Ingia

Sema Jambo 2025

Unsplashb
750+ Trending Pictures | Download Free Images on gonga94
  gonga94 official track

Miaka 4 iliyopita mke wangu aligundua kuwa niliwahi kuchepuka na kwa bahati nikapata mtoto wa nnje ambaye ki umri alikua ni sawa na mtoto wangu wa kwanza

27th Aug, 2025 Views 17

, wakati huo alikua na miaka minne. Ingawa nilikua nimeshaachana na huyo mwanamke nalea tu mtoto kwani nilitambua kosa langu lakini mke wangu alikasirika sana.

Niliomba sana msamaha lakini hakutaka kunisikiliza, aliniambia moja kwa moja kuwa nichague kati ya mtoto niliyezaa na huyo mwanamke au ndoa yangu. Aliniambia kama nataka abaki basi nisiwasiliane na huyo mwanamke na hataki kusikia kitu chochote, hata matumizi alikua hataki nimtumie.

Kwakua nilikua nampenda sana mke wangu nilikubali kukata mawasiliano kablsa na Mama wa mtoto wangu lakini sikua tayari kumtelekeza mwanangu, nilimfungulia mtoto akaunti na kila mwisho wa mwezi nilikua namuwekea mtoto bila kuwasiliana naye, sikutaka hata kujua anaendeleaje, mwanamke nilimblock kwenye kila kitu.

Nilikua nafanya hivyo kimya kimya bila mke wangu kujua. Lakini miezi miwili iliyopita nilisahau kile kikaratasi cha kuwekea pesa kwenye gari yangu, mke wangua likiona, alinibana sana nikalazimika kumuambia ukweli kuwa nilikua namhudumia mwanangu kwakua hana hatia.

Mke wangu hakunijibu, alinyamaza kimya kw aisku mbili, siku ya tatu natoka kazini nikakuta mke wangu kachukua kila kitu chake kaondoka. Ananiambia nimechagua kumhudumia mwanangu hivyo nibaki naye, nilihisi utani lakini wiki ilipita, nikamaua kutafuta watu kuongea naye.

Tukaitishwa kikao na kila mtu ila mke wangu kaweka msimamo kuwa ili anisamehe na kubali kurudi nilazima niache kumhudumia mtoto wangu na tuandikishe mahakamani kuwa simtambui huyo mtoto na kama niki*fa basi asirithi kitu chochote, naomba ushauri wako nifanye nini?

Mke wangu nampenda tena sana lakini naona shida kumtelekeza mwanangu, makosa nilifanya mimi hivyo sioni kama ni sawa kumuadhibu mwanangu! Nimemuambia basi kama ishu ni mawaisliano maana siwasiliani na Mama wa mtoto basi pesa niwe napeleka ustawi wa jamii hata nisitume kwenye akaunti yake lakini hatak.

Anachotaka ni mimi nisimhudumie mwanangu, sasa hapo naona shida maana kama ni pesa ya kuhudumia ni nayo, yeye namhudumia nampe pesa zaidi ya mara kumi ya ninazotuma kule lakini ananiambia hataki tu nimhudumie, nishauri nifanye nini?.
   

X
SHARE TO SOCIAL MEDIA

Miaka 4 iliyopita mke wangu aligundua kuwa niliwahi kuchepuka na kwa bahati nikapata mtoto wa nnje ambaye ki umri alikua ni sawa na mtoto wangu wa kwanza  >>> https://gonga94.com/semajambo/miaka-4-iliyopita-mke-wangu-aligundua-kuwa-niliwahi-kuchepuka-na-kwa-bahati-nikapata-mtoto-wa-nnje-a

#Nk #gonga94 #trending #instagood #explore #viral #challenge #simulizi #hadithi #israel #iran #war 

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on LinkedIn
Share on Pinterest
 

Maoni

You're not logged in
Click here to login and comments
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
gonga94 official track
ZETU
SIMULIZI NA SAUTI ZETU
gonga94ads - The Best Popunder Adnetwork
Kama wewe hujatimiza miaka 18+ usije nasema usije kabisa ni wakubwa tu
Kama wewe hujatimiza miaka 18+ usije nasema usije kabisa ni wakubwa tu

RATIBA YA SIMULI ZETU

Hakuna ratiba iliyopangwa kwa sasa.


Home Login Signup
Top 20 Popular Contact us
Terms & Conditions About us Latest