Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

*TABIA ZA MKE WANGU ZILIVYONIFANYA NITEMBEE NA HOUSEGIRL*❤️ *SEHEMU YA 01----05*

28th Aug, 2025 Views 33



Kulikucha mapema asubuhi, kama kawaida ya nyumba nyingine ambapo mke humuandalia mumewe mambo ya nyumbani kama maji ya kuoga, chai na nguo za kuvaa pindi anapotaka kwenda kazini lakini siyo kwa mke wangu Joanitha ambae si kwamba alikuwa hajaamka, alishaamka mapema asubuhi lakini alikuwa bize na simu yake janja (smartphone) kubwa ambayo nilimnunulia mimi mwenyewe kwa pesa yangu, akibofya bofya tangu saa kumi na moja alfajiri mpaka sasa saa kumi na mbili na dakika kadhaa, nikajinyoosha nyoosha huku nikimtazama

"Za asubuhi?" nilimsalimia
"Safi" ndilo jawabu alilonipa, la mkato tu huku akiendelea kutazama simu yake aliyoigeuzia upande mwingine tena akitabasamu, nikasogeza uso wangu kutaka kutazama kinachomfanya atabasamu huenda na mimi nikapata tabasamu kama lake asubuhi asubuhi lakini akaiwahi simu yake na kuificha nisiione

"Vipi siruhusiwi na mimi kutabasamu asubuhi mke wangu?"
"Wala vya kawaida tu"
"Oky" nilitikisa kichwa na kuinuka kitandani nikashuka nikiwa kifua wazi na kwenda moja kwa moja kuchukua mswaki wangu na kikombe cha maji ili nielekee bafuni nikajiandae

"Kaka nakusalimia, habari ya asubuhi" nilisalimiwa na dada wa kazi aitwae Debora ambae kumbe alinisalimia mara kadhaa na sikumuitikia kwa sababu mawazo yangu yalikuwa mbali

"Oooh Debora, salama vipi za kwako?"
"Salama kaka kwani upo sawa?" aliniuliza dada huyo ambae tulimleta kwa ajili ya kumsaidia mke wangu ambae ana mtoto wa miaka mitatu, amsaidie kazi za hapa na pale na hilo likiwa ni wazo la mke wangu mwenyewe

"Nipo sawa Debora, nipo sawa kabisa"
"Mh mbona nimekusalimia mara tatu hujaniitikia, unaonekana ulikuwa unawaza mbali kweli?"
"Kawaida, si unajua asubuhi akili yote inakuwa kwenye kazi"
"Kweli kaka"
"Haya majukumu mema, mimi naenda kuoga niondoke"
"Nimekuandalia maji ya kuoga kaka"
"Maji ya kuoga?"
"Eeh?"
"Debora, kwanini unajisumbua namna hiyo?"

"Nimeona unapata shida kujiandalia mwenyewe kila siku" aliongea mwanadada huyo ambae huvaa magauni makubwa, mapana na marefu kutokana na sheria aliyopewa na mke wangu, hasa kutokana na maumbile yake kubwa

"Jamani asante"
"Haya nipo jikoni nakutengenezea chai unywe"
"Hapana usijipe shida Debora"
"Mimi nakuonea huruma kaka Eddy kwa jinsi unavyopata shida asubuhi kuandaa maji ya kuoga, chai na....."

"Na nini, hebu malizia" tukamsikia mke wangu ambae alisimama kwenye mlango wa chumbani akituangalia, kumbe alikuwa anatusikiliza......

*SEHEMU YA 02*❤️

"Si nakuuliza wewe Debora, unapata shida unapoona mume wangu anahangaika maji ya kuoga, chai na nini, rudia?"

"Shikamoo dada" dada huyo wa kazi (housegirl) kabila msukuma alimsalimia kwa kupiga goti la kuchuchumaa
"Sihitaji shikamoo yako, nataka jibu"
"Hamna dada nilikuwa tu nina...."

"Shenzi kabisa wewe unashindwa kufanya majukumu yako unang'ang'ana kuwasemesha waume za watu" alimshika sikio akimvuta kwa nguvu

"Dada sikio linauma"

"Mke wangu, mambo gani hayo unayofanya, unamuumiza" ilibidi nimtetee msichana huyo wa miaka ishirini lakini mwenye mwili mkubwa kama unavyojua wasukuma walivyojaaliwa miili huwezi kumdhania kama ana miaka ishirini tu mpaka akwambie na uthibitishe mwenyewe

"Toka hapa, kuna kazi ya kuosha vyombo kule jikoni umekaa unasimama simama hapa?" alimkaripia akimpiga kibao cha mgongoni, Debora akaondoka mbio mbio akilishika gauni lake refu lililokuwa linamfanya akimbie kwa tabu kwa sababu lilitaka kumuangusha, huku nyama za mwili wake hasa makalio makubwa yakitikisika tikisika, nikamwona mke wangu akimtazama kwa hasira huku akisonya

"Mambo gani sasa hayo unayofanya mama?"
"Nawewe usinitibue umenisikia, mnasimamishana hapa mnaongeleshana nini?"
"Alikuwa ananisalimia tu sasa ningefanyaje, au vibaya kusalimiana na kujuliana hali?"
"Tena nitamuhamisha na kumleta housegirl mwingine"
"Kakukosea nini dada wa watu kwani?"
"Utajua hujui" alinijibu na kusonya akaondoka akiniacha nimesimama huku nimejishika kiuno nikimshangaa tu

"Hivi huyu mwanamke siku hizi ana nini?" nilijiuliza mwenyewe na kutikisa kichwa tu kusikitika, kisha nikaelekea chumbani kwa mtoto wetu wa kiume aitwae Erick na kumchungulia akiwa bado amelala kitandani kwake lakini alilala vibaya shuka alilitupa pembeni nikamfuata na kumfunika vizuri kisha nikaelekea bafuni kwa ajili ya kuoga nikakuta kweli kuna maji ya kuoga yameshatengwa na dada wa kazi (housegirl) Debora, tena ya moto kidogo, nikayaoga na kurejea chumbani nikimkuta mwanadada huyo jikoni anaosha vyombo huku akiimba nyimbo za kwao za kisukuma, nikamtazama kwa sekunde kadhaa akiwa bado hajaniona ndipo akageuka

"Ooh kaka Edmund"
"Debora"
"Ndo tunaosha osha vyombo hapa"
"Oooh vizuri, asante kwa kunitengea maji ya kuoga"
"Usijali kaka" alijibu huku akitabasamu nami nikatabasamu na kuendelea na safari yangu kuelekea chumbani na ndipo nikamsikia mke wangu akiwa anazungumza na simu nje na siyo ndani na ndipo nikaamua kwenda mlangoni kumtazama

"Jamani baba mchungaji amina" aliongea kwa kudeka na aliponiona akakata simu, ikionekana alikuwa bado hajamaliza maongezi
"Aaamh nilikuwa naulizia pafyumu yangu umeihamisha pale?" nilizuga
"Pafyumu yako si iliisha"
"Oky"
"Halafu nitasafiri kesho"
"Wapi tena?"
"Kuna huduma tunaenda kuifanya Mbeya kwa siku tatu na mchungaji, kuna mkutano wa Injili tumealikwa, yeye atahubiri na mimi kama muimbaji wa nyimbo za injili"
"Joanitha mke wangu mbona safari nyingi siku hizi, juzi tu umerudi kutoka Arusha kihuduma, leo tena?"
"Sasa mi nifanyaje wakati ni muimbaji wa nyimbo za injili na ndo kazi yangu ninayopata pesa, wewe kazi yenyewe umefukuzwa unafanya kibarua tu sasa, tutakula nini na kile kiwanja tunajengaje sasa?"
"Sijamaanisha hivyo nime..."
"Sitaki maswali, safari nimeshalipiwa tiketi tena ya ndege, kuondoka naondoka tu, full stop, sikuagi, nakupa taarifa"
"Kila siku safari tena za kulala huko huko, kila mara mchungaji, mchungaji, hivi ni mchungaji gani huyo asiyejua kuwa wewe ni mke wa mtu hata kama ni muimbaji wa nyimbo za injili?"
"Kwahiyo unawaza naenda kufanya nini, kulala na mchungaji au?"
"Siyo hivyo ila..."
"Ila nini, ndo unachowaza hicho, utalaaniwa kwa mawazo yako ya ovyo" alinijibu akiondoka kwenda ndani mbio mbio akiwa amejawa na hasira na mimi nimejawa hasira kwa sababu siku hizi safari zimezidi na mikesha kila siku mpaka naanza kushikwa na wasiwasi

"Joa, Joa??!!" nilimwita lakini alinisonya tu, ikabidi nipandishe ngazi kumfuata na nikamkamata mkono wake nikitaka kumsimamisha lakini cha ajabu alinisukuma mzima mzima nikaanguka na kufikia kukaa chini kitako, nikabaki nazishangaa hasira za mke wangu ni za aina gani mpaka amefikia kiwango cha kunisukuma.....

*SEHEMU YA 03*❤️

"Joa mke wangu unafikia kiwango cha kunisukuma?"
"Sasa ulikuwa unanishika ili iweje, nianguke ama?" Aliniuliza swali badala ya kunijibu na haraka haraka akaondoka kwenda chumbani akiniacha na taulo langu nimejifunga tu nikimtazama kwa mshangao, nikiwa siamini kilichotokea, nikibaki nimetoa macho

"Kaka Edmund vipi mbona umekaa chini tena?" Debora alikuja mbio mbio kunitazama akiwa amesikia kishindo wakati alipokuwa jikoni
"Hamna nipo sawa tu, niliteleza nikaanguka"
"Pole kaka, ngoja nikusaidie inuka" alitaka kunishika mkono
"Hapana Debora wewe kaendelee na majukumu yako tu, asante" nilimjibu nikiinuka chini kiunyonge

"Kaka Eddy uuuwiiii?" nikamsikia dada huyo wa kazi (housegirl) akipiga mayowe na kuficha uso wake akitazama pembeni
"Kuna nini kwa...." ndipo nilipoinamisha uso kujitazama mwenyewe nikajikuta nipo uch** (mtupu) sijavaa vitu, muhogo🍆 wangu ukining'inia na kumbe taulo nililokuwa nimejifunga mwilini lilikuwa limelegea na kuchomoka kiunoni wakati nilipokuwa nasimama nikiwa sina habari

"Hamna kitu kaka" aliongea na kugeuka akatoka mbio mbio kuelekea jikoni huku akiwa amejiziba uso kwa aibu asinitazame
"Aisee, mitihani hii" nilijiambia mwenyewe huku nikiokota taulo langu haraka haraka na kwenda chumbani alipokuwa ametangulia mke wangu, Joanitha ambae nilimkuta kwenye meza ya urembo (dressing table) akijitazama huku akiwa amejifunga upande wa khanga nyepesi mwilini, nikamsogelea na kumkumbatia kwa nyuma nikimshika kiuno akasitisha zoezi lake la kujitazama kwenye kioo na kunigeukia

"Niache, sipendi usumbufu"
"Usumbufu wa aina gani mke wangu, kukushika tu leo hii umekuwa usumbufu?" nilimwuliza huku nikimbusu busu shingoni mke wangu huyo ambae ni mweupe na mrembo akiwa na nywele ndefu anazopenda kuzisuka mara nyingi

"Eeh, kufanya jambo kwa wakati ambao siyo wake ni usumbufu tosha huo"
"Kwahiyo hili jambo siyo wakati wake mke wangu, kumshika mke wangu siyo wakati wake huu?"
"Ndiyo, kwa sababu nina mambo mengi, natoka"
"Wapi tena mke wangu na wakati leo uliniambia kuwa utakuwepo nyumbani utakaa na mtoto?"
"Kuna mambo naenda kufuatilia na mchungaji"
"Kwani tiketi hamjakata si umesema tiketi za ndege tayari mmeshakata sasa mambo gani tena hayo?" nilimwuliza akanigeukia na kunikata jicho kali

"Kwahiyo kama kukata tiketi ndo tumeshamaliza mambo yote au, mbona unakuwa msumbufu sana na una maswali mengi sana, kwani nikikaa nyumbani unafaidika nini?"
"Siyo nafaidika nini, tatizo safari zako ni za ghafla ghafla na mimi kama mumeo lazima nikuulize, kosa langu liko wapi, kuuliza tu ndo imekuwa shi...."

"Ngoja simu inaita, mtumishi wa Mungu ananipigia" alinisimamisha kuzungumza akapokea simu na kutoka chumbani kwenda kuongelea sebuleni akiniacha nimesimama chumbani huku nimejishika kiuno nikisikitika kwa kutikisa kichwa

"Kila siku mchungaji mchungaji mbona sasa ni too much?" nilijiongelesha mwenyewe na kwenda sebuleni nikamkuta amekaa kwenye kona ya kochi (sofa) kubwa akiongea na simu huku akicheka, aliponiona nimesimama kwenye mlango wa chumbani kwetu akainuka kwenye kochi na kutoka kwenda nje kuendelea kuzungumza na simu akiwa hataki kabisa nisikie maongezi yake na mchungaji, nikaishia kusikitika tu na kurejea chumbani taratibu, badala ya kujiandaa kwenda kazini na nikajikuta badala ya kujiandaa nakaa tu kitandani na kujiinamia nikiwaza mengi yanayonikabili kwenye maisha yangu hasa ya ndoa

Ni mwezi umekatika sasa siujui mwili wa mke wangu Joanitha, kila siku yeye ni safari za kwenda kwenye injili na uimbaji, mikutano ya kikanisa kwa sababu ni muimbaji binafsi anayejitegemea, sikatai kuwa analeta chochote nyumbani lakini safari za siku hizi zimezidi sana tofauti na hapo awali ambapo nilikuwa nina kazi nzuri ila kwa sasa nikiwa ninafanya kibarua tu kwenye ofisi za watu na kulipwa posho kidogo na si mshahara baada ya kufukuzwa kwenye ofisi yangu ya awali ambayo nilikuwa napokea mshahara mzuri na marupurupu ya kutosha yaliyonifanya nilipie kodi ya nyumba nzima ninayoishi na familia yangu, ninunue kiwanja na gari ambalo kwa sasa lipo gereji kwa ajili ya kukosa pesa za matengenezo wakati huo huo simu yangu ya mkononi ikaita nikatazama namba ni ya baba mwenye nyumba hiyo tuliyopanga nzima, ikiwa ni sebule na vyumba viwili vya kulala, kimoja ninacholala mimi na mke wangu Joanitha na kingine akilala dada wa kazi (housegirl) Debora pamoja na mtoto wetu mdogo Erick, nikashusha pumzi kabla ya kupokea simu hiyo maana ni wiki moja imeshakatika mzee huyo akiwa ananidai kodi ya miezi sita na sijamlipa bado, na niliyoiazima kwa mtu rafiki yangu ili nilipie kodi nikiwa sijapewa nikiwa nimeahidiwa kutumiwa kesho yake, nikashusha pumzi na kupokea kiunyonge nikiwa bado sijaanda majibu ya kumpa mzee huyo mtata

"Edmund unaendeleaje?"
"Salama mzee wangu, shikamoo"
"Marahaba, upo kimya sana mwanangu, hata kunisalimia?"
"Hamna mzee ndo nilikuwa nasubiria pesa yangu fulani hapa nikaona nisikusumbue tena" nilijitetea kabla hata sijaulizwa habari za kodi maana nilijua ndiyo anachokimaanisha
"Pesa gani tena?"
"Si kodi mzee wangu?"
"Kodi kwani si mmeshanitumia?"
"Lini?"
"Juzi, mkeo kanirushia pesa yote kamili hauna habari?"
"Yote kamili, mke wangu mimi?"
"Eeh, mimi nilitaka tu kukusalimia maana niliongea nae yeye tu wala wewe sikukushukuru nikajua utanipigia sasa nika..." kabla hajamaliza sentensi yake simu ikakata akiishiwa salio
"Mke wangu kalipa pesa yote ameipata wapi?" nilijiuliza na kutoka mbio mbio kwenda mpaka sebuleni na sikumkuta na ndipo nilipoenda mpaka nje nikamkuta anazungumza na simu bado huku amekaa kabisa kwenye ngazi akitabasamu, tangu muda ule mpaka sasa

"....halafu pia nashukuru sana kwa kunilipia kodi nyuma jamani ubarikiwe sana uuuwiii mpaka nimeshangaa, nilijua utanilipia miezi michache tu kumbe yote jamani, sina cha kusema kwakweli..." nilimsikia mke wangu akizungumza na simu, macho yakanitoka.....

*SEHEMU YA 04*❤️

"...asante sana jamani kwa...!" kabla mke wangu Joanitha hajamalizia sentensi yake aligeuka na kuniona akashindwa kuendelea na maongezi yake akakata simu haraka

"Mbona umekata simu, si ungeendelea tu kuzungumza kwani kusimama kwangu mimi kunakuzuia kuzungumza na simu?" nilimwuliza
"Hamna mbona imejikata tu yenyewe kwa sababu tangu awali aliniambia kuwa hana salio la kutosha"
"Sasa si umpigie tu kwani shida iko wapi au nawe hauna salio?"
"Nitaongea nae baadae haina shida"
"Ni nani kwani?"
"Yaani mimi nakereka sana na maswali yako Eddy hujui tu, nani kwani si mchungaji au?"
"Mchungaji, ohoo sasa mimi ningejuaje kama ni yeye?"
"Halafu habari za kuulizana ulizana nani aliyepiga simu sizipendagi hizo yaani hujui tu"
"Nina uhalali wa kuuliza unaongea na nani, mimi ni mumeo"
"Unafikiri nilikuwa naongea na nani kwa ujinga wako, mchungaji tu, namba hii hapa" alinionyesha kwenye simu ikiwa imeseviwa 'PASTOR BUKUKU' ni mchungaji ninayemfahamu vizuri nikiwa nimewahi kuwa muumini pia kwenye kanisa hilo na mpaka sasa ninaenda mara moja moja aliyenipeleka kwenye kanisa hilo ni mke wangu mwenyewe na si mchungaji tu akiitwa pia 'Nabii' au kwa lugha ya Kiingereza iliyozoeleka 'Prophet Bukuku'

"Kila wakati ni mchungaji, mchungaji, mchungaji, huduma huduma tu, safari juu ya safari muda wangu uko wapi Joanitha,?"
"Muda gani tena Edmund, kwani shida yako nini, hupendi mimi nifanye kazi ya Mungu unataka nifanye nini sasa, nikadange nikuletee wanaume hapa ndo uridhike?"

"Sijamaanisha hivyo ila..."
"Ila nini, mbona unakuwa kama pepo, hupendi mkeo afanye kazi ya Mungu, nitakusomea maandiko mpaka ukome yanayozungumzia watu kama wewe, endelea tu kunitibua" alijibu kwa hasira na kuondoka kuelekea ndani

"Joa, Joa!?" nilimwita nikamfuata nyuma nyuma na kumshika mkono wake akageuka kwa hasira kama kawaida yake

"Niache Edmund"
"Nani aliyelipa kodi ya nyumba?"
"Ni mimi shida yako?"
"Umepata wapi hiyo pesa?"
"Kwenye kazi hii hii unayonizuia nisiende"
"Mbona sasa unamshukuru mchungaji kwenye simu, anahusikaje sasa na kodi yetu?"
"Ndiyo amenipa yeye"
"Amekupa, kivipi na kwa misingi gani?"
"Sasa si nafanya huduma, nikamshirikisha akasema ni jambo dogo hilo basi akanilipia, kuna shida gani?"
"Mbona hujanishirikisha ukaamua tu kujifanyia utakavyo kimya kimya?"

"Kwani pastor Bukuku hamfahamu au ndo ilimradi tu uzungumze tuanze kulumbana ujisikie vizuri?" alibinua mdomo na kuondoka kuelekea chumbani nami nikabaki nimesimama huku nimejishika kiuno nikiwa natikisa kichwa tu kusikitika kwa ninayoyaona, nikakaa kwenye kochi (sofa) kubwa nikiwa nimejawa hasira zilizonipanda mpaka kichwani, nilichokiwaza kichwani ni kumpigia mchungaji Bukuku mwenyewe ikibidi nimwambie kuwa mke wangu asiende hiyo safari ya kesho na hata leo, nikampigia simu ikaita na kupokelewa

"Halow?!" aliitika kwa sauti ya chini akionekana kama alikuwa amelala
"Habari yako pastor?"
"Njema nani mwenzangu?"
"Edmund hapa, mume wa Joanitha"
"Oooh Edmund mtumishi wa Bwana, Bwana asifiwe sana?"
"Amen mchungaji nilikuwa nina..."
"Yaani ndo nilikuwa nataka kukutafuta nikuambie kuhusu safari ya mke wako nikasema ngoja nimsubiri mkeo mwenyewe azungumze na wewe, kesho tunakwenda Mbeya kihuduma, yeye anaenda kwa ajili ya kuimba amealikwa, hakika Joanitha atakuwa muimbaji mkubwa wa kimataifa ambae atatikisa ulimwengu huu kwa sababu sasa naiona neema kubwa juu yake ya mialiko, nazidi kumwombea akawe juu na juu zaidi kuliko viwango alivyo sasa" mchungaji aliniwahi kabla hata sijamuuliza nikabaki nimenyamaza kimya nikitafuta cha kuzungumza

"Sasa unaonekana huna namba yangu ungeniambiaje, au kwa sababu nimekupigia mimi?" niliuliza kimoyo moyo

"Nataka niachilie maombi ya kibali juu yenu, yupo hapo mke wako Joanitha?"
"Hayupo ha..." kabla sijamalizia sentensi yangu nikashangaa nikiporwa simu na Joanitha mke wangu ambae alikuwa nyuma kumbe akinisikiliza, akaiweka sikioni mwake

"Baba mchungaji Bwana asifiwe" alimsalimia akiweka sauti ya juu (loud speaker) ili namimi nisikie mazungumzo yao, akiwa ameshajiandaa tayari

"Amen nilikuwa nazungumza hapo na mume wako nilitaka kuachilia maombi ya kibali kwenu leo"
"Ni kweli ila utatuombea tu usiku mimi ndo nataka nitoke sasa hivi nakuja huko" alijibu akiitoa sauti kubwa (loud speaker) na kuiacha ya kawaida, sikusikia tena walichozungumza, akaingia chumbani na simu yangu akiniacha sebuleni nimesimama tu natazama na baada ya dakika takribani tano akatoka na mkoba (handbag) yake na kunipa simu yangu

"Safari njema" nilimwambia akatikisa kichwa na kuondoka taratibu nikiwa namtazama tu na ndipo nikainuka na kwenda chooni taratibu nilipotoka chooni wakati narudi sebuleni simu yangu ikaita nikawa natazama namba ya aliyenipigia na ndipo nilipojikuta nikigongana na dada wa kazi (housegirl) debora, kiuno changu kwa makalio yake, akiwa ameinama anapiga deki kwenye korido ya kuelekea bafuni na chooni safari hii akiwa amejifunga kitenge.....

*SEHEMU YA 05*❤️

"Jamani nani tena ana michezo mibaya?" alilalamika na kugeuka
"Oooh sorry ni mimi Debora, samahani sana sana sikukuona nilikuwa ninazungumza na simu hapa, samahani sana, niwie radhi" nilimjibu huku nikijikuna kichwa

"Oooh kaka Edmund jamani, samahani sikujua kama ni wewe ndo maana nikaongea vile"
"Usijali, natoka sasa naenda kazini pia"
"Kwani dada Joanitha ameshaondoka?"
"Ndiyo ameondoka"
"Ooooh sawa" Debora akiwa amesuka nywele za twende kilioni alitikisa kichwa akikipandisha pandisha vizuri kitenge chake na kuinama kuendelea kufagia, nikashusha pumzi na kuondoka taratibu huku nikijikuna kichwa na nilipotazama kwenye suruali yangu mambo yalikuwa yameshabadilika tayari, muhogo🍆 ulisimama ndani ya suruali hiyo nyembamba iliyonishika mwili ukitaka kuitoboa kabisa utoke nje ikabidi nisimame kwanza na kuiweka weka vyema suruali yangu maana muhogo🍆ulijichora sana kwa sababu ulishtuka kuyagusa makalio makubwa ya dada wa kazi (housegirl) Debora, msichana wa Kisukuma mwenye sura ya kawaida, vijana wanaita 'sura ya baba' lakini 'mwili nyumba' akitembea vitu vinatikisika vyenyewe, mweusi wa rangi ambayo kwangu haikuwa rangi rafiki na ndiyo maana hata mke niliyemuoa, Joanitha ni mweupe, na kingine ni uchu wa muda mrefu, zaidi ya mwezi, wa tendo ambalo sijalipata kwa mke wangu kutokana na kila siku kupigwa kalenda tu na kupewa kila aina ya visingizio kwa sababu ya mambo yake ya uimbaji na safari zake za 'kihuduma' zisizokwisha pamoja na mchungaji wake

Nilipogeuka baada ya kuipandisha pandisha suruali yangu nikakuta Debora ameacha kufagia ananitazama ingawa hakujua nilikuwa nafanya nini, nilipomtazama haraka haraka akajifanya anaendelea na shughuli yake ya kufagia nikaendelea na safari yangu mpaka chumbani nikamalizia kujiandaa na kuanza safari ya kutoka nikamkuta Debora ameniandalia chai ya maziwa na mikate mezani huku amesimama akinisubiri

"Ndo naenda, kama kuna lolote utanitumia ujumbe mimi au dada yako Joa"
"Kaka chai"
"Hapana nitachelewa"
"Angalau na kipande kimoja cha mkate kaka" alinibembeleza kwa kupiga goti nikabaki namtazama tu kwa sekunde kadhaa nikikumbuka tukio la kumgonga kwenye makalio yake makubwa dakika chache zilizopita nikajikuta naduwaa

"Sawa nitakunywa" nilimjibu akatabasamu na kunivutia kiti nikae, nilipokaa akaninawisha maji kwa goti huku nikimtazama tu
"Karibu chai kaka"
"Asante sana Debora" nilimjibu akainuka na kugeuza njia akiondoka kuelekea jikoni nami nikabaki nikimsindikiza kwa macho huku nikitikisa tu kichwa na ndipo muda huohuo simu yangu ya mkononi ikaita nikatazama namba ni ya mfanyakazi mwenzangu kwenye kazi mpya ninayojishikilia kwa malipo madogo ya posho tu

"Eddy vipi rafiki yangu?"
"Safi kwema?"
"Kwema kaka uko wapi?"
"Nipo nyumbani ndo nataka kutoka hapa nije ofisini"
"Ndo unataka kutoka tena uje wapi?"
"Si ofisini?"
"Ofisini hahaha unachekesha kwani hujapata taarifa?"
"ipi hiyo?"
"Upo nyuma sana, ofisi wameifunga kuanzia leo kwa muda usiojulikana, TRA wanadai kodi ndefu sana haijulikani lini itafunguliwa"
"Dah sasa itakuwaje?"
"Ndo hivyo, mimi kuna mishe nyingine nimeipata mahali kama kutakuwa na nafasi nitakuunganisha nawewe maana wewe mwanangu sana haunaga baya"
"Nitashukuru sana rafiki yangu"
"Poa halafu kwani upo wapi, umetoka?"
"Hapana kwanini, si/muda ule nimekwambia ndo nataka kutoka kuja ofisini?"
"Ahaa maana nimemwona shemeji Joa nikadhani yupo na wewe maana mlikuwa mmeshikana mikon...koh koh" rafiki yangu huyo aliongea akikohoa mara kadhaa

"Umetuona wapi, mimi na Joa mke wangu?"
"Hamna aah macho yangu yalitazama vibaya, ngoja nitakucheki baadae naingia saluni kupunguza ndevu kwanza hapa" alinijibu na kukata simu akiniacha na maswali kichwani

"Ameniona na Joa tumeshikana nini, sijamuelewa vizuri au sijamsikia tu vizuri?!" nilijiuliza nikiwa nimejawa na wasiwasi na muda huo huo ujumbe mfupi (SMS) wa rafiki yangu huyo huyo ambae alisita kuniambia alipopiga ukaingia kwenye simu yangu ukisomeka;

"...SAMAHANI MY BRAZA, NIMEPATA UKAKASI KUKUAMBIA NILIPOPIGA NA NDIYO MAANA NIMEKUTUMIA UJUMBE, NIMEMWONA SHEMEJI JOANITHA NA MWANAUME WAMESHIKANA MIKONO NJE YA HOTELI MOJA HIVI WAKATI NIKIWA KWENYE BAJAJI NIKADHANI LABDA NIWEWE, USIFIKIRIE VIBAYA LAKINI NIMEONA NIKWAMBIE TU HUENDA MNAFAHAMIANA NA YULE MTU VILEVILE LAKINI SINA NIA YA KUKUPA WASIWASI" aliniambia maneno hayo ambayo yalinifanya mwili wangu wote nihisi umeshikwa na ganzi......

Inaendelea.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

*TABIA ZA MKE WANGU ZILIVYONIFANYA NITEMBEE NA HOUSEGIRL*❤️ *SEHEMU YA 01----05*  >>> https://gonga94.com/semajambo/tabia-za-mke-wangu-zilivyonifanya-nitembee-na-housegirl-sehemu-ya-01-05

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
profile
majario 28 Aug 2025 05:51
SAMAHANI MY BRAZA, NIMEPATA UKAKASI KUKUAMBIA NILIPOPIGA NA NDIYO MAANA NIMEKUTUMIA UJUMBE, NIMEMWONA SHEMEJI JOANITHA NA MWANAUME WAMESHIKANA MIKONO NJE YA HOTELI MOJA HIVI WAKATI NIKIWA KWENYE BAJAJI NIKADHANI LABDA NIWEWE, USIFIKIRIE VIBAYA LAKINI NIMEONA NIKWAMBIE TU HUENDA MNAFAHAMIANA NA YULE MTU VILEVILE LAKINI SINA NIA YA KUKUPA WASIWASI" aliniambia maneno hayo ambayo yalinifanya mwili wangu wote nihisi umeshikwa na ganzi......
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Kama wewe hujatimiza miaka 18+ usije nasema usije kabisa ni wakubwa tu
Kama wewe hujatimiza miaka 18+ usije nasema usije kabisa ni wakubwa tu

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest