KWANINI MTU MWENYE MOYO WA UPENDO, HURUMA,KUJALI HUWA ANATESEKA SANA KWENYE MAHUSIANO?
Katika huu ulimwengu maisha yapo tofauti kabisa na hadithi ambazo huwa tunasimuliwa.
Watu ambao huumizwa Sana iwe kwenye mahusiano, kazini,katika jamii n.k huwa ni wale watu ambao huwa wenye moyo wa huruma,kujali, unyenyekevu, kusamehe.
Kwanini mtu ambaye ni mwema sana huwa anaumizwa sana?
Kuna sababu hapa chini
Kwanini mtu mwenye kiburi, jeuri, majivuno, ujuaji, misimamo mikali sana, ubishi, ukorofi,uchoyo huwa anachagua mwenza ,au rafiki mpole sana , mwenye huruma kupitiliza,kujali, uvumilivu, mwenye moyo wa kusaidia sana,mtu ambaye hawezi kusema neno "Hapana" akiombwa kitu chochote?
Jibu lake ni
-Kutaka kumuelewa kila mtu.Mtu mwema sana kwenye jamii huumizwa Sana kwa sababu huwa anataka kumuelewa kila mtu.Akifokewa, kutukanwa,kudhalilishwa, kupigwa,kugombezwa, kuibiwa,kutapeliwa, kupokonywa mali huwa anataka amuelewe mkosaji wake.Mara nyingi mtu mwema sana huanza kuweka visingizio mbalimbali juu ya tabia mbaya za watu wengine.-
-Kuweka visingizio juu ya tabia mbaya za watu wengine.Kwa mfano anaweza kuishi na mtu ambaye ni mlevi kupindukia,mwizi,mvivu,mtu mbabe,mtu mgomvi mgomvi,mtu jeuri,mtu mzembe,mtu ambaye anafanya makosa kwa makusudi kisha anageuza kibao kwa wenzake,mtu ambaye hataki kazi lakini anataka maisha ya kifahari,mtu ambaye hana nidhamu ya fedha lakini anaomba sana fedha,mtu ambaye hana shukurani.
Mtu mwema sana huwa anaweka visingizio juu ya tabia mbaya za wapendwa wake kwa kudai hawajafanya makusudi bali walikuwa na "stress",wengine husema huyo yupo na hasira kupitiliza kwa sababu amepitia manyanyaso utotoni,wengine husema huyo ni jeuri kwa sababu hajapata upendo wa baba na mama yake.
Lakini tukija kwenye uhalisia wa maisha je kila mtu ambaye amepitia manyanyaso utotoni huwa anakuwa jeuri,anakuwa mbabe,anakuwa mbishi,anakuwa na hasira kupitiliza,anakuwa mkorofi sana,anakuwa mlevi kupindukia? Jibu lake ni HAPANA.
Mtu anakuwa jeuri kwa sababu ameamua kuwa jeuri sio kwa sababu ya manyanyaso.Mtu anakuwa mwizi kwa sababu ameamua kuwa mwizi sio kwa sababu ya kupitia manyanyaso.
Kuna watu utotoni mwao wamedekezwa sana lakini hivi sasa wamekuwa jeuri kupitiliza hivyo mtu kuwa jeuri ni maamuzi yake binafsi na anatakiwa kuwajibika kwa makosa na tabia zake.
-Kutaka kumbadilisha tabia.Sababu nyingine inayofanya watu wenye huruma kupitiliza kuumizwa sana ni wao kutaka kumbadilisha tabia mtu ambaye ni jeuri,mtu mzembe sana,mtu mwenye majibu ya mkato,mtu mbabe sana,mtu asiyekuwa na huruma wala shukurani.
Ikiwa unajipa jukumu la kutaka kumbadilisha tabia mwenzako upo hatarini kuangamizwa na mtu huyohuyo ambaye unataka kumbadilisha tabia.
Mtu ambaye hana hofu yoyote juu ya tabia zake huwa anasumbua sana.
Mtu ambaye anaweza kuongea kitu chochote na kufanya kitu chochote bila kuhofia madhara yake kama akiwa rafiki yako wa karibu lazima akutoo machozi tu.Utabeba lawama kwa makosa yake,utaingia hasara kifedha kwa kuvumilia makosa yake yenye kujirudia rudia,utapigwa faini kwa makosa yake,utafukuzwa kazi kwa sababu zake, utapoteza wateja kwa sababu ya makosa yake.
Mtu jeuri sana huwa haambiliki, hashauriki,huwa hapewi onyo au karipio bali huachwa huru aende kuishi anapotaka kisha ataona madhara ya tabia zake na maamuzi yake.Lakini ukitaka kumbadilisha tabia lazima tu akutoe machozi.
-Kutaka kupendwa badala ya kutaka kuheshimiwa.
Mtu ambaye huwa anataka kupendwa,kusifiwa,kuitwa majina mazuri,kupongezwa, kuonekana mwema sana huwa yupo hatarini kuangamizwa na watu ambao anajitoa mhanga kuwafurahisha.
Mtu yeyote ambaye anajua kwamba unataka akupende ili uwe na furaha lazima atakupanda kichwani kwa sababu akili yake inajua kwamba unampenda sana,hauwezi kuishi bila yeye,hauwezi kumuacha hata akifanya makosa makubwa sana.
Hata ofisini ikitokea mfanyakazi yeyote akijua kwamba anapendwa sana na bosi wake basi huanza dharau, kiburi, majivuno, ujuaji,ubishi, kuchelewa kazini,kufanya makosa makusudi,kutumia fedha vibaya sana, kuwagombeza wafanyakazi ambao wanamkosoa kwa utendaji kazi mbovu,akifanya makosa anageuza kibao kwa wenzake,anaondokakazini mapema wakati huohuo anaingia kazini kwa kuchelewa,akienda likizo anachelewa kurudi kazini kwanini? Ni kwa sababu kumpenda mtu na kumheshimu ni vitu viwili tofauti.
Kama unamheshimu mtu hata kama haumpendi utatii maagizo yake na sheria zake lakini kama unampenda unaweza kugomea maagizo yake kisha unaomba msamaha unajua tu utasamehewa.
Ndiyo maana mtu hata akiwa mlevi kupindukia hawezi kwenda kambi ya jeshi kufanya vurugu lakini akiwa nyumbani kwao anafanya vurugu kwa sababu anajua wanampenda sana watamvumilia.
Heshima haina uhusiano wowote na kujali, kumliwaza, kumbembeleza, kumnyenyekea mtu mwingine.
Mtu ambaye unamheshimu anafanya uwe makini lakini mtu ambaye anakupenda huwa anafanya ufanye chochote kwa sababu unajua atakulinda .
Kama unataka kuishi kwa amani na watu wengine dai HESHIMA sio upendo .
Upendo au mapenzi ni hisia lakini HESHIMA haina uhusiano wowote na hisia.
Uwe na upendo au uwe hauna upendo wowote mbele ya kiongozi wako unakuwa na HESHIMA lakini mbele ya mwanaume au mwanamke ambaye unaempenda sana unaweza kumfanyia vituko kwa sababu unajua anakupenda atavumilia.
Hakuna mtu ambaye anaweza kumpima mwenza wake kama yupo na HESHIMA lakini watu huwa na desturi ya kuwapima wenza na marafiki zao kuhusu UPENDO WA DHATI.
Ukifanya makosa mbele ya mtu ambaye unamheshimu ile HESHIMA yako inatoweka papohapo lakini ukifanya makosa kwa mtu ambaye unaempenda sana bado hisia za upendo wako au upendo wake unakuwa palepale japokuwa ataumia sana.
Mtu ambaye unaempenda sana au anayekupenda sana anaweza kukupuuza, vilevile unaweza kumpuuza,anaweza kukufokea,unaweza kumfokea,anaweza kukushambulia kwa maneno makali sana,unaweza kumshambulia kwa maneno makali sana lakini mtu ambaye unamheshimu hauwezi kumfokea, kumtukana,kumjibu vibaya,kumgombeza kwa sababu lazima tu atakuletea MADHARA.
Amani, furaha na utulivu unapatikana sehemu yenye HESHIMA sio sehemu yenye upendo.
Mtu anaweza kumuibia mama au baba yake kwa sababu anajua kuna upendo msamaha upo lakini mtu ambaye unamheshimu ukifanya makosa tu mahusiano yenu yameharibika.Heshima hufanya mtu kuwa makini sana lakini upendo humfanya mtu kuwa jeuri sana kama anajua anapendwa sana kuliko mtu mwingine yeyote.
Kazi kwako je unataka watu wakupende au wakuheshimu.
Heshima inahusisha majukumu lakini upendo upo kwa mtu yeyote hata ambaye hana majukumu yoyote.
Unaweza kumshitaki mtu mwingine kwa kukukosea HESHIMA lakini hauwezi kwenda kumshitaki mtu yeyote kwa kukosa UPENDO kwako.
Upendo ni hisia lakini HESHIMA ni utii ambapo hakuna hisia zozote eneo hilo.
haya yapo ndani ya kitabu cha JINSI YA KUPONA MAUMIVU MAKALI SANA MOYONI.
#Spirit_Warrior
#Wounded_Healer
??
Kama tatizo lako ni kubwa zaidi tunaweza kuwasiliana kwa ajili ya Counselling session na ufafanuzi wa kilichoandikwa hapo juu na utaona mabadiliko na kujisikia nafuu ndani ya muda mfupi baada ya mazungumzo.(Counseling kwa njia ya simu gharama Tshs 30000 , kuonana uso kwa uso Tshs 40000
Kwa wapenzi wa kusoma vitabu unaweza kupata nakala zangu orodha ipo chini ?
Kupata kitabu cha
1.JINSI YA KUPONA MAUMIVU MAKALI SANA MOYONI - (Softcopy Tsh 30000)
2.UTULIVU WA AKILI KIPINDI KIGUMU (Softcopy)
3.FIKRA ZAKO FURAHA YAKO (softcopy)
4.TIBA YA MSONGO WA MAWAZO (by & Softcopy)
5.MALEZI YA UBONGO KISAYANSI( hardcopy & softcopy)
6.TABIA ZA WATU WALIOFANIKIWA (Hardcopy & softcopy)
7.MISINGI 10 YA FURAHA SIKU ZOTE (hardcopy &softcopy)
8.BADILI FIKRA ZAKO BADILI MAISHA YAKO
BEI Kitabu kimoja softcopy 5000 isipokuwa kitabu namba 1 bei yake ni Tsh 30000, hardcopy moja 10000
Mawasiliano
+255766862579
+255622414991
Imeandikwa na Psychologist
Said Kasege
Temeke,Dar es salaam.