubwa katika mawasiliano duniani.
.
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.
Maoni
Click here to login and comments