Ibrahim tulilelewa na mama tu baada ya baba yetu mzazi kufariki kipindi nipo na miaka saba hapo mama yangu ndio ana ujauzito wa Ibrahim...
Baba yangu alikuwa anafanya kazi huko machimbo chunya ila ni mzaliwa wa Dar es salaam, maisha yetu yalikuwa mazuri na yenye furaha nilikuwa nasoma shule ya kulipia nitake nini lazima nipewe kipnzi cha baba
maisha yetu yalikuja kuharibika baada ya kifo cha baba kwani baada ya msiba kuisha ndugu zake baba walichukua kila kitu wakagawana wenyewe
vingine wakauza hawakumpa mama hata shilingi mia mbovu hadi mama akapata tatizo la moyo kwa ajili ya mawazo🥹🥹.
Lilibaki shamba tu ambalo lilikuwa huko chunya na hapo walikuwa hawalijui mbona wangeshaliuza hawa ndugu waliokosa haya ndipo mama akaamua turudi tu huko chunya tuishi pale huku akifanya vibarua ili tule na kusoma mimi na mdogo wangu.......
Nilijitahidi kusoma hivyo hiyo kwa shida hadi nilivyofika kidato cha nne. Matokeo yalitoka nimefaulu ila nikashindwa kuendelea na masomo ikabidi nimsaidie mama kufanya vibarua, na kulima ili maisha yaende huku mdogo wangu akiendelea na masomo yake.
Sikutaka ndoto zake na yeye zikatike kama zilivyokatika ndoto zangu za kuendelea na shule ...
Siku hiyo mama alikuwa ameenda kufanya kibarua kwenye shamba la mtu kuvuna ghafla tu alianguka akiwa shambani🥹🥹
Walimchukua na kumkimbiza hospitali nililetewa taarifa muda huo nilikuwa napika niliacha kila kitu nikaelekea hospitali kumuona. Hali ya mama yangu haikuwa nzuri ila alikuwa amepata
nafuu kidogo
nilimkuta ameamka amekaa kitndani
anakunywa uji aliopewa na mgonjwa wa kitanda cha pili....
Nilivyomuona nilitamani kulia ila nikawa najikaza tu kumtia moyo mgonjwa....
Dr aliniita akaniuliza kama kuna mtu mzima ili aongee nae kuhusu hali ya mama yangu...
Mimi ndio mkubwa Dr anenifuatia yupo darasa la tano unaweza tu kunipatia
hayo majibu ...
Sawa hamna shida mama yako vipimo vinaonyesha ana tatizo la moyo ..... una tundu inabidi haraka sana apatiwe matibabu la sivyo utampoteza mama yako maana ili tatizo linaonekana ni la muda mrefu kweli .....
SEHEMU YA 02
Nilihisi kuchoka na majibu aliyonipatia Dr. Niliitikia tu sawa nitafanya hivyo hapo sijui hata hela natoa wapi
...ndugu wenyewe ndio walituacha tangu baba alivyofariki..
Kesho yake mama aliruhusiwa tukarudi nyumbani majibu yake nilimficha sikumwabia kabisa..
Mama aliniita nikaenda kumsikiliza anasema nini?
Leen, binti yangu wewe ndio mkubwa hapa nakutegemea kwa kila kitu, hali yangu yenyewe si unaiona lakini.....?
Ndio mama hauko sawa Basi naomba upambane kama mama sasa hivi , sidhani kama naweza kwenda kibaruani kufanya kazi kwa sasa tunahitaji chakula na mambo mengine...
Mama sio kula tu hadi matibabu yako inabidi utibiwe ili upone......nikaishia hapo hapo sikutaka kuendelea.
Mama alifungua kitenge akatoa elfu ishirini akanipatia..... mama hela ya nini hii ? Nilimuuliza
Hela hiyo nakupa ufanyie biashara nakutegemea sana.
Sawa mama niliitikia tu ila sikujua nifanye biashara gani na mimi sio mzoefu na biashara..
Nilitoka nje nikaenda kumpikia mama uji .....
Kesho yake asubuhi nilihakikisha nimemuandalia mama chakula na mdogo wangu ameenda shule ,
niliondoka nikaenda mashambani huko kulangua nyanya kwa bei ya jumla nikapanga kwenye sado nikapanga pembezoni mwa barabara.
Nikaanza kuuza Biashara ilienda vizuri vyote vikauzika ....
Nikawahi kurudi nyumbani
nilikuta mdogo wangu amesharudi kapika hadi chakula tulikula nikapumzika nikiwaza siku ya kesho.....
Faida niliyouza niliweka pembeni kesho yake asubuhi sana niliamka nikamuandalia mama uji nikampelekea chumbani kwake....
Nilimsalimia nikamwambia ajitahidi anywe huo uji pamoja na dawa kisha nikamuaga...
Sawa nakuombea heri siku ya leo ufanikiwe....
Asante mama yangu kwa dua yako nilimjibu kisha
nikaondoka....
nikaenda kulangua nyanya nikaenda kuuza barabarani kama kawaida...
Nikiwa nimekaa sina hili wala lile lilipita gari ndogo likaenda kusimama mbele kidogo kama kawaida wafanyabiashara tukiona gari tunakimbilia kutafuta riziki ...
nilivyoona watu wameenda wengi niliamua nibaki na vile nilikuwa na uoga wa biashara ...
Mwenye gari alisema haitaji kitu watu wakarudi kukaa mara akashuka dereva aliyevaa suti nyeusi akanifuata hadi nilipokaa...
Binti unaitwa pale kwenye gari na mzee...... nikamuuliza mimi?Akaniambia ndio wewe unaitwa ..
Nilishangaa nani tena huyo anayeniita nisije kuchunwa tu ngozi mzee tena mzee nani huyo ? ...
Nilisimama nikaongozana na yule kaka hadi kwenye gari nikasimama kwa njee kioo kikashushwa ..
Nikamuona mzee wa makamo mweupe kama muarabu akaniita jina langu Leen hujambo...?1
Itaendelea.......
Full 1000
Whatsapp 0742133100
MMMMMMMH UNIFANYE TARATIBU MM NI YATIMA❤️🔥
SEHEMU YA 03
Nilishtuka kajuaje jina langu hata simfahamu huyu mzee sijawahi kumuona hata siku moja ....ikabidi tu nijikaze kuitikia nisije kuitwa na majini ...
Sijambo shikamoo mzee nilimsalimia huku nikiwa na maswali ni nani huyu...
Marahaba yaani umekua sana binti vipi mama yako ajambo..?
Hajambo wewe ni nani baba yangu mbona sikufahamu? Nilimuuliza huku nikimtazama kwa umakini...
Huwezi kunifahamu ila mimi nakufahamu vizuri sana wewe si mtoto wa Salim ..? Alimtaja baba yangu mzazi aliyefariki kitambo sana....
Ndio mimi ni mtoto wa Salim... Dah Salim alikua rafiki yangu sana tulifanya kazi wote machimbo kipindi hicho nimeshangaa kukuona hapa kweli milima haikutani binaadamu hukutana kwahiyo unauza nini?.
Niko nauza nyanya mzee wangu nilimjibu.
Sawa we Jamal yule mzee
alimuita dereva wake kamuungishe binti yangu vitu vyote vilete hapa kesho nitakuja kumsalimia mama yako kama nikipata nafasi naomba namba yako tafadhali....
nimekuja huku kununua mashamba nataka nilime. Nilimtajia yule mzee namba ya yangu akaisevu kisha akanipigia...
Namba yangu hiyo isevu Mr
Abdul Khalil niliitikia sawa
aliingiza mkono mfukoni akatoa wallet yake akatoa elfu hamsini akanipa.
Nilimshukuru hadi nikapiga magoti tuliagana na yule mzee akaondoka...
Wenzangu walishangaa
wakaniuliza kama najuana na yule mzee . … Ndio alikua rafiki yake na baba zamani niliwajibu nikarudi nyumbani haraka huku nikiwa na furaha..
Nilimkuta mama amekaa nje kwenye mkeka nilimsalimia mama kisha na mimi nikakaa pembeni yake.
Mbona kama una furaha binti yangu? Mama aliniuliza
Umejuaje mama kama na furaha nilimuuliza mama.
Nakujua tu wewe si ni mwanangu nakujua ukiwa na furaha hadi ukiwa na huzuni...
Nimekutana na Mr Abdul Khalil mama vipi unamfahamu huyu mzee?
Mama alishtuka kwa mshangao unasema nani ?
Mr Abdul rafiki yake na baba kajitambulisha kwangu hivyo pia kanunua vitu kwangu kanipa na hii hela elfu hamsini nikuletee....
Mwanangu huyu mbaba
namfahamu sana alikua ni
rafiki wa baba yako pika pakua alivyofariki baba yako alinipaga namba yake nimtafute baada ya mazishi kupita ila namba yake ilipotea hapo ndipo tulipoteza mawasiliano....
SEHEMU YA 04
mimi na yeye ni miaka mingi imepita kumi na tano sasa
jamani
Amekujuaje na alikuacha mdogo sana una miaka minne tu akaondoka na familia yake kuishi Dar kweli ana
kumbukumbu sana ...
Sijui mama ila ndio hivyo pia kasema kesho kama akipata nafasi atakuja akusalimie.
Yaani bora aje tu kwa kweli yule baba hanaga roho mbaya kabisa hata mkewe atatusaidia kwa kweli. ...
Nilimpa mama ile hela akae nayo mimi nikaenda kuendelea na shughuli zingine kesho yake asubuhi kweli Mr
Abdul alipiga simu
nikamuelekeza akaja hadi
nyumbani nikamuacha na mama mimi nikaenda kwenye biashara yangu... Sijui waliongea kitu gani jioni nilirudi nyumbani nilimkuta mama amejikokota anapika chakula cha mchana.
Nilimsalimia nikapeleka vitu ndani nikaja kukaa nje..
Mwanangu huu mwaka ni wa
bahati sana nahisi ni
Mungu ameamua kutusaidia kwa njia yake.. mama aliongea.
Kwanini mama unasema hivyo?
Nilimuuliza huku nikikaa vizuri niisikie hiyo bahati.
Mr Abdul kasema
atanikarabatia hii nyumba pili hataki ukaribu wetu upotee anataka kuendeleza undugu ili kumuenzi rafiki yake Salim..
Sijakuelewa mama kuendeleza undugu kivipi? Namaanisha anataka mtoto wake wa kiume akuoe Wewe...
Enhe mama inawezekana vipi ina maana kusoma tena mimi ndio sisomi na mtu mwenyewe anayetaka kunioa simfahamu vipi akiwa hana vigezo navyotaka mimi?
Niliuliza
Vigezo gani unavyotaka wewe kama hela wanayo, Leen au unataka mwanaume mzuri kimuonekano mbona yule mzee ana watoto wazuri tu japo nimewasahau ....
Mama mshanikera tayari wewe na huyo Mr nani sijui mnafanya maamuzi bila kutushirikisha wahusika sijui mnataka nini kwa kweli?
Nililalamika kiukweli
Hebu fikiria Leen umeolewa kwenye familia kama ile wana pesa tutakuwa na shida gani hapa hata mpango wako wa kusoma utatimia tu ....
Dah nipe muda basi nijifikirie mama yangu imekuwa ghafla sana....
Basi fanya haraka huko kufikiria unipe jibu kesho anarudi dar uende naye ili mkapate muda wa kujuana na mwenzio ndoa ipite ... Sawa ..... niliinuka nikaingia ndani huku nikiwa nimenuna
SEHEMU YA 05
Nilikaa chumbani nikawa najifikiria maisha tunayoishi, hali ya mama yangu na huo ugonjwa wake nikajikuta tu nimefanya maamuzi ya kukubali kwenda kuolewa tu huko dar na mwanaume ambaye simjui hata kwa sura ......
Nilitoka nje nikamwambia mama kuwa nimekubali kwenda kuolewa huko dar ....
Mama alifurahi baada ya kumwambia kuwa nimekubali kuolewa akampigia simu Mr Abdul akamwambia kuwa nimekubali akamwambia mama aniambie kesho nijiandae basi tuende dar wote..
Basi kesho nilijiandaa nikatia nguo zangu kwenye shangazi kaja langu nikawa namsubiri Mr Abdul aje kweli bhana walikuja mida ya jioni kunichukua nilimuaga mama kishingo upande sikutamani kumuacha jinsi hali yake ilivyo na maisha yake ila ngoja tu
nijikaze niende tu nilijipa moyo tukaondoka kwenda Dar na
MrAbdul Khalil..
Tulisafiri usiku kucha asubuhi tulifika dar mida ya saa mbili... tukaelekea huko Goba tulifika kwenye bonge la jumba geti lilifunguliwa tukaingia ndani..
Tulishuka kwenye gari Mr Abdul akawaita
wafanyakazi walikuwa wawili...
Mgeni huyu hapa naombeni mumpokee vizuri hadi
atakaporudi zayn mimi
nitakuja kesho naenda nyumbani kwangu..
Wakaitikia sawa baba Mr
Abdul alinigeukia na kuniita jina langu.
Leen jisikie upo nyumbani usiogope msubiri mwenzio
atarudi baadae toka kazini nishampa taarifa za ujio wako mimi naenda nyumbani sikai hapa siku nyingine utakuja nyumbani kwangu ili upajue.
Sawa baba nashukuru nilimjibu....
Mr Abdul aliingia kwenye gari lake akaondoka.
Niliwasili kwenye jumba la kitajiri ili nionane na mtoto wa huyo mzee tujuane kwanza kabla ya kuoana.
Dada twende ndani
mfanyakazi mmoja huyu aliongea
alikuwa anaitwa Aisha..
tulikuwa tunalingana kidogo..
Vipi ushakunywa chai?
Aliniuliza nikamjibu hapana sijanywa bado.
Basi sawa nifuate nikuonyeshe chumba uweke begi lako .... nilimfuata hadi kwenye hicho chumba ... hiki ni chumba chako ingia ubadilishe nguo .
ngoja nikakuandalie chai mimi naitwa Aisha.
Asante sana Aisha naitwa
Leen..
Nilingia chumbani nikaenda kuoga nikavaa nguo zingine nikatoka sebuleni kunywa chai.
JE NINI KITAENDELEAA.
Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.
Maoni