Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

*VERY HANDSOME* *🌸Lover boy💓💓 *_________________________________* *SEHEMU YA 06*

27th Aug, 2025 Views 26



Enhe kumbe mimi sijui ndio nasikia leo nilimjibu
Ndio hata mimi nina kazi yangu napokea mshahara nimekuja kujiendeleza tu nilisoma mwisho diploma...
Ohoo basi ndio maana una akili sana nilimjibu
Kawaida tu mbona hata wewe unazo mara mvua ikakata nilimuaga Gerson nikawa nafungua mlango ila nikashindwa..
Ngoja nikusaidie kufungua alisogea akapitisha mkono ili afungue mlango tukajikuta tunagusana...
Nilihema kwa kasi hadi mapigo ya moyo 💓 wangu Gerson akasikia.
Alifungua mlango wa gari 🚗 kisha akatabasamu 😁 kuna mtu unampenda? Aliniuliza
Hapana simpendi mtu yoyote kwanini umeniuliza hivyo ?
Kwa sababu macho na moyo 💓 wako vinaongea na ninasikia.... Gerson aliongea
Umejuaje? Niliuliza
Najua tu kwasababu nimesomea na saikolojia kwahiyo naelewa...
😂😂 Upo vizuri hongera sana nilimjibu huku nacheka..
Asante 🙏 ila ni vizuri ukamwambia huyo unayempenda ukweli kabla hajaambiwa na wengine....
Nilishusha pumzi kisha nikamuangalia usoni Gerson....
Unadhani ni rahisi kumwambia mtu nakupenda Gerson 🤔 ....
Yah chelewachelewa utakuta mwana sio wako.
Sawa nashukuru kwa kunileta nyumbani.
Usijali ila usimwambie mtu kama nina gari au nimekuleta nyumbani.
Sawa....
Nilishuka kwenye gari nilimuangalia anavyogeuza hadi gari likapotea ndipo na mimi nikaingia ndani..
Nilienda chumbani nikajitupa kitandani akili yangu ikawa inamuwaza sana Gerson nikajikuta nampenda sana kiasi kwamba akisimama na mtu au kuongea moyo 💓 wangu unaenda kasi kisha nachukia sana..
Moyo wangu tulia naomba usipende tafadhali huyu kaka atakuja anitese kwa kweli...
Moyo koma hivi vitu vina wenyewe nilipitiwa na usingizi hadi wenzangu waliporudi nyumbani..

We nawe hebu amka unalala kwani unaumwa mbona umeondoka chuo mapema vipi unaumwa? Penina aliniuliza.
Ndio nilibanwa na tumbo la kuhara we nikaona cha kufia nini ngoja nitimkee
Pole haya pumzika maana tumeshangaa ghafla tu umeondoka kwenye discussion ...
Asante 🙏 niliwadanganya nikaendelea kulala kumbe wivu tu unanisumbua tena kwa mtu ambae hata sijawahi wala hajawahi kunitamkia neno nakupenda...
Usiku usingizi ulikata nikaamka nikakaa sebuleni nikawa naangalia tv huku nasoma meseji ikaingia kwenye simu yangu..
Vipi unaendeleaje na tumbo by Gerson maana sikuwa na namba yake..
Naendelea vizuri kidogo nashukuru.
Sawa basi kesho nitakuja nikuone katibu wangu....
😁😁 Usijali hadi kesho nitakuwa sawa nahisi nitakuja chuo..
Sawa nikutakie usiku 🌃 mwema.
Na kwako pia nilifurahi baada ya kuchati na HB wa darasa...


Kesho yake asubuhi niliamka mapema nikaelekea chuoni nikawaacha wenzangu wanajiandaa.
Nilifika mapema nikamkuta Gerson yupo darasani amekaa na laptop 💻 yake yupo bize..
Nilimsogelea nikamsalimia sasa hivi nilikua nishamzoea..
Hivi unalalaga hapa hapa chuo au ?. Nilimuuliza kwanini umeniuliza hivyo
Maana nashangaa umewahi ghafla nielekeze basi maswali mliyojadiliana jana...
Itaendelea
.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

*VERY HANDSOME* *🌸Lover boy💓💓 *_________________________________* *SEHEMU YA 06*  >>> https://gonga94.com/semajambo/very-handsome-lover-boy-_________________________________-sehemu-ya-06

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Kama wewe hujatimiza miaka 18+ usije nasema usije kabisa ni wakubwa tu
Kama wewe hujatimiza miaka 18+ usije nasema usije kabisa ni wakubwa tu

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest