yalipotea na kuibwa, kuna vitu vingi navyo vilipotea, mpaka leo watu hawajui vipo wapi.
Wengine wakaingia kazini na kuvitafuta kwa kuhisi vipo huku na kule, wakapoteza muda, pesa lakini bado hawakuviona. Haya ni baadhi ya vitu vilivyopotea ambavyo kama kuna siku utaviona mahali, hakika utakuwa tajiri mkubwa sana.
Taji lenye utajiri wa dola milioni 6.
Hili lilikuwa la mfalme katika jumba la kifalme la Dublin. Liliibwa mwaka 1907 na mpaka leo hakuna anayejua lilipo. Je, liliuzwa? Liliharibiwa ama? Nobody knows.
Vitu mfano wa mayai vya nchini Urusi
Kabla ya mapinduzi nchini Urusi kulikuwa na vitu mfano wa mayai ambavyo vilitengenezwa kwa kutumia madini ya bei mbaya. Vilikuwa saba na vilitengenezwa mahususi kwa ajili ya nyumba ya mfalme. Vitu hivyo vina gharama ya dola milioni 230 lakini baada ya mapinduzi makubwa nchini humo, havikuonekana tena mpaka leo hii. Nani aliviiba? Alivipeleka wapi? Hakuna ajuaye.
Dhahabu na Almasi nyingi huko Virginia
Kulikuwa na kikabati kikubwa kilichokuwa kimehifadhiwa dhahabu na almasi ndani yake. Kilifungwa vizuri na mnyororo na ndani vitu hivyo vilikuwa na thamani ya dola milioni 60. Miaka ya 1800 vilizikwa huko Virginia lakini mpaka leo hii hakuna mtu anayejua mahali vilipozikiwa. Vimetafutwa mpaka leo hii sehemu hiyo imekuwa siri.
Dhahabu nyingi kupotea nchini Marekani
Marekani ilijikusanyia dhahabu zake nyingi sana, zilikuwa na thamani ya dola milioni 400. Zilihifadhiwa vizuri kabisa lakini baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kutokea mwaka 1861 chini ya rais Jefferson Davis, dhahabu hizo zikapotea na mpaka leo hakuna anayejua mahali zilipo. Wahuni walipita nazo baada ya vita kumalizika.
Meli ya dhahabu ikapotea baharini
Hiyo ilitokea mwaka 1511. Kulikuwa na meli ya Ureno iliyobeba dhahabu zenye thamani ya dola bilioni moja, ilipotea baharini na mzigo huo mkubwa na kwa bahati mbaya sana hakuna anayejua mahali ilipopotelea. Je, ilizama? Ilitekwa ama ilikuwaje? Nobody knows.
Meli ya almasi nayo ikasepa
Miaka ya 1600 napo meli ya Waingereza ikapotea baharini. Ilibeba almasi za Kihispania zenye thamani ya dola bilioni 1.25. Ilikuwa meli ya kifalme, ikapotea baharini ikiwa na mzigo huo mkubwa. Ilitafutwa kila kona, haikuonekana. Taarifa zilisema tu kulikuwa na wajanja waliamua kusepa nazo. Hapo ndipo ninapowakumbuka akina Jack Sparrow
Aztec treassure nayo ikasepeshwa
Yaap! Kulikuwa na dhahabu kubwa ya Montezuma Aztec ambayo ilikuwa na thamani ya dola bilioni 3, nayo iliwahiwa na wana, meli ikapotea na dhahabu hiyo haikuonekana tena mpaka leo.
Mji wenye dhahabu nayo umepotea
Kulikuwa na mji uitwao Paititi ambao ulikuwa na dhahabu nyingi sana mpaka kuitwa mji wa dhahabu. Inakadiriwa kuwa na dhahabu zenye thamani ya dola bilioni 10 ila cha ajabu mpaka leo hakuna ajuaye huo mji ulikuwa wapi. Umejaa dhahabu ila nao umepotea. Wanahistoria waliingia chimbo na kuutafuta kila kona wakaambulia patupu.
Wahispania nao walilia sana
Wakati mapigano yanaendelea mwaka 1708, Whispania walikuwa na meli yao iliyokuwa na dhahabu nyingi sana zenye thamani ya dola bilioni 20, meli ilizamishwa huko pwani ya Colombia na mpaka leo dhahabu hizo hazijaonekana tenaaaaa.
Wajapan nao hawakuachwa na kisanga hiki
Wakati wa mtawala wa Japan aitwaye Yamashita, aliamua kukusanya dhahabu nyingi sana mpaka kufikia za dola bilioni 400. Baada ya dita kutokea, jeshi lake likaamua kuzichukua dhahabu hizo na kwenda kuzificha huko karibu na Ufilipino na mpaka leo hakuna anayejua mahali dhahabu hizo zilipofichwa. Zimetafutwa, hazijaonekana..
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.
Maoni
Click here to login and comments